Kili Music Awards 2011

Kili Music Awards 2011

kweli hizi ni tuzo za bla blaa tu... yaani MPOKI ANAMSHINDA MRISHO MPOTO??? Haiingii akilini kabisa...
 
Wana JF,naomba mnijuze.matokeo yalikwisha toka na hapa lengo si kuyabadili.
MPOTO alituletea ujumbe kwa mjomba.
MPOKI akaja na shangazi,naye tukampokea.
*Je kwa wanajamii,(hapa nina maana woote bila kuzingatia uwezo wa kutuma sms za kur)a.ni nani kati ya hawa aliyeisemea jamii katika hali halisi ya sasa na ambaye kwa maoni ya wengi bila uwepo wa luninga ambaye alistahili tuzo hiyo?(au ujumbe kwa mjomba ulifika na hayo ndio majibu?)
 
Sio hvyo bob, kuchukua nyimbo bora ya hip hop haimaanishi ni msanii bora wa hip hop, ... kuwa msanii bora wa hip hop maanake ni over all perfomance ya msanii katika Hip hop.. hatumjaji msanii bora wa hip hop kwa nyimbo moja bora but kwa nyimbo nying ambazo ni Bora. Joh ana nyimbo nyingi na ktk hip hop kwa mwaka huu kajitahidi kutoa misumari ya maana so i gues alistahili.
 
Wana JF,naomba mnijuze.matokeo yalikwisha toka na hapa lengo si kuyabadili.
MPOTO alituletea ujumbe kwa mjomba.
MPOKI akaja na shangazi,naye tukampokea.
*Je kwa wanajamii,(hapa nina maana woote bila kuzingatia uwezo wa kutuma sms za kur)a.ni nani kati ya hawa aliyeisemea jamii katika hali halisi ya sasa na ambaye kwa maoni ya wengi bila uwepo wa luninga ambaye alistahili tuzo hiyo?(au ujumbe kwa mjomba ulifika na hayo ndio majibu?)

No comment cause hapa si mahala pake jamani....peleka kwenye jukwaa husika.......
 
utakuaje overall winner wa category ambayo huja win hata wimbo mmoja? Its common sense and does not make sense. Tukubali tu hiki cha mwaka huu ni kituko, Ni sawa na kusema wimbo wa mpoki unaweza kushinda wa mpoto. Huu ni upumbavu yaani a joker vs a professional hivi huo wimbo wa shangazi unaimba nini? umeimbwa lini na umepigiwa kura na nani? they are joking, hivi inawezekanaje wimbo wa mama ntilie usishinde popote? wimbo unaoeleza hali halisi ya mtanzania, hali ambayo nauhakiki 100% of washiriki wa mashindano hadi waangaliaje wame experience. nachojiuliza hivi hilo deal la George kavishe na wakina ruge wasingeweza kufanya bila kutudanganyia hiyo show? hebu angalia uchafu walioimba washindi wa mwaka jana? what was that? ndio maana hakujawa na breakthrough miaka yote hiyo 12 walicho succeed ni kupeana 10% na wakina Minja na hao kivishe na wachaga wengine kupata mishiko wakitoka hapo miaka mitano ijayo hakuna kinachoonekana. KMA haijawa na mafanikio yoyote despite the big budget inayoishia kwenye matumbo ya waandaaji very sad kweli Tanzania shamba la bibi.
 
No comment cause hapa si mahala pake jamani....peleka kwenye jukwaa husika.......

Thanks,lakini UJUMBE WA MPOTO KWA MJOMBA UNASTAHILI HAPA,tafakari kwa kina. usomapo topic anza kujenga taswira yake.nakushukuru na tuendelee kuwa pamoja.
 
kila mtu ana mshindi wake.
si walio bora ndio washindao mara zote.
 
1. Wimbo Bora wa Asili

– Shangazi – Mpoki Ft. Cassim

2. Wimbo Bora wa Bendi

– Shika Ushikapo – Mapacha Wa3 Ft. Mzee Yusuph

3. Wimbo Bora wa Taarab

– My Valentine – Jahazi

4. Wimbo Bora wa R&B

– Nikikupata – Ben Paul

5. Wimbo Bora wa Hip-Hop

– Ukisikia Paah! – JCB Ft. Fid Q, Jay Mo & Chidi Benz

6. Wimbo Bora wa Afro-Pop

– Tamaa Mbaya – 20%

7. Wimbo Bora wa Zouk/Rhoumba

– Nabembelezwa – Barnaba

8. Wimbo Bora wa Reggae

– Ujio Mpya – Hard Mad Ft. Enika & BNV

9. Wimbo Bora wa Ragga Dancehall

– Action – Cpwaa Ft. Ms. Triniti, Dully Sykes & Ngwear

10. Wimbo Bora wa Kushirikiana

– Ukisikia Paah! – JCB Ft. Fid Q, Jay Mo & Chidi Benz

11. Wimbo Bora wa Afrika Mashariki

– Nitafanya – Kidum Ft. Lady Jay Dee

12. Video Bora ya Mwaka ya Muziki

– Action – Cpwaa Ft. Ms. Triniti, Dully Sykes & Ngwear

13. Mtunzi Bora wa Nyimbo

– 20%

14. Mtayarishaji Bora wa Nyimbo

– Lamar

15. Rapa Bora wa Mwaka(Bendi)

-Khalid Chokoraa

16. Msanii Bora wa Hip-Hop

– Joh Makini

17. Msanii Bora Anayechipukia

– Linah

18. Hall of Fame

(a) Taasisi – Tanzania Broadcasting Cooperation(TBC)/Radio Tanzania Dar -Es-Salaam(RTD)
(b) Binafsi – Said Mabela

19. Mwimbaji Bora wa Kike

– Linah

20. Mwimbaji Bora wa Kiume

-20%

21. Wimbo Bora wa Mwaka

– Tamaa Mbaya – 20%

22. Msanii Bora wa Muziki wa Kike

- Lady Jay Dee

23. Msanii Bora wa Muziki wa Kiume

- 20%
 
20 Percent awabwaga masharobaro

Sunday, 27 March 2011 21:28

20zawadi.jpg


Msanii wa muziki wa kizazi kipya, 20 Percent

Michael Momburi

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, 20 Percent jina lake halisi Abbas Kinzasa juzi alifanikiwa kutwaa tuzo tano kati ya sita kwenye kinyang'anyiro cha tuzo za muziki Tanzania za Kili 2011.

Katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo iliyofana kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam, msanii huyo alinyakua tuzo tano huku akiwafunika nyota wengine kama Diamond na Ali Kiba ambao walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo mwaka huu.

Msanii huyo ambaye mashabiki walikuwa wakimshangilia kila alipotajwa ingawa aliwakilishwa na prodyuza wake, Man Walter ukumbini hapo, alishinda tuzo ya msanii bora wa kiume, mtunzi bora wa nyimbo, mwimbaji bora wa kiume.

Wimbo wake wa ‘Tamaa Mbaya’ ulitwaa tuzo ya wimbo bora wa mwaka na wimbo bora wa Afro Pop huku Banana Zorro akisema; “Nilijua 20 angewafunika, nyimbo zake zinagusa maisha halisi ya Mtanzania wa kawaida na hata mwaka usishangae akaendelea kutawala.”

Wasanii wengine waliofuatia kwa kujikusanyia tuzo mbili kila mmoja ni Linah, JCB na CPwaa. Linah alitwaa tuzo ya msanii mpya anayechipukia na mwimbaji bora wa kike wakati CPwaa na singo yake ya ‘Action’ alinyakua tuzo ya wimbo bora wa Ragga na video bora ya mwaka.

Wimbo wa ‘Ukisikia Paah’ wa JCB ambao amewashirikisha Fid Q, Chid Benz na Jaymoe uliwapa tuzo ya wimbo bora wa hip hop pamoja na wimbo bora wa kushirikishwa.

Wasanii wengine waliotwaa tuzo ni Lady Jaydee, ambaye aliibuka msanii bora wa kike, ‘My Valentine’ wa Jahazi ndio wimbo bora wa Taarab, wimbo bora wa Kiswahili wa bendi ni ‘Shika Ushikapo’ wa Mapacha Watatu huku ‘Nikikupata’ wa Belle 9 ukitajwa wimbo bora wa R&B.

‘Ujio Mpya’ wa Hardmad akimshirikisha Enika ndio wimbo bora wa Reggae, rapa bora wa bendi kwa mwaka ni Khalid Chuma 'Chokoraa', msanii bora wa Hiphop ni Joh Makini huku ‘Nitafanya’ ya Kidumu na Jaydee ikibuka nyimbo bora ya Afrika Mashariki na Lamar prodyuza bora.

Wimbo bora wa asili wa Tanzania ni ‘Shangazi’ wa Mpoki aliofanya na Cassim wakati ‘Nabembelezwa’ ya Barnaba ndio wimbo bora wa Zouk.

Mashabiki walionekana kufurahia maandalizi pamoja na programu ya shoo hiyo ingawa waliguna kwa nguvu alipotangazwa mshindi wa prodyuza bora wa mwaka ambaye ni Lamar na mshindi wa wimbo bora wa asili, Sylvery Mujuni au Mpoki, mchekeshaji wa Orijino Komedi.

Wengi wao waliwataja msanii Mrisho Mpoto au Mjomba na prodyuza Man Walter kuwa walistahili kwenye badala yao.

Msanii Diamond ambaye aliambulia patupu katika tuzo hizo licha ya kupewa nafasi kubwa alisema, “Nimeridhika na mchuano ulikuwa mkali walioshinda walistahili.”

SOURCE: 20Percent awabwaga masharobaro
 
The guy is pretty.... one of the very best singers in Tanzania!!! He has accurately filled the vacuum ambayo waimbaaji wengine wa kizazi kipya wameshindwa kui-fil... i.e., songs other than love songs.
 
nimefurahi sana kwa huyu jamaa kushinda maana anaimba nyimbo zinazogusa maisha ya kila mtanzania na pia mie huwa namfananisha na bob marley ambaye aliimba nyimbo za maana sana na pia hakuwai kuimba nyimbo za mapenzi ndo namshauri apambane aweze kujenga misingi ya nyimbo zake katika maisha ya watanzania na sio kuzungumza mapenzi kila wakati
 
Kila lakher 20 percent.kaza zaid.wapo wengne chipukiz wanakuja,usibweteke
 
Nyimbo zenu vijana wa sasa hazidumu sana ingawa mnatajirika haraka sana. Akina Juma Nature, Profesa J, Selemani Msindi, AY, Crazy GK, FA, TID, wako wapi?
 
Back
Top Bottom