Kilichonikuta

Kilichonikuta

Wakanda2021

Member
Joined
Apr 27, 2013
Posts
70
Reaction score
8
Habari za mida hii ndugu jamaa na marafiki wa jamii forum:
Naomba ushauri wenu wa kufanya baada ya kuguswa na haya yaliyonikumba,

Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 27 nilitokea kupendana na kijana mmoja wakati niko nasoma chuo,alinieleza ana mtoto mmoja yuko vijijini kwa wazazi wake na ndiko anakolelewa huko,nilimuuliza kuhusu mwanamke aliyezaa naye akanieleza kuwa hawana mahusiano yaani walishatengana muda mrefu sasa,kwa sababu nilimpenda sana sikuona mbaya niliona yule mtoto hana sababu ya kunifanya nisiendelee kumpenda huyo kijana kwa bahati nzuri nikabahatika kupata mtoto naye mmoja,baada ya kumaliza chuo akaniambia twende tukaishi kwao,sikuwa na namna ya kukataa ukizingatia nishamfahamisha kwetu na tuna mtoto.
huwezi amini niliyoyakuta huko,hapo nyumbani kama ilivyo kawaida ya jamii za kiafrika huwezi ishi wewe na mume wako tu lazima mtakuwa familiya kubwa basi nilikuta watoto kama wawili na mama mkwe. siku moja mtoto mkubwa katika kupiga story alijikuta akiniambia kwamba yeye ndiye mtoto wa kwanza wa huyu mwanaume niliyenaye na yuko chuo,wa pili yuko form 2,wa tatu yuko la 5 na wa nne yuko nasari.mh! kweli sikuamini niliumia sana mpaka yule mtoto alijuta kwa nini aliniambia, alifahamu kuwa nafahamu.Mume wangu alivyorudi nilimuuliza alikiri lakini alistuka nimejuaje nilimtuhumu kwa nini alinidanganya,aliomba msamaha sana sana.
Sasa naomba ushauri kutoka kwenu NIFANYEJE?
 
wewe endelea nae tu,kwani watoto wana tatizo gani?kama angekuwa kaoa hapo sawa?sasa nikuulize kwa nini hamuishi wote?kwa nini wewe unaishi ukweni?
 
soon mtapata na wajukuu maana huyo wa chuo kesho kutwa tu analeta mwali.
ila ndo maisha watoto hawana shida..uhue saa zingine ukweli unauma labda huyo mwanaume alikuwa akitokea wadada walikuwa wanamkataa kwa ajili ya watoto akaona abadili style bahati nzuri au mbaya ikaangukia kwako..tulizana
ila nikuulize kwa nini kuishi kwa mwanaume bila ndoa? je kama ndo tabia yake yas kutifua tifua then anakutimua? utajibebaje?...unaona hao watoto wengine ukute na mama zao alishawai ishi nao kawatimua.tafakari!
 
tatizo la wadada wa siku hizi pia kushadadia mibaba kisa ina gari na nyumba hapo chacha,huna jinsi mamie zigo lako hilo jenga mji,ila hao watoto wanne ni wa mama mmoja?
 
Ina maana hao watoto kila mmoja ana mama yake? Duuh..! Huyo Kaka Chiboko..!
 
Akhaaaa bibi katoto kamoja tu, chapa lapa!!!!!! Ila hujasema kianaubaga JE WATOTO WOTE MAMA YAO MMOJA AU KILA MTU NA MAZA WAKE??????

Kama mama yao mmoja unaweza kubaki, coz sometimes life dsnt go as we plan! Ila kama kila mtu na mamushka wake ujue huyo bwana mkorofi sanaa ndo maana wanawake hawadumu nae!
 
mimi nawachukia sana hawa viumbe basi tu (wanaaume)ndo maana najikalia zngu peke angu
 
We kaa dada yangu ulee familia.
Hapa nilipo nafukuzia kabinti kamoja, namimi nimekazuga kuwa sina mtoto ila ninae mmoja, maana nahisi nikimweleza ukweli ndege wangu atapaparuka nibaki na manyoya.
 
