Kikwete Umekosea Mno! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete Umekosea Mno!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Wa Ndima, Oct 2, 2010.

 1. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Wote tumesikia au kusoma kuhusu tamko la Jeshi kuhusu Uchaguzi Mkuu wa 31 October, 2010.

  JWTZ kutoa angalizo hili ni kujidhalilisha ingawa ninaamini kabisa kuwa amri hii imetoka kwa KIKWETE akiwa kama Amiri Jeshi Mkuu watoe tamko hilo. Kwa nini, na kwa wakati gani kama hatujafikia kipindi hicho cha vurugu kiasi kwamba Jeshi la Polisi Tanzania limeshindwa? Basi watwambie kama hakuna Jeshi la Polisi Tanzania kiasi cha wao kutoa angalizo hilo.

  Huku ni kutisha wananchi katika haki yao ya msingi, ni kupumbaza watu na kuwafanya wajinga uendelee kutawala. Kikwete ukiwa kama amiri jeshi mkuu kwa wakati huu kabla ya Oktoba 31 umekosea sana na tumekutambua wewe ni mtu usiyekubali kushindwa, kwako ushindi ni lazima. Unadhani itakuwa rahisi kihivyo?

  Watanzania wasiotaka mabadiliko na maendeleo kwa nchi yao wataichagua CCM, lakini ikumbukwe kuwa ni hiyohiyo CCM iliyotufikisha hapa kwenye umasikini huu mkubwa tulionao. Ni hawahawa walioshindwa kudhibiti mfumuko wa bei. Ndio hawahawa wanaotuletea uchungu na shida katika nchi yetu wenyewe. Wakoloni Weusi, ndugu zetu,jamaa na rafiki zetu wa tangu udogoni.Wananchitwendeni tukapige Kura kisha tuzilinde kura hizo dhidi ya madhalimu. Tusikae jirani ya vituo vya kupigia kura ila mbali na eneo la kupigia kura na kuchukua tahadhari kwa yeyote atakayekwenda eneo la kuhesabia kura baada ya muda wa mwisho wa kupiga kura hasa kipindi cha kuhesabu kura hizo. Najua Polisi watamwagwa kuhakikisha mmerudi majumbani nafasi ambayo wataitaka sana, jigaweni katika zamu zenu kulinda haki yenu mpaka kieleweke, msiamini mawakala pekee nao ni binadamu, kila mmoja awe mlinzi wa kura yake. Je wataweza kutuhonga sote?

  Kama kuumia kwa miaka mingine mitano tutaumia sote na kizazi chetu. Tusifanye makosa tena

   
 2. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #2
  Oct 2, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kwani wewe ni mgeni wa huyu jamaa? Maana kila wakati yeye ni kukosea. Nadhani ni kutapatapa tu maana ameona watu wamekigeuka chama chake na hawana imani naye na serikali yake.
   
 3. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #3
  Oct 2, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  hivi , kuna wiki inapita bila jk kuongopewa au kuingizwa mkenge na washauri wake
   
 4. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #4
  Oct 2, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Anguko kuu linakuja
   
 5. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #5
  Oct 2, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Walidhani ujio wa Dr Slaa ni mbwembwe tu! wakachomeka upadri na kutumwa na kanisa, watanzania wakasema No,no! wakachomeka ndoa na maisha binafsi,Watanzania wanazidi kusema No,no, no! CCM wameangalia upepo na kutambua wazi kuwa ushindi 2010 ni mtihani. Ndio maana wamealika taasisi nyeti. Ni wiki moja tu iliyopita Mwenyekiti wa NEC amesifu kampeni kuwa za kistaarabu na zisizo na fujo, huyu ni Jaji Makame! Sasa Luteni Kanali Shimbo anaposema amani inavunjika atueleze wapi, vinginevyo katumwa na boss atishe watz.
  GO WAPINZANI GO!
   
