Kikwete: Nilikwishakabidhi orodha ya 'wauza unga'!

Kikwete: Nilikwishakabidhi orodha ya 'wauza unga'!

Chadema Diaspora

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2010
Posts
480
Reaction score
644
JK: Nilikwishakabidhi orodha ya "wauza unga"

WAKATI sakata la dawa za kulevya likiwa limeichafua Tanzania katika uso wa kimataifa, orodha ya majina ya wanaohusika na biashara hiyo ambayo Rais Jakaya Kikwete alidai kuwa nayo, amesema amekwishaipeleka kwenye Mamlaka husika. Rais Kikwete mara kadhaa amekuwa akisema kuwa anayo orodha ya watu wanaouza dawa za kulevya hapa nchini, hivyo gazeti hili lilimtafuta kupitia kwa msemaji wake, kufahamu suala hilo lilikofikia.

Akizungumza na gazeti hili kupitia kwa Msemaji wake, Salvatory Rweyemamu, Rais Kikwete alisema orodha ambayo alisema anayo alikwishaikabidhi kwa vyombo husika kwa ajili ya hatua zaidi.

“Rais atembee nayo mfukoni ya nini? Hata Nzowa katika taarifa yake alisema alipatiwa… wamepewa vyombo husika, Serikali haiendeshwi kwa vyombo vya habari, kuna vingi vinafanyika bila kutangazwa. Mtafute Nzowa atakwambia vyema,” alisema Rweyemamu, wakati gazeti hili lilipotaka kufahamu juu ya orodha hiyo ya Rais ilikofikia.

Orodha ambayo Rais Kikwete amekuwa akielezwa kuwa anayo, inadaiwa kuwahusisha vigogo mbalimbali nchini, wakiwemo wabunge, mawaziri na wafanyabiashara wakubwa ambao hata hivyo imebainika kuwako kwa ugumu wa kuwachukulia hatua, kutokana na kutokuwa na ushahidi ili kuwabana wahusika.


Kutokana na kauli hiyo ya Rais kupitia kwa msemaji wake, Gazeti hili liliamua kutafuta moja ya mamlaka zinazohusika kupambana na dawa za kulevya ili kufahamu juu ya orodha hiyo iliyokabidhiwa na Rais na hatua ambazo zimechukuliwa.

Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya cha Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi (ACP), Godfrey Nzowa, hakukiri wala kukana kupokea orodha hiyo kutoka Ikulu.

MTANZANIA Jumapili: Kamanda sisi ni MTANZANIA Jumapili, tumepata taarifa kwamba Ikulu imekupatia majina ya watu wanaojihusisha na dawa za kulevya, vipi umefikia wapi katika kuishughulikia?

NZOWA: “Kutoka wapi? Mimi napata kutoka sehemu mbalimbali, tunakuwa na watu ambao tunakamata na tunawapekua, ikithibitika tunawapeleka mahakamani Na hivi karibuni nimepatiwa orodha ya watu 261 wanaodaiwa kufanya biashara hiyo, lakini katika upekuzi wetu hatukukuta kitu.



MTANZANIA Jumapili: Kwa hiyo hao mliowapekua ndiyo orodha mliyopatiwa kutoka Ikulu?
Nzowa: Siwezi kutaja moja kwa moja kwa sababu ninapokea orodha kutoka sehemu mbalimbali, kwa hiyo si salama kutaja jina la mtu. Siwezi ku ‘mention’ kuwa ni Ikulu ama nani. Ushahidi wa moja kwa moja haupo, lakini wa kimazingira upo, tulipeleka kiapo ili washitakiwe Mahakamani.

Kwa mujibu wa Nzowa, wengine zaidi ya 260 waliopatikana na ushahidi wamefunguliwa kesi katika mahakama za hapa nchini.

Hivi karibuni katika Bunge linaloendelea Dodoma, kuliibuka hoja ya kuitaka serikali kutaja orodha ya wanaodaiwa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya, ambapo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alishindwa kufanya hivyo.

Badala yake, Lukuvi alisema baadhi ya majina ya wabunge yametajwa miongoni mwa watu wanaoshukiwa kujihusisha na biashara hiyo na kwamba angetaja majina, Bunge lisingebaki salama.


Lukuvi alisisitiza kuwa serikali haiwezi kuwataja hadharani kwa haraka, kwani inaogopa kukurupuka na kushindwa mahakamani.

Hata hivyo, Lukuvi alisema ukubwa wa biashara hiyo hapa nchini unadhihirishwa na idadi ya Watanzania 274 waliokamatwa kati ya mwaka 2008 hadi Julai, mwaka huu kwa kosa la kujihusisha na dawa za kulevya katika nchi mbalimbali za nje.

