Hii habari ya kuomba umeipata wapi mkuu? Ivi unadhani bila kuwa na wawekezaji wakutosha tutapiga hatua za haraka? Jk anatafuta wawekezaje kwenye sekta muhimu,,china amepata wawekezaji kwenye reli ya kati,,tusubiri na Vietnam atakuja na wawekezaji wa aina gani ili tupige hatua..acheni kubeza kila kitu hizo nchi za asia mashariki hazikuendelea tu hivi hivi...
huyu rais wetu alianza mchezo huu mapema sana wa kutembelea kila kona ya nchi na watu walipohoji toka awamu ya kwanza wakajibiwa Rais wetu anatafuta misaada.
na safari hizi hazijawahi kukoma na zaidi zinaongezeka kila siku.
hata wewe unanipa picha ya aina ya watu waliopo ambao wanakatisha tamaa watanzania kama nchi ina watu wenye fikra za kulisaidia taifa.
sekta muhimu ni viwanda. safari za Rais wetu sasa zinakaribia kuwa miaka miwili katika miaka 10.
kwa wingi wa safari zote hizo ni kiwanda gani ambacho mpaka sasa kimepatikana kwa mamia ya safari zilizopita?
kama kasafiri ndani ya miaka 9 na hajapata wawekezaji wa maana je huu mwaka mmoja una matumaini kushinda miaka 9 aliyopoteza?
NIMESEMA HAKUNA NCHI ILIYOWAHI KUENDELEA KWA MISAADA.
umetaja nchi za Asia mashariki.
unaweza kunimbia China na India zilipata msaada toka kwa nchi gani ?
Rais Kenyatta alipoingia tu madarakani alipiga marufuku misaada ya nje katika serikali yake na asasi zote za kiraia.
lakini kasi yao ya maendeleo kwa muda mfupi ni yakutisha.
hata mtangulizi wa Kenyatta ambaye ni Mwai Kibaki sidhani kama alifikisha hata safari 20 kwenda ughaibuni ndani ya miaka 10 ya uongozi wake.
na juzi taifa lao limekuwa la uchumi wa kati duniani.
ndio maana wengine wamefikia hatua ya kumuita huyu rais ni RAIS MTALII