haa mym
JF-Expert Member
- Jul 7, 2014
- 4,832
- 4,627
Mkuu wasipoelewa na hapa basi yaani umeeleza kinagaubaga hilo lipo wazi na ndio maana walikua wanasema ataongozwa na "remote from msoga" Nashangaa leo hii wanatubadilikia kwamba JPM sio chaguo la JK. Wakati Magufuli mwenyewe hakuwa hata na wazo la kuchukua fomu JK ndio kamwaambia tena kwa masharti afanye "kimya kimya" na SHOW kaisimamia mwanzo mwisho JPM mwenyewe hakuna alichokua anajua siri za ushindi alikua nazo JK,Kinana na akina Mangula ivi wanafikiri JK angeamua Membe awe rais ingeshindikana nini?Acha waendelee kujifariji, akiaga Mabalozi wanaowakilisha Afrika nchini China Jk alinukuliwa akisema Amechoka kazi ya Urais anatamani siku zuende na akasema atakuja Rais kijana kwa maana ya umri kama wake wakati anaingia (55) mchapakazi kuliko yeye. Tangu kuanza mwaka 2015 miradi yote ya ujenzi alienda kuifungua huku akimsifu sana.
Benard membe aliwekwa kama chambo muda wote bila hata ya Membe mwenyewe kujua ili kuwazubaisha akina Bashe waliotumia nguvu,resource na maarifa yao yote kumuandama Membe na kumuacha Magufuli.
Jina la Membe na January yaliwekwa kwny 5 bora kwa makusudi ili kuwa frustrate team Lowassa waache kushinikiza kurudishwa lowassa badala yake watumie nguvu nyingi kumtoa Membe na January na walivo kichwa maji walipokutana tu St Gasper ili kugomea Zoezi akapelekwa Muhindi na Pesa pale wakavurugwa wakaacha kujadili hoja walizopangiwa na Kingunge ikiwemo kupiga kura ya kumkataa Mwenyekti kwny NEC ikishindikana wote wasuse hivyo akidi isingetumia kwa kuwa 70% ya NEC walikuwa watu wa Lowassa.
Kamati kuu ya CCM kila jina ililoweka ililiweka kwa sababu na hata karatasi ya kura aliyopewa Lowasaa kwny NEC iliwekwa alama ya kutambua atakuwa kampigia nani na ikajulikana baadae na JK akasema baadae kuwa mchakato ulikuwa sahihi na ndio maana wakapiga kura na Lowassa akapiga kwa kumchagua JPM
Sema CCM wanacheza ngoma wanzopigiwa kwa wakati huu ilibidi wampate Magufuli ili kurudisha matumaini kwa wananchi yalikaanza kupotea. Na Magufuli anamuhitaji sana JK sababu ndio Mfumo uliomuweka pale kama ilivyokawa kwa JK miaka yake ya mwanzo akina Rostam na Lowasa ndio walikua wanamcontrol lakini baadae alijua mfumo akawatumbua na kuwa na mfumo wake hata JPM baada ya miaka 5 ndio anaweza kumtumbua JK.