Kilichomuua ‘mtoto wa boksi’ chabainika; wahusika kunyongwa!

mada ni ndefu, inawezekana kabisa kumbadilishia mazingira kwa ghafla kumesababisha hali ya afya yake kuzoofu kwa haraka!! ni sawa na mtu ambaye hajala chakula siku 5 then umpatie pilau kisha ashushie na maji hapo utakuwa umemmalizia.
 
Mtoto Nasra kauawa na nani? Aliyemweka kwenye boski au aliyemtoa na kumpeleka hospitali

Kaishi kwenye boski kwa miaka 4 akiwa hai, lakini kakaa kwenye hospitali zetu kwa wiki 2 tu akafariki. Wapi bora kwenye boksi au hospitali?

Hiki ni kielelezo tosha kuwa tanzania jama hakuna hospitali wala wataalam. Kwanini wafanyakazi wa hospitali wasiunganishwe mahabusu na wale waliomuweka Nasra kwenye boksi?

Ukiumwa bora ukae kwenye boksi utasogeza siku kuliko kwenda hospitali zetu
Mkuu Kavulata hoja yako inahitaji MJADALA MPANA!

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Hapo wanasheria wameandaa hoja dhaifu za kuwafanya washtakiwa washinde rufaa kama kesi ikifika ngazi hiyo!
 
Sheria ikae vema wote wahukumiwe waliomweka na waliomtoa na kumpeleka hospitalini na walikuwa wanamtibu wameamua kumdedisha ili ishu iwe hoti
 
Hapo wanasheria wameandaa hoja dhaifu za kuwafanya washtakiwa washinde rufaa kama kesi ikifika ngazi hiyo!

Mkuu, hakwepi mtu hapa---kama wakikwepa kitanzi lazima wafungwe kifungo cha maisha kwa makosa haya waliyoyatenda hawa MBWA!
 
Mtoto Nasra kauawa na nani? Aliyemweka kwenye boski au aliyemtoa na kumpeleka hospitali

Kaishi kwenye boski kwa miaka 4 akiwa hai, lakini kakaa kwenye hospitali zetu kwa wiki 2 tu akafariki. Wapi bora kwenye boksi au hospitali?

Hiki ni kielelezo tosha kuwa tanzania jama hakuna hospitali wala wataalam. Kwanini wafanyakazi wa hospitali wasiunganishwe mahabusu na wale waliomuweka Nasra kwenye boksi?

Ukiumwa bora ukae kwenye boksi utasogeza siku kuliko kwenda hospitali zetu

Mkuu, hili nalo linahitaji kuchunguzwa kwa umakini na ikibiki na serikali iunganishwe kwenye kesi hii kwa kushindwa kuboresha huduma za hospitali zilizopelekea mtoto kufa mara baada ya kufikishwa hospitali.
 
Mkuu, hakwepi mtu hapa---kama wakikwepa kitanzi lazima wafungwe kifungo cha maisha kwa makosa haya waliyoyatenda hawa MBWA!

Ili tu atiwe hatini kwa kuua kwa kukusudia lazima vitu viwili vianishwe bayana! NIA & TENDO
Kifo kitokeapo ambacho kinakuwa kimesababishwa na mtu kinafanya makosa mawili KUUA KWA KUKUSUDIA & KUUA BILA KUKUSUDIA, makosa haya yana adhabu mbili tofauti...adhabu ya kifo kwa kuua kwa kukusudia na adhabu ya kifungo cha maisha kwa kuua bila kukusudia.
Na tukumbuke KIFO ili kihusianishwe moja kwa moja na mshtakiwa ni lazima ushahidi ea dane na tukio husika na urandane....... hebu kidogo tufikiri tofauti....
." UZEMBE WA NESI KUTOKUMCHOMA SINDANO KWA WAKATI NDIO ULIOSABABISHA KIFO..."
Umeona hapo? Uchunguzi unaweza ukathibitisha vinginevyo na hivyo ndipo niliposema ni mwanya kwa watu hawa kutoka na kuachiwa huru
 
Mkuu, kwa mazingira ya kesi hii sioni hawa MBWA watapanyokea wapi kitanzi. Kuna kila dalili kwamba kifo cha mtoto kimetokana na mateso aliyopewa na hao wanahizaya watatu....hawaponi katika kesi hii...lazima waende na maji.
 
Kesi za kimahakama huwa haziendeshwi na kufikiwa maamuzi kwa hisia bali ushahidi usio na shaka ndani yake (ukiacha mazingira ya rushwa ambayo yameota mizizi ktk mahakama) ili mtu atiwe hatiani kwa kosa linalomkabili basi ni lazima tkio liunganishwe naye moja kwa moja! Mi sipingwi wao kufikishwa mahakamani, JE KOSA WALILOTENDA NDILO WANALOSHITAKIWA NALO.????
Kwa nini hao washitaki wanatoa mwanya ulio wazi?? ( may be ni mazingira ya rushwa) na sidhani kama baadhi ya wanasheria hawajaliona hilo, hisia tulizonazo zinaweza zikawa si sahihi halafu ikaleteleza washtakiwa kuachiwa huru! Je nani aliye na ushahidi usio na shaka kuwa wameua kwa kukusudia....?
 
hebu tuone sheria inasemaje, katika Sheria ya adhabu ya makosa ya jinai sura ya 195 ambayo inaelezea kuua bila kukusudia yaeleza
"(1) Any person who by an unlawful act or omission causes the death of another person is guilty of manslaughter. (2) An unlawful omission is an omission amounting to culpable negligence to discharge a duty tending to the preservation of life or health, whether the omission is or is not accompanied by an intention to cause death or bodily harm."

kwa kimatumbi inasema
"195.-(1) Mtu yeyote ambaye, kwa kitendo kisicho halali au kuacha
kutenda , anasababisha kifo cha mtu mwingine, ana hatia ya kuua bila
kukusudia.

