Kipenzi Chao
Member
- Oct 12, 2010
- 99
- 3
Hope you all fine....! Jamani naombeni wataalamu wanisaidie, hasa wanawake na wale wanaume wenye wapenzi wao. Mimi nimekuwa nikisafiri mara kadhaa na hivyo kupishana na mpenzi wangu wa kike kwa muda takribani miezi miwili hadi mitatu...! Lakini kila ikifikia miezi miwili, hudai kuumwa tumbo la chini na kiuno...! hudai maumivu haya sio serious sana kiasi cha kushindwa kuendelea na shughuli za kila siku...! Nimejaribu kufanya uchunguzi nikatambua kuwa nikikaa pamoja naye kwa muda wa mwaka mzima hakuna hata siku ananiambia hivyo! Sasa naombeni mnisaidie hii hali husababishwa na nini? na suluhisho lake ni nini?