Kikwete na usanii wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete na usanii wake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 28, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,753
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #FFFFFF"]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]Kikwete awaasa wawekezaji
  na Mwandishi Maalum, Australia


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]RAIS Jakaya Kikwete amesema uwekezaji katika bara la Afrika ni lazima ulenge kunufaisha wananchi na sio wawekezaji wageni.
  Kikwete alitoa kauli hiyo jana mjini Perth, Australia, alipozungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Umoja wa Biashara katika nchi Wanachama wa Jumuia ya Madola, Dk. Mohan Kaul.
  Taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana ilieleza kuwa Kikwete alisema Afrika kwa sasa inakabiliwa na changamoto ya uwekezaji na kwamba ili uwe na manufaa kwa wananchi na Waafrika hauna budi kuwasaidia kuondokana na umaskini.
  Kikwete alisema ni muhimu kwa Jumuia ya Madola kuelekeza nguvu sawa katika kuzisaidia nchi wanachama kuondokana na umaskini kwa nguvu na kasi iliile ya jumuia hiyo katika kuimarisha masuala ya ujenzi wa demokrasia, utawala bora na haki za binadamu.
  "Changamoto kubwa kwa jumuia yetu sasa ni jinsi ya kuzisaidia nchi maskini za Afrika kuondokana na umaskini na jinsi gani ya kusaidia mataifa madogo ya jumuia hiyo ambayo pia ni visiwa kupambana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.
  "Ni jambo zuri kuwa katika Jumuia ya Madola tumeelekeza nguvu za kutosha katika utawala bora, demokrasia na haki za binadamu. Hili ni jambo zuri. Sasa ni wakati pia kwa nchi tajiri ndani ya jumuia yetu kusaidia nchi maskini," alisema Rais Kikwete.
  Wakati huohuo, Rais amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Shell, Bwana Guy Outen.
  Katika mkutano huo, viongozi hao wawili wamezungumzia mipango ya kampuni hiyo katika kuwekeza katika utafutaji wa gesi asilia katika Bahari ya Hindi.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,419
  Likes Received: 3,767
  Trophy Points: 280
  Kabla ya wawekezaji wapya, anajuwa hawa waliopo nchini wanawasaidia ni wananchi wa TZ? Kama si mahesabu ya MEGAWATI lakini umeme hakuna?
   
 3. undugukazi

  undugukazi JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 305
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Embu watanzania mbadirike na kua na roho za ku appreciate hata kwa kidogo anachofanya raisi wenu??? Yote yanafanywa kwa ajili yenu na nyie walalamikaji mmeifanyia nini nchi yenu...mwisho wa siku kila mtu na mzigo wake aisee jitumeni kwa uwezo na nguvu zenu muache kulalamika kila kona...tunaelewa kuna sehemu anapaswa alaumiwe lakini hata hili la kuongea na watu wa jumuiya ya madola mnaita usanii...yani kuongea tu tena point za ukweli kbs
   
 4. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hongera JK endeleza mapambano ya mabadiliko ya kiuchumi barani afrika. Najua wapo wanaobeza juhudi zako , ila hizo ni chuki tu binafsi kutokana na misukumo ya kisiasa kutoka ndani na nje ya nchi yetu au kwa sababu tu haukuwateua wao ama ndugu zao katika nafasi mbalimbali za uongozi , insingwezekana kwa maana hatuwezi kuwa viongozi wote . Wale wote wanaofuatilila mambo watakiri unavyokubalika si nchini mwetu tu bali hata kimataifa.


  "NABII HAKUBALIKI NYUMBANI"
   
 5. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Anahakikisha mabara yote ameshatia timu.Sijui kama safari hizi zina faida kwetu
   
 6. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  sawa,,,ila wewe ni msudani?madini ni kwa ajili ye2?umeckia ashanti?wao wataanza kulipa kodi mwaka huu,tangu 99,tuwaite wa mafuta na gesi,hawa wa sasa wameleta nin'
   
 7. MANI

  MANI Platinum Member

  #7
  Oct 28, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,410
  Likes Received: 1,863
  Trophy Points: 280
  Hivi Iceland ameshafika?
   
 8. BBJ

  BBJ JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 1,183
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Antactica je?
   
 9. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  Sijawahi mskia kikwete akiongea kitu cha maana zaidi uongo wake na kujichekesha chekesha rafiki akina dhando. Bakhresa na wengineo wamesaidi nini zaidi ya kutolipa kodi na kuwanyanyasa wazawa?
   