Pamoja na kukamatwa kwa Watanzania hao nje ya nchi, wageni 31 wanashikiliwa mahabusu katika Magereza ya Keko na Ukonga, Dar es Salaam, ambao ni raia wa Iran, Pakistan, Senegal na Afrika Kusini.

Sakata la dawa za kulevya nchini lilitikisa zaidi baada ya kukamatwa kwa wasichana wawili, Agness Gerald (25) na Mellisa Edward (24) katika Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo, Afrika Kusini, wakitokea Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, (JNIA) wakiwa na dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine kilo 150, zenye thamani ya Sh. bilioni 6.8 za Tanzania.

Hatua hiyo ilimlazimisha Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kuwafukuza kazi wafanyakazi wa JNIA, wanaodaiwa kuhusika na upitishwaji wa mzigo huo, huku baadhi ya watendaji wakihamishwa vituo vyao vya kazi. Moto huo uliowashwa na Mwakyembe, ulikuja baada JNIA kutajwa kuwa moja ya chochoro kubwa za kupitisha dawa hizo, hali ambayo pia imeshuhudia Jeshi la Polisi kuwaondoa kwa kuwahamisha vituo vya kazi, Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, Kamishna Msaidizi (ACP) Deusdedit Kato na Mkuu wa Upelelezi wa Viwanja hivyo, David Mwafwimbo.


Chanzo: Mtanzania
 
Bao la mkono hilooooo kama Maradona vile na mkono wa mungu
 
ushahidi muhimu sana na si kukurupuka mtaumbuka
 
Baada ya miaka 7???!! Bado ni Ile Ile au nae kaandaa yakwake??!! CCM bora mngebinafsisha na urahisi kuliko hii dhihaka ya utawala bora!!
 
Kwa hiyo inamaanishi rais naye siku hizi anachukua mambo ya kwenye vijiwe vya kahawa na kuyaingiza kwenye hotuba ya mwezi! Nataraji rais anaposema ana orodha ni orodha kweli iliyokamilika kwamba vielelezo alivopewa vinawatia hatiani,hope hiyo orodha watachukuliwa hatua stahili na atakayenusurika kukatwa mapembe bahati yake atasimulia.
 
Kwa hiyo inamaanishi rais naye siku hizi anachukua mambo ya kwenye vijiwe vya kahawa na kuyaingiza kwenye hotuba ya mwezi! Nataraji rais anaposema ana orodha ni orodha kweli iliyokamilika kwamba vielelezo alivopewa vinawatia hatiani,hope hiyo orodha watachukuliwa hatua stahili na atakayenusurika kukatwa mapembe bahati yake atasimulia.
Kwani kukabidhi ndio nini si kutoa kopi tu na kuwapelekea watendaji au ilibidi achome kabisa hata original kwa kuhofia maisha yake; hata kama kakabidhi orodha bado anayo tuuuuuu hata ingekuwa imeibukia ofisi zingine ni ofisi zake tuuu hakuna kujivua kihunihuni hapa
 
wapi na wapi apeleke wakati yeye na mwanae nao wamo kwenye mchongo yani hii ni ukinitaja nami nataja so mkubwa anawasiwasi kua asije taja watu wakataja zaidi ya uko china si unajua
 
Hali halisi inaonyesha kuwa serikali haina nia ya kukomesha biashara ya wafanya biashara wa madawa ya kulevya. Ni rahisi sana kuwakamata, si kwa kujishughulisha na biashara hiyo tu, bali kwa kuulizia mapato na utajiri walio nao. Mara nyingi watashindwa kuelezea kwa kikamilifu wapi walipopata utajiri huo. Vilevile kwa sababu utajiri huo haukupatikana kihalali, watakuwa hawakulipia kodi mapato hayo. Vyote hivyo ni ushahidi tosha wa kuwafikisha mahakamani na kuwafungulia mashtaka.

Mbinu kama hii inatumika sana USA na nchi nyingine wakitaka kuwakamata wafanya biashara ambazo si halali. Mbinu nyingine ni kuthibiti benki na kuweka sheria ambazo itafanya vigumu kuosha pesa zilizopatikana kwa biashara haramu. Sijui haya yatatekelezwa lini hapa nchini mwetu.
 
Tarifa za mtanzania hazinatofauti na tanzaania daima ni udaku tu.
 
Serikali ilishasema anayejua wauza unga na ushahidi apeleke hayo majina yatangazwe.
 