 6. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #6
  Oct 2, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Noted
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  Oct 2, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mkuu umenena vyema kabisa. unisome kwenye bold yako.
  Kama vyama vya upinzani vinasoma hapa, wajipange vyema na mawakala wao kwani inawezekana hizo kura zisiletwe bali zikawa zimeingizwa kituoni usiku wake au jana yake. Hivyo kabla ya kupigwa kura mawakala wakague vituo vya kura chini ya uangalizi wa polisi na waangalizi kuhakiki emptiness na uhakika wa masanduku yaliyopo. Mwaka huu kuna vioja vingi vitatokea. kuna watu wameapa kuwa hatoki mtu hata kama tukisema nooooooo!!!!
   
 8. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #8
  Oct 2, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Nimekusoma sana
   
 9. Mchizi

  Mchizi JF-Expert Member

  #9
  Oct 2, 2010
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 675
  Likes Received: 847
  Trophy Points: 180
  mwache ajidanganye kutegemea jeshi, lakini lazima ajifunze kwa kuangalia nchi nyingine nazo zilikuwa na majeshi kama yeye
   
 10. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #10
  Oct 2, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  The Following User Says Thank You to Wa Ndima For This Useful Post:

  Msanii (Today) ​
   
 11. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #11
  Oct 2, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Mwanzo nilidhani utani Jamaa kuanguka ila kwa sasa naona mzee wa Kaya anazidi kuongeza urefu wa shimo lake mwenyewe.
   
 12. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #12
  Oct 2, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Sisiem ni ya kukemewa kama PEPO.
   
 13. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #13
  Oct 3, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nguruvi3; Your amnalysis is very good.
  Walidhani ujio wa Dr Slaa ni mbwembwe tu! wakachomeka upadri na kutumwa na kanisa, watanzania wakasema No,no! wakachomeka ndoa na maisha binafsi,Watanzania wanazidi kusema No,no, no! CCM wameangalia upepo na kutambua wazi kuwa ushindi 2010 ni mtihani. Ndio maana wamealika taasisi nyeti. Ni wiki moja tu iliyopita Mwenyekiti wa NEC amesifu kampeni kuwa za kistaarabu na zisizo na fujo, huyu ni Jaji Makame! Sasa Luteni Kanali Shimbo anaposema amani inavunjika atueleze wapi, vinginevyo katumwa na boss atishe watz.
  GO WAPINZANI GO!

  Keep it up
   
 14. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #14
  Oct 3, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  mwenye akili zake anajua nn cha kufanya, mm nitawashangaa wananchi ambao baada ya kupiga kura watabaki vtuoni iwe mbali au karibu kwa dai la kulinda kura

  na ninawashangaa wenye kuwashawishi wananchi kubakia kwa dai hilo hilo

  wanataka kuwaingiza wananchi kwenye matatizo na vyombo vya dola makusudi, wao watakuwa wametimiza matashi yao kisiasa na kuchafua jina la nchi yetu, ila wananchi watakuwa wameumizwa kwa kuhatarisha amani, na maisha yao yatakuwa hatarini

  nakumbuka vyema CUF walipowatumia wananchi kuwa kama ngao yao ya kufanikisha ajenda yao, wananchi wengi walikufa, walikua vilema na kuhama nchi kwa matashi ya watu wachache

  jee sasa malengo yao yamefanikiwa wamewakumbuka walioumia kwa matashi yao ?

  nasisitiza hakuna haja ya kuhatarisha maisha ya wananchi huku sote tukijua kwamba:-

  kila chama kimepewa nafasi ya kuwa na mawakala wa kutosha kwenye vituo vya kuhesabia kura(kitu ambacho kama kuna udanganyifu wataripoti kwa vyama vyao)

  kutakuwa na wasimamizi wa ndani na wa nje kushuhudia jinsi gani uchaguzi unavyoendeshwa na mwisho watatoa ripoti zao ambazo kila mtu anaamini wataeleza mapungufu na matimilifu ya zoezi zima

  wagombea watatakiwa kusaini matokeo katika vituo vyao kukubali kushinda au kushindwa na kama kweli kuna dhuluma wagombea watakataa kusaini

  sheria zipo ambazo tumezitunga kwa kushirikiana ni nn cha kufanya baada ya matokeo kutangazwa na haujaridhika

  sasa nani anaweza kutwambia kuna mchango gani wa hao wananchi watapokaa nje ya kituo iwe mbali au karibu na uhesabuji wa kura na kulinda kura?


