Kikwete na Lowassa kunani tena?

Kikwete na Lowassa kunani tena?

Hata kama wangekaa ama kukumbatiana kabisa huyo JK ndo anatuchagulia Rais? Badala ya kujadili mambo yenye tija kwa taifa tunajidili ooh wamekaaje, wamevaa vp, suit ilishonwa wapi, kama mademu wako salon wanadiscuss mabuzz. Watu hawana dawa mahospitalin huko tunadiscuss mambo ya Rais 2015? Hapa pamekuwa so kwa ma Great thinkers tena!

Kwa hiyo we ndio una jifanya una akili saaana..by the way we ni nani mpaka ukataze watu wasi discuss mambo ya urais 2015? mambo ya madawa hospitalini na agenda kibao na za maana tume jadili mara ngapi hapa jamvini? Au we ni mgeni humu ndani huna ulijualo?

Jiheshimu mdogo wangu.
 
Labda LOWASA huyu anakubalika japo Richmond ilimchafua kidogo ila alizitumia kwa kuwapa wananchi wa MONDULI maendeleo.Ila kuna mmoja hapo akiiba tu yeye anasaidia tu wanawake kwa kuwaoa hovyo.
 
...Lowasa atakuwa Rais utabiri wa nabii TB JOSHUA utimie
 
Kwa nini Watanzania wengi wanadhani Rais wa Jamhuri ya Muungano atatoka CCM?

Tanzania kwa sasa tuko kwenye multiparty system, kwa maana kwamba, kwa nini hatuangalii nje ya CCM, hasa ikichukuliwa kuwa kuna hili dubwasha kwa sasa linaitwa UKAWA linalobeba one nominee for four political parties.
 
No wonder watu wanachota pesa tu!!!
Yaani hili nalo ni mjadala??!!!!
 
Nilikaa jukwaa kuu leo sherehe inaanza hadi mwisho,hakuna eneo ambalo JK na EL waliweza kusimama karibu hivyo Zaidi ya salamu tu - tena JK alitaka kumpita EL bila kumpa Mkono isipokuwa alifanya kulazimishwa, anyway angalieni hiyo Picha yenu vizuri mbona EL hana miguu?

Una mambo ya kimaku sana wewe
 
Kwa nini Watanzania wengi wanadhani Rais wa Jamhuri ya Muungano atatoka CCM?

Tanzania kwa sasa tuko kwenye multiparty system, kwa maana kwamba, kwa nini hatuangalii nje ya CCM, hasa ikichukuliwa kuwa kuna hili dubwasha kwa sasa linaitwa UKAWA linalobeba one nominee for four political parties.

huwezi ukachukua uraisi tanzanzania huku umetumia mwaka mmoja au miwili kujipanga, angalia CUF zanzibar tangu 1995 imeanza kua na nguvu zanzibar na 2010 imekuja kushindwa kwa 1%, sio mwanasiasa sana ila ukawa waendelee kupinga katiba na vyama vya siasa vibakie kama vilivo ili chadema waitafute JMT NA CUF WAITAFUTE ZANZIBAR otherwise ni kuipa ccm nafasi ya kushika madaraka mpaka mwisho wa dunia
Kwa siasa zetu.vyama vya kipinzani vinahitaji kujipanga na sio kutumia nguvu
 
Hata mimi siipendi sana CCM ila kama watamuweka mgombea uraisi wa JMT kutokea zanzibar, basi CCM vile vile itajiwekea nafasi kubwa ya kushinda kule zanzibar. Kwa vyovyote iwezekanavyo CDM lazima wajifunze kwa CUF hata kama CDM ni wasomi kuliko CUF.
Naunga mkono hoja inayoelezwa na Pasco
 
Last edited by a moderator:
Dah nchi hii sasa ni mipango, timing, na propaganda ukizubaa tu utapigishwa picha bila kujua na picha yako itatumika ambavyo hukutarajia.
 
Ni swali tuu nauliza?.

Jee inawezekana kuwa mmoja kati ya watu hawa, ndiye rais wetu 2015?!.

Sababu nilizieleza kabla.

Japo hakuna kupokezana: Kiukweli, kihaki, kihalali, 2015 ni Zamu ya Zanzibar!.

Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa..

Pasco
Mkuu najua mnampenda sana Lowassa lakini tatizo wakina Mkapa et al,wameshamuandaa mtu wao na wengi mtashangaa 2015.Wanataka kurudisha system ya Mwalimu kupata rais kwasababu JK kawaangusha.Salim alipaswa kuwa rais 2005 ila kuna kitu alifanya then yupo alitakiwa kufuata badala yake ndiyo uyo rais ajaye.Team Membe & Lowassa note my words.
 
zanzibar msubiri kwanza mpaka 2035 ndio zamu yenu,nyie si muna marais wenu kule sasa uroho wa nini kutaka huku na huku
 
Picha ni ya jana Mungu hugeuza mabaya kuwa Baraka.
Wanaomtakia Edo mabaya wataumbuka
 
Ni protocol ipi iliyoandaa kiti pembeni ya Raisi akae pembeni na Lowassa? - Kumbuka ule usemi wa Lowassa MIMI NA KIKWETE HATUJAKUTANA BARABARANI!

IMG_7973.jpg
Hii picha ukiangalia haraka haraka unaweza kudhani kwamba EL yupo pembeni ya JK lakini ukiiangalia kwa makini, utagundua kwamba EL yupo kiti cha nyuma...second row. UKitaka kugungua, angalia mguu wa kushoto wa JK ambao ni kulia kwako... JK hapo anaonekana yupo mbele ya kiti wakati EL yupo nyuma ya kiti... kwahiyo hawajakaa kwenye same row hao, EL yupo viti vya vyuma!
 
namkubali sana Edward, ila alikuwa amekaa mstari wa nyuma,na alikuwa amekaa na Msuya
 
Hiyo picha ni ya jana kwenye sherehe za Uhuru wa Tanganyika. Kilichopo hapo Lowassa kasimama mstari wa pili yaani nyuma; dili lililofanyika hapo ni kuhakikisha kikwete anaacha mwanya wa kutosha ubavuni mwake na Mwamnyange ili mkakati wao ukamilike. Ndipo mpiga picha akaichukua usawa wa nyuzi 45 ili aonekane wako pamoja kama mtaji wa kuwachanganya wananchi kisiasa kwamba ndiye aliyeandaliwa 2015. Huu upuuzi hauvumiliki na ukomeshwe mara moja.
 
Pasco, kwa nini umeiedit hiyo picha? Weka kama ilivyochukuliwa na michuzi blog
image.jpg
 
zanzibar msubiri kwanza mpaka 2035 ndio zamu yenu,nyie si muna marais wenu kule sasa uroho wa nini kutaka huku na huku

wazanzibari wa CCM waliowengi hao wa CCM hawana wasi wasi kuhusu huku bara nani atashinda. Wasi wasi wao ni kule zanzibar je ccm wataipata nchi. Hapa ni hekma tu zinazotumika za kisiasa. Huyu mtoa mada sio mzanzibar
 
Back
Top Bottom