Kila ninaposaidia mtu, narudishiwa jeuri

Kila ninaposaidia mtu, narudishiwa jeuri

Tenda wema nenda zako, usingoje kurudishiwa - Sababu ukisaidia ili usaidiwe wewe sio mtoa msaada bali mwekezaji....

Blessed is he who expects nothing, for he shall never be disappointed.
 
Kila ninayeshikamana nae kwa shida na raha ikifika zamu yangu naambulia kupotezewa au jeuri, au mie ndo nina shida guys?

Siwekagi matarajio kabisa, najitoa kwa kidogo nilicho nacho, kwa muda nilionao, kwa utu na ama kwa nguvu nilizonazo, lakini kama ujuavyo maisha kuna nyakati yananifika inakuwa my turn, nikiomba kwa watu wale naambulia jeuri, block ama ukimya. Sio kwamba hawajawahi, wamewahi lakini mara nyingi zaidi naambulia hivyo.

Nina wenzangu tumekulia maisha ya shida, tumehangaika kwenye nyumba za watu hatuna wazazi wala pa kwenda, lakini wao kutangulia kukipata wanageuka jeuri miungu watu sababu wapo juu.

Mfano mwingine akiwa katika shida anaumwa hajuia ale nini, analala njaa na mimba juu kaachwa, mie nikipata hela moyo wa upendo unanijaa naenda kumnunulia mazaga sokoni nampelekea ili apate lishe nzuri hata kwa week, likapita ikafika my turn bila kutarajia nikalazwa hospitali sijiwezi, kumwambia nna shida ya kitu kidogo niliambulia blue tick na Block, ila wengine nikiwauliza wanadai wanawasiliana nae😊

Kuna mwingine nae akizipata zake, akiwa na shida namsaidia kwa moyo, ila nikikwama hanijibu kabisa.

Nilitarajia upendo na mshikamano miongoni but hamna kitu. Hata wale ninaowajali katika dharura zao ikifika dharura yangu naambulia kiburi.

Most of the time mikwamo yangu nashikwa mkono na watu nisioshea nao ukaribu Wala nisiowadhania.
Imefika wakati Sasa nahesabu sina baba mzazi, sina mama mzazi(washaenda zao)
Na ndugu Sina😊

Au mimi ndio nakosea?
Sasa watu wasioweza kukusaidia wewe utawachukuliaje?

Utawasaidia kwa kujua kuwa unawasaidia tu, hawana uwezo wa kukurudishia?

Au utawapoyezea, kwa sababu hawana uwezo wa kukurudishia?

Waswahili walisema "Tenda wema uende zako, usingoje shukurani".

Na kama unataka kulipwa, usizaidie watu, fanya biashara.

Kuna walimwengu wengine hawana maana.

Ushawahi kumpa ntu mkopo, akakuahidi atakulipa, halafu kabla hajakulipa akataka kukukopa tena?

Yani huyo ni bora anayeku block unajua huyu nishamalizana naye, kuna mtu unampa mkopo, halafu kabla hajakulipa anakuomba mkopo tena 😂😂😂
 
Ndio binadam hao mama mkwe.
Kikubwa tu, tenda wema usingoje shukrani.

Kwa mafunzo ya imani yangu ya kidini..
Hakuna wema ama ubaya ambao haulipwi malipo haya duniani ni mafogob saana ukicompare na ya akhera..
Wema wako utaukuta huko siku ya kiyama.

Ukitenda wema umejitendea mwenyewe(utaukuta siku ya kiyama, na utalipwa)
Ukitenda mabaya, umejitendea mwenyewe(utayakuta na utalipwa siku ya kiyama)

Ukinitendea mimi wema nami nikakutendea wema haimaanishi hautalipwa kesho.
Wema wako utalipwa na wangu utalipwa.
Ukinitendea wema nikalipa baya, wema wako utalipwa na ubaya wangu nitalipwa kesho kiyama.

ISHI HUMO mama mkwe, dunia tunapita tu KIPENZI ♥ ❤ 💖
 
Dunia inafikirisha aisee..
Mtu ananingia kwenye matatizo anadaiwa fine police ili atoke anaomba unisaidie umtoe unamtoa
Unapotezea hutarajii chochote
Kesho yanakukuta wewe unakumbuka nna mtu wangu wa karibu Fulani ngoja nimtafute atanitoa nami kwenye hili tatizo labda.
Unashangaa mtu anakufokea bwana wee usinisumbue

Au unamkopa tukipata shida unamkumbusha Kila siku wimbo ni uleule "nimekwambia ntakupa Hela yako,si nimekwambia ntakupa
Na hakupi😊

Sitaacha kutenda wema Tena namsaidia sana wahitaji na watoto.ila watu kama hawa nawaweka alama ya ❌
 
Inategemea huwa unawaomba msaada kwa njia zipi njia zingine zinakera, au Unatatizo linaloitwa Histrionic , ni hali ya kupenda umakini wa watu uwe kwako, watu wakiwa bize uwepo wao ukakosekana kwako unaanza kuhisi umetengwa, hupendwi au wanakudharau, unaanza kuwa mtu wa kulalamika hadi watu wanakuchukia.

Usipoteze muda mwingi kuwawaza, msaada wako nuia kama sadaka na wala usidhani ni sababu ya wewe kulipwa mema na unaowasaidia alafu jiweke bize na shughuli yoyote ya kukuingizia kipato au kuongeza ujuzi utapata circle mpya , kwa sasa hao watu unaohisi hawakupendi au wanakudharau haipo hivyo isipokua kwa sasa watu hao haupo kwenye circle yao kwahiyo umuhimu wako unapungua kwao.

Ndo nature ilivyo huwezi kupambana nayo.
 
Unatatizo linaloitwa Histrionic , ni hali ya kupenda umakini wa watu uwe kwako, watu wakiwa bize uwepo wao ukakosekana kwako unaanza kuhisi umetengwa, hupendwi au wanakudharau.

Usipoteze muda mwingi kuwawaza , jiweke bize na shughuli yoyote ya kukuingizia kipato au kuongeza ujuzi utapata circle mpya , kwa sasa hao watu unaohisi hawakupendi au wanakudharau haipo hivyo isipokua kwa sasa watu hao haupo kwenye circle yao kwahiyo umuhimu wako unapungua kwao.

Ndo nature ilivyo huwezi kupambana nayo.
Hapa umeongea ukweli mtupu.
 
Ndio binadam hao mama mkwe.
Kikubwa tu, tenda wema usingoje shukrani.

Kwa mafunzo ya imani yangu ya kidini..
Hakuna wema ama ubaya ambao haulipwi malipo haya duniani ni mafogob saana ukicompare na ya akhera..
Wema wako utaukuta huko siku ya kiyama.

Ukitenda wema umejitendea mwenyewe(utaukuta siku ya kiyama, na utalipwa)
Ukitenda mabaya, umejitendea mwenyewe(utayakuta na utalipwa siku ya kiyama)

Ukinitendea mimi wema nami nikakutendea wema haimaanishi hautalipwa kesho.
Wema wako utalipwa na wangu utalipwa.
Ukinitendea wema nikalipa baya, wema wako utalipwa na ubaya wangu nitalipwa kesho kiyama.

ISHI HUMO mama mkwe, dunia tunapita tu KIPENZI ♥ ❤ 💖
Asante baba mkwe
Mioyo yetu binadamu haifanani
 
Waswahili walisema "Tenda wema uende zako, usingoje shukurani".
Hapa ndipo watanzania wengi tunapokoae. Mbongo akikufanyia kitu kizuri bila kumsifia anakasirika, anataka walau asikie neno la shukrani kutoka kwako ndipo roho yake itulie.
 
Inategemea huwa unawaomba msaada kwa njia zipi njia zingine zinakera, au Unatatizo linaloitwa Histrionic , ni hali ya kupenda umakini wa watu uwe kwako, watu wakiwa bize uwepo wao ukakosekana kwako unaanza kuhisi umetengwa, hupendwi au wanakudharau, unaanza kuwa mtu wa kulalamika hadi watu wanakuchukia.

Usipoteze muda mwingi kuwawaza, msaada wako nuia kama sadaka na wala usidhani ni sababu ya wewe kulipwa mema na unaowasaidia alafu jiweke bize na shughuli yoyote ya kukuingizia kipato au kuongeza ujuzi utapata circle mpya , kwa sasa hao watu unaohisi hawakupendi au wanakudharau haipo hivyo isipokua kwa sasa watu hao haupo kwenye circle yao kwahiyo umuhimu wako unapungua kwao.

Ndo nature ilivyo huwezi kupambana nayo.
Sipo kwenye circle yao.lakini kesho nkifanikiwa utashangaa nipo kwenye mawazo yao.how comes?
 
Dunia inafikirisha aisee..
Mtu ananingia kwenye matatizo anadaiwa fine police ili atoke anaomba unisaidie umtoe unamtoa
Unapotezea hutarajii chochote
Kesho yanakukuta wewe unakumbuka nna mtu wangu wa karibu Fulani ngoja nimtafute atanitoa nami kwenye hili tatizo labda.
Unashangaa mtu anakufokea bwana wee usinisumbue

Au unamkopa tukipata shida unamkumbusha Kila siku wimbo ni uleule "nimekwambia ntakupa Hela yako,si nimekwambia ntakupa
Na hakupi😊

Sitaacha kutenda wema Tena namsaidia sana wahitaji na watoto.ila watu kama hawa nawaweka alama ya ❌
Mimi nilihamia nchi ambayo sina mjomba sina shangazi najitegemea mwenyewe kwa kiasi kikubwa.

Nilishayaona yote haya nikasema hata utamaduni wa kutegemeana tegemeana sitaki.

Ndiyo maana wenzetu wamejiwekea mifumo ya kuwa na insurance, lawyer, savings etc.

Of course tutahitaji watu wa karibu tu, that is the human condition. Ukianguka ndani hela haikubebi.

Lakini mimi najaribu sana kupunguza kutegemea watu najiwekea mifumo. Na watu ninaoweza kuwategemea labda ni wa my immediate family tu, my nucleus family, ambao najua hawawezi kuniangusha.

Waingereza wana msemo "No good deed goes unpunished".

Ukielewa hilo kabla hujatoa msaada, unatoa msaada si kwa kujua kuwa utarudishiwa, unatoa msaada kwa kujua kuwa ule msaada utakuja na punishment.

Siku usipoweza kusaidia utaitwa maneno "Huyu anaringa siku hizi" . As if wewe kazi yako ni kutoa misaada tu kila siku na huyo anayedai ana haki ya kupata misaada tu.

Kama huwezi timbwili hili ukiombwa sema tu nimemaliza bajeti yangu ya kusaidia.
 
Hapa ndipo watanzania wengi tunapokoae. Mbongo akikufanyia kitu kizuri bila kumsifia anakasirika, anataka walau asikie neno la shukrani kutoka kwako ndipo roho yake itulie.
Mimi sipendi wanisifie. Kwanza sitaki sifa.

Lakini pia, wakinisifia ndiyo napata mzigo zaidi.

Nimemsaidia mtu mmoja kumlipia ada kuanzia sekondari mpaka chuo.

Kaenda kunisifia wamekuja wengine wanne.

Kazi imezidi 😂😂😂

Nao hao naenda nao poa tu lakini.
 
Siwekagi matarajio kabisa, najitoa kwa kidogo nilicho nacho, kwa muda nilionao, kwa utu na ama kwa nguvu nilizonazo, lakini kama ujuavyo maisha kuna nyakati yananifika inakuwa my turn, nikiomba kwa watu wale naambulia jeuri, block ama ukimya. Sio kwamba hawajawahi, wamewahi lakini mara nyingi zaidi naambulia hivyo.
Pole sana ila nikwambie kitu kimoja cha kukusaidia.. punguza huruma ikiwa hakuna anaekuhurumia wewe
 
Mimi sipendi wanisifie. Kwanza sitaki sifa.

Lakini pia, wakinisifia ndiyo napata mzigo zaidi.

Nimemsaidia mtu mmoja kumlipia ada kuanzia sekondari mpaka chuo.

Kaenda kunisifia wamekuja wengine wanne.

Kazi imezidi 😂😂😂

Nao hao naenda nao poa tu lakini.
Kusifiwa kunakufanya kuwa mtumwa. Utafanya juu chini watu wasikuchukulie tofauti (negative) na walivyokuchukulia mwanzo.

Binafsi nachukia watu wanione bora ninapofanya jambo kwa mara ya kwanza, maana najua ipo siku nitaboronga na hao watu walioamini uboro wangu wakinishusha wamenishusha mazima.

Ni Bora nionekane lofa ili hata nikija kufanya vyema watu watambue kuwa no one is perfect 😂.

Katika haya maisha mi naamini kuwa yule mtu aliyeaminiwe kwa mara ya kwanza halafu akaja kufanya makosa baadaye ataonekana hafai, lakini mtu aliyedharaulika mwanzo akaanza kufanya vizuri ataonekana anafaa.
 
Back
Top Bottom