Kikwete: Nilikwishakabidhi orodha ya 'wauza unga'!

Kikwete: Nilikwishakabidhi orodha ya 'wauza unga'!

Tuulizane wenyewe hapa jf nani anaweza kumtaja yule mhusika mkuu wa unga akawa na ushahidi wa kutosha ukiacha hawa akinamasongange wao wanatumiwa tu,

Nani anamjua mwenyewe hasa au wenyewe hasa na ushahidi usio na shaka atuambie bila mizaha ya kitoto.
 
Serikali ilishasema anayejua wauza unga na ushahidi apeleke hayo majina yatangazwe.

Wewe mjepo wewe,

Nyie ndio watu mnaoleta mizaha kwenye serious issues!

Unazungumzia Serikali ipi ambayo ilishasema anayejua wauza unga na ushahidi apeleke?Amina Chifupa(RIP) yuko wapi we mbepo? Hivi hujui kuwa dada Amina alitamka Bungeni kuwa alikuwa na orodha ya WAUZA UNGA NA ALIKUWA TAYARI KUWATAJA? Mbona serikali yako haikumpa ushirikiano wa kuyaomba hayo majina?

Kilichofuata baada ya kauli hiyo ya marehemu Amina ni historia! Wewe ni shahidi kabisa kuwa kauli hiyo iligharimu UHAI wa binti huyo aliyekua kijana mbichi na mwenye uchungu na nji hii!

mjepo nakusihi uache mzaha kwenye hili. Kama huna cha kuchangia you better keep quite! Watu watakuona una busara!
 
Kweli madawa ya kulevya ni mtandao mkubwa sana na una watu wazito sana serikalini ndio sababu wakubwa wanakuwa na kigugumizi linapokuja suala la kukemea wauza na watumia madawa ya kulevya. Si ajabu mtumiaji anapozidiwa na akawa na ka-umaarufu atasaidiwa na IKULU au viongozi wakuu ili asiseme saana.
 
Alipotangaza kwamba ana list ya wauza unga alifanya hivyo hadharani, lakini alipoamua list hiyo kuwakabidhi vyombo husika akaamua kufanya kimya kimya!!!! Sasa alipoona vyombo husika havifanyi lolote katika kudhibiti biashara ya unga iliyokuwa ikikithiri nchini na nje ya mipaka yetu kutokana na kukamatwa kwa Watanzania wengi alichukua hatua gani kama kiongozi wa nchi!? Kweli DHAIFU ni Janga la Kitaifa.
 
Nitarudi baadae maana sielewi vizur hii kauli ya Rais
 
Kweli madawa ya kulevya ni mtandao mkubwa sana na una watu wazito sana serikalini ndio sababu wakubwa wanakuwa na kigugumizi linapokuja suala la kukemea wauza na watumia madawa ya kulevya. Si ajabu mtumiaji anapozidiwa na akawa na ka-umaarufu atasaidiwa na IKULU au viongozi wakuu ili asiseme saana.

Unawapa kichwa wauza unga,hawana ukubwa huo
 
Hivi CHADEMA wapo salama na hii kadhia? Mbona siwaoni vinara was matamko na miongozo wakiibana Serikali kwa ukali na ushujaa ule ule wakati wa mijadala mwingine.

Hii vita no ngumu na haijapata mpiganaji hodari au haina maslahi kwako kupigana.
 
Mimi ninapita lkn ninashangaa swala la madawa ya kulevya likisemwa hapa JF hwa wakina HAMY-D, Lukosi na RIT.. hawachangii! Kuna mtu anajua sababu za kutochangia jamani?

Sababu ni mgongano wa kimaslahi. Hapo walipo wanabana miguu kwa nguvu zote ili huu upepo upite
 
eti jina la mwanae limo kama halimo hiyo jk kachakachua..
 
ushahidi muhimu sana na si kukurupuka mtaumbuka

Nimeumia na kushangazwa sana. Inawezekana vipi mtu anyamaze kimya huku rais akishutumiwa kumbe alishakabidhiwa majina? Huyu mhusika nashauri akamatwe mara moja na aeleze kisa cha kukalia hayo majina huku rais akiendelea kushutumiwa na vijana wakiendelea kuumia.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
"Na hivi karibuni nimepewa orodha ya watu 261 wanaodaiwa kufanya biashara hiyo...."

nimeipenda hii kauli maana ndio imezidi kunifunua ubungo zaidi kujua utendaji wa kazi katika suala hili ulivyo....!! Labda la kujiuliza kwa haraka haraka je Mh. Rais yeye alipatiwa orodha hiyo lini.???????
LETS READS BETWEEN THE LINES.
 
Hivi CHADEMA wapi salama na hii kadhia? Mbona siwaoni vinara was matamko na miongozo wakiibana Serikali kwa ukali na ushujaa ule ule wakati was mijadala mwingine.
Hii vita no ngumu na haijapata mpiganaji hodari au haina maslahi kwako kupigana.

hapa hakuna cha matamko cha msingi na sekondari kikwete kama lowasa, riz1,azan,juma pinto, manji...
 
ni nini chanzo cha majina aliyokabidhi? Amepewa na vyanzo vyenye uhakika?
Ameviamini hivyo vyanzo? Hayo majina aliyokabidhi ameridhika kabisa kuwa ni kweli ni ya wauza unga? Sasa kama tayari mkubwa ameshakabidhi majina na ushahidi anao, hawa watu wanangoja nini uraiani?
 
Sababu ni mgongano wa kimaslahi. Hapo walipo wanabana miguu kwa nguvu zote ili huu upepo upite
Nimekupata mkuu kumbe mawazo yako hayapo mbali na yako. lkn kama ni hivyo kuna haja ya kusoma zile mods zao?
 
jk anajaribu kuficha udhaifu wake, kwani waliomkabidhi hiyo list yeye hawakumuona nzowa?? nzowa ni ofisa ktk taasisi ya kuzuia madawa ya kulevya unapomkabidhi jukumu la kupambana na mawaziri na wabunge wauza unga unamaanisha nini?? yaani wewe ndio bosi wao huchukui hatua ila unamkabidhi watu wenye limited power kufanya hivyo. This is called political scapegoating.
 
Back
Top Bottom