Kila nikiikumbuka ESCROW siitaki kuisikia CCM!

Kila nikiikumbuka ESCROW siitaki kuisikia CCM!

Yaani nikikumbuka jinsi baadhi ya wabunge wa CCM walivyotokwa mapovu kuitetea ESCROW naumia sana, naichukulia CCM kama chama cha watu wasiomjua Mungu! Hawastahiki kupewa tena nchi, wanatufilisi! Watu walibeba pesa kwenye magunia, Stanbick bank hawataki kutoa majina ya walioiba pesa kama wale wa Mkombozi bank.

Huyu huyu mgombea urais wa CCM hajawahi kutoa msimamo wake kuhusiana na wizi wa pesa za ESCROW, Bora hata Mwandosya na Mwigulu walionekana kukerwa na jambo hilo!

Lakini Magufuli alikua kimyaaa! Leo akaanzishe mahakama ya mafisadi kweli?


Mmeshapoteza mtaji wezi mmewakumbatia msamiati umebadilika maneno UFISADI na WIZI hayapo tena kwenye Kamusi yenu, itawachukua miaka zaidi ya 50 kufikia hatua ya Dr Slaa.
 
Alishiriki vzr katika kamati ya bunge iliyoiumbua serikali kuhusu wizi wa fedha za escrow akaunti. Najua mengine waliyajua wakamezea. sasa umefika wakati serikali ikatekeleza juhudi za mpigania haki huyu aliyetutoka.
 
Tatizo la escrow ni nini? Ulitaka umeme wa bure? Au ulifikiri ile mitambo inayofua umeme ilijiweka yenyewe? Au siku hizi Tanzania mnaunda mitambo ya kufua umeme?

Mama yangu huwa kuna wakati unapoteza kabisa sikuelewagi kabisaaaa
 
Bora hakukemea mafisadi akiwa Bungeni kwani angefanya hivyo wangemuwahi maana hilo litaasisi siyo mchezo. Magufuli hata bila kukemea Bungeni sura yake tu wakiiona ikulu mafisadi ni presha inapanda na kushuka ndiyo maana wamekimbilia kwenye chaka la chadema. Ufisadi haukemiwi kwa maneno bali sura ya anayekemea inatakiwa ikiri kuwa kweli yeye na ufisadi hawaivi chungu kimoja. Sura ya Magufuli ni dawa ya Mafisadi.

Pima mwenyewe:
http://www.raiamwema.co.tz/hebu-tudurusu-‘ufisadi’-wa-lowassa-na-‘usafi’-wa-magufuli
 
Mama yangu huwa kuna wakati unapoteza kabisa sikuelewagi kabisaaaa

= sikuelewi

Nisome tena:

quote_icon.png
By FaizaFoxy
Tatizo la escrow ni nini? Ulitaka umeme wa bure? Au ulifikiri ile mitambo inayofua umeme ilijiweka yenyewe? Au siku hizi Tanzania mnaunda mitambo ya kufua umeme?
 
KWANINI UKAWA NA SIO CCM
  • ESCROW NA RUSHWA NYINGINE - AMBAZO ZIMELIINGIZIA TAIFA HASARA
  • USIRI WA MIKATABA AMBAZO NDIO MOJA ZA SABABU ZAKULETA UMASIKINI AFRICA (WORLD BANK)
  • KULINDANA KWA VIONGOZI HASA WAKATI WA KASHFA KUBWA ZINAZOLIINGIZIA TAIFA HASARA
  • BUNGE KUTOKUWAJIBISHA SERIKALI
  • CCM KUSHINDWA KUWAJIBIKA KWA WANANCHI
  • UKOSEFU WA AJIRA, HALI NGUMU YA MAISHA
  • UMEME WA MGAO
  • MFUMUKO WA BEI
  • RASIMU YA WARIOBA

Kwa hayo hapo juu, hata kama umpendi Lowasa utakubaliana na mimi kuwa kura yako lazima uipeleke UKAWA, Kwa mazingira yaliopo hapo juu "people have no other alternative but UKAWA"
 
Mkuu Kenethedmund Salute!,umemaliza kila kitu kaka,yaani kama upo kwenye fikra zangu!...japo najua watokwa mapovu watakuja kubwabwaja kijinga kwenye huu uzi wako.
 
