Kikwete: Wanaokwepa Kodi hawataacha kirahisi, Magufuli endeleza mapambano

Typical mkwere! He has never been Serious on anything! Strange he ever became president!

kila siku nawalaani kina edo na rostam kwa kutuwekea hiki kimeo kama rais, for 10 yrs tulikuwa na rais hewa
 
kikwete ni raisi aliyeshindwa , haache kujiaibisha kwa kutoa kauli za kushindwa. Yeye alikuwa mfanya biashara na maswaiba wake wote ni wafanya biashara utawezaje kukusanya kodi kwa marafiki zako. Magufuri ni mtu wa kazi hana urafiki na mtu katika kazi

...lkn hata magufuli na majaliwa na samia walikuwa ni marafiki zake pia...!uhalifu ni uhalifu tu...! lkn uhalifu mbaya ni uhalifu wa roho...wivu, majungu, husuda.....!
 
Hana huzarendo wowote kikwete. Alikwenda Ikulu kutimiza ndoto zake, NA SIO KUENDELEZA TAIFA. Siasa imemjaa, vijembe sana. Anajiaibisha tu, acheni kumtetea.
 
moja ya mambo ambayo MUNGU amemjalia jk ni ana ngozi nene ajabu. mtarusha mishale kutoka katika ndimi zenu zilizojaa sumu kali lakini ndo kwanza anatabasamu. bila shaka ataishi maisha marefu.
MUNGU akubariki mzee wetu jk.
 
Hili swala la kodi za Tanzania si rahisi kama linavyozungumziwa.

Kila ninayemsikia anasema wengine walipe kodi, wafanyabishara wakubwa walipe kodi nk. Lakini kodi za Tanzania ni kama ifuatavyo:

1. Kodi ya Mapato ambayo wanalipa wale wanaolipwa mishahara tu na baadhi ya wanfanyabiashara. Hakuna mkulima anayelipa kodi hii.

2. VAT ni 18%, kwa kiwango hicho hiyo kodi wa mauzo hailipiki. Kama kweli sisi wote ni wazalendo basi kila muuzaji wa bidhaa au huduma anatakiwa atoze hiyo kodi, muuza karanga, muuza sigara, kinyozi, mama lishe, wenye grocery nk. Hizi kodi mbili zinaweza kuongeza sana mapato ya serikali kuliko bandari nk.

Lakini sisi Watanzania "wazalendo" tunataka wengine walipe kodi hakuna ambaye yuko tayari kulipa yeye mwenyewe. Kisiasa CCM haitaweza kuwatoza kodi wakulima kwa vile "Uhuru" ulipiganiwa kwa mwangalio wa wakulima ili wasilipe kodi ya kichwa ya mkoloni. Serikali ipime ardhii ya nchi nzima, wote tulipe "Land Rent" na "Property Tax". Tuone makusanyo yatakuwa kiasi gani? Takriban 10% ya Watanzania ndiyo wanaolipa Income Tax, hii haitoshi.

VAT ya 18% hailipiki, iteremshwe kuwa 5% kwa bidhaa za ujenzi, 10% kwa bidhaa zingine na 15% kwa bidhaa za anasa. Halafu ndiyo wafanyabiashara wote walazimike kutumia EFD.

Lakini wote kwa pamoja tunaimba nyimbo za kushabikia "Wafanyabiashara Wakubwa". Kwa taarifa tu, wafanyabisha wakubwa wanakuwa na wahasibu wao binafsi ambao kazi yao ni kuhakikisha wanalipa kodi kidogo iwezekanavyo, na hii ni dunia nzima.

Mapato ya Serikali na Utajiri wa Nchi unatokana na Tabaka la Kati "Middle Class" na siyo Economic Elite au Lower Classes.
 
Hivi Kikwete kwani lazima uongee kwa sasa? Busara kwako ni kukaa kimya!
Hawezi kukaa kimya wakati hajui kesho linatumbuliwa jipu la sehemu ipi. Mwili umetapakaa majipu kila kona, umemskia mwenyewe akiwataja mwanae na mkewe.
 
Watanzania bwaana, huyo huyo jk mlimchagua kwa mbwembwe kama huyu magufuli ni muda mtakuja kula matapishi yenu

Nawajua nyie kabila la wa Mmawia wachawi sana lazima mtakuwa mmefanya mazindiko ya Chui ili kupunguza spidi ya JPM....tutawarudisha kwenu 'Nchumbiji'
 
Kuna wale waliopata tuzuwadi twa IPTL kupitia Mkombozi bank waliombwa na aliye kuwa naibu waziri wa fedha M. Nchemba walipie kodi zawadi walizopewa. Mbona wale walio pewa kupitia stanbic hawakuambiwa walipie kodi zawadi zao?
 
Leseni za biashara zitolewe TRA, na ziwe zinantolewa kila mwaka kama Motor Vehicle Licence. Na kwa vile leseni hizo zitahusisha TIN na namba ya simu na GPS coordinates za bishara hiyo itarahisisha ukusanyaji wa kodi kwa wale wakwepaji.

Pia kila aina ya leseni itakuwa na kiwango cha chini cha Income Tax. Ukusanyaji wa Business Licence uende pamoja na ukusanyaji wa Income Tax.

Hivyo kwa watati wowote ule TRA watafahamu ni kiasi gani cha kodi kutegemewa na ni wakina nani bado hawajalipa, kama MVL. Leseni za Biashara kutolewa kwenya mamlaka za halmashauri ni kosa na chanzo cha rushwa na ukwepaji kodi.
 
Kalale mzee,hufai mzee,sijui umekula maharage ya wapi wewe.ni naaaaani aliyekuroga
Unaweza kusema hukubaliani na maoni take,lakini una haki ya kumtukana mzee WA watu - Uhuru WA kuandika chochote kinacho kujia kichwani usipitilize mipaka,waheshimu watu walio kuzidi umri,usijifanye mjanja ukajidanganya kwamba uwezi kufatuliwa na kutiwa mbaroni kwa kukashifu watu. ...been warned.
 
huyu jamaa akitumia vizuri kiaji chake anaweza kumfunika mzee yusuph!
 
Back
Top Bottom