Kila mtu ni fisadi - Jadili

Idda

Member
May 22, 2009
64
0
Suala la UFISADI linatumiwa vibaya.
Kwa mawazo yangu, kila mtu ni FISADI kwa sehemu fulani.
Tatizo ni kwamba watu wengi wanauangalia ufisadi kwa viongozi wa ngazi za juu tu.
Kutokana kwa huu mtazamo wangu, hata mimi na wewe ni mafisadi kwa sehemu fulani.
Kinachotofautiana ni kiwango cha ufisadi.
Wanajamii mpo hapo?
 
Last edited:
kila mtu ni mbakaji, kila wanamke malaya, kila muislamu ni taliban, kila mnigeria mwizi and so on sasa equate that to ur topic...dont generalise!
 
Suala la UFISADI linatumiwa vibaya.
Kwa mawazo yangu, kila mtu ni FISADI kwa sehemu fulani.
Tatizo ni kwamba watu wengi wanauangalia ufisadi kwa viongozi wa ngazi za juu tu.
Kutokana kwa huu mtazamo wangu, hata mimi na wewe ni mafidai kwa sehemu fulani.
Kinacotofautiana ni kiwango cha ufisadi.
Wanajamii mpo hapo?

Rudi na lile jina lako la zamani...! Umekuja na jina jipya lakini mambo yako yale yale...ya zamani.
 
Suala la UFISADI linatumiwa vibaya.
Kwa mawazo yangu, kila mtu ni FISADI kwa sehemu fulani.
Tatizo ni kwamba watu wengi wanauangalia ufisadi kwa viongozi wa ngazi za juu tu.
Kutokana kwa huu mtazamo wangu, hata mimi na wewe ni mafidai kwa sehemu fulani.
Kinacotofautiana ni kiwango cha ufisadi.
Wanajamii mpo hapo?
you are too general...hata maana ya ufisadi huajaileza kiasi cha kujumuisha kwamba kila mtu hapa ni fisadi..come on guy...there are better info to share here instead of drawing unnecessary attention from people...

you may have a point, make it clear...usilete mada kama unaimba taarabu...
 
Suala la UFISADI linatumiwa vibaya.
Kwa mawazo yangu, kila mtu ni FISADI kwa sehemu fulani.
Tatizo ni kwamba watu wengi wanauangalia ufisadi kwa viongozi wa ngazi za juu tu.
Kutokana kwa huu mtazamo wangu, hata mimi na wewe ni mafidai kwa sehemu fulani.
Kinacotofautiana ni kiwango cha ufisadi.
Wanajamii mpo hapo?
Du! IDDA..

Hii fungua yako jamvi tena imekaa kikorofi!

Si kweli kwamba kila mtu ni fisadi. Kwa mfano wewe

mwenzetu ni fisadi maeneo gani?

Jenga hoja inayosomeka ma-mdogo...Hii uliyoanza nayo

imekaa kufikirika zaidi, au niseme ni ya kwenye ile nchi ya

'maziwa na asali' zaidi!
 
Suala la UFISADI linatumiwa vibaya.
Kwa mawazo yangu, kila mtu ni FISADI kwa sehemu fulani.
Tatizo ni kwamba watu wengi wanauangalia ufisadi kwa viongozi wa ngazi za juu tu.
Kutokana kwa huu mtazamo wangu, hata mimi na wewe ni mafidai kwa sehemu fulani.
Kinacotofautiana ni kiwango cha ufisadi.
Wanajamii mpo hapo?

Tupe mfano wa ufisadi wako dada Idda, tafadhali.
 
