Kila kitambulisho cha Taifa kimegharimu tsh 89,800

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,908
51,907
NIDA walipewa shilingi bilioni 179.6 kwa ajili ya kutengeneza vitambulisho vya taifa.Vitambulisho walivyotegeneza na kugawia wananchi ni milioni mbili.Ukigawa pesa walizopewa na vitambulisho walivyotengeneza utapata jawabu kuwa kila kitambulisho kimoja kimegharimu shilingi 89,800

Nchi hii ina wezi.Ndio maana Maghufuli kweli ana hasira nao.

======
*Matumizi ya bilioni 179.6/- hadharani

*Kila kitambulisho chatafuna Sh 89,800
Na Bakari Kimwanga, Dar es Salaam

WINGU zito limetanda ndani ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kuhusu matumizi ya Sh bilioni 179.6 ambako kila kitambulisho cha taifa kimegharimu Sh 89,800 zikiwamo gharama za utawala, MTANZANIA limebaini.

Hayo yamebainika siku chache baada ya Rais Dk. John Magufuli kushangazwa na watendaji wa mamlaka hiyo ikizingatiwa vitambulisho vilivyokwisha kutengenezwa hadi sasa havifiki milioni mbili na havina saini.

“Utaona ugumu wa kuongoza, nchi inatawaliwa na madudu ya kila aina. Wapo watu wanacheza na fedha wanavyotaka wakati wapo watu masikini sana wengine wanataka bodi zao wakakae Ulaya.

“Hapo ndipo tulipofikia, wengine wanalipwa mshahara wa Sh milioni 35 kwa mwezi…naomba mniombee kabla ya kunihukumu, toeni hukumu kwa haki kwa hawa wanaotaka kuifikisha nchi pabaya, toeni hukumu zao haraka,” alisema.

Rais Dk. Magufuli, licha ya kushangazwa na hali hiyo, alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilipewa Sh bilioni 70 lakini iliweza kutengeneza vitambulisho 23,253,982 ambavyo vilikuwa na saini ya kila mpiga kura na kila kimoja kimegharimu Sh 3,010.

Kutokana na hali hiyo, tofauti ya gharama kati ya kitambulisho kimoja cha NIDA na cha NEC ni Sh 86,790.

Pamoja na hayo, hivi sasa Watanzania wanasuburi ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad, kuhusu matumizi ya fedha hizo za NIDA.

Januari 26 mwaka huu, Rais Magufuli alitangaza kumsimamisha kazi ili kupisha uchunguzi dhidi yake, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu.

Maimu alisimamishwa kazi pamoja na maofisa wengine wanne, kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za Serikali.

Maofisa hao ni Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Joseph Makani, Ofisa Ugavi Mkuu, Rahel Mapande, Mkurugenzi wa Sheria, Sabrina Nyoni na Ofisa Usafirishaji, George Ntalima.

Akitangaza uamuzi huo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Sefue, alisema taarifa zilizomfikia Rais zinaonyesha kuwa NIDA hadi wakati huo ilikuwa imetumia Sh bilioni 179.6, kiasi ambacho ni kikubwa.

Alisema Rais angependa ufanyike uchunguzi na ukaguzi kujua jinsi fedha hizo zilivyotumika, maana amekuwa akipokea malalamiko ya wananchi kuhusiana na kasi ndogo ya utoaji wa Vitambulisho vya Taifa.

Licha ya kumuelekeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, afanye ukaguzi maalumu wa hesabu za NIDA ukiwamo ukaguzi wa “value for money” baada ya kuthibitisha idadi halisi ya vitambulisho vilivyotolewa hadi sasa, pia aliitaka Takukuru ifanye uchunguzi kujiridhisha kama kulikuwa na vitendo vya rushwa au la.

Historia ya NIDA

Mradi wa Vitambulisho vya Taifa umekuwa na historia ndefu. Ulibuniwa mwaka 1972 ikiwa ni zaidi ya miaka 38 iliyopita kwa kupitisha bungeni Sheria ya Vitambulisho na Uraia ya mwaka 1972.

Tangu wakati huo, mawaziri waliopita Wizara ya Mambo ya Ndani waliukuta na kuuacha kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo mgongano wa masilahi ya umma na ya binafsi.

Oktoba 1999 mradi huo ulitangazwa na kampuni 27 za nje na ndani ziliomba kazi hiyo. Kutokana na mizengwe, urasimu na hila za ufisadi makampuni 22 yalijitoa kwenye kinyang’anyiro hicho na zabuni ikafutwa katika mazingira ya kutatanisha.