 10. BBJ

  BBJ JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 1,183
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Sisi walalamikaji ni MASIKINI,sasa unataka masikini aifanyie nini nchi yake?Na mind you kwamba umasikini huo umeletwa na haohao unaotaka tuwasifie.Hebu kua na roho ya uzalendo kwa WATANZANIA wenzako,sio unakurupuka na kutuletea PUMBA hapa jamvini kwa ajili tu ya interest zako.Shirikisha akili ki kamilifu na si MASABURI.Shame on you!
   
 11. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  Sijawahi mskia kikwete akiongea kitu cha maana zaidi uongo wake na kujichekesha chekesha rafiki akina dhando. Bakhresa na wengineo wamesaidi nini zaidi ya kutolipa kodi na kuwanyanyasa wazawa?
   
 12. BBJ

  BBJ JF-Expert Member

  #12
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 1,183
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Antactica je?
   
 13. BBJ

  BBJ JF-Expert Member

  #13
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 1,183
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  mkuu wewe ni mariki?
   
 14. Josephine

  Josephine Verified User

  #14
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 787
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hatufanyi hivyo kwakuwa anayoyasema na dhamira ya moyo haviambatani kabisa.
   
 15. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #15
  Oct 28, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  Sijawahi mskia kikwete akiongea kitu cha maana zaidi uongo wake na kujichekesha chekesha rafiki akina dhando. Bakhresa na wengineo wamesaidi nini zaidi ya kutolipa kodi na kuwanyanyasa wazawa?
   
 16. B

  Baba Collins JF-Expert Member

  #16
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  There is no need to be helped by developed countries,we have enough resources to develop ourselves. I think its high time for us to stand on our own feet. Shame on you Mr.President !!!!!!!!!!!!!
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  Oct 28, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hata mimi nashangaa sana. Unajua siku zote najiuliza hivi ikija serikali ya Chama kingine tofauti na CCM itafanyakazi kweli? Nauliza hivyo kwa sababu tayari wapo wananchi waliokwisha shiba maneno ya watu kwamba kazi ya kuhakikisha wanakuwa na maisha bora ni Serikali na kwamba wao hawawajibiki. Sasa kikatokea Chama kilichokuwa kikieneza propaganda kama hiyo kikashika hatamu kweli kitaweza kuwaambia wananchi kushiriki ujenzi wa taifa? Itakuwepo kazi kweli kweli. Wewe miaka 41 kwenye nyumba ya serikali bure leo ukataa kutoka kisa unavimbishwa kikchwa eti ni uonevu.
   
 18. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #18
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hakuna usanii hapo.
  Kama akili yako nzima utaelewa nini anamaanisha.
  Kama masaburi yamehamia kichwani siwezi kukulaumu.
  OTIS.
   
 19. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #19
  Oct 28, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hiyo ni ASHANT! Vipi kuhusu Songosongo ambayo haijaanza kulipa hiyo kodi ilhali gesi imekwisha ardhini [kwa mujibu ya ripoti yao iliyoeleza sababu za kutozalisha umeme wa kutosha]!!
  Je, hayo ni mema?
   
 20. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #20
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,419
  Likes Received: 3,767
  Trophy Points: 280
  Nalipa PAYE kila mwezi, nakatwa kodi kwenye kila ninachonunua n.k lakini kila kukicha nasikia EPA, LAPF, MEREMETA, BoT, KIWIRA, MAGEREZA, VETA, RUSHWA, MADAWA YA KULEVYA, MGAO WA UMEME, KUJIUZIA MAGARI YA SERIKALI, NGORONGORO NA MSEKWA, ARDHI YA WANANCHI WA KILOMBERO KUGAWIWA KWA VIGOGO, RICHMOND, DOWANS, MOHAMED ENTERPRISES, MFUMUKO WA BEI, BEI YA UMEME IMEPANDA KWA ASILINIA 18 LAKINI MSHAHARA ULE ULE, KUPEANA UDA, KUFIKIRI KWA MASABURI, VIJISENT, KAMPUNI YA KUKUSANYA USHURU UBUNGO (UBT), KUUZWA JENGO LA MAHAKAMA KUU, WAUWAJI WA KOMBE KUACHIWA, WAUWAJI WA WACHIMBA MADINI WA MAHENGE KUACHIWA, MAZISHI YA BALALI HAKUNA ALIYEHUZURIA, LOLIONDO IMEUZWA NA NDIYO MAANA UKIINGIA PALE SMS UNAYOIPATA KWENYE SIMU YAKO NI KAMA UPO UARABUNI.

  Wanachokifanya ni kuniibia 10 milioni na baadaye wanakuja kunipa pole ya 2 milioni toka kwenye hizo hizo hela walizoniibia, halafu wewe unataka nishangilie wakati najuwa wana 8 milioni zangu.............. ACHA UJINGA, TUWE WAKWELI
   
Loading...