Mfumo wa CCM uliiba pesa ya EPA na hivi majuzi wakaiba kupitia ESCROW na walioiba hawakuchukuliwa hatua hadi leo!Nauliza kama Mfumo wa CCM unaweza kuiba pesa ya umma mchanamchana na usifanywe chochote,je watashindwa kuiba kura mbazo ni karatasi tu?Je watashindwa kuiba hizo kura ili kuhakikisha maslahi ya mfumo wake katika miaka 5 ijayo? Je mfumo wa CCM utakubali kufunuliwa tako ili mikataba iliyoingia kwenye gesi,madini nk iangaliwe upya kwa maslahi ya nchi?

Naomba majibu tafadhali.
 
kwani anayekubali ni CCM au ni sisi wenye nchi ndo tunaoamua kwa kupitia box la kura?wao waeleze watz waliotufanyia na wanaotegemea kutufanyia wakitukuna sisi hatuna shida tutawachagua lakini kwa kuiba kura hapana tutaingia barabarani safari hii
 
Nimenunua ukwaju kilo nzima nimesha uloweka toka jana.. jumapili nikiaamka tu nakunywa glass 2 naoga nakunywa tena glass 2.. sinywi chai.. nachukua kisu changu uelekeo kibra... naweka kwenye chupa ya lita moja ukwaju wangu mwingine uelekeo machinjioni.... kita eleweka tu
 
Waliokerwa na Escrow CCM ni Prof Mwandosya, Mwigulu na Wassira.
Waliobakia wote mpaka Rais wao walifurahia dili la Escrow.Mpaka Pinda nae alitoka povu anadai si pesa yetu.
 
Nimenunua ukwaju kilo nzima nimesha uloweka toka jana.. jumapili nikiaamka tu nakunywa glass 2 naoga nakunywa tena glass 2.. sinywi chai.. nachukua kisu changu uelekeo kibra... naweka kwenye chupa ya lita moja ukwaju wangu mwingine uelekeo machinjioni.... kita eleweka tu
Hahaha ....ngoja na mie nikainunulie familia yangu ukwaju wa kutosha.
 
Yani inauma sana kuna watz leo ukikutananae barabarani huwezi jua kama ni mtu mwenye akili timamu au chizi mana anashinda jalalani anaokota okota ovyo mradi tu apate chochote kitu alaf ccm wamekaa wananeemesha matumbo yao tu hawawajali hawa watz wengi wenye maisha magumu, inauma sana na vigumu sana kuelewa kwanini watu bado wanashabikia hili lichama
 
Yaan wewe faizafoxy kichwa hamana kitu kabisa......
Hivi umeelewa alichokiandika kweli?
 
Binafsi nakumbuka nilitoa chozi, kutoka pale ndipo chuki dhidi ya CCM iliwaka moyoni mwangu..... hili siwezi kulificha. Kwa macho yangu nilishuhudia kwenye television Wabunge walio wengi wa CCM, Muhongo na Mwanasheria Mkuu wa wakati ule wakitoa lugha za dharau na khebei kwa Ndugu Kafulila juu ya msimamo wake wakufanyika uchunguzi juu ya Akaunti ya ESCROW. Baada ya Report ya Kamati kusomwa na Mr Kabwe, ilitoa picha jinsi watu hawa walivyo kuwa wakiangaika kuficha wizi na ufisadi mkubwa kabisa. Kutoka hapo nikagundua kuna majizi mengi ndani ya serikali, lakini ikanipa picha jinsi CCM ilivyo, kwamba inalinda uchafu ambao unawaumiza masikini wa Taifa hili. #CCM_OUT
 
Ongezea mabehewa mitumba hapo, hivi leo Mwakyembe anamnanga LOWASA , our god must be crazzy to put CCM back in power
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom