Kikwete: Nisingepewa Elimu na Kanisa ningekuwa nafanya biashara ndogondogo Chalinze!

Kumbe kanisa Katoliki ndilo lilimsomesha hadi kafika hapo eeeeh ama kweli hii shule nzuri sana inabidi nasi tujipange...

Sioni historia tofauti ama kitu exceptional ktk elimu yake kiasi kwamba iwe ni sifa kwa kanisa badala ya babu yake chief alomlea na kumpa elimu hiyo..Hawa ndio watu wanaoshindwa kumshukuru Mungu au wazazi wao wakawapa sifa watu wasiostahili..

Jamani, sisi wote tumepata elimu ktk shule hizi hizi ambazo zilikuwepo katika mazingira tuliyokulia..Kama isingekuwepo shule ya Katoliki ingekuwepo shule ya AgaKhan au mfanyabiashara mwingine. Yaani leo hii Mkandara nende kumsifia Agakhan kuwa ndiye mwokozi wangu badala ya mzazi wangu aliyepiga jembe na kujinyima kihakikisha napata elimu hiyo!..

Pengine JK angekuwa mbora zaidi kama angekuwa kituo cha mabus ya Chalinze akiuza biashara ndogo ndogo kuliko mtu aliyepata elimu kisha akashindwa kuongoza..Na sidhani kama tutalitendea haki kanisa tukianza kulilaumu kwa shule waliyompa Muislaam huyu..maanake hafai!


Mkandara,

Hapo juu umenena, JK anafnya kazi ambayo si stahiki yake - angekuwa more effective and productive km angekuwa Chalinze bus stand.

Kikubwa zaidi ulichobayanisha hapo para ya kwanza juu ni ukweli kwamba the pres has failed to deliver.... yupo yupo tu akikenua meno.

Ni achievement gani atayojivunia nayo in his presidential term?
 
Sioni historia tofauti ama kitu exceptional ktk elimu yake kiasi kwamba iwe ni sifa kwa kanisa badala ya babu yake chief alomlea na kumpa elimu hiyo..Hawa ndio watu wanaoshindwa kumshukuru Mungu au wazazi wao wakawapa sifa watu wasiostahili!

Mkuu naona ni kweli alipewa elimu na shule sidhani kama ni baba yake. Inawzekana baba yake alipenda mwanawe apate elimu alifanya kila analoweza kuona Jakaya anakwenda anakopenda aende just opinion. Na wasiosoma leo huwa hawawalaumu wazazi wao kwa kuwa siio wao wenye elimu, elimu iko shule.
 
Ngoja nikuelimshe kwanza: Waislamu hawaiti mtu anayeamini Mungu Kafiri. Huyo Mkapa anaamini Mungu.


Wewe Shamu be liberal na muelimishaji wa jumuia. Acha uchochezi wa kijinga mimi mwenyewe muislamu sichochei upumbavu ambao unaujua wewe be creative ndivyo watanzania walivyo na wanavyosadikika nje ya nchi.
 
hapo kikwete alikuwa anauza sura enzi zake kwa hiyo kusema kasomeshwa na kanisa katoliki ilikuwa mtaji mkubwa kwake mpaka akabadilishiwa jina badala ya kikwete wakamwita chaguo la mungu''YOU CAN LIE SOME PEOPLE SOMETIME BUT YOU CANT LIE ALL PEOPLE ALL THE TIME''Kikwete upo??????????????
 
Nyerere ndiye aliyesababisha Waislamu wasipewe Elimu. Jina lako likiwa la Kiislamu unakatwa ili usiende shule. Waliosoma ni wale tu ambao walitumia majina ya vitu; kama Kikwete, Malima,Kitu, Kigoda nk.

Unajua wakati mwingine ukisoma post ya mtu unagundua uwezo wake wa kufikiri. Sasa Nyerere angeweza kuwatoa watu Madrasa akawapeleka kwenye Elimu Dunia?

Umesikia wapi kwamba wenye majina ya kiislamu walikuwa wanakatwa? na ni nani aliyekuwa anawakata?
 