Maada yako ni ngumu imejaa ukweli, ila ukweli huu sio wa kugeneralise watu wote! ni kweli usiofichika kuwa wengi WA watanzania wanaishi katika criminalised society. society ambayo swala la rushwa linaanzia ngazi ya kaya!, kata, mashuleni, taasisi mbalimbali, walinzi, wafagizi, mamesenja etc, kifupi ndio BONGO, lakini bado japo wengi wanaishi katika hali hiyo, na ofcourse wakineemeka na mafiadi wakubwa (papas and nyangumis) lakini bado SIO KILA MTU, SIO WOTE, STILL WE HAVE SOME PEOPLE WHO ARE LEGALLY AND HONESTLY MAKING LIVES.

so change title please
 
Maada yako ni ngumu imejaa ukweli, _________________

Nakubali kuwa mada hii ni ngumu na imejaa ukweli.
Ndiyo maana wengi imewagusa na hawapendi kuukubali ukweli.
Ukweli unauma, lakini watu waungwana huukubali ukweli.

Swali: Hivi mnadhani hao baadhi ya viongozi tunaowaita mafisadi WANAKUBALI?

Sioni ajabu watu kuwa wakali kwamba nimegeneralise.
Ukichunguza bila jazba, utagundua kwamba mada hii inaukweli mtupu.
 
.........
Kwa mawazo yangu, kila mtu ni FISADI ...........

IDDA,
Sikuhukumu kwa mawazo yako,
Kumbe ni mawazo yako.
Kama ni mawazo yako, lazima yawe kweli kwako.
Na kama wewe ni FISADI, lazima utadhani watu wote ni mafisadi.

Ushauri,
Tueleze ufisadi wako ili tukusaidie uondokane nao.
 
Hawa akina Idda waliongia humu JF hivi karibuni ni maajenti wa mafisadi. Kuna wengi tu ambao wameji-register humu JF miezi hii ya karibuni bila shaka kwa kutumwa na hao mabwana zao kwa lengo la kuzipotosha mada kwa kutumia thread ambazo hazina kichwa wala miguu.

Inasikitisha kuona huyu jamaa anavyoitetea mada yake kwa hoja za kiajabu ajabu kama vile eti "imewagusa kwa hivyo ni ya ukweli." Kuna mada kadha dhidi ya vile RA ambaye ameamsha maelfu ya posts humu JF -- kwa hivyo yote hayo dhidi yake ni ukweli mtupu kwa sababu RA kawagusa wengi!

Acheni kuvuta jamani!
 
Inasikitisha kuona huyu jamaa anavyoitetea mada yake kwa hoja za kiajabu ajabu kama vile eti "imewagusa kwa hivyo ni ya ukweli." QUOTE]

Sitetei maada ila nasema ukweli.
Nimejua kuwa watu hawapendi ukweli.

Ili kuleta mahusiano mazuri, niamue kutogusa dhambi za watu?
 
Idda, ningependa kukupa ushauri ili wewe uwe sawa hapa JF, lakini kabla sijakupa ushauri, ningependa kuuliza swali personal, je wewe ni wa jinsia gani?

Natanguliza shukrani na samahani kama nitakuwa nimeuudhi au kukubughudhi kwa kukuuliza swali hilo.

Asante.
 
Suala la UFISADI linatumiwa vibaya.
Kwa mawazo yangu, kila mtu ni FISADI kwa sehemu fulani.
Tatizo ni kwamba watu wengi wanauangalia ufisadi kwa viongozi wa ngazi za juu tu.
Kutokana kwa huu mtazamo wangu, hata mimi na wewe ni mafisadi kwa sehemu fulani.
Kinachotofautiana ni kiwango cha ufisadi.
Wanajamii mpo hapo?


