Kilichomuua ‘mtoto wa boksi’ chabainika; wahusika kunyongwa!

kuna mwingne leo kamfunga mtoto mchanga wa siku moja tena wa kumzaa mwenyewe plasta mdomoni na puani,dah mimi moyo unashtuka kila nikisikia habari za watoto nachanganyikiwa,i love kids hawaelewi chochote then wanauwawa na mateso kama hayo,mmm inauma,

Mkuu, hukutoa taarifa Maendeleo ya Jamii au dawati la jinsia? Huyo mshenzy naye anastahili adhabu sawasawa na matendo yake.
 
Kuna kitu kinanitatiza kila wkt. Hivi mtu anaweza kunyongwa bila kufa? Maana huwa nasikia adhabu ya kunyongwa mpaka kufa kila mara

Hapo ni masuala ya sheria mkuu, ni sawa na wale wanaotekeleza ile ya kupigwa mawe hadi kufa. Lazima kuna sababu iliyopelekea kuweka hiyo ''hadi kufa''
 
Kwa wale mnaotaka picha, hawa ndio akina LUCIFER waliomuua mtoto Nasra:
View attachment 162315

Kulia: Lucifer no 2 (Mama mkubwa wa marehemu, Mariamu Said)
Katikati: Lucifer no 1 (Lucifer Mkuu na Baba mzazi wa marehemu, Rashid Mvungi)
Kulia: Lucifer no 3 (Mume wa Lucifer no 2, Mtonga Omar)

Hii ndio timu (Lucifer 1-3) ya kishetani iliyoshiriki kuondoa uhai wa mtoto Nasra. Walaaniwe wote pamoja na shetani wao mkuu wanayemtumikia.

Ukiwaona kwa harakaharaka utadhani watu, kumbe mashetani wakubwa waliokubuhu. Heri ya mchawi kuliko hawa watumishi wa shetani.

MASHETANI wakubwa aisee,,afu baba mtu mtu kafanana nae kweli mwanae.

Inna lillah WainnaliRaajiun,,,I know you are in a better place,I know nasra you are smilling now in heaven. M/Mungu akuweke Salama.
 
walilitumia box kama baby walker, hawakuwa na fedha za kununua za dukani ambazo huuzwa ghali na hazidumu.

Mkuu sio lazima uchangie kwenye Jambo seriously kama hili maana hata -------- huonekana ana hekima akikaa kimya.
 
kumbe TZ sheria ya kunyongwa mpaka kufa ipo? km ndiyo hao waliohusika wanyongwe wakifariki miili yao icharangwecharangwe vipande vidogovidogo alafu viwekwe kwnye box theni vifukiwe ..ahsanteni nilikuwa sijui km sheria ya kunyongwa ipo hapa nchini kwetu

Sheria iko hiyo sema marais wanakwepa kutia Sign ili mtuhumiwa anyongwe,nasikia aliyeSign ni nyerere tuu hawa waliomfuatia hawajafanya hivyo so,wanakula mvua za maisha.
 
Niko pamoja na wote wanaopinga ukatili dhidi ya Binadamu especially innocent children,Inshala huyu mtoto Mungu atampokea na laana zote zitawashukia wahusika wa tukio ili.
Hata hivyo ukija kwenye upande wa sheria kesi hii ina utata mwingi sana na it may end up being Manslaughter,kwanza hao wakatili wamemuweka kwenye boksi na mateso yote kwa miaka minne hakufa,leo kachukuliwa na kupelekwa kunako huduma nzuri na tiba kafariki,je hao wazazi hawawezi kuwageuzia kibao waliomchukua kuwa ndio waliochangia kifo chake?hakuna murder ya causation,na ni ngumu sana ku-prove kuwa wakati wanamchukua alikuwa na pumu au hiyo pumu ili develop akiwa mikononi mwa rescuers,tuwe na analytical thinking.

Sheria bhana, ajabu sana.
Nadhani watu kuwa "critical and analytical thinkers" ni vizuri lakini hizo hoja hapo zinamaanisha kumtuhumu mtu na kumtia hatiani ni kazi kubwa sana. Ninavyoona sheria itahoji hata watoto wanaobakwa pengine walipochukuliwa kwenda hospitali kwa vipimo ndiyo wakabakwa mikononi mwa waokozi. Ajabu kabisa.

R.I.P mtoto Nasra, pengine umetendewa hivyo ili kunusuru watoto wenzio uliowaacha nyuma. Ninachofurahi hakuna atakayeishi duniani zaidi ya siku anayotakiwa kufa.
 
nilisikia nikiwa ofisini kupitia redioni of course kichanga kimeokotwa maeneo ya kawe na kilishafariki looooh majitu megine mjinga sanaa ,linalia tamu tamu na viuno ilnakata halafu inatia motto plasta domoni pmbv sana
 
Kwa mtu yeyote aliye mwangalia mtoto Nasra kwa vyombo vya habari .Lazima ujiulize mara mbili mbili hivi kwanini sisi binadam tunatesana kiasi hiki af mtu ana mtesa mtoto mdogo
Jamani hii dunia tunaish na wanyama na sio binadam

Si ajabu hii mibazazi ilikuwa inaingia ktk nyumba za ibada.
 
Lakini wakati haya yanatoke Mungu si alikuwa naona.., tumwachie yeye ndio atawaadhibu.., haya mambo ya visasi ni ushetani..!
 
Hawa wapuuzi lazima wanyongwe
boksi.jpg
Gari ya Polisi iliyobeba watuhumiwa wa kesi ya mtoto wa boksi, Nasra Rashid ikiwasili Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Morogoro.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Morogoro, imelazimika kuahirisha kesi ya washtakiwa watatu dhidi ya unyanyasaji kwa mtoto marehemu Nasra (4) (mtoto wa boksi), baada ya kesi iliyokuwa ikiwakabili washtakiwa kubadilika na kuwa ya mauaji.

Akiahirisha kesi hiyo jana, Hakimu wa mahakama hiyo, Mary Moyo, alisema mahakama imeamua kuahirisha kesi hiyo hadi Juni 12, mwaka huu, kufuatia shtaka la kesi hiyo kubadilika na kuwa la mauaji baada ya mtoto huyo kufariki dunia.

Hakimu huyo alisema kuwa, washtakiwa hao wanatakiwa kupelekwa kituo kikuu cha polisi cha mkoa huo kwa ajili ya kuchukuliwa maelezo upya jana, ili yatumike wakati wa kusoma mashtaka hayo mapya keshokutwa wakati washtakiwa hao watakapopandishwa tena kizimbani.

Baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, washtakiwa walipandishwa kwenye teksi na kupelekwa kituo cha polisi kuhojiwa upya.

Hata hivyo, licha ya kuwapo askari polisi mahakamani hapo, wananchi walionekana kuwa na hasira kutokana na kuendelea kuguswa na tukio la utesaji mtoto huyo hadi kufariki, walitaka kuwashambulia watuhumiwa baada ya kulizingira gari walilopanda.

Washtakiwa wa kesi hiyo mama mkubwa wa mtoto huyo, Maria Saidi na baba mkubwa Mtonga Saidi, pamoja na baba mzazi, Mohamed Nasoro Mvungi, walifikishwa mahakamani hapo wakikabiliwa na mashtaka mawili; la kula njama na kufanya ukatili dhidi ya mtoto huyo.

Awali ilidaiwa kuwa, washtakiwa wa kwanza na wa pili walifanya ukatili wa kutisha dhidi ya marehemu tangu akiwa na umri wa miezi tisa kwa kumuweka kwenye boksi na kuibuliwa miaka minne baadaye na kuanza kufanyiwa matibabu na hatimaye kufariki dunia kwa ugonjwa wa pneumonia akiwa kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Juni Mosi, mwaka huu, wakati akipatiwa matibabu.

UMATI
Kesi hiyo ilifiikishwa mahakamani hapo kwa mara ya pili, ilijaza umati wa watu ukitaka kuwapiga washitakiwa, baada ya kufikishwa mahakamani hapo kutoka mahabusu. Hata hivyo, hali hiyo ilidhibitiwa na askari polisi.

Hakimu Moyo aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo ambayo ilipangwa kwa ajili ya kusikiliza maelezo ya awali, alikubaliana na ushauri uliotolewa na upande wa mashtaka ulioongozwa na waendesha mashtaka watatu wa Serikali, Sunday Hyera, S Edgar Bantulaki na Inspekta wa Polisi Zablon Msusi.

Hyera aliieleza Mahakama juu ya kifo cha mtoto Narsa na kwamba kutokana na hali hiyo, washtakiwa wote watatu, Mariam, Mtonga na Mvungi wanapaswa kuhojiwa upya na kufanyiwa uchunguzi upya na kuomba tarehe ya karibu ili kesi hiyo ifikishwe mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.

Hyera aliiomba mahakama kuruhusu washitakiwa hao kurudishwa Kituo Kikuu cha Polisi cha Mjini Morogoro kwa ajili ya mahojiano mapya, ombi ambalo llilikubaliwa na Hakimu Moyo.

Washtakiwa hao waliondolewa na Polisi kwa gari ndogo la binafsi, lililozungukwa na umati mkubwa wa watu, wengi wao wakiwa ni kina mama, ambao waliwazomea washtakiwa na walikimbiza gari hilo huku wakitoa maneno ya kuwashutumu kwa madai kuwa walihusika na kifo cha mtoto huyo kutokana na kumtesa.