Ninaomba viongozi wa BAKWATA wanionyeshe na kunifahamisha :
-Angalau shule moja waliyopora na wanayomiliki hivi leo inayoendeshwa vizuri.
-Shule moja ambayo ada za wanafunzi haziporwi na masheikh wakuu na walimu wanalipwa mishahara yao kwa wakati.
-Hawajachemsha kwa Chuo Kikuu kimoja tu walichopewa majengo bure na serikali,
-Shule au vyuo visivyoajiri watoto wa mjomba au shangazi na badala yake vinaajiri watu bila kujali dini zao, rangi, jinsia n.k. ila ubora wao kama walimu tu,
-Nani anaua Redio Quran kama sio viongozi wenyewe wa Bakwata,
-Kijihospitali kimoja cha Bakwata kinachoendeshwa na chenye matumaini ya kuwa hospitali kubwa baada ya miaka mitano hivi.
-Orodha ya viongozi wa juu wa BAKWATA na elimu zao,
-Kama wana orodha ya juu ya viongozi wa Makanisa na elimu zao na kama wamejifananisha nao?
-Msikiti hata mmoja unaoendeshwa kwa tija ukawa na manufaa kwa muumini wa kawaida na sio kwa viongozi wao tu,
-Wilaya yoyote Tanzania yenye mradi wa maana wa Waislamu unaotoa huduma za kijamii kama elimu, afya, mazingira, maji, umeme na kadhalika ?
-Fedha za majengo ya wakfu zilipo na zinavyotumika ?
-Orodha ya misikiti, viwanja au ploti zote za misikiti na Waislamu nchini na kama zina title deeds?
-Mradi wa BAKWATA kuwafundisha Waislamu vijana wanaopenda sana kujifunza masula ya Information, Communication Technology (ICT)
-Jambo lolote KUBWA NA LA MAANA linalofanywa na Waislamu hapa nchini ukilinganisha na yale yanayofanywa na dini nyingine.

Majibu ya maswali hayo hapo juu yakipatikana nina hakika yatakionesha kidole pale panapostahili kulaumiwa.

Uislamu unaweza kweli kusaidiwa kwa dua na kunuti, lakini, kunuti kubwa kuliko zote ni ile ya Waislamu kubadilika na kumgeukia kikwelikweli Mwenyezi Mungu ili awaongoze na wauone udhaifu mkubwa ulio ndani ya dini na imani yao unaotokana na:
-Kukosa umoja;
-Kutoshirikiana;
-Kutokuwa au kutokukubali kuwa na viongozi waliosoma kidunia na wanaoona mbali na mbele,
-Kutotanguliza ubinafsi mbele,
-Kujifunza kutoka dini zingine,
-Kutokuwa na muundo unaowaongoza Waislamu na kukubalika toka chini hadi juu,
-Kula, kuiba na kutumia vya Beit-ul -Mal,
-Kutotoa zaka wala michango mingine ya kuendeleza miradi ya Waislamu ili kutoa ushindani wa uhakika unaoweza kutuweka mahala ambapo nasi tunaweza kuandikiana MoU na SMT,

Sharrif,

Maneno mazito sana Mkuu. Yananikumbusha maneno ya mwisho wakati anaaga kutoka Post ya PM wa Malaysia, bwana Mahathir bin Mohamad. Huyu jamaa alikuwa akitema CHECHE kali sana kwa Waislaam ili wabadilike na wawe wachapa kazi haswahaswa. Aliibadilisha sana nchi yake.

Kama Kikwete alisomeshwa na kanisa au hakusomeshwa, hilo ni tatizo lake binafsi. Kuna vitu ambavyo hata usomeshwe wapi, bado utabaki vilevile. Ni kama DNA ya mtu.
 
Mkandara

Jamani tusipindishe ukweli. Kama kasoma kwenye shule za wakatolki mi sioni ubaya kuwashukuru hao wenye shule ambapo alipatia elimu hata kama wazazi wake ndiyo waliomsomesha.

