Kikwete's most embarassing statements...

Kikwete's most embarassing statements...

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,320
Reaction score
117,612
mara nyingi kikwete akizungumza huwa sometimes nafeel embarased

top three ya mazungumzo ya kikwete yaliyo ni disappoint ni hii

1. Alienda Mwanza mara baada ya kuchaguliwa kuwa rais alizungumza mengi lakini mwisho alisema namnukuu "Wananchi wa Mwanza nataka kulibadilisha hili jiji lenu liwe kama Carlifornia" na hii ilikuwa hadharani kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

2. Akifanya mkutano wa waandishi wa habari mwanzoni kabisa, kuna mwandishi mmoja wa kike alimuuliza swali kuhusu nchi kurusu bidhaa duni kuingia na uhai wa manufacturing industry, yeye alijibu huku akijionyesha mtoto wa mjini anaejua mavazi, akaanza kutaja labels za nguo, na mwisho akasema kwa kuwa sio wote wanamudu nguo mpya, basi ruksa watu kuingiza nguo duni

3. HII ilikuwa ile hotuba yake maarufu ya bungeni, watu nchi nzima tunasubiri ripoti ya EPA ataizungumziaje, yeye akatumia muda mwingi kuchekesha watu, top ilikuwa pale aliposema "Kula uliwe"
 
Kwangu his most embarassing speech ni pale aliposema maisha bora kwa kila Mtanzania. Nilijua kutokana na rekodi yake hataweza lakini nikabishiwa, nikabezwa, nikaambiwa JK we acha tu...
 
Ndio tumeliwa ndugu yangu, maisha bora kwa kila mtz menyewe hayazungumzii siku hizi, tukiachana na ahadi hewa nyingi alizoahidi kwa KWAZO MPYA, SHARI MPYA NA JUNGU MPYA! Tusubiri mwakani tena akifanikiwa kuhonga chumvi, kanga, vitenge, kofia na T-Shirt bila kusahau takrima itakayotokana na ule mfuko mbaya sana wa maendeleo ya Jimbo ndio tuhesabu tena maumivu ya awamu ya nne kwa mara nyingine!
 
Kwangu his most embarassing speech ni pale aliposema maisha bora kwa kila Mtanzania. Nilijua kutokana na rekodi yake hataweza lakini nikabishiwa, nikabezwa, nikaambiwa JK we acha tu...

Ndugu yangu hata nchi nipewe mimi au wewe au yule, kamwe haiwezekani kuleta maisha bora kwa KILA mtanzania. Si mtalamu wa Jiographia au siasa au history; naomba kuuliza kuna nchi hapa duniani ambayo KILA mwananchi wake anamaisha bora?....jamaa yangu hapa ananiambia Luxembourg.

KILA mtanzania kuwa na maisha bora ni kazi....haiwezekani. Si kwamba nimekata tamaa kuwa raisi wetu hataweza, nachofahamu na nilivyofahamu tangia hii style ya uombaji wa kula KAMWE maisha bora kwa KILA mtanzania hayataletwa. Inawezekana "kwa kila mtanzania" ina maana yake.

Ni kweli watanzania yatubidi kufanya kazi kwa bidii ili tuwe na maisha bora; lakini kumbuka background ya mtu, mazingira ya mtu, uwezo wa mtu na support ya mtu. Hivi vyota, na mengineyo, yanamfanya mtu kuwa na uwezo wa kujuwa/kufikili ni jinsi gani ya kutatua au ya kuwa na maisha bora. mf Elimu tuipatayo mashuleni, shule nyingi zilizopo Tanzania, si elimu inayoweza kumkwamua mtu pindi aiishiapo kidato cha nne. Haimfanyi mtu awe endelevu. Hebu fananisha contents za mtu wa computer science aliemaliza pale UDSM na yule aliemaliza pale Bath university; je wanafanana? waliandaliwaje walipokuwa primary, secondary au utotoni.

Kwahiyo, HATA NIWE MIMI AU WEWE AU YEYE AU YULE, kamwe haiwezekani kuleta maisha bora kwa KILA mtanzania
 
Hakuna kitu kipya hapa zaidi ya yale yale na watu wale wale na tena mwakani watakuja na nyimbo nyingine, huwezi kuwajaza watu matumaini watu bila ya kufanya njia safi za kuboresha maisha yao na sio Politica kama hivi mzee wangu,
 
..the most embarassing statement ni pale aliposema kuwa serikali ikiruhusu wanafunzi waliojifungua kurudi shuleni matiti yao yatakuwa yakichirizika maziwa madarasani.

NB:

..naomba mwenye ile speech atuletee hapa jamii forums.
 
Nimekubali hiyo kali kwa kweli,too boring!
 
Mimi kilichoniboa ni pale alipodai kuwa hajui kwa nini TZ ni maskini na kabla hata ya kupata jibu la swali hilo ameendeleza umatonya toka nchi za nje mtindo mmoja! Wakati mwenzake Mkapa anasikitika kuhusu matokeo mabaya ya ubinafshaji alioupigia debe wakati wa utawala wake JK anazunguka nchi mbalimbali kutafuta wezi kwa mgongo wa "uwekezaji."
 