Mshtakiwa wa kwanza na wa pili walikuwa mahabusu baada ya kushindwa kukidhi masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili wa kuaminiwa watakaokuwa wamesani dhamana ya maandishi ya Sh. milioni tano kila mmoja, huku mshtakiwa wa tatu akitimiza masharti na kuwa nje kwa dhamana.

Katika maelezo ya awali ya mashtaka, washtakiwa hao walidaiwa kula njama na kumfanyia ukatili mtoto huyo, ambaye mama yake mzazi alifariki dunia na jukumu la malezi kuachiwa mama yake mkubwa ambaye ni mshtakiwa wa kwanza.

Shitaka lingine ni kumfungia kwenye boksi na kunyima huduma za msingi kama mtoto ikiwemo chakula, tiba, mavazi na malazi, hali iliyosababisha apate magonjwa ya pneumonia, utapiamlo, maumivu ya kifua na kuvunjika kwa mifupa ya miguu na mikono.

CHANZO: NIPASHE
 
MUNGU ameruhusu huyo mtoto akapumzike sasa baada ya kazi ya kuwaumbua wenye roho mbaya kukamilika. Siku hizi malipo ni hapa hapa duniani ndio maana vitu vingi vibaya vinaonekana hadharani.



Umeongea ukweli sana! Mungu ni wa ajabu sana kitendo cha kumchukua huyu mtoto siku chache baada ya kuokolewa kutoka kwa hawa mbwa watesaje ni uthibitisho tosha wa uwepo wa Mungu!
Hivi huyu mtoto angefia mikononi mwa hawa mafisi wangechimba shimo kimyakimya na kumzika na wala uovu wao usijulikane!!!
Acha Mungu aitwe Mungu! Lala salama upo kwenye mikono salama hutateseka tena Nasra.
 
Kwa wale mnaotaka picha, hawa ndio akina LUCIFER waliomuua mtoto Nasra:
View attachment 162315

Kulia: Lucifer no 2 (Mama mkubwa wa marehemu, Mariamu Said)
Katikati: Lucifer no 1 (Lucifer Mkuu na Baba mzazi wa marehemu, Rashid Mvungi)
Kulia: Lucifer no 3 (Mume wa Lucifer no 2, Mtonga Omar)

Hii ndio timu (Lucifer 1-3) ya kishetani iliyoshiriki kuondoa uhai wa mtoto Nasra. Walaaniwe wote pamoja na shetani wao mkuu wanayemtumikia.

Ukiwaona kwa harakaharaka utadhani watu, kumbe mashetani wakubwa waliokubuhu. Heri ya mchawi kuliko hawa watumishi wa shetani.
Masikini mtoto kamfanana babake kweli. Hivi hata majirani kwa siku hizo zote hawakuuona ukatili huu, je ndugu wengine nao pia hawakuona . Ingefaaa na ndugu wahojiwe iweje wasijue kinachoendelea juu ya mtoto wa marehem. Sijui sana sheria ila hili tendo lazima liwatese maisha yao yote
 
nilisikia nikiwa ofisini kupitia redioni of course kichanga kimeokotwa maeneo ya kawe na kilishafariki looooh majitu megine mjinga sanaa ,linalia tamu tamu na viuno ilnakata halafu inatia motto plasta domoni pmbv sana

Mkuu, ni kweli mtoto huyo alifungwa bandage mdomoni hadi akafa na kuokotwa na wapita njia. Mijitu mingine bhana ina roho mbaya zaidi ya shetani.
 
Mtoto Nasra kauawa na nani? Aliyemweka kwenye boski au aliyemtoa na kumpeleka hospitali

Kaishi kwenye boski kwa miaka 4 akiwa hai, lakini kakaa kwenye hospitali zetu kwa wiki 2 tu akafariki. Wapi bora kwenye boksi au hospitali?

Hiki ni kielelezo tosha kuwa tanzania jama hakuna hospitali wala wataalam. Kwanini wafanyakazi wa hospitali wasiunganishwe mahabusu na wale waliomuweka Nasra kwenye boksi?

Ukiumwa bora ukae kwenye boksi utasogeza siku kuliko kwenda hospitali zetu
 
Andamana kesho na mabango kama unajiona uko sawa na hicho unachojaribu kiiaminisha jamii.
 
Mkuu...Mambo ya Mungu ni makubwa....Mtoto yule siku za MUNGU kumchukua zilikua zimeshafika...sema Mungu alivyo wa ajabua akaamua kabla Nasra hajafa lazima hao waliomtesa wayapitie mateso aliyopitia...Nasra akatoka ndani ya boksi..wakakamatwa then Nasra kaenda Mbinguni...ambao ataishi kwa furaha tele.....
 
Back
Top Bottom