Hapa huwa kuna nguvu gani?

Ben-adam

JF-Expert Member
Jun 2, 2023
765
1,669
Mkiwa wawili/watatu mmetulia sehemu fulani mpo kimya, kila mmoja atakuwa akiwaza yake kimya kimya, ktk hali hiyo ghafla utasikia mmojawapo anaongea kwa sauti kile unachowaza wewe!

Au mkiwa watu wengi (kwenye kikao au vyovyote vile), utatoa hoja au maoni fulani juu ya mada fulani, hapo tena utasikia mtu anasema "ooh umeniwahi, hata mimi nilitaka kusema hivyo" (hata hapa hapa jf naliona hili) it maana yake hapo umesema mawazo ya mtu mwingine!

Wengine watasema kwamba mawazo yamefanana; je kwa nini yafanane, kuna nguvu gani hapo?

Umekaa zako kimya, kimoyo moyo unaimba wimbo wa alikiba, utasikia mtu anaimba wimbo huo kwa sauti!

Ni kwanini?
 
Back
Top Bottom