Kilichotokea Singida FG nimeshindwa kukiweka Kihasibu

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,238
103,899
Singida Fountain Gate FC ipo nafasi ya sita na alama zake 16 baada ya michezo 16! Mwendelezo wake umekuwa si mzuri inawezekana hii ni baada ya kuondeokewa na nyota wake kadhaa waliojiunga na Ihefu wakati wa dirisha dogo la usajili.

Kumekuwa na story nyingi kuhusu uendeshwaji wa Singida Fountain Gate FC na uhusiano na Ihefu.

Watu wengi wanahofia kuusema ukweli kuhususiana na kinachoendelea kati ya Singida Fountain Gate FC na Ihefu. Siku zote maji na mafuta hayawezi kuchanganyika, ndivyo ilivyo siasa haiwezi kwenda sambamba na biashara ya mpira kwa wakati mmoja.

Kama ni biashara ya mpira basi ifanyike kwa mujibu wa taratibu na weledi ili biashara ya mpira iweze kufanyika na mwisho wa siku ionekane faida na hasara.

Kama unaanzisha timu halafu unataka uitumie kama daraja/jukwaa la kufanya siasa maana yake haiwezi kuendeshwa kwa faida badala yake itakuwa kama ni taasisi isiyo ya kibiashara ‘non profit organization’ lengo lake ikiwa ni platform ya kufanya siasa.

Kwa hiyo Singida Fountain Gate FC ilitakiwa ichague upande, wakati wanatuambia wameingia ubia kati ya Singida Big Stars na Fountain Gate Schools.

Kwa sababu nyuma ya Singida Fountain Gate kuna mwanasiasa sio mtu wa biashara ya mpira, halafu kuna mtu mwingine anawekeza pesa kwa ajili ya kutengeneza miundombinu akitegemea baadae gharama zake anazozitumia zirudi.

Wanapokutana watu wawili wenye malengo tofauti hawawezi kupiga hatua! Mwanasiasa ana vitu anataka kufanikisha kwenye siasa mwingine anataka kufanikiwa kwenye upande wa biashara. Ndio maana mwisho wa siku wametengana kila mmoja kaenda kivyake.

Upande mmoja uliokuwa Singida Fountain Gate FC umehama na rasilimali zake na kwenda Ihefu, kwa sababu aliyekuwa nyuma ya mchakato mwanzoni amehamia Ihefu.

Kwa hiyo upande wa Fountain Gate Schools umebaki na jina la Singida ambalo naamini baada ya muda na lenyewe litabadilishwa kama ambavyo Ihefu itakavyobadilishwa huko mbele ya safari

Credit Shaffi Dauda
 
Wengine tulionyesha wasiwasi na umiliki wa hiyo Singida Big Stars na Singida Fountain Gates halafu hao wachaa mbuzi wakawa wanajifanya kama vile hawaoni wala hawasikii. Tutegemee Ihefu kuhamishiwa Singida (bila idhini ya wadau wakuu wa Mbarali) halafu SFG kutimuliwa kwa nguvu kutoka Singida kama siyo kufanyiwa fitna hadi ishuke daraja.

Singida ni timu yenye makandokando sana. Sasa academy inainunua timu ya ligi kuu tena yenye kikosi na mafanikio kama SBS?

Nayajua yote hayo ila taarifa rasmi iliyotolewa ni kuwa zimeungana kikamilifu na SBS haipo tena. Sasa inakuwaje baada ya hapo nembo ya kwenye jezi inaonyesha nembo ya zamani ya SBS. Anyway, nadhani labla mzabuni hakuwa na chapa mpya ya lebo ya kuweka, labla watakuwa wamelirekebisha.
 
Wengine tulionyesha wasiwasi na umiliki wa hiyo Singida Big Stars na Singida Fountain Gates halafu hao wachaa mbuzi wakawa wanajifanya kama vile hawaoni wala hawasikii. Tutegemee Ihefu kuhamishiwa Singida (bila idhini ya wadau wakuu wa Mbarali) halafu SFG kutimuliwa kwa nguvu kutoka Singida kama siyo kufanyiwa fitna hadi ishuke daraja.
Wewe umethirika na nini kwenye hayo mambo? mbona hua mnajipa majukumu yasio kua yenu!
 
Wengine tulionyesha wasiwasi na umiliki wa hiyo Singida Big Stars na Singida Fountain Gates halafu hao wachaa mbuzi wakawa wanajifanya kama vile hawaoni wala hawasikii. Tutegemee Ihefu kuhamishiwa Singida (bila idhini ya wadau wakuu wa Mbarali) halafu SFG kutimuliwa kwa nguvu kutoka Singida kama siyo kufanyiwa fitna hadi ishuke daraja.
Usijipe umuhimu usokuwa nao, wewe una mchango gani katika hizo timu au shobo tu za kike dada?
 
Niliwahi sema msimu wa 2021/2022 kiwaonya Hawa sugar sugar, mtibwa sugar na Kagera sugar kuwa mmoja wao hatavuka msimu wa 2023/2024 bila kishuka daraja Kwa mienendo waliyokuwa nayo. Naona sasa Mtibwa ndio anamuaga Kagera. Lkn pia msimu uliopita nikasema hii singida haitovuka msimu 2025/2026 bila kushuka daraja. Soka la bongo sikuhizi ushindani mkubwa Sana ni basi tu bado timu ndogo zinahitaji jitihada kidogo kuuondoa ufalme wa hao ma giant wawili hapo juu
 
Kwahiyo Point 3 na goli moja alilonyimwa Kagera Sugar na waamuzi dhidi ya Yanga ndio ushindani wenyewe???
Ligi inakuwa ngumu kutokana na mmaamuzi tata sio vinginevyo.
 
Back
Top Bottom