Mbona hapa JF tunaona watu wnaibuka na threads zenye kusifu na kushurku shule walizosomea? Mara Tambaza, oh, UDSM, nk. JAmani shule uliyosomea inakupa ufahari hata kama haikuwa bora sana. Tena shule tulizosomea zinajulikana kama "Alma mater" -"Mama mlezi". Kama ni hivyo kwa nini Kikwete asiwashukuru na kuwapongeza waliompa hiyo elimu? KAma shule hiyo isingekuwepo wazazi wangefanyeje na hizo pesa? Pesa pekee ingemsomesha?

Jamani tuitendee haki historia. Tunajivunia tena hata walimu wetu walotufundisha hata kama walikuwa wanalipwa mshahara. Tukikutana nao tunafurahi na hata kuwapa zawadi. Kosa liko wapi? Mwacheni Kikwete awashukuru wakatoliki na shule aliyosomea kama ni kweli alisomea huko kama anavodai.
 
Last edited by a moderator:
Akina Prof Ibrahim Lipumba, Isa Shivji, na labda wewe mwenyewe walisomaje? Uwongo haujengi! Nani aliwaambia mzamie madrasa na kuacha masomo mengine? Shule hamjengi mnasubiri 'Mkapa' mwingine awape Chuo cha umma bure kama Rais mstaafu Mkapa alivyowapa chuo cha TANESCO, chuo cha umma! Mnasubiri mnaowaita makafiri wawaundie mdudu kadhi na wawalipie! Wangepewa wakristo Chuo hicho pangetosha hapo? Si ingetolewa MoU ya kupewa chuo mtandaoni ili watu waijadili na kuona 'uonevu' huo?
kaka hapo umegusaaa...

BWM aliamua kwa makusudi kuwapendelea kwa kuwapa chuo cha umma BUREEEE...

Kawasaidiaa ila sitrambui kama wanasaidika vizuriii...vipi maendeleo ya hicho chuo?? hawajaweza hata kuwa na campus dar au kilwa??
 
kaka hapo umegusaaa...

BWM aliamua kwa makusudi kuwapendelea kwa kuwapa chuo cha umma BUREEEE...

Kawasaidiaa ila sitrambui kama wanasaidika vizuriii...vipi maendeleo ya hicho chuo?? hawajaweza hata kuwa na campus dar au kilwa??

Jibu la swali lako ni dogo tu na alilitoa memba mmoja katika thread moja nalo ni hili hapa:-

Mtume Muhammad alipokataliwa Mecca na akakimbilia Medina watu wa huko walimpokea kwa huruma na kumkaribisha kama mwungana. Wakristo, Mayahudi na wapagani. Kadri alivyopata nguvu kila siku kutokana na shughuli zake za biashara na ambush ya misafara ya wafanyabishara hatimaye jamaa wa Medina walilazimishwa kuchagua au kusilimu au kukutana na makali ya jambia. Wale wale waliompokea na kumhurumia. Tanzania subirini, huruma ya leo kwa jamii ya watu waliosahauliwa, wenye kuhitaji msaada wa serikali katika kuimarisha utamaduni wa dini yao siku moja utawatokea puani. Inaweza isiwe katika miaka 10 ya Kikwete, haya ni malengo ya muda mrefu. Kikwete anaweka msingi.
 
Jibu la swali lako ni dogo tu na alilitoa memba mmoja katika thread moja nalo ni hili hapa:-

Mtume Muhammad alipokataliwa Mecca na akakimbilia Medina watu wa huko walimpokea kwa huruma na kumkaribisha kama mwungana. Wakristo, Mayahudi na wapagani. Kadri alivyopata nguvu kila siku kutokana na shughuli zake za biashara na ambush ya misafara ya wafanyabishara hatimaye jamaa wa Medina walilazimishwa kuchagua au kusilimu au kukutana na makali ya jambia. Wale wale waliompokea na kumhurumia. Tanzania subirini, huruma ya leo kwa jamii ya watu waliosahauliwa, wenye kuhitaji msaada wa serikali katika kuimarisha utamaduni wa dini yao siku moja utawatokea puani. Inaweza isiwe katika miaka 10 ya Kikwete, haya ni malengo ya muda mrefu. Kikwete anaweka msingi.


