Kuna tofauti katiya kukumbukana kuelewa.
Unaweza kukumbuka 2+2 = 4, lakini usielewe kwa nini, kwa hiyo mtu akikuuliza 4+2 = ? ukashindwa kujibu, au unaweza usikumbuke wala kuelewa 2+2 = 4 .
Kanuni moja inayosaidia sana kuelewa (na hivyo kukumbuka) ni kuoanisha mambo.
Kwa mfano, mimi nilisaidiwa sana na kuuliza maswali darasani na kuhojiana na walimu sana. Nikaja kujikuta kusoma kunaniongezea tu mambo, nilikuwa nakumbuka mambo mengi sana na kuyaelewa kwa sababu nakumbuka nilivyokuwa najibizana na kuhojiana na walimu.
Kama shule haiwekei mkazo wanafunzi kuuliza na kuhojiana na walimu, kuna hatari kubwa ya wanafunzi kutokumbuka wala kuelewa.
Njia nyingine ya kuelewa na kukumbuka ni kushika vitu muhimu kwanza. Wengi hupenda ku cram kila kitu. Hili litamchosha mtu uwezo wake wa kuelewa na kukumbuka kwa sababu anajaribu kukumbuka na kuelewa mengi.
Kamaukiweza kuwa na muhtasari mzuri (hususan unaoandika mwenyewe kama notes wakati mwalimu anasema) utakumbuka na kuelewa.
Nje ya shule, nasoma sana na sitegemei kukumbuka kila kitu. Kwa mfano, miakakama 12 iliyopita nimesoma kitabu cha David McCullough "Truman' cha historia ya rais wa Marekani. Kitabu hiki nikizuri sana, kimefanyiwa research nzuri sana na kimeshinda mpaka tuzo ya Pulitzer, ni kikubwa kimezidi kurasa 1,000. Leo sitegemei kukumbuka yote yaliyoandikwa humo (vitabu vingi hujaza vitu unnecessarily pia) lakini, mtu akitakakuja na story ya uongokuhusu Truman nitajua, kwa sababu nitakumbuka habari zote za kweli nikitajiwa.
Kuna siku dogo mmoja alikuwa na mshua, kamletea ripoti mbovu. Kafeli masomo kibao. Mshua akamuuliza, mbona unafelisana? Dogo akasema mimikwa kweli sina uwezo darasani, sina kumbukumbu ya kukumbuka ninachosoma.
Mshua akamuachia dogo aende zake.Ila yule mshua mimi nikajua hajamaliza issue, anamlia timing dogo tu.
Baadaye, dogo akawa anachonga sana na wenzake, kuhusu mpira.
Dogo alikuwa ana uwezo wa kuelezea ule msimamo wa ligi ulivyo bila kuangalia jedwali gazetini,atakwambia timu gani ipo nafasi ya ngapi na ina magoli mangapi ya kufunga na kufungwa na details zote.
Basi yulemshua akawa anamsikia.Akamuita. Akamwambia wewe si umesema huna kumbukumbu ndiyo maana unafeli? Sasa mbona unaweza kukumbuka msimamowa ligi vizuri hivyo bila hata kuangalia gazeti? Akasema wewe tatizo lako si kumbukumbu, una kumbukumbu nzuri kunishinda mimi. Wewe inaonekana huna interest na hayo masomo kama ulivyo na interest na mpira.
Kwa hiyo interest nayo ni kitu muhimu. Ukisoma kitu hukipendi kuweza kukumbuka vizuri ni kazi sana.