OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,391
- 104,535
Singida Fountain Gate FC ipo nafasi ya sita na alama zake 16 baada ya michezo 16! Mwendelezo wake umekuwa si mzuri inawezekana hii ni baada ya kuondeokewa na nyota wake kadhaa waliojiunga na Ihefu wakati wa dirisha dogo la usajili.
Kumekuwa na story nyingi kuhusu uendeshwaji wa Singida Fountain Gate FC na uhusiano na Ihefu.
Watu wengi wanahofia kuusema ukweli kuhususiana na kinachoendelea kati ya Singida Fountain Gate FC na Ihefu. Siku zote maji na mafuta hayawezi kuchanganyika, ndivyo ilivyo siasa haiwezi kwenda sambamba na biashara ya mpira kwa wakati mmoja.
Kama ni biashara ya mpira basi ifanyike kwa mujibu wa taratibu na weledi ili biashara ya mpira iweze kufanyika na mwisho wa siku ionekane faida na hasara.
Kama unaanzisha timu halafu unataka uitumie kama daraja/jukwaa la kufanya siasa maana yake haiwezi kuendeshwa kwa faida badala yake itakuwa kama ni taasisi isiyo ya kibiashara ‘non profit organization’ lengo lake ikiwa ni platform ya kufanya siasa.
Kwa hiyo Singida Fountain Gate FC ilitakiwa ichague upande, wakati wanatuambia wameingia ubia kati ya Singida Big Stars na Fountain Gate Schools.
Kwa sababu nyuma ya Singida Fountain Gate kuna mwanasiasa sio mtu wa biashara ya mpira, halafu kuna mtu mwingine anawekeza pesa kwa ajili ya kutengeneza miundombinu akitegemea baadae gharama zake anazozitumia zirudi.
Wanapokutana watu wawili wenye malengo tofauti hawawezi kupiga hatua! Mwanasiasa ana vitu anataka kufanikisha kwenye siasa mwingine anataka kufanikiwa kwenye upande wa biashara. Ndio maana mwisho wa siku wametengana kila mmoja kaenda kivyake.
Upande mmoja uliokuwa Singida Fountain Gate FC umehama na rasilimali zake na kwenda Ihefu, kwa sababu aliyekuwa nyuma ya mchakato mwanzoni amehamia Ihefu.
Kwa hiyo upande wa Fountain Gate Schools umebaki na jina la Singida ambalo naamini baada ya muda na lenyewe litabadilishwa kama ambavyo Ihefu itakavyobadilishwa huko mbele ya safari
Credit Shaffi Dauda