Kila mtu ni fisadi - Jadili

Idda I said you better change the title! refer my earlier comment. say wengi ni mafisadi
 
I don't want to blame you for presenting what you think. That is what you you think, and it is not necesarily that whatever comes to your mind its true. You must have good reasons to support your argument, otherwise you might find yourself sinking in a deep water. Upo!!!!!!!
 
kila mtu ni mbakaji, kila wanamke malaya, kila muislamu ni taliban, kila mnigeria mwizi and so on sasa equate that to ur topic...dont generalise!

Ahsante sana Kapinga. Majibu yako yamenifurahisha mno kutokana na swali hilo linalotaka kuhalalisha Watanzania wote ndani ya nchi yetu ni mafisadi. Kitu ambacho hakina ukweli wowote.
 
Kule Usovieti na baadae Urusi baada ya Desemba 24, 1991 , nilisoma Riwaya ya enzi za Dola ya Kirusi 'Russian Empire' kuna mtunzi aliandika 'Kamu vu Rasia zhit kharashoo?' Yaani nani katika Dola ya Urusi anaishi maisha mazuri? Na kuulizeni wote hapa 'Duniani nani anaishi maisha mazuri? halafu tutakwenda nani Tanzania anaishi vizuri mapaka tutafika kijijini Namtumbo au Mwandoya nakuuliza katika vijiji hivyo nani anaishi vizuri? Lazima kwa ulinganisho Dar es salaam watu wanaishi vizuri kuliko mikoani halafu tunakuja Watu Masaki, Mikocheni Mbezi Beach nk wanaishi vizuri kuliko wa Manzese, Keko, Tandika, Mbagala nk! japo huko huko Manzese, Tandika nk kuna baadhi wanaishi vizuri kuliko baadhi ya wachache wanaoishi 'vibaya' kule Masaki au Mikocheni nk! Mfumo wa samaki mkubwa kuliwa na samaki mkubwa zaidi na samaki mdogo zaidi kuliwa na samaki mdogo bado baada ya Binadamu kushindwa kukubali mfumo wa kijamaa na kuendeleza hulka ya kujilimbikizia ukwasi ! nyie Watanzania mlio majuu hisia zetu mnaishi vizuri kihali na mali japokuwa tehehee..tehee mnatemwa mate na kunyanyapaliwa teheeh! si hatujali hayo kama ni wa nene na mnaleta pesa huku bongo za sisi kujikimu nyinyi ni mashujaa wetu mko huru kusema chochote! lakini lazima ni kutanabaisheni kuwa nchi hizo mlioko wameacha ugonjwa wa 'uzio' aleji ya watu wa kuwa na hamu ya kupata ukwasi wa kirahisi! walifanyisha babu zetu kazi kama punda bila utu wakaiba mali hazina idadi majengo hayo ya kisasa yanatokana na mali za afrika na kwingineko walikoiba-nasema kote Dola ya Uingereza, Hispania, Ujerumani nk waliiba sana tu! sasa vigezo viwango na taasisi za hawa wezi ndio zinatawala! kilichobadilika ni kuwa wezi wa sasa kupitia IMF na WB wako mahiri sana na ndio maana wajanja wote wanafanya kila jitihada kuingia katika katika klabu cha kimataifa cha mazungumzo UNO na taasisi zake anuai! katika mataifa yetu kuna viji UNO vidogo vidogo kuna miradi ya IMF na WB na kila mjanja anajiunga au anahakikisha mwanae au mjukuu yupo sasa serikali zetu ziko chini ya mamlaka inayotawala dunia na sifikiri hiyo mamlaka itawaambia hizi serikali kuwafungia kila mtu bomba la maziwa! kama walikuwa wanahuruma wasingehomola na wasingeweka masharti magumu ya kila kitu halafu wanatuzeveza kuwa waafrika na viongozi wetu HATUWEZI kama wizi ubadhirifu wanatufundisha wao! kuwepo na matabaka wanatufundisha wao! nyinyi mlio ulaya na usa endeleeni kumtumikia kafiri mpate mradi wenu! msichonge sana! hujui kesho na keshokutwa utakuwa mgeni wa nani! hakuna maisha ya ovyo kama yale ya kimaabara! yaani kila kitu kinafanyiwa hesabu! wanachuo maisha yenu ya bandia iwe hapa nchini tanzania au ughaibuni. sasa msitumie vigezo hivyo kupata majawabu halisia ya maisha. huyo hayati rais wa korea kusini amejiua kupinga kundi la wanafiki waliotaka kumfanya yeye mbuzi wa kafara! hata huku kwetu ikitokea 'fisadi' mmoja maarufu akajinyonga watu wengi watajaa majonzi! kuhusu rushwa, magendo na matumizi mabaya ya madaraka watanzania wote wana hatia na hasa nyie mlio majuu ndio nambari wani! tokea ulipopata wazo iwe wewe mwenyewe au kupitia mjomba, babu, shangazi au boi frendi utaona katika mlolongo huo mmoja atakuwa amehalifu sheria ama kwa kuhonga au kutumia ushawishi wa kimadaraka au kijinsia au yote pamoja! wengine wamekuwa huko kwa visa za kawaida halafu mnaita 'kujilipua'! mtanzania aliyejilipua majuu baadae anakuja kuwa mbunge waziri huyu atakuwa na simile! na sisi tulitoka nje tuna tabia ya kufikiri wabongo wengine ni wachovu wajinga na kadhalika! kwa miaka 6 niliokuwa Usoviet (5), Urusi (1) nimegundua mtu kama lenin alikuwa kruk au jangili! na kwa ujangili wake ndio maana akaweza kuuondoa utawala wa nusu mungu Tsar Nikolai wa wa pili. lakini nikasema katika makala zangu nikirejea mapinduzi ya ufaransa kwamba mapinduzi yote duniani ni ajali ya kijamii na athari zake zinaendelea kuitesa dahari na dahari! sasa labda tumwambie komredi zuma tutengeneze bomu la nyuklia la afrika tuwaaambie wajivuni wa magharibi sasa basi tunataka maisha mazuri wote ama sivyo tunakufa wote pamoja! nawaonea wivu korea kaskazini tungekuwa na hayo matopito na sisi tungelazimisha wakoloni wote watulipe fidia za vitu kuanzia miundo mbinu hadi fursa muhimu kama za elimu, afya na za uchumi. hivi sasa AFRIKA hata tungepata viongozi werevu saaana taasisi zinazotawala dunia na masharti yake YATATUKWAMISHA TUU! MAFISADI kwa kila moja wetu ajiangalie kwa makini kama sio fisadi basi amewahi kula hisani ya fisadi iwe katika kusaifiri au katika harusi au sherehe yoyote hata kupokea kofia khanga au fulana wakati wa kampeni ambao ninaweza kuwasamehe ni watanzania marehemu tu! wote sisi niiii ..... sisi tuliokulia enzi Mwalimu hatuna imani na mfanya biashara bepari awe mweusi, mweupe au wanjano kwetu sisi ni wezi tuu maana tuna hisi kuna wakati lazima .. AMEDHULUMU NA DHAMBI YA KUDHULUMU HAIJIKOSHI KWA KUTOA MSAADA WA MILIONI 400!! ENEWEI KUTOA SI UTAJIRI NI MOYO WAKATABAHU!
 
Back
Top Bottom