Kikwete ni Masiha

...... Angekuwa SILAA, tungeambiwa yupo huko kaenda kupigana, huyu.... kaenda kutaliii.
 
...... Angekuwa SILAA, tungeambiwa yupo huko kaenda kupigana, huyu.... kaenda kutaliii.
Ni kweli kabisa. Slaa angeenda kupigana. Tumemsikia tangu bungeni hadi kwenye uwanja wa mapambano. Na hata akienda kwa kutalii si mbaya kwa kuwa tunajua atakayoacha nyuma si haba
 
Hakuna kiumbe kilichopo na kitakacho zaliwa na binadamu chenye kufanana na MASIHA, ONLY JESUS. Jina Lipitalo Majina YOTE
 
Hakuna kiumbe kilichopo na kitakacho zaliwa na binadamu chenye kufanana na MASIHA, ONLY JESUS. Jina Lipitalo Majina YOTE

This is Disgrace,how can some one compare Jesus Christ with a man???????
It is blasphemy!!!!!!
 
Soma tena vizuri ndugu. Mi sio mfuasi wa CCM wala JK bali kwa wana wa fasihi hiyo tunaita irony. Ila ukweli ndio huo kuwa kwa kupitia udhaifu wake sauti ya umma itafanya kazi. Hilo ndilo wazo langu kuu

Hata Mhubiri Mkubwa TZ Moses Kulola 2005: alisema JK ni chaguo la MUNGU. Ni kweli mkuu acha wabishe maana hawajui walisemalo
 
Mimi mtazamo wangu ni huu;
Mhe. Kikwete sivyo mnavyomtafsiri sivyo alivyo; kikwete kiongozi safi sana. Anaipenda nchi yake sana, kuwapenda watanzania. Mimi bado ninampa credit . Kinachomponza ni umaskini wake, yeye si mroho wa kujilimbikizia mali; ninavyomjua mimi ila mfumo wa chama hauna utaratibu mzuri wa vitega uchumi na kwa kuchangisha pesa kwa wanachama wake ili kukidhi mahitaji ya chama, kama vile kampeni na mambo mengine. Hali hiyo inatoa mwanya kwa watu wabaya wasioitakia mema nchi yetu kujichomeka na kujidai kukisaidia chama lakini kwa masharti. Masharti hayo ndio yanayomponza Rais wetu. Mimi naamini Mhe. Rais anaweza kuyaweka mambo sawa, na ndio maana kanyamaza kimya bado anatafakari mambo ya busara; hawezi kukurupuka tu na kuongea hovyo!!! Mimi nashauri tuondoe jazba tumpe muda Rais wetu, bado anayo nafasi nzuri ya kutufanyia mema zaidi kama alivyoahidi kuwa atahakikisha "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA" si kitu cha mara moja tu kutekeleza, unahitajika muda wa kutosha!!!!!!!!!!!!Tumuombe MUNGU atupe nyoyo za subira!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mkuu katika miaka 10 kabakiza mitatu tu.. Sasa unataka tumpatie muda gani zaidi ili aturekebishie maisha yetu..? Mshauri basi abadilishe katiba agombee muhula wa tatu ili apate miaka 5 mingine..
 
Mkuu katika miaka 10 kabakiza mitatu tu.. Sasa unataka tumpatie muda gani zaidi ili aturekebishie maisha yetu..? Mshauri basi abadilishe katiba agombee muhula wa tatu ili apate miaka 5 mingine..

ni kweli kabisa huyo jamaa kaandika vizuri BILA KIKWETE CHADEMA INGEPATA NGUVU!! CUF ILIKUW ANA NGUVU KULIKO CHADEMA LAKINI JK KAIRAHIHISHIA CHADEMA JAMANI TUKUBALI KUWA UKOMBOZI UKITOKEA NI KWA JILI YA JK HILO HALINA UBISHI THINK BEFORE KUKTAA KUWA SI KWELI! JK ADUMU ADUMU ZAIDI ILI MABADILIKO YA KUIOKOA NCHI YETU YATIMIE ANATAKA TUBADILI MIKATABA YA MADINI LAKINI SI KUPITIA CCM BALI CHAMA PINZANI NA HILO NI LENGO LAKE!
 
Sijapenda uchambuzi wako wa kumfaninisha yesu na jk na usirudie kamwe.

Lakini na kubali kuwa jk ndio amekuwa matundu ya kupitia hasa kuelekea kwenye ukombozi wa nchi yetu, maana ata tetemeko hupitia sehemu dhaifu.

Nasikweli jk alitegemea haya bali alijitega na kujichanganya,najua nyinyiemu wanajuta kumpitisha huyu jamaa wako,kwani yeye ndio amekizika chama.
 
Jaribuni kutuliza mawazo na kusoma tena kwa uzuri ndio mjue ninamaaisha nini. Nimesema si CCM itatupatia maisha bora bali CCM kupitia jk ni chombo tu cha kutufanya watanzania tuamke. Mdau mmoja hapo juu katumia lugha ya kawaida ya kusema ni ajent. True, ila nina sababu za kutuia jina la masiha

Kweli ni chombo cha kutufikisha hapo. Lakini amini usiamini kuwa ili uwe Masiah ni lazima ujitambue kuwa unatumika kwa ajili ya watu kwa niaba ya Mungu. Umesema kuwa inawezekana anajua au hajui. Mimi nakuhakikishia kuwa hajui! Na kama hajui ameshapoteza sifa ya kuwa Masiah. Kilichopo ni kwamba ameshindwa, hata kama anatamani kufanya mambo yaende kama anavyotaka hawezi tena. Tusubiri tuone wapi tutafika lakini sio kwa sababu yeye ametupeleke tufike huko. Asije kujisifia kuwa hapo tutakapofika kama ni pazuri basi yeye ndiye akiyesababisha tufike hapo. La, ni kwa sababu ya jitihada za makusudi zinazoendelezwa na wanaoshiuhudia kushindwa kwake. Ili awe sehemu ya wanaweza kujisifia ni lazima sasa hivi aonyeshe mwelekeo kuwa anataka kufika mahali fulani lakini sio kupitia SLOGAN ya maisha bora kwa kila mtanzania. Huo sio mwelekeo au target, bali ni wimbo wa kisiasa ambao yeyote anaimba hata kama hana sifa za unabii au umasiah.
 
May be Masihi wako, na watu wa aina yako; kwa Watanzania wengi, your comments are not only irritating but offending....masihi, you you even know what the meaning of Messiah is? The "anointed" of the Lord, used particularly for Christ; you you confer Christ's title to JK? What an abomination....Mwombe Mungu akusamehe kwa kufuru hizo...Wewe kweli unafaidi vya wafisadi, ndio maana hata unazungumzia juu ya ahadi, nchi yetu tunayo, na maziwa na asali wanakula watu kama wewe na those of the likes of huyo unayemfagilia...you provoke others to the limits, stop such nonsense[/QUOT

Ni masia kaka unawazaje kuwa na mtu juha kama huyo ikulu, kama si mipango ya Mungu kuwaondoa CCM kinyesi kwenye utawala wa nchi; yeye ndio kaja kumalizakazi nchi ikomboke 2015
 
attachment.php

Haya ndio mambo ambayo jk huyafuata huko nje?
 
Inawezekana halijui hilo. Na kama analijua basi ni genious. Ametumwa kuleta mabadiliko katika taifa hili. Kupitia yeye tutaona mengi yakifumka na mengi yakikaa sawa baiadae japo 'wino' wa kutosha waweza patikana.

Bagenda nae hakukosea pale alipoandika kuwa Jakaya ni tumaini lililorejea. Matumaini yana namna nyingi ya kuwafikia walengwa. Hata Yona alitaka kumkimbia Mungu alipopewa kazi ya kwenda Ninawi lakini alifika huko via the hard way-alikaa tumboni mwa samaki kwa siku 3!

Ukimya wa Jakaya ni dalili tosha kuwa nguvu ya umma imeachiwa kufanya kazi. Mtauliza iweje achakachue matokeo ya urais ili aendelee kuwepo madarakani. Wakati fulani hata Yesu aliwahi kusema kabla ya mateso kuwa. 'Baba ikiwezekana kikombe hiki nikiepuke, ila si kwa mapenzi yangu bali yako'. Mungu ili lengo lake litimie ilimbidi mapenzi yake yatimie.

Mifano hii inafanana ila inapishana. Yesu alitaka kuyaepuka mateso lakini Jakaya hakutaka kuiachia ikulu, japo wakati unakuja atafanya hivyo. Ni lazima kupitia yeye nchi hii itakaa sawa. Patakuwa na rabsha hapa kati lakini mwisho wa siku mambo yatakaa sawa. Ndio maana tukapewa mfano wa punje ya ngano, kwamba ili ngano izae ni lazima ioze kwanza. Hata Ngugi wa Thiong'o aliwahi kuandika kuhusu A Grain of Wheat. Lakini si ngano pekee huoza ili ipate kuzaa. Ngano ni mfano wa msingi. Nafaka aina zote pamoja na mbegu huoza kwanza ndipo zikazaa zaidi.

Kwa hiyo wana wa nchi tujue kabisa kwamba jakaya ni Tumaini lililorejea, japo si lazima iwe kufumba na kufumbua ndipo tuyaone maisha bora kwa kila mtanzania. Mungu alipowatoa wana wa Israel toka utumwani Misri aliwapitisha katika jangwa penye kila aina ya shuruba na mahangaiko kwa muda wa miaka arobaini! ili kufikia nchi ya asali na maziwa-naam, nchi ya ahadi. Mungu hakushindwa kuwapaisha mara moja ili kufika Kanani bali alitaka wana wa Israel wajue kuwa yeye ndiye ALIYE! Wajue kuwa maisha si lelemama bali ni tibwili zito. Ili mwisho wa siku watu wathamini maisha pamoja na kile walicho nacho. Wamthamini na yeye (Mungu) pia.

Hata dhahabu ili iweze kuitwa dhahabu safi ni lazima ipitie kwenye moto wa nyuzi elf kadhaa ili iwe dhahabu. Tusione vyaeelea bali vimeundwa. Ndivyo wasemavyo wahenga.

Kwa hiyo ndugu watanzania tukae tukijua kabisa kuwa masiha wetu-Jakaya yupo kazini kutimiza kile alichoitiwa kutimiza-Maisha bora kwa kila mtanzania. Na haya maisha bora hayataletwa na CCM bali CCM inatumika kama chombo tu cha mchakato kuelekea hayo maisha bora. Hata Musa aliambiwa na Mungu kuwa nchi ya ahadi ni ile paleeeee lakini hutaikanyaga!

Watanzania tujiendae kuifikia nchi ya ahadi. Nchi ya asali na maziwa

Mkuu naomba niulize swali tena unamaanisha masiha au masihi,?au tukinukuu kwa lugha ya wenzetu messiah,naogopa kuchangia nisije nikakufuru,kama ulikuwa una manna ya mojawapo nilizozitaja muombe MUNGU wako akupishie mbali na kufuru uliyosema,
Kikwete ni binadamu kama wewe tena mchemkaji hata kuzidi wewe ulivyochemka kwa kuandika kufuru.
 
Back
Top Bottom