Kikwete Mzee wetu, mbona bashasha imepotea ghafla?

Kikwete Mzee wetu, mbona bashasha imepotea ghafla?

WATANZANIA BUANA,SASA WEWE ULITAKA ASIZEEKE KWANI YEYE NI JIWE? HATA JIWE NALO LINAZEEKAGA JAMANI LIKIPIGWA NA JUA SANA LINAPASUKA LENYEWE,ACHENI MAMBO YA AJABU AJABU HAPA,WE ULITAKA AWEJE SASA,JUA JK SASA ANAKIMBILIA 70 YRS MUDA SI MREFU PENGINE AKAFIKISHA MIAKA YA AHADI YA BINADAMU YA KUISHI MIAKA 70
Kujua hilo usemalo inahitaji busara, hongera sana
 
Kati ya vitu ambavyo JK alijipotezea heshima ni kuingia kikao cha CC na majina yake mfukoni

Pili aliyemtegemea kama atamrithi akapigwa mweleka

Tatu ni usaliti mkubwa aliyomfanyia rafiki yake wa muda mrefu Na aliyemsaidia kwa hali na mali kuingia magogoni 2005, kitu hiki hasa ndo kinachomtesa

Nne ni tumbua tumbua ya kipenzi cha wananchi Mh JPM

kwa mkutadha huu lazima anyauke na kusinyaa
Na wewe ulitaka amwachie huyo rafiki yake kipenzi wa cku nyingi!? Km ni hivyo je wengine wasio rafikize vipenzi pengine pamoja na wewe mngenufaika na nini juu ya upenzi wao!? Hoja nzuri la hapo kwenye rafkie kipenzi pameharibu!
 
Hakuna mzazi anekuwa na furaha mwanae anapo huzunika, tangu mirija ya kina Riz moko imekatwa familia nzima imekuwa kama imepata ugonjwa wa kupooza, yule doo aliekuwa anatoa kashfa kwa vyama vya upinzani sasa hivi kazama kabisa hajitokezi hata kumpa pongezi Magufuli kwa kazi ILIYOTUKUKA ya kuwapoteza waliokuwa wanaishi kama malaika. Lazima baba awe mnyonge tu.
 
Kwa taarifa yako JK ni mkubwa kwa umri kuliko Lowasa! Kikwete kazaliwa 1950 na huyo Edo 1953 kwa hiyo unavyosema eti alionekana ni mzee kuliko Edo ni kweli ni kaka yake!
 
Unapigania kumtetea mtu hata asiyekujua wala kukuthamini, utakuwa na matatizo ya akili siyo bure,
fisadi Lowasa hajui hata kama unaishi Dunia hii,
kwa nini usijali familia yako zaidi?
Hivi na wewe Barbarosa ambaye tunakuona siku zote humu JF ukiwakingia kifua viongozi wakubwa wa CCM hata kwa yale maovu ya dhahiri, tukuulize na wewe hao akina JPM wanakufahamu?

Au angalau siku moja waliwahi kukutembelea huko madongo poromoka unakoishi na kukupa pongezi kutokana na kazi kubwa unaofanya mitandaoni ya kuwatetea?

Zaidi sana ninachojua unachoambulia ni T/Shirt za bure za kijani unazopata kila inapofika wakati wa uchaguzi, tena T/Shirt zenyewe unazipokelea kwa mjumbe wako wa shina wa Chama kwenye mtaa unaoishi...........
 
Na wewe ulitaka amwachie huyo rafiki yake kipenzi wa cku nyingi!? Km ni hivyo je wengine wasio rafikize vipenzi pengine pamoja na wewe mngenufaika na nini juu ya upenzi wao!? Hoja nzuri la hapo kwenye rafkie kipenzi pameharibu!
Hapana mkuu. Jamaa katoa comments zake kuhusu mada pendwa inayojadili sura na uzee wa m/kiti cha kijani mtarajiwa,basi.
Mambo ya 'unufaika' ni athari za umma. Yy yupo sahihi.
 
Kiukweli mzee wetu Kikwete kachoka jana tulikuwa wengi sehemu tunaangalia taarifa ya habali kila kila mtu aliongelea hilo.. Kakonda harafu kazeeka sana
 
Hapa Edo anaingiaje kaka? Acha ushabiki usio na tija
Kumbe mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu eeh?

Mwaka jana wakati wa kampeni mlipokuwa mnafanya jokes kuwa Edo anaumwa hadi anajisaidia jukwaani si mlikuwa mnachelelea?

Ujumbe ambao tunapata hapa ni kuwa sisi binadamu hatupaswi kushangilia matatizo ya wengine, vile Vile tunapata meseji ya usimtukane mamba Kabla hujavuka mto.............
 
JK atakumbukwa kuwa alikuwa mzee wa vicheko na bashasha hata pale aliposhambuliwa kwa maneno ya kuudhi.

Kwa waliomuona Jana akifungua KK kwa hakika sio yule tunayemjua. Kwanza anaonekana mgonjwa na mzee kuliko hata mzee Mwinyi.