Tarifa za mtanzania hazinatofauti na tanzaania daima ni udaku tu.
Mimi nafikiri sasa mmeamua kujivua akili zenu kabisaaa, hivi taarifa kama hii nayo unaita ya Udaku, tatizo hapa ni kurugenzi ya Ikulu haijitambui kwani tumeshuhudia matamko mengi ya utata kutoka taasisi hiyo.
 
Mbona rais ana mamlaka makubwa kikatiba na hayatumii ipasavyo?
Kila jambo nyeti JK anakwepa sana kulishughulikia ama ni kweli na kijana wake yumo?
 
Hivi watu wanategemea Mkuu wa Kaya Bwana Kiwete aseme nini zaidi ya blabla? Lazima tujiulize hii orodha ni ile ile aliyokuwa nayo marehemu Amina Chifupa au ni nyingine?

Kama mwanaye RIZ-1 yuko kwenye orodha ya WATUHUMIWA wa MADAWA ya kulevya ataanza anzaje kutaja majina ya wahusika? Hii haiwezekani. Kilichobaki ni kupiga porojo na longolongo nyingi ili muda uende na baadaye WATANZANIA WATASAHAU TU si tunajua msemo wa mkulu kuwa huo ni upepo tu wa kisiasa?

Mimi nasema wazi kabisa kuwa Serikali ya CCM tuliyonayo haina nia ya dhati ya kumaliza tatizo la madawa ya kulevya maana inaendeshwa na MAFISADI na DRUG BARONS! Kwa hiyo basi HAKAMATWI MTU HAPA! Watanzania lazima wajue kuwa MFUMO WOTE WA SERIKALI KUANZIA IKULU UMEKUFA NA UMEOZA! Kama ROSTAM AZIZI aliyekuwa mweka Hazina wa CCM Taifa NI MMOJA WA WATUHUMIWA WA MADAWA YA KULEVYA NA NI MFADHILI MKUBWA WA CCM WATU WATEGEMEE NINI?KAMA FEDHA HII CHAFU/HARAMU NDIYO ILITUMIKA KUMUINGIZA KIWETE KWENYE URAHISI MWAKA 2005 NA 2010 KWA KUGHARAMIA KAMPENI ZAKE NA RUSHWA KWA WAPIGA KURA ATAKUWAJE NA UJASIRI WA KUWATAJA WAHUSIKA NA HATIMAYE KUWAFIKISHA MAHAKAMANI??NI JAMBO LISILOWEZEKANA!

Watanzania wasitegemee lolote la maana kwenye vita hii ya Madawa ya Kulevya. Hakuna. Kinachotakiwa kwa Watanzania kwa sasa ni kujipanga kuipumzisha CCM na Serikali yake mwaka 2015 ili kupata matokeo chanya kwenye vita hii ya Madawa ya kulevya ambayo hakika ni janga la Kitaifa kwa vijana na wazee. Midhali CCM itaendelea kuwa madarakani BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA HAITAKWISHA ASILAN BADALA YAKE ITAENDELEA KUSHAMIRI SIKU HAD SIKU!

Lazima kwenye UCHAGUZI WA MWAKA 2015 kuwa na slogans kama: CHAGUA CHADEMA TOKOMEZA MADAWA YA KULEVYA TANZANIA.

Wasalaamu.
 
Mimi ninapita lkn ninashangaa swala la madawa ya kulevya likisemwa hapa JF hwa wakina HAMY-D, Lukosi na RIT.. hawachangii! Kuna mtu anajua sababu za kutochangia jamani?
 
Baada ya miaka 7???!! Bado ni Ile Ile au nae kaandaa yakwake??!! CCM bora mngebinafsisha na urahisi kuliko hii dhihaka ya utawala bora!!

'halaf ni vizuri wawabinafsishie wazungu watatutia ndani ya ndege kama zaabu watupeleke ulaya kidogo inaeza kua nafuu aisee...'
 
Ukitaka kuumbuka nennda na swala la unga mahakamani kama huna ushahidi wa kutosha utazalilika vibaya sana,
Ni muhimu kuwa na ushahidi wa kutosha kabula kwenda mahakamani vinginevyo itakuwa manyago tu na miguu juu kichwa chini.
 
Biashara hii ni dili la magamba kujipatia hela chafu za kugawa kwa ajili ya uchaguzi wa 2015.Hii ni kwa sababu wanahitaji pesa zaidi za kugawia kila mtz mburula angalau buku 7-7 (kama wanavyogawiwa kina HAMMY-D,simiyu yetu,radhia, baba yao na wale lumumba fc) ili wachaguliwe,lkn kura zote ni CDM kula CCM kama tulivyowacheza shele Arumeru.
 
Back
Top Bottom