We kaa dada yangu ulee familia.
Hapa nilipo nafukuzia kabinti kamoja, namimi nimekazuga kuwa sina mtoto ila ninae mmoja, maana nahisi nikimweleza ukweli ndege wangu atapaparuka nibaki na manyoya.

kwanini usimwambie ukweli ili achague moja nyie ndo mnasababisha ongezeko la ndoa zinazovunjika kuwa nyingi,mweleze mtu ukweli ili afanye maamuzi kutoka moyoni sio kumfanya mtu zombie.
 
Habari za mida hii ndugu jamaa na marafiki wa jamii forum:
Naomba ushauri wenu wa kufanya baada ya kuguswa na haya yaliyonikumba,

Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 27 nilitokea kupendana na kijana mmoja wakati niko nasoma chuo,alinieleza ana mtoto mmoja yuko vijijini kwa wazazi wake na ndiko anakolelewa huko,nilimuuliza kuhusu mwanamke aliyezaa naye akanieleza kuwa hawana mahusiano yaani walishatengana muda mrefu sasa,kwa sababu nilimpenda sana sikuona mbaya niliona yule mtoto hana sababu ya kunifanya nisiendelee kumpenda huyo kijana kwa bahati nzuri nikabahatika kupata mtoto naye mmoja,baada ya kumaliza chuo akaniambia twende tukaishi kwao,sikuwa na namna ya kukataa ukizingatia nishamfahamisha kwetu na tuna mtoto.
huwezi amini niliyoyakuta huko,hapo nyumbani kama ilivyo kawaida ya jamii za kiafrika huwezi ishi wewe na mume wako tu lazima mtakuwa familiya kubwa basi nilikuta watoto kama wawili na mama mkwe. siku moja mtoto mkubwa katika kupiga story alijikuta akiniambia kwamba yeye ndiye mtoto wa kwanza wa huyu mwanaume niliyenaye na yuko chuo,wa pili yuko form 2,wa tatu yuko la 5 na wa nne yuko nasari.mh! kweli sikuamini niliumia sana mpaka yule mtoto alijuta kwa nini aliniambia, alifahamu kuwa nafahamu.Mume wangu alivyorudi nilimuuliza alikiri lakini alistuka nimejuaje nilimtuhumu kwa nini alinidanganya,aliomba msamaha sana sana.
Sasa naomba ushauri kutoka kwenu NIFANYEJE?
Nafikiri umeshajua tabia ya mumeo kwa undani na mahusiano yake na wanawake. Kama watoto hao 4 amezaa na wanawake tofauti basi kwa haraka haraka naweza kusema huyo mpenzi wako HUENDA ana sifa hizi
  • Yuko tayari kuzaa na yeyote yule aliyempenda bila kufikiria future yake na ya aliyezaa naye
  • Hayuko siriaz kwenye relation
  • Anapenda watoto na ndiyo maana anazaa sana
  • Hauyuko makini na ndiyo maana anawapa mimba wasichana
  • Ni muongo
  • nk
Lakini kama alizaa na mwanamke mmoja, basi huenda waliachana kwa sababu ambazo ni tofauti na hizo. Hivyo chunguza kwanza kama watoto hao ni wa mwanamke mmoja. Baada ya kupata ukweli, waweza kufanya maamuzi kwa sababu, mjukuu wangu, dunia ni yako na chaguo ni lako pia!
 
What's done can't be undone, hiyo ndio family yako sasa kazi kwako kuilea kama mnapendana.
 
ningekuwa mimi ningejiondokea zangu mapeema kabla ya mtoto wa sita kuja!
 
Sasa bi dada unachoshangaa ni kipi, maana hata wewe ndani ya maelezo naona umebebwa kama ubwabwa wa shughuli.
Sioni mahali kuwa ulifunga ndoa, bali umesema ulizaa tu na huyu kifanyio dind.a.
Hivyo kaa hapo hapo bi dada lea wana wa wanawake wenzako.
 
...tatizo lako mleta mada umesahau kabisaa zile chipsi kuku, simu, mitoko, vitopu, skuna na pesa ya matumizi alivyowekeza huyo kidume mpaka ukajisikia unampenda. ACHENI USAHAULIFU ENYI VIUMBE.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom