Kila Nikiwatajia Kabila Wananikimbia

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,983
12,702
Naombeni ushauri kutokana na tatizo linalonikumba ktk haya mambo ya kimahusiano. Ni muda mrefu nimekuwa nikikimbiwa na wapenzi, na hii hutokea kila ninapowatajia KABILA langu. Mpenzi wangu wa mwisho niliamua kumueleza nia yangu ya kwenda kujitambulisha kwao, lakini alikataa kwa sababu kuwa hawezi kuolewa na mimi, hata kwao watamshangaa kuolewa na mtu kutoka kabila linalosifika kwa uchawi(sina uhakika na hili) na uhusiano uliishia hapo. Kutokana na umri kuanza kunitupa mkono, nimekuja kwa staili ya kuoa na nimepata binti mmoja ambae bado hajapata details zangu. Kutokana na experience niliyopata kutoka kwa wapenzi wa zamani, nafikiria kumdanganya kuhusu kabila langu ili naye asije akanibwaga.
Naombeni ushauri nikaoe kijijini mtu wa kabila langu au niendelee na mpango wa kumdanganya huyu kuhusu kabila langu!
 
...kudanganya ndio unaharibu kabisaaaa... kwani huko 'Lyamba la Mfipa' hakuna mabinti wazuri uoe ili kudumisha mila na desturi?
 
heheee,kabila lako ni mfipa? maana hilo jina lako ni la mbuga ya wanyama huko Rukwa na nasikia zamani kulikuwa na kibabbu cha miujiza huko.
Lakini isikupe tabu.Nenda kanisani hawaangalii makabila,pengine wewe huwa unawapatia club bilicanas.
Hata ukidanganya haisaidii,unaweza funga ndoa mkaishia kwenue talaka.Hujafanya bidii tu kutafuta atakayekupenda kwa dhati bila masharti.
 
Wapo mkuu ila tatizo ni kuwa huu utandawazi umesababisha muda mwingi tunakuwa mbali na jamii zetu.
 
Mweleze ukweli, akikimbia ina maana hakuwa wako. Mbona wapo mademu wengi wasiojali huo upuuzi wa kabila, uchawi nk.
 
heheee,kabila lako ni mfipa? maana hilo jina lako ni la mbuga ya wanyama huko Rukwa na nasikia zamani kulikuwa na kibabbu cha miujiza huko.
Lakini isikupe tabu.Nenda kanisani hawaangalii makabila,pengine wewe huwa unawapatia club bilicanas.
Hata ukidanganya haisaidii,unaweza funga ndoa mkaishia kwenue talaka.Hujafanya bidii tu kutafuta atakayekupenda kwa dhati bila masharti.
Ndio mimi Mfipa. Ila kupata hao watakaopenda bila masharti inakuwa ngumu, kama hawapo vile!
 
Mweleze ukweli, akikimbia ina maana hakuwa wako. Mbona wapo mademu wengi wasiojali huo upuuzi wa kabila, uchawi nk.

...Lol!

unajua, umesema pointi moja nzuri sana.
Si kila mwanamke/mwanaume utayetaka kumuoa/kuolewa naye anafikiria au kulitaka hilo toka kwako.

Vuta subira na endelea kutafuta, ipo siku utajaaliwa aliye wako... ila nawe umtunze, umlee, umheshimu na umthamini uamuzi wake kukubali kuolewa na/kukuoa wewe!
 
Pole aisee zingine ni stereotypes ambazo kazi kubomoa na sio maendeleo. lakini ni bora kuwa m-wazi akikupenda ajue kabisa amependa nini. kwani anaoa kabila? karne hii bado watu wana haya maupuzi!!!
 
Hata mimi nashangaa, tena wengine wameenda kidato!

hao hawapo tayari kabisa, wana wenyewe...wanakubalije muwe wapenzi then ukitamka ndoa wanagoma, kwani hawakuona kabila lako toka mwanzo....uckate tamaa wala ucjali umri endelea kuomba wako yupo mwema/mzuri tu.
 
MKUU RUDI HUKO HUKO KIJIJINI!
kwakua kutokana na kanuni za fizixi, TO EVERY ACTION THERE IS EQUAL AND OPPOSITE REACTION!, means kwamba kama wewe mabinti wengine wanakukataa kwa kabila lako, inamaana hata mabinti wa kabila lako watakua wanaogopwa kwa kitu hicho hicho, unanipata hapo mpwa?
inamaana sasa wewe tafuta hao hao mabinti wa kabila lako hawatakutosa, simple and clear!.
 
Mkuu GP, dada mmoja wa kabila langu niliwahi kumuapproach akakataa eti akadai mimi ni kaka yake(eti watu wa kabila moja ni ndugu).
 
wewe bado wako hajafika, kuwa mpole tu ma bro! vuta subira upate mke mwema.
 
Mkuu GP, dada mmoja wa kabila langu niliwahi kumuapproach akakataa eti akadai mimi ni kaka yake(eti watu wa kabila moja ni ndugu).

dah, mkuu!.
jaribu tena na tena mazee usiseme tuu subira yavuta heri, pengine ulimtongoza mara moja tu, watu tumeshafukuzia miaka 2, si nchezo yataka moyo!.
 
Ndio mimi Mfipa. Ila kupata hao watakaopenda bila masharti inakuwa ngumu, kama hawapo vile!

Mkuu nakushauri usali sana na uzidishe maombi maana mke mwema anatoka kwa Mungu shukuru hao walio kukimbia ni wachunaji tu na ungebahatika kumuoa mmoja usinge dumu nae
 
mpwa umeongea point hapa, nimekugongea
 
Back
Top Bottom