Kila mwanamke anazaliwa na mapenzi ya kweli

Daby

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2014
Posts
34,961
Reaction score
80,242
Nitaeleza kwa uzoefu wangu. Nimeandika mwanamke kwasababu ambayo itajidhihirisha kwenye comments.

Tutakubaliana kila mwanamke anapozaliwa anazaliwa akiwa na mapenzi ya kweli kabisa. Lakini hatua anazopitia katika mahusiano zinaweza kumfanya kujifunza kuwa na mapenzi ya ulaghai.

hatua ya Kwanza

Wanaume mtakubaliana nami yule binti uliyeanza kumfundisha mapenzi alikuwa na mapenzi ya dhati yasiyo kifani. Hawa mabinti huwa hawaangalii pesa, sura wala six packs. Huwa wanapenda kiukweli ukweli kabisa. Wanawake karibia wote wapo hivyo pindi wanapoanza mahusiano.

Hatua ya Pili

hapa mwanamke huanza kuona taswira tofauti juu ya mahusiano na mapenzi kwa ujumla. Kama mwanamme utamwonyesha mapenzi ya dhati anayokuonyesha basi ataendelea kuwa na mapenzi ya dhati. Pia kama shida za maisha hasa za kimahitaji hazitamwandama ataendelea kuwa na mapenzi ya dhati kama awali.

Lakini, ikitokea mwanamme akamchezea akamcheat na kushindwa kumpa mapenzi ya dhati huyu binti penzi lake la dhati akilini na moyoni litaanza kuyeyuka taaratibu.

Hatua ya tatu

Huyu binti kama hakuumizwa na akapata mwanamme ambaye hata kama hamsaidii shida zake za kimaisha ila japo kwa ushauri tu, huyu binti penzi lake litabaki pale pale.

Upande wa pili

-kama huyu mwanamke Ameshaumizwa ba wanaume basi atakuwa amepoteza ladha ya mapenzi na atakuwa ana date kibiashara. Atajiuliza kama nilimpenda Daby akanitenda kwanini niendelee kumpenda Juma anitende! aheri nimchune RRONDO maisha yaendelee. huyu mwanamke atakuwa na roho ngumu na itaendelea kuwa hivyo.

Hatua ya nne

Yule binti ambaye hakuumizwa kama hakuumizwa kwenye hatua ya tatu basi asilimia ni nyingi kwake kufanikiwa katika sekta ya mapenzi. Ataolewa mapema, ataishi maisha ya furaja na atakuwa na fikra chanya juu ya mahusiano.

kwa upande wa pili
Yule binti aliyeumizwa atakuwa addict wa kuyachukia mapenzi. Hawa ni wale wanawake tunaokutana nao wanakuambia wanaume ni wale wale. Hawa ndiyo wale wanawake mnaowaomba namba leo kesho amekuomba laki mbili...yeye hataki utani. Akishakuwa addict anaona ndiyo mfumo sahihi wa maisha.

hapa kama familia haina uwezo atageuka kahaba au malaya. Huyu binti asilimia za kufanikiwa katika sekta ya mahusiano ni ndogo saana.

Hatua ya mwisho

Yule binti ambaye hakuumizwa atakuwa ashakuwa mtu mzima ataolewa(wengi wao) na hata ikitokea akapata matatizo katika mahusiano yake atachukulia ni sehemu ya makosa madogo madogo ya kibinaadamu.

Upande wa pili.

Huyu binti atakuwa mkatili saana kwenye mahusiano akija kuolewa anakuwa wale wanawake wa tit for tat. Huyu muda wote yupo standby...Hawana mapenzi ya dhati kwa waume zao kutokana na historia yao ya mapenzi. Na kwake ndoa sio ishu muda wowote ukimletea za kuleta haogopi kuchukua talaka.
kama hataolewa basi hawa ndiyo wale wanakuwa na dhana hasi kuhusu mapenzi.

NB: kuna outliers.

Jiulize Upo wapi au mwenzi wako yupo wapi.
 
Kiukweli ngoja niseme wanawake wa kinyakusa wana mapenzi ya dhatii kabisaa sijui kwann

Nirud kwenye madaa wanaume ndio chanzo kikuu cha kumbadilisha mwanamke na baadae mwanamke huyo huyo anakuwa mbayaa zaidiii.