Si kweli hata kidogo kwamba kila mtu ni Fisadi.
Kwa mfano Rushwa ambayo ndiyo mama wa ilipandikizwa ikaelelewa kutetewa na kukuzwa na Uongozi wa Awamu ya Kwanza. Rushwa katika ngazi nyingine zote za chini ni matokeo ya kushindwa kwa utaratibu mzima katika ngazi ya taifa katika awamu ya kwanza. Kifupi Nyerere anahusika kwa kiwango kikubwa kabisa na mauza uza yote yanayoendelea.
Wakati wa Nyerere kuna makundi ya watu yalijua namana ya kunyenyekea na kuweka mambo yaonekane swafi usoni lakini kwa ndani kulikuwa na ushenzi mkubwa ukiendelea bila watu kuwa na mahali pa kutolea pumzi.
Viongozi walikuwa nusu miungu wasio guswa wala kuelekezwa jambo.
Usalama wa Taifa walijitahidi sana kupeleka taarifa za Wahuni ndani ya Sysytem Nyerere mara nyingi aliishia kuwahamisha Ofisi za kazi na kuwapa ofisi nyingine.
Watu wachache wenye damu za kunguni ndiyo walio adabishwa.
Kutokana na undava wa utawala mzima kuna kundi la watu wengi waliovuta subira ili wakati ukufika wafanye vitu vyao, wakati uliokuwa ukisubiriwa ndo huu.
Ukifuatilia kila Ufisadi utaona uan mizizi kadhaa na makovu kutoka awamu ya kwanza.
Kuna wakati ulifika Nyerere hakujali nini kinaendelea Tanzania, alicho jali ni utukufu wa jina lake kimataifa na ukombozi kusini mwa Afrika. hayo ni mambo amabayo Nyerere aliona ni ya maana.
Miaka ile ya 75 kurudi nyuma ni kweli Nyerere alionyesha seriousness fulani lakini ghafla akatuacha Watanzania tufanye vile tupendavyo.
Mfano ni Marehemu Bryceson aliyekuwa wazir wa ardhi alikuwa akikataza watu kujenga kiholela maeneo ya Mwembe Chai kule kinondoni akidai wasubiri viwanja vipimwe. Ni mwalimu Nyerere aliyewaambia watu wa Dar waendelee kujenga vile wapendavyo na matokeo yake ni ule mseto wa nyumba mithili ya mseto wa nazi majimbi korosho na mananasi mji mzima , hauliki.
Utawala wa Nyerere kimya kimya ulifumbia macho dalili na ugonjwa wenyewe wa Rushwa kwa kipindi kirefu sana mpka ikafika wakati mambo yakawa hayawezekani. Kila mtu leo hii ukimwuliza kuhusu Rushwa atakutajia Rushwa za Watendaji wadogo wa serikali kama Katibu kata katibu tarafa na Polisi wa vyeo vya Chini.
Wala Rushwa wakubwa walao Rushwa zisizo bebeka wanaongozwa na Rais wa nchi mwenyewe. Majaji, Makamishna wa Polisi, Majenerali wa Jeshi Mkuu wa Usalama wa taifa na Ikulu yote kuanzia katibu mkuu. Asiyepoke rushwa Ikulu na pengine anayesingiziwa kwa kila ovu ni mfagizi.
Sasa kupoteza lengo, waheshimiwa hawa hawashindwi kupandikiza watu kila kona ili kutawanya uongo kwamba Watanzania wote ni wala Rushwa.
Sijui yule mkulima wa mahindi kule Kondoa na mchunga ng'ombe wa kimasai kule Arusha na kibarua mpasua mbao kule Sao Hill wanababatizwa vipi na tuhuma za Ufisadi??

To do you do you to say you say me is that fair??
 
Ufisadi wangu sioni aibu kuuweka wazi.

Ufisadi wangu ni kwamba kila nipatapo nafasi huhihujumu CCM.

You are mocking us, it is better you delete this thread. Ubatili, ubatili, ubatili mtupu na kujilisha upepo.
 
Idda una matatizo ya kimsingi.Ufisadi ni antisocial na ni kinyume na maadili ya jamii.
Mtizamowako ni kuuhalalisha ufisadi na kuwater down revulsion ya wananchi juu ya hii antisocial behaviour.
Ili uelewe matokeo ya proposition yako inabidi ukubali vilevile ubakaji, uuajiwa maalbino, wizi wa mbenki na benki kuu, ujambazi na kadhalika.
Embracing of antisocial behaviour is a cancerous tendency.
 
Back
Top Bottom