(2) Kuacha kutenda isivyo halali ni kuacha kutenda ambako
kunasababisha kuzembea kutimiza wajibu unaohusika na hifadhi ya
maisha au afya, iwe kutofanya hivyo kumeandamana au hakukuandamana
na kusudi la kusababisha kifo au maumivu ya mwili. "
 
Ili tu atiwe hatini kwa kuua kwa kukusudia lazima vitu viwili vianishwe bayana! NIA & TENDO
Kifo kitokeapo ambacho kinakuwa kimesababishwa na mtu kinafanya makosa mawili KUUA KWA KUKUSUDIA & KUUA BILA KUKUSUDIA, makosa haya yana adhabu mbili tofauti...adhabu ya kifo kwa kuua kwa kukusudia na adhabu ya kifungo cha maisha kwa kuua bila kukusudia.
Na tukumbuke KIFO ili kihusianishwe moja kwa moja na mshtakiwa ni lazima ushahidi ea dane na tukio husika na urandane....... hebu kidogo tufikiri tofauti....
." UZEMBE WA NESI KUTOKUMCHOMA SINDANO KWA WAKATI NDIO ULIOSABABISHA KIFO..."
Umeona hapo? Uchunguzi unaweza ukathibitisha vinginevyo na hivyo ndipo niliposema ni mwanya kwa watu hawa kutoka na kuachiwa huru

Umesema sahihi kabisa. Unajua jazba na mihemko ya wananchi na wanaharakati ndio itapelekea kesi kuwa aquital, kwa sababu kosa wanaloshitakiwa nalo haliwahusu. Sheria inasema wazi kabisa kuua ili upatikane na sheria kuna ingridients zake.
1. Ill will au nia ovu.
2.Intention
3.Overt act
4.Actus reus
Sasa je hao waliomuweka kwenye box kama walitaka kumuua si wangempa sumu au vinginevyo,mbona walimuhifadhi? Je nia yao ya kuua hapo iko wapi?
Pili dhamira yenye utashi wa kuua haipo, kwa nini tusiseme wale madokta wamemuua makusudi ili kuwapa hawa walezi capital offence?
Je dhamira hiyo ilianza kutekelezwa kwa matendo halisi ya nia ya kuua, (overt act)?
Na mwisho hata mnapomuua mtu kwa kumpiga kwa ushirikiano, sheria inataka kumjua who made the last blow, which lead to the death? Kwa hapo last blow ni nesi au dokta? Maana kafia hospitali. Swala la pumu, ni maradhi yanayoweza kutibika tu, bora wangebaki na lile shitaka la mwanzo ingesaidia sana. Ni maoni tu.
 
PAMOJA NA WAUAJI WA MTOTO WA BOKSI NA MTESAJI WA MTOTO WA PASI KUFIKIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA, BADO UTESAJI UNAENDELEA
===================================================================================================
Dar es Salaam. Polisi wamefanikiwa kumnasa mwanamke anayedaiwa kumtesa kwa kipigo na kumng'ata mtoto Merina Mathayo (15), kumsababishia majeraha makubwa kichwani.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camillius Wambura akizungumza na gazeti hili jana alisema walifanikiwa kumnasa juzi, mwanamke huyo akiwa mafichoni Mbagala wilayani Temeke.

"Tumefanikiwa kumnasa juzi usiku akiwa mafichoni kwa jamaa zake, ni mwanasheria wa kujitegemea ana umri wa miaka 44, lakini inashangaza kwa hayo aliyoyatenda, anaendelea kuhojiwa wiki ijayo tunatarajia kumpandisha kizimbani," alisema Wambura.

Mtuhumiwa huyo ambaye ni mkazi wa Boko, anadaiwa kumtesa mtoto huyo ambaye ni mtumishi wake wa kazi za nyumbani, ambaye sasa amelazwa katika wodi ya dharura ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa(MOI) Muhimbili Dar es Salaam.

Wakati huo huo, Uongozi wa MOI umejizatiti kulinda usalama wa mtoto huyo, kwa kuzuia vyakula kutoka nje ya taasisi hiyo, ikiwa ni pamoja na kudhibiti watu kumtembelea na kuzungumza naye.

Mmoja wa wauguzi katika wodi aliyolazwa alieleza mtoto huyo kwa sasa anahudumiwa kila kitu na taasisi hiyo.

Ofisa Uhusiano wa MOI, Patric Mvungi , alieleza kwamba majibu ya kipimo kikubwa cha CT Scan alichofanyiwa yametoka, ambapo yameonyesha hakuna mfupa uliovunjika kichwani.

Mtoto Merina amelazwa Moi baada ya kupewa rufaa na Hospitali ya Mwananyamala alipokuwa amelazwa awali, kutokana na majeraha hayo ya kung'atwa meno na kupigwa na vitu mbalimbali.

Source: Mwananchi
 
Back
Top Bottom