Naandika nafuta ngoja nisome tena vizuri
 
Hilo nitakubaliana nalo.

sio la wanawake wa kinyakyusa lakini sijawajua.
 
Brother Daby umeniumiza kweli aiseh nimemkumbuka Rey wangu, too bad she was the first girl to me and i was a 5th man to her.....
 
Nirud kwenye madaa wanaume ndio chanzo kikuu cha kumbadilisha mwanamke na baadae mwanamke huyo huyo anakuwa mbayaa zaidiii.

Ila wanaume kuwa chanzo kikuu isiwe ndiyo excuse.

Kama umeweza kutambua tatizo kushindwa kulitatua ni uzembe wako.
 
Mwanamke huwa anajifunza kumpenda mwanaume...jinsi mwanaume anavyomuonyesha kumjali na kumpenda nae anampenda...ila mwanaume ndio anapenda...mwanamke anajifunza...

Ila sasa mwanamke akipenda anazama mpaka basi...
Njoo uchangue chochote hapa mlimani city ntalipa mm
 
Kiukweli ngoja niseme wanawake wa kinyakusa wana mapenzi ya dhatii kabisaa sijui kwann

Nirud kwenye madaa wanaume ndio chanzo kikuu cha kumbadilisha mwanamke na baadae mwanamke huyo huyo anakuwa mbayaa zaidiii.

Naandika nafuta ngoja nisome tena vizuri
We Demiss usije ukanajisi tena Jukwaa kwa kuwataja wanyakyusa humu, nimehuko, Hakuna wanawake waigizaji kama wanyachusa ukiwa nae utajihisi ni wewe tu ukitega mgongo atakayoyafanya hutaamini ukija kugundua, na wanao waharibu ni bibi na mama zao kwa kuwaambia wawakamate wanaume kwa ndumba hafu mwanamke wa kinyachusa ukimtongoza akakukatalia kabisa kaogee mwarobaini uondoe mikosi
 
Mwanamke huwa anajifunza kumpenda mwanaume...jinsi mwanaume anavyomuonyesha kumjali na kumpenda nae anampenda...ila mwanaume ndio anapenda...mwanamke anajifunza...

Ila sasa mwanamke akipenda anazama mpaka basi...
Nahitaji elimu pana juu ya hili.

Ninachojua huwa tunawatongoza baada ya kuwatongoza mkishatukubali...

Kila mmoja anaplay role yake kwenye mapenzi.

Kwangu kwa experience niliyonayo sijawahi kupenda kama navyowaona nyie.

labda wanaume wenzangu naombeni mnieleweshe... nyie huwa mnapenda au mnapendwa???
 
Hahahahahah
 
Oouh kumbe wapo hivyo.
 
Wewe ndiyo unanajisi jukwaa sababu mkeo na ukoo wake ni vimeo unajumlisha kabila lote?

Kama mkeo ni walu walu ni wewe Mkuu.
 
Mwanamke huwa anajifunza kumpenda mwanaume...jinsi mwanaume anavyomuonyesha kumjali na kumpenda nae anampenda...ila mwanaume ndio anapenda...mwanamke anajifunza...

Ila sasa mwanamke akipenda anazama mpaka basi...
Kuna stages za mapenzi ya dhati kwa wanasichana mara nyingi kama binti hajachepuka kwenye foolish age, akajikuta kazalishwa au katolew bikra na mme wa mtu kweli huwa wanapenda kwa dhati kwasasabu wengi bado wanakuwa shuleni,
Kuna umri wa kuanzia 21-26 hivi hapo asilimia kubwa huanza kupenda kama unamsaidia shida zake maana anakuwa anafikiria maisha na hapo ndo bond nyingi huvunjika, maana mwanamke anataka kutatuliawa matatizo yake zaidi hafu akijifanya anakupenda, hafu kuna 27-35 uhenga unaanza make up zinaanza kutumika ili kulinda uso hapo, kama mambo yake hayakwenda vizuri ndo utaona anaanza kuwatafuta waume za watu kuanza kujigongesha kama alikuwa classmate utakuwa unatumiwa sms za lawama kuwa unajidai sana (lakini wakati yupo binti hata salamu alikuwa hakupi), hiyo age wale wanaume above 40 hunaswa sana.
 
Back
Top Bottom