..hii hapa chini aliitoa ktk mkutano wa UWT-CCM uliofanyika Dodoma.
]KINA MAMA ENDELEENI KUZAA WASICHANA WAZURI KWANI KATIKA MIAKA HII MIWILI HATA KWENYE MASHINDANO YA UREMBO DUNIANI TUMETAMBA.
..tena hii anaelekea iliandikiwa ktk hotuba yake.
Masanilo,
..nimesema alitoa kauli hiyo ktk mkutano wa UWT-CCM.
..najua ni vigumu kuamini kwamba alitoa kauli hiyo. mimi kilichonishangaza zaidi ni kuikuta ktk text ya hotuba yake. sasa naogopa kuamini kwamba aliandikiwa na akaisoma.
..au labda aliandika mwenyewe hiyo hotuba, manaake kama wewe ni speech writer lazima uwe na uoga kidogo kumuandikia Raisi utumbo kama huo.
..hotuba mzima iko kwenye link hii hapa chini ambayo ni website ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
.. bonyeza hapa
mara nyingi kikwete akizungumza huwa sometimes nafeel embarased
top three ya mazungumzo ya kikwete yaliyo ni disappoint ni hii
1. Alienda Mwanza mara baada ya kuchaguliwa kuwa rais alizungumza mengi lakini mwisho alisema namnukuu "Wananchi wa Mwanza nataka kulibadilisha hili jiji lenu liwe kama Carlifornia" na hii ilikuwa hadharani kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
2. Akifanya mkutano wa waandishi wa habari mwanzoni kabisa, kuna mwandishi mmoja wa kike alimuuliza swali kuhusu nchi kurusu bidhaa duni kuingia na uhai wa manufacturing industry, yeye alijibu huku akijionyesha mtoto wa mjini anaejua mavazi, akaanza kutaja labels za nguo, na mwisho akasema kwa kuwa sio wote wanamudu nguo mpya, basi ruksa watu kuingiza nguo duni
3. HII ilikuwa ile hotuba yake maarufu ya bungeni, watu nchi nzima tunasubiri ripoti ya EPA ataizungumziaje, yeye akatumia muda mwingi kuchekesha watu, top ilikuwa pale aliposema "Kula uliwe"
nakubaliana na wewe mkuu Buchanan, huyu bwana mimi alinimaliza kabisa aliposema kuwa haelewi sababu kwanini nchi yake ni maskini tena anazungumza mambo haya akiwa ughaibuni kwenye nchi za watu!! Kila siku toka enzi za Mussa nchi hii tunaimba kuwa tuna maadui wakuu watatu na mmoja wao ni umaskini; kwahiyo mtu unatagemea yeyote atakayeusaka urais wa nchi yetu kazi yake kubwa ni kutafuta jinsi ya kupambana na maadui hawa na huwezi kumshinda adiu bila kumjua na kutafuta mbinu za kumshinda. Inaelekea Jakaya aliusaka urais bila ya kujua akiupata ataufanyia nini zaiadi ya uVASCO DAGAMA!
Ndugu yangu hata nchi nipewe mimi au wewe au yule, kamwe haiwezekani kuleta maisha bora kwa KILA mtanzania. Si mtalamu wa Jiographia au siasa au history; naomba kuuliza kuna nchi hapa duniani ambayo KILA mwananchi wake anamaisha bora?....jamaa yangu hapa ananiambia Luxembourg.
KILA mtanzania kuwa na maisha bora ni kazi....haiwezekani. Si kwamba nimekata tamaa kuwa raisi wetu hataweza, nachofahamu na nilivyofahamu tangia hii style ya uombaji wa kula KAMWE maisha bora kwa KILA mtanzania hayataletwa. Inawezekana "kwa kila mtanzania" ina maana yake.
Ni kweli watanzania yatubidi kufanya kazi kwa bidii ili tuwe na maisha bora; lakini kumbuka background ya mtu, mazingira ya mtu, uwezo wa mtu na support ya mtu. Hivi vyota, na mengineyo, yanamfanya mtu kuwa na uwezo wa kujuwa/kufikili ni jinsi gani ya kutatua au ya kuwa na maisha bora. mf Elimu tuipatayo mashuleni, shule nyingi zilizopo Tanzania, si elimu inayoweza kumkwamua mtu pindi aiishiapo kidato cha nne. Haimfanyi mtu awe endelevu. Hebu fananisha contents za mtu wa computer science aliemaliza pale UDSM na yule aliemaliza pale Bath university; je wanafanana? waliandaliwaje walipokuwa primary, secondary au utotoni.
Kwahiyo, HATA NIWE MIMI AU WEWE AU YEYE AU YULE, kamwe haiwezekani kuleta maisha bora kwa KILA mtanzania
Hizi ndio hotuba wanazoandika akina January?
..hii hapa chini aliitoa ktk mkutano wa UWT-CCM uliofanyika Dodoma.
KINA MAMA ENDELEENI KUZAA WASICHANA WAZURI KWANI KATIKA MIAKA HII MIWILI HATA KWENYE MASHINDANO YA UREMBO DUNIANI TUMETAMBA.
..tena hii anaelekea iliandikiwa ktk hotuba yake.
Lakini hata Mwalimu aliwahi kuuambia mkutano wa akina mama kwamba "uchumi wanao, wameukalia"! Na mzee Mwinyi aliwahi kuuongelea "ukuni" mmoja hauvishi chakula.
Juzi kwenye maswali mwisho aliwaomba radhi eti ohh kachukua muda mwingi hadi mechi ya mpira karibia inaisha ..... lol
mpira ni muhimu!!!!