Kilichojiri uchukuaji wa fomu ya mgombea Urais kupitia UKAWA-Lowassa

Swadakta kamanda!
Jumatatu ya mafuriko,Lumumba ingizeni siku hii kwenye vitabu vyenu vya kumbukumbu
 
Asante saana Mkuu Molemo na wote. Tunakuaminia mkuu kwa live updates
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli au ni maneno tu jamana mbona nasikia lowasa hana wapenzi Dar ?ana watu wachache ?ila siamini kama anaweza kosa watu time will tell.
 
Lowassa gani yule aliyekuwa CCM na nyie mkamtusi sana? Au Lowassa mwingine? Dunia ina mambo sana hii!

Ushauri Wangu ndugu zangu wa Bavicha tujifunze kuweka akiba ya Maneno maana mwisho wa siku mnalazimika kula matapishi yenu!

Kwa mfano mlimpenda sana Dr Slaa na kumsifia sana kwa namna yeyote ile mlimtetea leo Hii ndio anayeongoza kutukanwa JF kuliko mtu yeyote same applies to EL mlimponda sana leo hii kawa lulu kwenu!

Wito Wangu Kwenu tujifunze kuweka akiba ya maneno!
 
Leo ngoja nigande chini ya mti nikifuatilia makamanda.

Itakuwa tishio kwa mustakabali wa magamba.
 
Lowassa gani yule aliyekuwa CCM na nyie mkamtusi sana? Au Lowassa mwingine? Dunia ina mambo sana hii!

Ushauri Wangu ndugu zangu wa Bavicha tujifunze kuweka akiba ya Maneno maana mwisho wa siku mnalazimika kula matapishi yenu!

Kwa mfano mlimpenda sana Dr Slaa na kumsifia sana kwa namna yeyote ile mlimtetea leo Hii ndio anayeongoza kutukanwa JF kuliko mtu yeyote same applies to EL mlimponda sana leo hii kawa lulu kwenu!

Wito Wangu Kwenu tujifunze kuweka akiba ya maneno!

Kwa hiyo?
 
Nipo Posta natokea masaki..naomba mnielekeze nakuja na dala dala nimeacha gari Leo nitatembea kwa miguu
 
Kila sehemu ni shamra shamra,nimekuta moja ya gari ya matangazo hapa karibu na vingunguti inatangaza,amsha amsha
 
Nendeni mkamsindikize!

WanaJF,

Ni asubuhi tulivu kabisa ya Jumatatu tarehe 10/8/2015.Ni siku ya kihistoria katika Taifa letu.Hii ni kwa sababu Kamanda mpambanaji na asiyechoka mzee wa Maamuzi magumu Edward Ngoyai Lowassa akiwa na mgombea mwenza Juma Duni Haji watachukua rasmi fomu za kugombea Urais kupitia UKAWA katika ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Timu ya wanahabari wa JF tayari iko hapa buguruni katika ofisi kuu za CUF ili kuwaletea kila kitakachojiri.Tunatarajia maanadamano haya makubwa yataanza saa 3 asubuhi hapa ofisi za CUF na yatapitia katika ofisi za NCCR Ilala na kisha baada ya kuchukua fomu maanadamano haya yatendelea mpaka kumalizikia ofisi za CHADEMA Kinondoni.

Tunatarajia Edward Lowassa kusindikizwa na waendesha baiskeli,bodaboda,maguta,bajaji,magari na pia tayari tuna taarifa za idadi kubwa ya wanafunzi wa vyuo vikuu DSM kushiriki maandamano hayo.Pia watakuwepo akina mama Ntilie (mama lishe),wamachinga na wale wote watakaoguswa kushiriki tukio hili la kihistoria.

Tunaweza kusema kabisa ITAKUWA HISTORIA aisbaki mtu nyumbani.

Unagana na timu yote ya M4C ya akina Molemo, Tumaini Makene, Chademakwanza, Standalone na wengineo wote kuwaletea Live bila chenga kuanzia mwanzo mpaka mwisho..

Karibuni
 
Back
Top Bottom