Serikali iliipa kazi hiyo kampuni ya Gotham International Ltd inayomilikiwa na Jack Gotham aliyekuwa akishirikiana na Ofisa wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), John Kyaruzi, ambaye alisaidia kuiunganisha kampuni hiyo na Business Connections ya Afrika Kusini na kwa pamoja wakashughulikia ‘mchanganuo’ wa mradi huo.

Mabilioni yanavyopotea

Ripoti mbalimbali zinaonyesha Serikali imepoteza karibu Sh bilioni 500 kwa miaka tisa kutokana na matumizi mabaya ya fedha za umma ikiwamo rushwa na ubadhirifu wa mali mbalimbali.

Hiyo ni kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia katika moja ya ripoti zake alizowahi kuzitoa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Dk. Helen Kijo-Bisimba.

“Katika kipindi kisichozidi miaka tisa kumeripotiwa kashfa kubwa nne ambazo kwa ujumla wake zimelisababishia Taifa hasara ya karibu Sh bilioni 500 ambako kwa wastani inapoteza takriban asilimia 20 ya bajeti yake ya mwaka,” alisema Sungusia.

Alizitaja kashfa hizo kuwa ni mabilioni ya shilingi kupitia ununuzi wa rada iliyotumika kutoka Kampuni ya BAE Systems ya Uingereza, wizi wa mabilioni katika akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT) na kashfa ya mabilioni ya fedha walizogawiwa baadhi ya viongozi wa uuma, kutoka akaunti ya Tegeta Escrow.

Chanzo: Mtanzania
 
Waliamua kutengeneza ajira kwa vigogo(mchwa) na watoto wa ccm ndo wakawa wanakula kwa style hiyo
 
NIDA walipewa shilingi bilioni 179.6 kwa ajili ya kutengeneza vitambulisho vya taifa.Vitambulisho walivyotegeneza na kugawia wananchi ni milioni mbili.Ukigawa pesa walizopewa na vitambulisho walivyotengeneza utapata jawabu kuwa kila kitambulisho kimoja kimegharimu shilingi milioni 89.8.

Nchi hii ina wezi.Ndio maana Maghufuli kweli ana hasira nao.
Rekebisha hesabu zako kabla mtu hajaku-quote.
 
Jibu sahihi ni 89800

Umekosea umechukua bilioni ipi ile ya american bilioni au English BILION?

Bilioni ya mwingireza ina sifuri 12.Bilioni moja ni sawa na milioni milioni
ya mmarekani bilioni moja ina sifuri 9 yaani milioni elfu moja.
Kwa TANZANIA bilioni ni milioni milioni ndio niliyotumia
Nabaki na msimamo wangu Kitambulisho kimoja ni milioni 89.8 sio elfu 89.8 uliyotamka
 
Hizo pesa ni general cost za kununua Vifaa, kodi ya majengo nk vitambulisho nadhani havijagharimu hata elf 50,, hyo pesa ni jumla ya pesa ambayo serikali iliipa Nida tangu 2012 mradi ulipoanza, kila program inalipiwa vile vile wala usidhani ni vitambulisho vitatengenezewa hewani bila kununua vitu
 
YEHODAYA, mwaka 1974 ulikuwa na umri gani. Kwa ulinganisho tu CCM iliasisiwa mwaka 1977 miaka mitatu baadaye. Naomba usiniulize mwaka nilioutaja hapo mwanzo kulitokea nini ila tafuta mwenyewe.
 
Hizo pesa ni general cost za kununua Vifaa, kodi ya majengo nk vitambulisho nadhani havijagharimu hata elf 50,, hyo pesa ni jumla ya pesa ambayo serikali iliipa Nida tangu 2012 mradi ulipoanza, kila program inalipiwa vile vile wala usidhani ni vitambulisho vitatengenezewa hewani bila kununua vitu

Pesa zote walizopewa ilikuwa ni kwa ajili ya kutoa vitambulisho vya taifa.KUTOA HUKO KUNA GHARAMA zake majengo ,mishahara,makomputa nk hesabu niliyopiga ni kuchukua pesa zote walizopewa na idadi ya vitambulisho milioni mbili walivyotengeza mpaka sasa ni kuwa ukipiga gharama ya kitambulisho kimoja ni milioni 89.8 kwa kuwapa vitambulisho watu milioni 2 kati ya watanzania milioni 45 tulioko Tanzania
 
Labda kwanza tukuulize bilioni moja ina milioni ngapi ndani yake? Huenda ujinga uliosomea kwenye shule za kata umeshindwa kukufanya ujue hilo fumbo dogo
 
NIDA walipewa shilingi bilioni 179.6 kwa ajili ya kutengeneza vitambulisho vya taifa.Vitambulisho walivyotegeneza na kugawia wananchi ni milioni mbili.Ukigawa pesa walizopewa na vitambulisho walivyotengeneza utapata jawabu kuwa kila kitambulisho kimoja kimegharimu shilingi milioni 89.8.

Nchi hii ina wezi.Ndio maana Maghufuli kweli ana hasira nao.

Kwa investment cost ya equipment, software, building etc ghrama ya kila kitambulisho inatakiwa kushuka as number of IDs are issued. Ilitakiwa analysis yako hii itolewe siku ambayo wangetoa kitambulisho cha mwisho kwa sasa this is unfair judgement. Kwa kusema hivyo sina maana ya kuwatetea hata kidogo ila hesabu uliyofanya lazima ilete maana
 
Shule za kata ni janga la kitaifa. Na hivi wameamua kufanya elimu bure bila kuboresha maslahi ya walimu ina maana mzigo zaidi unamuelemea mwalimu na kuzalisha wajinga kama YEHODAYA wengi zaidi. Sidhani kama hata GPA ya Kikwete ya 2.1 ulifikisha wewe

Haya msomi wa HAVARD au OXFORD piga hesabu nimekupa bilioni 179.6 utengeneze vitambulisho vya taifa ukatumia hizo bilioni 179.6 kwa gharama mbali mbali kuhusiana na kutengeneza vitambulisho vya taifa milioni mbili.Nikikuambia nipe COST PER UNIT ya kila kitambulisho kwa pesa nilizokupa kwa kazi hiyo jibu litakuwa shilingi ngapi kama walau katika kupitia digrii yako ya kufikirika ya OXFORD au HAVARD kama walau uliwahi somea COSTING utapata jibu gani?
 
Labda kwanza tukuulize bilioni moja ina milioni ngapi ndani yake? Huenda ujinga uliosomea kwenye shule za kata umeshindwa kukufanya ujue hilo fumbo dogo

Bilioni moja ni milioni milioni moja.Ngoja nikuandikie kabisa bilioni moja ina sifuri 12.Kwa tarakimu inaandikwa hivi

1,000,000,000,000
 
Shule za kata ni janga la kitaifa. Na hivi wameamua kufanya elimu bure bila kuboresha maslahi ya walimu ina maana mzigo zaidi unamuelemea mwalimu na kuzalisha wajinga kama YEHODAYA wengi zaidi. Sidhani kama hata GPA ya Kikwete ya 2.1 ulifikisha wewe
Bora na wewe umesema. Huyu YEHODAYA sasa anatujazia tuu seva yetu. Elimu ni shida kwake ila jukumu alilopewa la kuanzisha thread JF linamtesa maana atafikishaje malengo ya idadi bila pumba wakati kichwani ni debe tupu?
 
Elimu ya Hapa na Pale haiwezi kujibu hoja yako!!

Queen Esther

Haya msomi wa HAVARD au OXFORD piga hesabu nimekupa bilioni 179.6 utengeneze vitambulisho vya taifa ukatumia hizo bilioni 179.6 kwa gharama mbali mbali kuhusiana na kutengeneza vitambulisho vya taifa milioni mbili.Nikikuambia nipe COST PER UNIT ya kila kitambulisho kwa pesa nilizokupa kwa kazi hiyo jibu litakuwa shilingi ngapi kama walau katika kupitia digrii yako ya kufikirika ya OXFORD au HAVARD kama walau uliwahi somea COSTING utapata jibu gani?
 
NIDA walipewa shilingi bilioni 179.6 kwa ajili ya kutengeneza vitambulisho vya taifa.Vitambulisho walivyotegeneza na kugawia wananchi ni milioni mbili.Ukigawa pesa walizopewa na vitambulisho walivyotengeneza utapata jawabu kuwa kila kitambulisho kimoja kimegharimu shilingi milioni 89.8.

Nchi hii ina wezi.Ndio maana Maghufuli kweli ana hasira nao.
Mkuu,
Hiyo namba (89.9 Mil) umeipataje!!??? Kwa hizo takwimu ulizotoa hapo namba sahihi ilitakiwa kuwa 89,800/=.
 
Back
Top Bottom