Nini kimemsibu mzee wetu hata katika siku aliyopaswa kuonyesha furaha? Siku ya kustaafu kabisa uongozi.

Kwa muonekano wa Jana jinsi alivyo choka na ukimuangalia kwa sasa rafiki yake Edward na ukiwasimamisha pamoja waweza kudhani Jakaya ni baba na Edo ni mwanae au mdogo wake wa mbali.

Kuna nini hii sudden change?
mzee kuliko mwinyi?????????????????? hah au lamda tezi dume imerusi kuugua kwa binadamu ni kawaida ........muombee afya iimarike
 
It is true kwa kila aliyeangalia taarifa za habari za luninga usiku wa jana aligundua kuwa yule siye JK walizoea kumuona mwenye full tabasamu......

Tunapata somo moja kubwa sana ya hiyo kitu kuwa kuugua siyo kufa............

Nakumbuka madongo ambayo masisiem walikuwa wakimpiga Edo (including na JK mwenyewe) walipokuwa wakisema Ikulu siyo ward ya wagonjwa ambayo wanapelekwa wagonjwa.......

Sasa ndiyo umethibitika ule msemo unaosema Mungu si Athumani...........

Sasa imekuwa vice versa, Edo aliyekuwa anakejeliwa kuwa mgonjwa mahututi hadi kudaiwa anajisasaidia majukwaani sasa yuko fit kweli kweli na JK aliyekuwa ngangari sasa ndiye anayeonekana yuko gonjwa gonjwa.......
Kwani Kikwete yupo Ikulu?
Au kutokua na furaha mpk mtu aumwe?
Unajua yamemsibu yapi mpk awe moodless?
What if ni family matter, business matter, etc.

Usimlinganishe Kikwete na huyo mgonjwa wa makorokocho plz.
Tena mumuache Kikwete wetu apumue.
 
Unapigania kumtetea mtu hata asiyekujua wala kukuthamini, utakuwa na matatizo ya akili siyo bure,
fisadi Lowasa hajui hata kama unaishi Dunia hii,
kwa nini usijali familia yako zaidi?
Nlijua utakuja wanguwangu ukipepesuka vp wewe unayemkingia kifua naye anahisa kwako nini. Sisi tunajadili Jambo lillilopo we unatokwa povu tuliza munkari.
 
JK atakumbukwa kuwa alikuwa mzee wa vicheko na bashasha hata pale aliposhambuliwa kwa maneno ya kuudhi.

Kwa waliomuona Jana akifungua KK kwa hakika sio yule tunayemjua. Kwanza anaonekana mgonjwa na mzee kuliko hata mzee Mwinyi.

Nini kimemsibu mzee wetu hata katika siku aliyopaswa kuonyesha furaha? Siku ya kustaafu kabisa uongozi.

Kwa muonekano wa Jana jinsi alivyo choka na ukimuangalia kwa sasa rafiki yake Edward na ukiwasimamisha pamoja waweza kudhani Jakaya ni baba na Edo ni mwanae au mdogo wake wa mbali.

Kuna nini hii sudden change?
Msoga kugumu jamani!1
 
Dah, bora hata na wengine mmeliona hili, juzi kati nilimuona kwenye TV moja yaani kaisha ile mbaya mpaka nikajiuliza inakuwaje Mh. Rais wangu mstaafu kaisha hivi
 
JK atakumbukwa kuwa alikuwa mzee wa vicheko na bashasha hata pale aliposhambuliwa kwa maneno ya kuudhi.

Kwa waliomuona Jana akifungua KK kwa hakika sio yule tunayemjua. Kwanza anaonekana mgonjwa na mzee kuliko hata mzee Mwinyi.

Nini kimemsibu mzee wetu hata katika siku aliyopaswa kuonyesha furaha? Siku ya kustaafu kabisa uongozi.

Kwa muonekano wa Jana jinsi alivyo choka na ukimuangalia kwa sasa rafiki yake Edward na ukiwasimamisha pamoja waweza kudhani Jakaya ni baba na Edo ni mwanae au mdogo wake wa mbali.

Kuna nini hii sudden change?
Hata mimi nilimshangaa sana. Kachoka mbaya. Dah! Sijui ni haya majipu yanayotumbuliwa au ni kukosa safari za nje? But why so soon? Amechoka mno Kikwete jamani. Hadi anatia huruma.
 
Kati ya vitu ambavyo JK alijipotezea heshima ni kuingia kikao cha CC na majina yake mfukoni

Pili aliyemtegemea kama atamrithi akapigwa mweleka

Tatu ni usaliti mkubwa aliyomfanyia rafiki yake wa muda mrefu Na aliyemsaidia kwa hali na mali kuingia magogoni 2005, kitu hiki hasa ndo kinachomtesa

Nne ni tumbua tumbua ya kipenzi cha wananchi Mh JPM

kwa mkutadha huu lazima anyauke na kusinyaa
Nadhani yote haya anapoyatafakari yanamnyima usingizi na hivyo kumzeesha.
 
Hata mimi niliona labda kama atakuwa alikuwa anaumwa vinginevyo anahitaji apate muda mwingi sana wa kupumzika.
 
Back
Top Bottom