Kilimanjaro: Askari mbaroni kwa madai ya kusafirisha dawa za kulevya

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) amekamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kusafirisha kilo 120 za mirungi.

Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Simon Maigwa alipoulizwa na Mwananchi kuhusu madai ya tuhuma hizo alisema anaifuatilia na hakutaka kuingia kwa undani juu ya ukamataji huo.

Awali, taarifa kutoka Wilayani Rombo, askari huyo anayedaiwa kutiwa mbaroni Mei 10, 2022 eneo la Mengwe, zinasema alikuwa akisafirisha mirungi kwenda Babati.

Taarifa zinadai kuwa askari huyo alikamatwa akisafirisha mirungi hiyo kwa gari aina ya Toyota Corolla.

Hii ni mara ya pili kwa Polisi Kilimanjaro kuwakamata askari wake kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya. Mei 18, 2013 walimkamata EX PC George Bisongoza akisafirisha bangi kwa kutumia gari la Polisi.

George ambaye alikamatwa usiku wa Mei 18 eneo la Kilema Pofu Barabara ya Moshi-Himo, alikuwa akisafirisha magunia 18 ya bangi kwa kutumia gari la FFU Arusha.

Hata hivyo, George alishahukumiwa kifungo cha maisha jela Desemba 15, 2017.



Chanzo: Mwananchi
 
59588790.jpg
 
Back
Top Bottom