wanaume tumebaki wachache sana, unadate na mwanamke kwa muda wa kutosha usijue kama ana watoto??Soma vizuri post yangu kwa utulivu kabisa,utaelewa,kumbuka hakuniambia kuwa ana watoto wengine watatu,nilipogundua hilo nikajisepesha tu,na kuamua kuanza upya,ndo yamenifika hayo,kosa langu mimi ni nini mkuu
wakati ameshikilia mtoto anataka kumnyonga wewe ulikuwa wapi??Jamani hapo nina kosa kweli???kama ndiyo kosa langu ni nini?😱🙁🙁🙁
[emoji23] [emoji23] [emoji23]Mkiambiwa msiikaribie zinaa mnajifanya wajuaji sasa hyo ni rasharasha tuuu mvua yenyewe bado kabsaaa
Wala huna haja ya kuwa na hofu Mkuu. Hakuna mwenye hatimiliki na wewe kati ya hao wawili. Huyo aliyeacha mtoto hajui kwamba analofanya ni kosa kubwa linaloweza kumletea matatizo kama utaamua kuchukua hatua. Kabla hujafika Polisi au ustawi Wa jamii wajulishe Viongozi wake Wa mtaa kuhusu kitendo alichofanya nao watawaita na mtajadiliana kwa busara na mtoto ataendelea kupata matunzo muhimu ya mama yake hadi atakapofikia umri wa kuweza kuwa mbali na mama yake. Lkn nakushauri kama hutamuoa mama yake jitahidi uchukue mtoto wako hata kabla ya miaka saba ya kisheria ili umtunze mwenyewe maana kutunza watoto watatu wa baba tofauti si mchezo. Kuhusu huyo Mbalabaigi hata mimi nadhani ni vema kama alivyoshauri mtu mmoja hapo juu, mwache aende; Maana kama ameshindwa kukaa na wewe kwa sababu tu umezaa na mwanamke mwingine basi hamtawezana mbeleni. Maisha ya ndoa yamejaa makosa na kujikwaa kwa pande zote, sasa mwanamke anayekushauri mumnyonge mtoto wakati mama mtoto anajua kamwacha hapo salama hafai hata kuwa hawala sembuse mke. Kuwa na amani brother maisha si meupe wakati wote.Soma vizuri post yangu kwa utulivu kabisa,utaelewa,kumbuka hakuniambia kuwa ana watoto wengine watatu,nilipogundua hilo nikajisepesha tu,na kuamua kuanza upya,ndo yamenifika hayo,kosa langu mimi ni nini mkuu
Mkuu ningeweza kumtembezea kichapo kitakatifu vizuri kabisa,lakini sikutakankabisa kujaza watu,co ingeniondolea heshima yangu kabisa hapa mtaani,that is why niliamua kutoa tu hizo pesawakati ameshikilia mtoto anataka kumnyonga wewe ulikuwa wapi??
au distance kati yake na wewe ulikuwa kilometa ngapi???
mpaka uanzee kutafuta pochi/waleti ilipo uanzee kuhesabu hela una mpaka ndio anamtupa mtoto na kuondoka huku unamwangalia......
wewe ni MPUUUUUUUZI.
Nashukuru kwa ushauri wako wa kunijenga mkuu!!Wala huna haja ya kuwa na hofu Mkuu. Hakuna mwenye hatimiliki na wewe kati ya hao wawili. Huyo aliyeacha mtoto hajui kwamba analofanya ni kosa kubwa linaloweza kumletea matatizo kama utaamua kuchukua hatua. Kabla hujafika Polisi au ustawi Wa jamii wajulishe Viongozi wake Wa mtaa kuhusu kitendo alichofanya nao watawaita na mtajadiliana kwa busara na mtoto ataendelea kupata matunzo muhimu ya mama yake hadi atakapofikia umri wa kuweza kuwa mbali na mama yake. Lkn nakushauri kama hutamuoa mama yake jitahidi uchukue mtoto wako hata kabla ya miaka saba ya kisheria ili umtunze mwenyewe maana kutunza watoto watatu wa baba tofauti si mchezo. Kuhusu huyo Mbalabaigi hata mimi nadhani ni vema kama alivyoshauri mtu mmoja hapo juu, mwache aende; Maana kama ameshindwa kukaa na wewe kwa sababu tu umezaa na mwanamke mwingine basi hamtawezana mbeleni. Maisha ya ndoa yamejaa makosa na kujikwaa kwa pande zote, sasa mwanamke anayekushauri mumnyonge mtoto wakati mama mtoto anajua kamwacha hapo salama hafai hata kuwa hawala sembuse mke. Kuwa na amani brother maisha si meupe wakati wote.
