Kikwete vs Wenje - Mwanza mjini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete vs Wenje - Mwanza mjini

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mamboleo, Oct 26, 2010.

 1. M

  Mamboleo Member

  #1
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 69
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 15
  Jioni hii kuna mikutano miwili mikubwa jijini Mwanza.

  JK ametua kumpigia debe mgombea wake wa CCM Laurent Masha dhidi ya Wenje wa CHADEMA.

  Ujio wa Dk.Slaa pamoja kampeni ya nguvu dhidi ya mgombea wa CCM imemfanya mgombea wa CCM kutokukubalika kwa wananchi wa jimbo la Nyamagana.

  Ama kweli siasa za mwaka huu ni kali maana huyo Wenje amewakosesha usingizi wana CCM kwani hivi karibuni Waziri Benard Membe,Lowassa na Ridhwan Kikwete walifika hapa kujaribu kubadilisha upepo wa kisiasa ambao ni mbaya kwa CCM.

  Leo usiku inasemekana JK ana kikao na viongozi wa dini mkoa wa Mwanza baada ya ziara ya Membe ya kutaka kuongea na waisaidie CCM Nyamagana kushindwa.
   
 2. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  hiyo haitosaidia wananchi HAWADANGANYIKI TENA imekula kwao, hata wakeshe wakisali na kuabudu na kutambika juu imekula kwao hiyo.......:rip: CCM mwisho wenu ni 31-10-2010
   
 3. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  aaaaaaah,me natamani niwaulize viongozi waliopo madarakani na wanao ondoka kwa nini wana ruhusu uchochezi wa kidini unao fanywa na gazeti la al-huda kila siku
   
 4. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  I am sorry JF, siamini macho yangu kuwa ni kweli Jamaa karudi tena Mwanza, ninachokumbuka ni kwamba tayari alishaenda Mwanza, kama nakosea naomba kurekebishwa. Kuna nini huko? lazima mwanza tu??? JK, tueleze
   
 5. E

  Edo JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Kuna mwanafunzi wa SAUT (alikuja ofisini kwetu) anasema Lau alienda kupiga kampeni na kumponda Wenje, bahati mbaya akajikuta imekula kwake na kulazimika kushuka jukwaani kwani wananchi(wapiga kura) walimzomea
   
 6. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Kuna mwananchi wa Nyamagana nilikutana naye jana ansema hali ni ngumu sana kwa Masha. Wananchi wameweka wazi hawamtaki Masha hata kwa dawa!!

  CCM hawana jipya. They have to let it go and go back to the drawing table to re-startegize!!!:bowl:
   
 7. T

  The King JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr Slaa kokote kule uliko hakikisha unarudi tena Mwanza kufanya vitu vyako ili kuhakikisha chadema inauteka mkoa huo.
   
 8. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa jinsi ninavyojua Nyamagana hawaongozwi na mbuge vipindi viwili, kama Masha atalazimisha basi akipata tu asionekane jimboni kabisa. Vinginevyo, watamfanya kama yule kabla yake.
   
 9. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Niijuavyo MZA mimi, hata angekuja na nec nzima sisiemu hawana lao mwaloni. Labda kwa yule bwana wa star tv naye wanachagua m2 siyo chama! Maji ya shingo hayo!
   
 10. Aza

  Aza JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2010
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 1,672
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  kwa ufupi mwanza hatulali kwa izo kelele za kujinadi since last week
  watu wanaweweseka sana,,,ngojeni matokeo ya leo!!
   
 11. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Usicheze na watu wanaokula samaki wa maji baridi.

  Ubongo wao hauna chumvi (hawali pweza wa maji chumvi)
   
 12. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,628
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 160
  Wananchi wa Nyamagana sio wajinga kiasi hicho kuona kama Masha anawatumia kwa manufaa yake zadi. Huyu alikataliwa toka 2005 ikalazimishwa kuwa yuko karibu na JK na ataupata uwaziri. Hakupata ubunge kwa utashi wa wananyamagana. I guess they were right. Kama waziri kuna kitu anachoweza kujivunia kama kiongozi zaidi ya routine work ya kusaini vocha, kujibu maswali bungeni. Kuna kitu anachoweza kujivunia kama WZ Magufuli? Badala ya kutumia nguvu nyingi ni vizuri kuheshimu maoni ya wananchi.
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  poa.. hii ni habari njema kwa lau
   
 14. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,668
  Likes Received: 21,901
  Trophy Points: 280
  Leo habari zilizopo ni kuwa vijana kwa wazee wengi wamejitolea kuwa mawakala wa Wenje hata kama kutakuwa hakuna malipo yeyote kwao,wako tayari kwa ulinzi wa kura. Wapambe wa Masha wanaendelea na vikao visivyo rasmi Mwanza Hotel na Mwanza Institute Club kutafuta njia za kunusuru anguko hili.
  Nadhani kinachotafutwa sio ushindi tena ila kunusuru asishindwe kwa aibu kubwa. Wamekata tamaa.
   
 15. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #15
  Oct 26, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,799
  Likes Received: 6,307
  Trophy Points: 280
  Naomba kufahamishwa - huyu Ridhiwani Kikwete ana nafasi/cheo gani ndani ya CCM/Serikali ya Baba yake??
   
 16. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Kwa nini asiwaite kina Lowassa, Karamagi, Rostam na Chenge wamuongezee nguvu kwenye Kampeni?
   
 17. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,504
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  I like Riz1 kwa vile ametusaidia kwenye ushindi!!!
   
 18. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #18
  Oct 26, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mwaka huu atachezza sindimba mpaka achoche lakini ni CHADEMA tu, Mungu naye yupo Upande wetu
   
 19. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #19
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Masha - it is QED - rudi IMMMA(+ Karume+Kikwete+Chenge) uendelee kuwatetea MAFISADI
   
 20. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #20
  Oct 26, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Mungu amesha tuvusha kwenye matope, nawashangaa wasio jua kuwa tuko mbali kwa sasa.
   
Loading...