Ndugu yangu hata nchi nipewe mimi au wewe au yule, kamwe haiwezekani kuleta maisha bora kwa KILA mtanzania. Si mtalamu wa Jiographia au siasa au history; naomba kuuliza kuna nchi hapa duniani ambayo KILA mwananchi wake anamaisha bora?....jamaa yangu hapa ananiambia Luxembourg.

KILA mtanzania kuwa na maisha bora ni kazi....haiwezekani. Si kwamba nimekata tamaa kuwa raisi wetu hataweza, nachofahamu na nilivyofahamu tangia hii style ya uombaji wa kula KAMWE maisha bora kwa KILA mtanzania hayataletwa. Inawezekana "kwa kila mtanzania" ina maana yake.

Ni kweli watanzania yatubidi kufanya kazi kwa bidii ili tuwe na maisha bora; lakini kumbuka background ya mtu, mazingira ya mtu, uwezo wa mtu na support ya mtu. Hivi vyota, na mengineyo, yanamfanya mtu kuwa na uwezo wa kujuwa/kufikili ni jinsi gani ya kutatua au ya kuwa na maisha bora. mf Elimu tuipatayo mashuleni, shule nyingi zilizopo Tanzania, si elimu inayoweza kumkwamua mtu pindi aiishiapo kidato cha nne. Haimfanyi mtu awe endelevu. Hebu fananisha contents za mtu wa computer science aliemaliza pale UDSM na yule aliemaliza pale Bath university; je wanafanana? waliandaliwaje walipokuwa primary, secondary au utotoni.

Kwahiyo, HATA NIWE MIMI AU WEWE AU YEYE AU YULE, kamwe haiwezekani kuleta maisha bora kwa KILA mtanzania
Kwa hiyo?
 
It is not easy to pick the best from this Soprano.

There was the time he told Tanzanians in New York "Serikali haihitaji hela zenu".

Then kuna pale aliposema "sijui tatizo la Tanzania ni nini"

Then kuna pale aliposema "Tanzania haifanyi chochote tofauti kukabiliana na mchafuko wa mfumo wa uchumi wakimataifa"

Then pale aliposema "Kula uliwe"

Then kuna pale alipo squander his 60 seconds on MSNBC kwa kutaja nchi jirani za Tanzania badala ya kuelezea

Then kuna ile hawkish speech ya "kuivamia Uganda"

And I am sure this is not by far the worst, given my limited access.
 
tatizo la JKanapiga sana story za kijiweni na watoto wake na marafiki wa watoto ndio maana anaweza kuongea pumba kama hio uliotaja "nataka kuibadilisha mwanza kuwa kama california".jamaa hayuko serious na hana kipaji cha kuwa kiongozi kabisa.
 
ni kweli na ndio hayo ya kuchagua rais bosheni kutoka saigoni mpaka ikulu,sasa story zote za kijiweni sasa ndo anatupigia sisi,hajui hata kama yeye ni mshika nchi na kuna maneno inabidi afikirie kabla ya kuropoka,na bado badae usishangae rais akawa komba,au kinje,au tambwe hiza hayo ndo mambo ya nambari wani CHAMA CHA MAFISADI
 
"matiti yao yatakuwa yakichirizika maziwa madarasani"

Pamba zinazolimwa na wakulima wa mwanza, Shinyanga na mara mpaka zinadoda hivi huwa zinafanyiwa nini hasa wakati huu wa credit crunch? Kwanini hao wanaochuruzika na kuchuruzukiwa maziwa madarasani wasipewe bure ili kuwapiga jeki wakulima wa kanda ya ziwa?
 
Ni aidha JK ni mswahili mno kufuata alicho andikiwa kwenye hotuba au hao wanaomuandikia hotuba nao hawajui kuandika. Kama anatoaga speeches spontaneous aache kwa maana siyo kila mtu anayeweza kuhutubia kutoka kichwani kwa mpangilio mzuri. JK charisma inamsaidia sana la sivyo mh...
 
mara nyingi kikwete akizungumza huwa sometimes nafeel embarased

top three ya mazungumzo ya kikwete yaliyo ni disapoint ni hii
1.alienda mwanza mara baada ya kuchaguliwa kuwa rais
alizungumza mengi lakini mwisho alisema namnukuu 'wananchi wa mwanza nataka kulibadilisha hili jiji lenu liwe kama carlifornia ' na hii ilikuwa hadharani kwenye uwanja wa ccm kirumba.
Kwani california ni JIJI or state?
Au alikua anamaanisha mkoa wa Mwanza uwe kama state ya California!?

Kwahio Mwanza iwe kama Bay area.

Mambo si haba basi.

Swali la mwisho kwa JK je amefikia hata 1/8 ya hio California sasa?
 
..................Then kuna pale aliposema "Tanzania haifanyi chochote tofauti kukabiliana na mchafuko wa mfumo wa uchumi wakimataifa"...............

yaani hapo nilichoka kabisa............hivi hajui kuwa hata vipanga huwa wanajiandaa inapofikia ocassions kama zile!!
 
Back
Top Bottom