  tuwe pamoja kudumisha amani ya nchi yetu na tusiwe wapuuzi na wajinga au kubomoa nyumba yetu kwa kuchochewa na wageni au nyumba za jirani
   
 15. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #15
  Oct 3, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Unajua JK anajua fika october 31 ataangukia pua so solution ni kuchakachua kura.
  Sasa kamwomba Shimbo asaidie kupiga bit ila watu ata kama hawataridhika na matokeo wawe watulivu.
  JK anashindwa soma alama za nyakati kuwa kuna watz wako tayari kufa kwa ajili ya kutetea haki yao.
  Ni kujiandaa na chemli za kutosha ili wakikata umeme kwa ajili ya kuchakachua watu mwawasha chemli niko tayari ata kuweka silence gari yangu ili mwanga wa taa utumike kuhesbia kura.
  TUMECHOKA KUONGOZWA NA WATU WASIOTUJARI
   
 16. Homo Habilis

  Homo Habilis Senior Member

  #16
  Oct 3, 2010
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 189
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimekusoma.! lakini naona nawe ni uko na hiyo system ya kutaka walio wengi waendelee kuumia na uongozi usio na manufaa kwao. Hongera kwa hilo mTu wa Pwani.
   
 17. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #17
  Oct 3, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  wahtever the case it is, tufate taratibu ambazo ni kweli zitasaidia na sio kuleta upuuzi

  kazi yetu kuu ni kuwahmiza wakapige kura, wasiuze shahada na wampigie wanaemuona anafaa na hapa si vibaya mkajinadi ati nyie hasa mnafaaa

  baada ya kupiga kura muwashukuru na muwambie kazi yenu imeisha na sasa ni kazi yetu kulinda kura zenu na subirini mushangirie hilo ndio jukumu la chama chenye akili sio kuwaangamiza wanachama wake wakijua nn kitafuatia

  mbona wao hawakai vituoni baada ya kupiga kura ?
   
 18. Homo Habilis

  Homo Habilis Senior Member

  #18
  Oct 3, 2010
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 189
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Haina haja hiyo itakuwa ni sawa na kujidhulumu tu kama una wasi wasi hutatendewa haki inabidi ujilinde dhidi ya hiyo dhulma mimi sioni vibaya iwapo watu watakaa mbali na kituo kwa madhumuni hayo ya kuwa asiingie mtu au kikundi chochote baada ya muda wa mwisho wa kupiga kura na sio lazima kila mpiga kura akawepo inaweza kuwa hata watu wa2 au wa3 tu ili kuwahakikishia wengine imani zao, unajua jambo moja kuu ni kwamba watu wamekosa imani na uongozi wao hivyo wana shauku ya kutaka mabadiliko na wako tayari kubadilika hiyo ni vyema wakaamini kile wakitakacho kuwa kiwe na hata kama kisipokuwa basi kimefanyika kwa haki, lakini sio kuwaambia wamwage damu au walete vurugu Tanzania sio nchi ya mambo haya mabaya abadn.
   
 19. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #19
  Oct 3, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  bado sijakuelewa, wao wanasema wakae wote, halafu hao waili si weshakuwamo kwenye vituo kama mawakala na wanajuana itakuwaje aje wa nje wasimtambue. huyo wa nje atawezaje kutofautisha akija observer na wizi wa kura? sioni logic ni kuwasumbua tu na kama watu wawili watatu kuna haja gani ya chama kutangaza si wawateue siri na wafuatilie kisiri siri

  huwaamini viongozi wepi ? wachama chako? maana wao ndio walioteuwa mawakala wenu, au tume ? kama tume kwa nn uliamua kuingia kwenye uchaguzi?

  hawa wanatafuta visingizio vya kuleta vurugu na kwa hilo katu nchi haiwezi kuwavumilia
   
Loading...