Mkuu huyu dada watoto wake aliwaacha Mkoani,na kwa namna alivyo huwezi kudhani kama ameshazaa!!wanaume tumebaki wachache sana, unadate na mwanamke kwa muda wa kutosha usijue kama ana watoto??
khaaa hii inatokeaje kwa mfano???
isha nini mkuu,nifafanulieConsequences of ur actions bro....sasa kusuffer ndo kunakuja....Kaza buti uyashinde
Kama ni kweli,Ndugu zangu wanaume wenzangu,kuna wakati tunafanya mambo na kuona ya kawaida sana,lakini ni hatari kuliko tunavyoweza kudhani.
Hapa nilipo siamini kilichonitokea,na sijui kesho yangu itakuwaje kwani vitisho nilivyopata vinaogopesha,wenzangu hapa mwaweza kunishauri.nisiwachoshe sana,iko hivi;
Nimekuwa kwenye mahusiano na msichana mmoja wa kiiraq mwenyeji wa huko Manyara,tulikuwa tunawasiliana vizuri kabisa kabla hatujaonana,kama miezi miwili hivi tukaonana Singida,it was very nice kwa kweli,tukapanga appointment nyingine msimu huu wa mapumziko,tukakubaliana aje Morogoro,(ndipo ninapoishi).
Pasipo hiana mtoto wa watu kafunga safari kutoka kwao katua Morogoro jana majira ya saa kumi hivi,nikamkaribisha nyumbani kwangu,tumefarijiana usiku kucha,pasipo na bugudha yoyote.
Kilichiharibia siku ni kwamba kuna mdada nilikuwa naye katika mahusiano,anakaa karibu na maeneo ninayoishi,nilikuwa naye katika mahusiano baada ya yeye kunishawishi sana,(tunafanya kazi ofisi moja) wakati tunaendelea na mahusiano aliniambia anataka mtoto wangu nikajua ananitania,lakini baadaye nikashangaa kweli ame-conceive,(bila makubaliano) kilichoniudhi zaidi nikagundua huyu dada ana watoto wengine wawili alikuwa amewaacha huko mkoani kwao,miezi kadhaa akawabeba watoto wake wote akakaa nao.
Sasa leo nikiwa na mgeni wangu,ambaye kiukweli ndo nimepanga kumuoa,mlango umegongwa,kufungua ni yule dada mwenye watoto wengi,hakuwa amewahi kuja karibia miezi 7 sasa,amekuja na mtoto ambaye kiukweli nimekuwa nikichangia malezi yake vema kabisa,amekuja akiwa amejaa hasira na kutaka kufanya fujo ndani kwangu,mwanaume nikalazimika kuwa mpole sana,ili kusolve mambo kimya kimya bila kujaza watu wengi,nimejitahidi sana kubembeleza mpaka kupiga magoti ili tu kulinda heshima yangu mtaani.
Akaamua kuondoka na kuniachia mtoto hapo ndani,na huyu mgeni wangu kageuka mbogo,mkali vibaya mno,akanambia anataka kuondoka,nimembembelez asiondoke kagoma,akanitaka nimpe nauli,nikampatia kama laki moja hivi akadai nimuongeze laki moja nyingine,otherwise anamnyonga mtoto,kwa muda huo alikuwa amembeba yeye,nikamuongeza laki moja akamtupa mtoto kitandani,akaondoka zake,lakini akaniambia "NAKWAMBIA UTANITAFUTA,LAZIMA NIKUTIE ADABU,LIKIKUPATA LA KUKUPATA KWETU KATESH,UTANIFUATA BILA KULAZIMISHWA" Maneno haya yameniogopesha sana japo sikuyajali sana.
Hapa nipo na mtoto wa miezi mitatu hivi,sielewi hata nifanye nini kwani mama yake hajarudi tena tamgu ameondoka.
kujaza watu kwa namna gani??Mkuu ningeweza kumtembezea kichapo kitakatifu vizuri kabisa,lakini sikutakankabisa kujaza watu,co ingeniondolea heshima yangu kabisa hapa mtaani,that is why niliamua kutoa tu hizo pesa