Nitaeleza kwa uzoefu wangu. Nimeandika mwanamke kwasababu ambayo itajidhihirisha kwenye comments.
Tutakubaliana kila mwanamke anapozaliwa anazaliwa akiwa na mapenzi ya kweli kabisa. Lakini hatua anazopitia katika mahusiano zinaweza kumfanya kujifunza kuwa na mapenzi ya ulaghai.
hatua ya Kwanza
Wanaume mtakubaliana nami yule binti uliyeanza kumfundisha mapenzi alikuwa na mapenzi ya dhati yasiyo kifani. Hawa mabinti huwa hawaangalii pesa, sura wala six packs. Huwa wanapenda kiukweli ukweli kabisa. Wanawake karibia wote wapo hivyo pindi wanapoanza mahusiano.
Hatua ya Pili
hapa mwanamke huanza kuona taswira tofauti juu ya mahusiano na mapenzi kwa ujumla. Kama mwanamme utamwonyesha mapenzi ya dhati anayokuonyesha basi ataendelea kuwa na mapenzi ya dhati. Pia kama shida za maisha hasa za kimahitaji hazitamwandama ataendelea kuwa na mapenzi ya dhati kama awali.
Lakini, ikitokea mwanamme akamchezea akamcheat na kushindwa kumpa mapenzi ya dhati huyu binti penzi lake la dhati akilini na moyoni litaanza kuyeyuka taaratibu.
Hatua ya tatu
Huyu binti kama hakuumizwa na akapata mwanamme ambaye hata kama hamsaidii shida zake za kimaisha ila japo kwa ushauri tu, huyu binti penzi lake litabaki pale pale.
Upande wa pili
-kama huyu mwanamke Ameshaumizwa ba wanaume basi atakuwa amepoteza ladha ya mapenzi na atakuwa ana date kibiashara. Atajiuliza kama nilimpenda Daby akanitenda kwanini niendelee kumpenda Juma anitende! aheri nimchune
RRONDO maisha yaendelee. huyu mwanamke atakuwa na roho ngumu na itaendelea kuwa hivyo.
Hatua ya nne
Yule binti ambaye hakuumizwa kama hakuumizwa kwenye hatua ya tatu basi asilimia ni nyingi kwake kufanikiwa katika sekta ya mapenzi. Ataolewa mapema, ataishi maisha ya furaja na atakuwa na fikra chanya juu ya mahusiano.
kwa upande wa pili
Yule binti aliyeumizwa atakuwa addict wa kuyachukia mapenzi. Hawa ni wale wanawake tunaokutana nao wanakuambia wanaume ni wale wale. Hawa ndiyo wale wanawake mnaowaomba namba leo kesho amekuomba laki mbili...yeye hataki utani. Akishakuwa addict anaona ndiyo mfumo sahihi wa maisha.
hapa kama familia haina uwezo atageuka kahaba au malaya. Huyu binti asilimia za kufanikiwa katika sekta ya mahusiano ni ndogo saana.
Hatua ya mwisho
Yule binti ambaye hakuumizwa atakuwa ashakuwa mtu mzima ataolewa(wengi wao) na hata ikitokea akapata matatizo katika mahusiano yake atachukulia ni sehemu ya makosa madogo madogo ya kibinaadamu.
Upande wa pili.
Huyu binti atakuwa mkatili saana kwenye mahusiano akija kuolewa anakuwa wale wanawake wa tit for tat. Huyu muda wote yupo standby...Hawana mapenzi ya dhati kwa waume zao kutokana na historia yao ya mapenzi. Na kwake ndoa sio ishu muda wowote ukimletea za kuleta haogopi kuchukua talaka.
kama hataolewa basi hawa ndiyo wale wanakuwa na dhana hasi kuhusu mapenzi.
NB: kuna outliers.
Jiulize Upo wapi au mwenzi wako yupo wapi.