Kilichonikuta

Kilichonikuta


lol! Hahahaha nilikuwa sijui kama kuna kubembeleza kwa design 🙂 🙂



QUOTE=FP;6293837]ha haaaa, rafiki salama tu....
hofu kwako.
ndo umekuja kutubembeleza kidisaini hii?[/QUOTE]
 
Hahahah...usicheke sana bhanaa unajua kuna wakati mwingine inabidi tu tusiwe wapole

hahahahahahahahahahahhahaha maneno kuntu aisee nimecheka mpaka bosi wangu kanifuata hapa
 
Sasa bi dada unachoshangaa ni kipi, maana hata wewe ndani ya maelezo naona umebebwa kama ubwabwa wa shughuli.
Sioni mahali kuwa ulifunga ndoa, bali umesema ulizaa tu na huyu kifanyio dind.a.
Hivyo kaa hapo hapo bi dada lea wana wa wanawake wenzako.
ahahahhahahahha hii ntakukumbusha ukizeeka !
 
CHUKUA MAAMUZI YA BUSARA KWA FAIDA YA MWANAO NA WEWE MWENYEWE. FANYA YAFUATAYO
  • Angalia umri wako na malengo yako ya mbele
  • weka mikakati thabiti ya kumlea mwanao[coz mume wako haeleweki]
  • Pima afya yako na ujilinde
  • Muombe mungu sana[Kama una imani kwamba mungu yupo]
 
FP labda unitafsirie hii thread labda nimeanza kuwa kilaza jamani,ana mtoto hadi wa chuo?????? Na mlikutana chuo????? duu inaelekea bidada kapendana na fataki aiseee.
 
Last edited by a moderator:
Jaribu kumdadis huyo huyo aliyekwambia hayo kuhusu mama yao mmoja au.....,daaaah hiyo ni kali na magonjwa nje nje!
 
FP labda unitafsirie hii thread labda nimeanza kuwa kilaza jamani,ana mtoto hadi wa chuo?????? Na mlikutana chuo????? duu inaelekea bidada kapendana na fataki aiseee.
HA HAAA, tena fataki asilolijua rangi wala size, lol!
 
Nashukuru kwa ushauri wenu wapendwa lkn kwa wanaosema mpnz mzr si masoni kumbuka hakuna mahali pameandikwa kuwa hapa kuna mpnz ya kweli, hutokea tu ukabahatika kwan si mtaani,makazin hata wapi km uongo upo upo tu kikubwa ni kumuomba mungu. asanten
 
...Pole dada....kama amekuomba msamaha na umeridhia...endelea kumpenda...ila ufanye udadisi wa kina....isijekuwa kuna wengine wako kabatini (usikojua)...ndoa mlishafunga? au mwaishi tuuuuu....?
 
Habari za mida hii ndugu jamaa na marafiki wa jamii forum:
Naomba ushauri wenu wa kufanya baada ya kuguswa na haya yaliyonikumba,

Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 27 nilitokea kupendana na kijana mmoja wakati niko nasoma chuo,alinieleza ana mtoto mmoja yuko vijijini kwa wazazi wake na ndiko anakolelewa huko,nilimuuliza kuhusu mwanamke aliyezaa naye akanieleza kuwa hawana mahusiano yaani walishatengana muda mrefu sasa,kwa sababu nilimpenda sana sikuona mbaya niliona yule mtoto hana sababu ya kunifanya nisiendelee kumpenda huyo kijana kwa bahati nzuri nikabahatika kupata mtoto naye mmoja,baada ya kumaliza chuo akaniambia twende tukaishi kwao,sikuwa na namna ya kukataa ukizingatia nishamfahamisha kwetu na tuna mtoto.
huwezi amini niliyoyakuta huko,hapo nyumbani kama ilivyo kawaida ya jamii za kiafrika huwezi ishi wewe na mume wako tu lazima mtakuwa familiya kubwa basi nilikuta watoto kama wawili na mama mkwe. siku moja mtoto mkubwa katika kupiga story alijikuta akiniambia kwamba yeye ndiye mtoto wa kwanza wa huyu mwanaume niliyenaye na yuko chuo,wa pili yuko form 2,wa tatu yuko la 5 na wa nne yuko nasari.mh! kweli sikuamini niliumia sana mpaka yule mtoto alijuta kwa nini aliniambia, alifahamu kuwa nafahamu.Mume wangu alivyorudi nilimuuliza alikiri lakini alistuka nimejuaje nilimtuhumu kwa nini alinidanganya,aliomba msamaha sana sana.
Sasa naomba ushauri kutoka kwenu NIFANYEJE?

Hata kama ingekuwaje yakupasa kulivua pendo. Wewe bado umri wako unaruhusu kuanza maisha mengine utakayo yafurahia, la sivyo unatafuta ugonjwa wa moyo hapo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom