Kila baba anatakiwa atoe somo kwa binti yake

Kila baba anatakiwa atoe somo kwa binti yake

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
KWA UFUPI
"Anatakiwa ajiamini katika kutekeleza majukumu yake, pia asiogope kushindwa kwani ni sehemu ya mapambano katika maisha. Hivyo, hatakiwi kuwa na hofu katika kutekeleza majukumu yake".


Baba yangu alinipa zawadi ambayo mtu yeyote angeweza kuitoa kwa mtoto wake. Alikuwa akiniamini. Kila baba ana nafasi maalumu katika maisha ya binti yake. Kama shujaa katika macho yake, baba ana jukumu kubwa la kumwonyesha binti yake jinsi mwanamume wa kweli anavyompa nguvu ya kuukabili ulimwengu kwa kujiamini, huku akiwa na nguvu zote. Pamoja na yote, anatakiwa amwonyeshe binti yake kuwa baba ni mwanamume wa kwanza katika maisha ya mtoto wa kike.
Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo kila baba anapaswa kumfundisha binti yake ili kumthibitishia kuwa yeye ni baba bora dunuani.
Yeye ni wa kipekee
Kimsingi kila mtu ni wa kipekee. Ni kwamba, baba anatakiwa kumsaidia binti yake kujitambua na kujua nafasi yake katika maisha. Pia anatakiwa kuelewa kuwa yeye ni ndiye pekee na hakuna kama yeye duniani. Baba mzuri ni yule anayemheshimu na kumkubali binti yake.
Kitendo hiki kitamsaidia kumfanya awe na furaha siku zote. Zaidi ya hayo kama mzazi, unatakiwa kumfundisha mtoto upendo. Hii itamsaidia kuwa na maadili mema na kuwa na mtazamo chanya wa maisha.
Anastahili mazuri katika maisha yake
Nafikiri kila baba anafahamu kuwa binti yake anastahili kila kilicho kizuri katika ulimwengu huu. Ni jukumu la baba kuhakikisha binti yake anaelewa kuwa anastahili heshima, upendo na shukrani.
Ikiwa unahitaji binti yako afurahie maisha, basi mfundishe kuwa anatakiwa kuangalia yeye anataka nini na siyo watu wengine wanamfikiriaje.
Anaweza kufanya moja kati ya mambo muhimu ambayo baba anapaswa kumfundisha binti yake. Kwamba, ana nguvu za kutosha kumudu na kuyakabili mambo na mitihani mbalimbali ya kimaisha.
Anatakiwa ajiamini katika kutekeleza majukumu yake, pia asiogope kushindwa kwani ni sehemu ya mapambano katika maisha. Hivyo, hatakiwi kuwa na hofu katika kutekeleza majukumu yake.
Katika jamii zetu, uwepo wa mfumo dume kwa kiasi fulani umetokomezwa, hivyo baba anatakiwa kumlea binti yake akihakikisha kuwa anakuwa shupavu na mwenye uthubutu.
Awe huru kueleza mawazo yake

Najua mara nyingi huwa ni vigumu kuukabili woga, pia kuwa na uhuru wa kuongea kile unachofikiria kwako ni sawa. Nilipokuwa mdogo, wakati mwingine nilikuwa najisikia vibaya kuuliza maswali.

Baadaye nilihofia kuumiza na kumvunja moyo mtu mwingine kutokana na kile ninachokiwaza juu yake. Wasichana wengi huwa na aibu katika kufanya mambo. Hivyo kama baba unatakiwa kumfundisha binti yako asione tabu kutoa maoni yake juu ya mtazamo wake.

Awe na nidhamu

Nidhamu pia ni jambo la msingi kabisa katika makuzi ya mtoto. Hivyo ni jukumu lako kama baba kuhakikisha binti yako anakuwa na nidhamu ya kutosha kwani huo ndiyo mwongozo madhubuti wa maisha yake ya baadaye.

Ajisimamie

Kuna imani kuwa mtoto wa kike hawezi kufanya kitu kikakamilika bila mkono wa mwanamume. Hili hutokea kutokana na kulegalega kwa kazi ya baba katika kutoa mwongozo wa malezi mema kwa mwanawe. Baba ni mtu nambari moja, anayejua jinsi ya kuilinda familia yake katika njia sahihi. Sasa kwa kuwa kila mtu anatakiwa kujua kujisimamia mwenyewe, baba ana nafasi kubwa ya kumfundisha binti yake jinsi ya kujilinda na kujisimamia.

Maisha yamejaa migogoro na mara nyingi unyonge wa wanawake huwasababishia kuoenewa na kunyimwa haki zao. Hivyo, baba akifanya vizuri kazi yake katika hili ni wazi kuwa hali hii itatoweka.

Awe anaridhika

Hili pia ni muhimu. Binti yako anatakiwa kuelewa kuwa jasho lake lina thamani kubwa katika maisha yake. Anatakiwa kujifunza pia kuwa utegemezi hauna nafasi katika maisha yake. Baba siku zote ni msaada wa familia, lakini kama mwanamke hatakiwi kumchukulia kama mashine ya kutolea pesa.

Unatakiwa kufundisha binti yako kujitegemea. Hatakiwi amtegemee. mwanaume kwa kila kitu.


Chanzo: Mwananchi
 
Ni wachache sana mwaya, baba akionekana kumpenda binti yake na kumtimizia kila kitu mama anakuwa mbogo.
 
True true
 

Attachments

  • 1408941927885.jpg
    1408941927885.jpg
    24.1 KB · Views: 192
kweli ila wazazi wetu wengine wanawasahau sana watoto wao wakikupa kula,kuvaa,elimu baas hana mda wa kujua nini kinaendelea tena juu ya watoto mwisho wa siku wanaharibika baba anakua wa mwisho kujua matatizo ya bintie
 
Ask my daughter about me and she'll tell you that I'm half-dad half-amazing!
 
Ni wachache sana mwaya, baba akionekana kumpenda binti yake na kumtimizia kila kitu mama anakuwa mbogo.

Most of the time ni wivu tu,anaona dogo anapewa attention sana kuliko yeye..
 
kwa sababu
mdida, tafadhali funguka rafiki...
i'm curious kujua kwa nini mama wengi wanakuwa mbogo baba akionyesha upendo na kuwa karibu na bintiye!!
 
Last edited by a moderator:
Most of the time ni wivu tu,anaona dogo anapewa attention sana kuliko yeye..

kuna wababa walikuwa wanatafuna binti zao wa kuwazaa, ilikuwa ni kizungumkuti usisikie wala usiombee.
 
kuna wababa walikuwa wanatafuna binti zao wa kuwazaa, ilikuwa ni kizungumkuti usisikie wala usiombee.

Hapo sasa ndio pagumu...siku hizi ukiona baba yuko karibu sana na bintie...maswali yanakuwa mengi kuliko majibu..maana wababa wa miaka hii...akili zao zipo chooni....
 
Pamoja na ubandidu wako wooote hapo ndo nakukubali. Hata hii tabia ya wanawake sleeping around like nobody's business inatokana na kuwa na baba lousy. Baba anapaswa ampe bintiye confidence, binti ajiamini kuwa anaweza kuhamisha milima.

hivi ulipata zile raba mtoni za princess?
Ask my daughter about me and she'll tell you that I'm half-dad half-amazing!
 
Back
Top Bottom