kensh
JF-Expert Member
- Jul 19, 2012
- 527
- 113
Uliingia kwa falsafa nzuri sana iliyotujaza matumaini. ARI Mpya,Nguvu Mpya na KASI Mpya. Ukanikosha sana pale ulipotuletea mabilioni ya KIKWETE. Ingawa sikujua yamefikia ofisi gani na nani ameyapeleka wapi na kufanya nini ! Ila niliamini ipo siku utatuma mabilioni mengine na yatanifikia.
Tukaamini kuwa mambo yatakua murua,swadaktaa au shwaaariii !
Taratibu tukaanza kuona kiza kinainyemelea falsafa yako.Yakaibuka mambo ya ajabu,RICHMOND,BUZWAGI,MEREMETA na funga mwaka 2014 ESCROW. Tukajua ungechukia na kuwatimua haraka waliopiga dili,ila ukaanza kuuzunguka na hata kujaribu kuukumbatia MBUYU !
Tulishuhudia watu wakianza kujadili na kujigamba kwa UDINI . Wengine wakawamwagia wenzao tindikali na hata kuwauwa kwa risasi na mabomu eti kwasababu sio watu wa DINI yao,hivyo hawafai kuishi !
Watu walienda katika nyumba za ibada wakiwa na hofu kubwa, nyumba za ibada zilichomwa na hakuna aliyekamatwa!?
Sasa kumezuka panya road,mbwa mwitu na wametunyima raha na wakataka hata kuyumbisha jeshi la polisi.Polisi walijikanganya kwa kauli zao walipojaribu kujibu kama kweli kuna panyaroad au la !
Mbaya zaidi, unakaribia kuondoka ofisini ukiwa unaacha tatizo la Polisi kuvamiwa na kuuwawa na hata kunyang'anywa silaha.Hatujui silaha hizo zipo kwa nani,zinafanya nini na kwanini?
Hayo yoote tisa,kumi ni hili sakata la UGAIDI. Vyombo vya usalama vinasema kuwa wale waliolianzisha timbwili kule tanga eti ni wahuni na si magaidi! wanamliwaza nani ? au wanakuliwaza JK ?
Hivi wahuni wanaweza kumuua mwanajeshi na wasikamatwe?! Hivi inawezekana muhuni akafungwa pingu na kumtoroka askari mwenye mafunzo thabiti? Kuna ubaya gani UKWELI ukisemwa ili watu wamtafute nyoka aliyemo chumbani mwao badala ya kutoa lugha zinazofanya tatizo lionekane ni dogo?
Kuna nchi zilipuuza matukio kama haya,zikasema kama sisi tunavyosema leo.Zikadai ni wahuni tu. Leo kule Nigeria kundi lililoonekana ni la kihuni miaka ya 2000,limegeuka kuwa BOKOHARAMU na sasa ni shiidah !
JK usipuuze mambo haya, vinginevyo utatuacha na vitu kama ISIS, BOKOHARAMU,AL SHA BAAB nk
Fanya hima utuache shwari kama ulivyotukuta,hatutaki UDINI ambao umekua ndiyo sababu ambayo vikundi vya MAGAIDI vinaitumia kuanzisha na kuhamasisha vurugu.
JK UNATUACHAJE ?