Kikwete ni Masiha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete ni Masiha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Raia Fulani, Jan 17, 2011.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Inawezekana halijui hilo. Na kama analijua basi ni genious. Ametumwa kuleta mabadiliko katika taifa hili. Kupitia yeye tutaona mengi yakifumka na mengi yakikaa sawa baadae japo 'wino' wa kutosha waweza patikana.

  Bagenda nae hakukosea pale alipoandika kuwa Jakaya ni tumaini lililorejea. Matumaini yana namna nyingi ya kuwafikia walengwa. Hata Yona alitaka kumkimbia Mungu alipopewa kazi ya kwenda Ninawi lakini alifika huko via the hard way-alikaa tumboni mwa samaki kwa siku 3!

  Ukimya wa Jakaya ni dalili tosha kuwa nguvu ya umma imeachiwa kufanya kazi. Mtauliza iweje achakachue matokeo ya urais ili aendelee kuwepo madarakani. Wakati fulani hata Yesu aliwahi kusema kabla ya mateso kuwa. 'Baba ikiwezekana kikombe hiki nikiepuke, ila si kwa mapenzi yangu bali yako'. Mungu ili lengo lake litimie ilimbidi mapenzi yake yatimie.

  Mifano hii inafanana ila inapishana. Yesu alitaka kuyaepuka mateso lakini Jakaya hakutaka kuiachia ikulu, japo wakati unakuja atafanya hivyo. Ni lazima kupitia yeye nchi hii itakaa sawa. Patakuwa na rabsha hapa kati lakini mwisho wa siku mambo yatakaa sawa. Ndio maana tukapewa mfano wa punje ya ngano, kwamba ili ngano izae ni lazima ioze kwanza. Hata Ngugi wa Thiong'o aliwahi kuandika kuhusu A Grain of Wheat. Lakini si ngano pekee huoza ili ipate kuzaa. Ngano ni mfano wa msingi. Nafaka aina zote pamoja na mbegu huoza kwanza ndipo zikazaa zaidi.

  Kwa hiyo wana wa nchi tujue kabisa kwamba jakaya ni Tumaini lililorejea, japo si lazima iwe kufumba na kufumbua ndipo tuyaone maisha bora kwa kila mtanzania. Mungu alipowatoa wana wa Israel toka utumwani Misri aliwapitisha katika jangwa penye kila aina ya shuruba na mahangaiko kwa muda wa miaka arobaini! ili kufikia nchi ya asali na maziwa-naam, nchi ya ahadi. Mungu hakushindwa kuwapaisha mara moja ili kufika Kanani bali alitaka wana wa Israel wajue kuwa yeye ndiye ALIYE! Wajue kuwa maisha si lelemama bali ni tibwili zito. Ili mwisho wa siku watu wathamini maisha pamoja na kile walicho nacho. Wamthamini na yeye (Mungu) pia.

  Hata dhahabu ili iweze kuitwa dhahabu safi ni lazima ipitie kwenye moto wa nyuzi elf kadhaa ili iwe dhahabu. Tusione vyaeelea bali vimeundwa. Ndivyo wasemavyo wahenga.

  Kwa hiyo ndugu watanzania tukae tukijua kabisa kuwa masiha wetu-Jakaya yupo kazini kutimiza kile alichoitiwa kutimiza-Maisha bora kwa kila mtanzania. Na haya maisha bora hayataletwa na CCM bali CCM inatumika kama chombo tu cha mchakato kuelekea hayo maisha bora. Hata Musa aliambiwa na Mungu kuwa nchi ya ahadi ni ile paleeeee lakini hutaikanyaga!

  Watanzania tujiendae kuifikia nchi ya ahadi. Nchi ya asali na maziwa
   
 2. i

  ibange JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  nilivyosoma mwanzo nilianza kukubaliana nawe ila hapa mwisho sikubaliani nawe. mimi namwona kikwete kuwa ni masiha kwa mtazamo tofauti. kwamba yeye ni kiongozi dhaifu na ni rahisi kumshinikiza afanye jambo. kupitia kwake twaweza kupata katiba mpya na mabadiliko ya kijamii na pia kuanguka kwa ccm. maisha bora ni ndoto wajameni
   
 3. s

  seniorita JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  May be Masihi wako, na watu wa aina yako; kwa Watanzania wengi, your comments are not only irritating but offending....masihi, you you even know what the meaning of Messiah is? The "anointed" of the Lord, used particularly for Christ; you you confer Christ's title to JK? What an abomination....Mwombe Mungu akusamehe kwa kufuru hizo...Wewe kweli unafaidi vya wafisadi, ndio maana hata unazungumzia juu ya ahadi, nchi yetu tunayo, na maziwa na asali wanakula watu kama wewe na those of the likes of huyo unayemfagilia...you provoke others to the limits, stop such nonsense
   
 4. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  imekaaa vizuri hiyo.
   
 5. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #5
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  mi nadhani kila jambo linawezekana kama tukiamuwa iwe,lakini kama tutakuwa wakusema ndio kwa kila kitu tutaishia kulalamika kila siku iendayo kwa mungu,wakati ndio huu timiza wajibu wako wewe mwana JF

  MAPINDUZIIIIII DAIMAAAAAAAAAAAAA
   
 6. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,381
  Likes Received: 3,141
  Trophy Points: 280
  A big joke to christians........namuomba mungu akusamehe bure
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Dhana yake ni nzuri tu!
   
 8. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Watu wanahasila humu duuuu!
   
 9. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Umechemka kabisa sehemu hii. Hakuna ufanano wowote baina ya Kikwete na Yesu Kristo. Kama hujui Mwandishi wa Biblia anasema nini pale anaposema baba kikombe hiki kiniepuke bora unyamaze. Je unataka kuniambia kwamba Kikwete ana ujasiri kuliko Yesu Kristo? shut up? Sipendi watu kutoa comment za kipagani.
   
 10. G

  Gashle Senior Member

  #10
  Jan 17, 2011
  Joined: Mar 30, 2007
  Messages: 119
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa mtazamo wangu (au tafsiri) yangu, ningesema kwamba yeye ni "agent" wa kubadilisha fikra za Wazalendo wa nchi hii. Mathalan, ujasiri wa Wazalendo tuliouona kule Arusha usingewezekana kama uongozi ungekuwa bora na uliotukuka. Ni nchi mpya inazaliwa, kizazi kipya cha Watanzania wanaoweza kusimama dhidi ya risasi za moto, achilia mbali mabomu ya vibaraka wa watawala!
   
 11. Innobwoy

  Innobwoy JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 980
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 60
  Binafsi cjaona jk akitatua mambo mazito yanayohusu Taifa, bt ninamsifu kwa mahudhulio ya birthday party,kuzindua program mbalimbali ie tht bt issue nzito za kitaifa No thank you, bush angekuwa bd yupo madarakani angeenda kupumzika bt kwa kuwa yule Mkenya sio mnafiki inabd avumulie.
   
 12. s

  seniorita JF-Expert Member

  #12
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Si za kipagani tu bali ni za kimashetani
   
 13. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #13
  Jan 17, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,936
  Likes Received: 673
  Trophy Points: 280
  nimekupata mkuu..... kipindi hiki cha JK lazima tupigike tu kwa sana mpaka pale atakapomaliza muda wake..... ndiyo tupate kukombolewa kutoka katika mateso .... hivyo maana ya makala hii ni.... JK atakapotoka madarakani atakuwa masiha kwani tutakombolewa

  ahsante wacha nisubiri masiha takapotoka madarakani ili kuwe na maisha bora kwa kila mtanzania
   
 14. l

  libaba PM Senior Member

  #14
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kikwete Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tz, ni masiha wa wapuuzi, wapotovu, na watu wenye mawazo yenye matege.
  huyo labda ni masiha wa Kifo, na maangamizo.
   
 15. Rodcones

  Rodcones JF-Expert Member

  #15
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 16, 2007
  Messages: 403
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mabadiliko ni mazuri lakini kwa muheshimiwa kikwete yatakuja baada ya yeye kutoka madarakani kwani itakuwa tayari tuna katiba mpya na itakuwa rahisi kuwafungulia mashtaka ma visadi wote na kila kitu but in one way or anather kwa sasa mheshimiwa kapotea.
   
 16. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #16
  Jan 17, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Soma tena vizuri ndugu. Mi sio mfuasi wa CCM wala JK bali kwa wana wa fasihi hiyo tunaita irony. Ila ukweli ndio huo kuwa kwa kupitia udhaifu wake sauti ya umma itafanya kazi. Hilo ndilo wazo langu kuu
   
 17. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #17
  Jan 17, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  USALAMA WA TAIFA WAnAMUITA KIKWETE MALAIKA SASA INAWEZEKANA KUNA UHUSIANO HAPA
   
 18. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #18
  Jan 17, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Jaribuni kutuliza mawazo na kusoma tena kwa uzuri ndio mjue ninamaaisha nini. Nimesema si CCM itatupatia maisha bora bali CCM kupitia jk ni chombo tu cha kutufanya watanzania tuamke. Mdau mmoja hapo juu katumia lugha ya kawaida ya kusema ni ajent. True, ila nina sababu za kutuia jina la masiha
   
 19. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #19
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Hoja yake ni kwamba haya mateso tunayopitia ni muhimu kutufungua macho na masikio,kwamba tuelewe uovu unaoendelea hapa nchini na tuungane na wapinga uovu kuondoa mafisadi ambao JK ni sehemu yao,unless yeye anataka kuwageuka wenzie.....JK ni massiah mwovu ndani ya waovu,so atawageuka waovu ili sisi tusalimike na Tanzania yenye neema ipatikane,kweli ukistaajabu ya Mussa utayaona ya firauni......mwiteni shetani shetani na messiah messiah...........:car:
   
 20. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #20
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,280
  Trophy Points: 280
  Halafu eti humu kuna watu wanajiita Great Thinkers wakati uwezo wao wakufikiri ni mdogo, mtoa mmada ana ujumbe mzito hata kama presentation amekosea kuipanga lakini kwa mtu yeyote anaesoma na kutafakari kabla hajacoment kitu atakubaliana na mada hii.
  Hata mimi nimeanza kuamini kwamba kikwete ni chaguo la mungu kwa sababu hizi hapa;
  1. ndio kiongozi dhaifu kuwahi kutokea hapa Tanzania huenda mungu ukombozi wetu anauleta kwa kumtumia kikwete ili muone ishara zote kwamba ccm haina tena uhalali wa kutawala, ili tuiondoe kwa amani kupitia masanduku ya kura.
  2. Mzee mwinyi aliwahi kuonesha ujasiri na maamuzi magumu kwa kumfukuza kazi Augustino Mrema, lakini kikwete hilo kwake sahau.
  3. kuendelea kumvumilia makamba kuwa katibu mkuu wa ccm wakati ccm imesheni wasomi na watu makini wenye vission, hiyo ni ishara ya nyakati kwamba mungu anamtumia kikwete na makamba ili Watanzania wairudishe nchi yao mikononi mwao na tuanze kujitawala wenyewe.
  Ushauri: tujifunze kwanza kujuwa mwandishi wa hoja yeyote ana maudhui gani kabla ya kubwabwaja bila kujuwa
   
Loading...