Duh!! Mie kwenye DINI simo!
 
we mpenda fisadi, unataka nani asaidie wanyonge? unyonge wa waislamu wametaka wenyewe, hata lhaj Mwinyi ailtuambia maneno hayo, madrasa kwa sana wakati wenzio wapo kindergatten na primary school, ooh enzi hizo mzazi muislamu hataki kumpeleka mwanae skuli kwani atabadilishwa, sasa aliekudanganya serikali iwasaidiae ni nani? au ndo kama mambo ya kumwinua mwnamke? sasa ainuliwe mwislamu? duh hapo uongozi utakuwa mgumu haswa!muwe moderate mjipange, somesheni watoto,wakirudi home uwaulize za skuli,acheni kuwaozesha mapema, acheni kuoa wake wengi,hapo matajikwamua, out of that upuuzi mtupu mtabaki hapo hapo m iaka yote!! JK anajitahidi kuwabeba lakini haisadii, mzigo ni mzigo tuu!
 
Sioni ubaya wa mtu kutoa shukrani baada ya kufanyiwa wema, bila ubaguzi wowote mpendwa wetu JK alipewa elimu bora na Kanisa Katoliki! Hata kama ingekuwa mimi ningeshukuru!
 
Kuna baadhi ya shule hazikuwa za kanisa kama Kibaha au Tanga school na University of Dar

Hata yeye hakushukuru kwa shule zote alizowahi kusoma! Huoni kama hapa kuna special thanks, kiasi kwamba kama asingesomeshwa angekuwa mpaka sasa sio Rais wa nchi, kulingana na maneno yake?
 
Kwa mujibu wa Dr. Ngowi wa University of Bagamoyo aliyealikwa katika kipindi cha malumbano ya hoja. Anasema alisomea shule za seminari na kutumia jina la Samwel Luhanga na baadaye ndipo akatumia jina la Jakaya Mrisho Kikwete. Tuna mengi ya kujifunza.

Hongera Samwel Jakaya Kikwete


Chanzo: ITV malumbano ya hoja
Nimetazama kipindi hicho, kimemalizika muda dakika kadhaa zilizopita. Siyo Dr Ngowi aliyesema hilo. Ni Dr Kasoga mhadhiri wa chuo kikuu cha Bagamoyo. Mimi pia nimeshangazwa na taarifa hiyo. Lakini kama ni ya kweli, inamuongezea credit Mwalimu Nyerere kwa uamuzi wake wa kutaifisha shule za misheni, kwamba baada ya utaifisho huo waislamu walikuwa na uhuru kamili wa kusoma katika shule hizo bila kulazimika kutumia majina ya kikiristo au kuigiza ukiristo.

Majuzi nimemaliza kusoma kitabu cha historia ya shule ya Ilboru kilichoandikwa mwaka 1969. Ilboru ilikuwa shule ya kiluteri na ilianza miaka ya mwanzoni ya 1940's. Katika sehemu fulani kitabuni mle, kuna ripoti ya mkutano mmojawapo wa bodi ambako walilalamikia suala la kulazimishwa na serikali (baada ya uhuru) kuanza kudahili wanafunzi wa imani nyingine. Bila msukumo na shinikizo la serikali ya Nyerere, baadhi ya shule za madhehebu ya dini kamwe zisingekubali kusomesha watoto wa dini tofauti na ya wenye shule.

Ndio maana naungana na wote wanaomsifu Mwalimu Nyerere kwa jitihada zake za kuondoa matabaka Tanzania, na mfano wa leo wa Mh Samuel Luhanga ni kumbukumbu nyingine nzuri sana to Nyerere's credit.
 
:juggle::juggle: ya kina Philipo Mulugo mpaka kwa JK:A S-coffee::A S-coffee::A S-coffee:
 
Back
Top Bottom