Bongolander
JF-Expert Member
- Jul 10, 2007
- 5,067
- 2,220
Dialogue ndio mpango mzima katika upatikanaji wa AMANI katika nchi hizi za mziwa makuu.... Mkuu wa Kaya amezungumza bila kumung'unya maneno!
Katika mambo ambayo naweza kusema ni lazima tumsifie Rais wetu, ni hasa pale anapotoa kauli za kiutu uzima ambazo ni measured. Nilimuona JK ni true statesman alipozungumzia mgogoro wetu na Malawi, na kumuita Joyce Banda, my sister na kufuatia na maneno very diplomatic, tofauti na baadhi ya wanasiasa waliokuwa wanaongea pumba huku nyumbani.
Hili la Rwanda, tutake tusitake, tupende tusipende roundtable ni lazima iwepo, otherwise there is another genocide in making. Kama RPF wataendelea kuwa manunda kwa kuwa sasa wako madarakani, yanaweza kuwakuta sikumoja yaliyomkuta Habyarimana. Kama hawataki kuongea sasa wanachotaka ni nini? kuwaua wote? au kuendelea kulia kila siku kila siku genociders? On this i will give my president a big thumb up.