Kilichojiri viwanja vya NMC na hatma ya Jimbo la Arusha Mjini

Yeye alisema kama Lema,sasa Chama ndio kimeamua kukata Rufaa hivyo ni lazima aheshimu maamuzi ya Chama la sivyo ajitoe kwenye Chama...sioni ukigeugeu wowote hapa maana hata yeye alisema anawasikiliza viongozi wake wa juu kuhusu Tamko watakalotoa.
 
hii hatua imechukuliwa zaidi kumuokoa LEMA na ndio kitu tulikuwa wengi tumependekeza kabla ya hapo.
Jaji aliyehukumu kesi hii uchafu wake unakwenda kuwekwa wazi na vichwa vingine lakini yeye mwenyewe
hajali kwa sababu alichokitaka ni fedha na ameshapata pesa zake kwahiyo kitakachotokea nyuma hakijali isipokuwa
hajui kuwa historia itamuhukumu. chadema nawapongeza kwa uamuzi wenu wa busara wa kukata rufaa kuipa tena chance
mahakama kulitazama upya swala hili na mumeonyesha kuwa siku zote mtachagua sheria badala ya vurugu. wengi
wetu tunataka uchaguzi but not without LEMA included. kwahiyo kuendelea na uchaguzi ingekuwa maana yake ni kumtupa
pembeni Lema kitu ambacho hatutaki kitokee. once again asanteni sana cdm kwa maamuzi yenu ya busara.
 
Dogo Janja anaenda kuapishwa jumanne. Kwa wale watakaopenda kumsindikiza dogo Janja msafara utaanzia ofisi za chama usa river
 
Tayari Lema ameshahutubia umati Mkubwa uliojitokeza hapa NMC,anayezungumza sasa ni mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe,na ameshatoa tamko kuwa CHADEMA inakata Rufaa kupinga hukumu iliyotolewa dhidi ya Mbunge Lema.

je RUFANI haiwez kuwapotezea muda CHADEMA?
 
Jamaa ni kigeu geu sana! Hata ile ya kujipeleka jela alijirudi mwenyewe akaomba atolewe!

Kwa uelewa wangu mdogo,Lema ni msikivu na anajali maamuzi ya chama na viongozi wa chama.Kwa hali hii ninaona nuru Tanzania kupitia chadema.Angekuwa mwingine angeshikilia misimamo binafsi,lakini sio Lema.Hongera sana na wengine tuige hivyo.
 
Ndugu naomba nijibiwe,hivi lema akikata rufaa anaendelea kuwa mbunge mpaka rufaa yake itakaposikilizwa?au hukumu ya mahakama kuu ya kumvua ubunge inaendelea huku akisubiri rufaa yake?
 
Nilikuwa namwambia rafiki yangu jana (yeye ni CCM damu damu!) kwamba CCM wanaegemea nguvu ya dola lakini kwa hakika hawana uwezo wa kubashiri wala kuzua madhara yatokanayo na matumizi ya nguvu hiyo ya dola kwa wananchi.

Wamemvua ubunge Lema, lakini kumbe ndio wamempa ticket ya kuzunguka nchi nzima kumwaga sumu.
lema ataweka kambi ndani ya Dar mpaka kieleweke.akitoka huko ni mtwara
 
CD takribani 7,800 zenye nyimbo za CDM zimeuzwa uwanjani pamoja na kadi za unachamawa wa CDM zipatazo 12,400 (SOLD OUT)
 
Kwa kauli hii, CDM haitachukua hii nchi kamwe, wengine wanaongea reconcilliation yeye anaongea kulipiza kisasi?


Reconciliation haimaanishi watu wasiwajibike kwa makosa waliyoyafanya, Kenya kulikuwa na reconcilliation na bado watu walifunguliwa na wanaendelea kufunguliwa mashtaka, Africa Kusini kulikuwa na reconcilliation na bado watu walishitakiwa. Unakipigia debe wewe ni impunity, kitu kinachopigwa vita na wapenda haki kote duniani.
 
Tayari Lema ameshahutubia umati Mkubwa uliojitokeza hapa NMC,anayezungumza sasa ni mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe,na ameshatoa tamko kuwa CHADEMA inakata Rufaa kupinga hukumu iliyotolewa dhidi ya Mbunge Lema.

MIMI NITAZIDI KUMWOMBA MUNGU ATUPE UJASIRI ZAIDI SISI WANA CDM ILI TUZIDI KUPAMBANA NA HAWA MAGAMBA.Lowasa,Chenge,Rostam,Mkapa,JK nk 2016 wote KISUTU wakajibu makosa yao.
 
Ndugu naomba nijibiwe,hivi lema akikata rufaa anaendelea kuwa mbunge mpaka rufaa yake itakaposikilizwa?au hukumu ya mahakama kuu ya kumvua ubunge inaendelea huku akisubiri rufaa yake?

Hukumu ya mahakama kuu ipo palepale mpaka mahakama ya rufaa itengue.
 
Ndugu naomba nijibiwe,hivi lema akikata rufaa anaendelea kuwa mbunge mpaka rufaa yake itakaposikilizwa?au hukumu ya mahakama kuu ya kumvua ubunge inaendelea huku akisubiri rufaa yake?
Hawezi kuwa mbunge wakati rufaa inasikilizwa,atakuwa mbunge iwapo tu hukumu yake itatupiliwa mbali...
 
Baba mwanaasha yupo njiani anaelekea kwa kanumba akitoka hapo aende Malawi anadai hotuba ya freeman lazima kaandikiwa na Obama ilivyo Kali na ya kusisimua
 
Back
Top Bottom