Kikwete: MZEE NYERERE

Kikwete: MZEE NYERERE

SABABU NI HII HAPA

JINSI KIKWETE ALIVYOONDOKA MONDOLI

Kipindi hicho mkuu wa chuo alikuwa Gideon Sayore, Kikwete alikuwa ni mmoja wakufunzi wa siasa chuoni hapo.

Sasa ilikuwa hivi,

Mzee Sayore alikuwa anafuga ng'ombewengi pamoja kufanya shughuli za kilimo kwawingi wakati huohuo akiwa mkuu wa chuo cha kijeshi Monduli.

Hivyo basi baada ya kuona ng'ombe wanatoa maziwamengi mno na mazao yametapakaa mashambani,. akaamua kuwa awe analiuzia jeshi mazao kama vile maharage na mahindi pamoja na maziwa na nyama kutoka kwenye mifugo yake.......na pesa anachukua yeye mwenye mazo.

Aliendelea kufanya hivyokwa kipindi kirefu tu.. ikiwa ni kama sehemu yake ya maisha....

Sasa bwana ,,kumbe Kikwette (JK) ilikuwa inamuuma sana sana, yaani mno! sasa haieleweki kama ilikuwa kweli ni kwa uzalendo ua wivu tu....akaandika barua kwa raisi kipindi hicho JK Nyerere.

Katika barua hiyo akaandika lawama nyiingi mno na majungu mengi sana dhidi ya Sayore, akimwita bepari, bwenyenye, mnyonyaji n.k huku akisema hafai kuwa mkuu wachuo hicho kwakuwa navunja miiko ya uongozi na mambo mengine meengi (si mnamjua JK anavyojua kupiga fitna!)...

Basi bwana, akamalizia mwisho kwakujiandika jina lake na sahihi yake huku akijiita mzalendo kamili barua ikapostiwa ikiwa imeadresiwa kwa rais wa nchi wakati huo!......

Mwalimu, aliipata barua ile aliifungua akaisomaaaa kisha akapiga hesabu zake....sijui aliwaza nini mzee yule, akaihifadhi ile barua ikaa sana ofini kwake bila kuchukua uamuzi wowote.

Siku moja alipokuja mkuu wa majeshi wakati huo "General Mtukula" (David Musuguli) ofisini kwa Mwalimu ndipo kipindi hicho, mwalimu akampa ile barua kutoka kwa Kikwete "akisema hayo ni maMbo yenu kayamalizeni hukohuko".

Basi bwana ile barua Mkuu wa majeshi alikaa nayo muda hivi kwenye makabrasha yakee...., sasa siku moja alikuja Mkuu wa chuo cha kijeshi Monduli(Sayore) Dar es salaam kufanya shughuli za kikazi akaenda hadi ofisini kwa Mkuu wa majeshi.

Baada ya shughuli kwisha na Sayore akiwa anajiandaa kwenda Monduli Mkuu wa majeshi alimwita, akampa ile barua ya Kikwete aliyomwandikia rais!!....

Sayore akaisoomaaa wee akashangaa mno!! na akafura kwa hasira yule mmasai...., akuliza mwalimu kasemaje? Akaambiwa mwalimu kasema yamalizeni wenyewe!!.... Akasema naam, na akaondoka na ile barua hadi Monduli...

Alipofika tu yule mmasai aliitisha kikao cha wakufunzi wote na wakuu wengine pale chuoni, wakati wanajikusanya kwenda kwenye chumba cha mkutano yeye aliamua kwenda kutoa copy ile barua ya Kikwete, kopi nyingi idadi sawa na wajumbe wa mkutano ule....

Alipoingia mkutanoni akawaona wakuu na wakufunzi wote wameketi wakimsubiri wajue alicho waitia,.. akaanza kwa kuwauliza..jamani kama kuna mtu ana matatizo, au anaona kuna jambo haliendi sawa anyooshe mkono na aseme kinacho mkereketa......watu wote wakawa kimya huku wengine wakisema hamna kitu wala tatizo mkuu akiwemo Kikwette!!!

Basi bwana, tumalizie mkasa huu wa kikwete..

Sayore akaanza kuwagawia zile nakala (copies) za ile barua ya Kikwete kwenda kwa rais akawagawia wooote including Kikwete!!! Huku yule mmasasi Sayore akiwa amefura kwa hasira, macho mekunduuu! Akagonga ngumi juu ya meza kwa hasira na kusema someni hiyo barua!! kisha akatoka na kusema anakuja muda si mrefu...

Hapo Kikwete akajua kifo chake kimefika, akikumbuka macho ya yule mmasai! akatetemeka macho yakamtoka kwa woga!.. na wenzie wakamwanzishia zogo mle ndani......

Alichokifanya ni kuondoka haraka pale kikaoni wenzie wakajua bado yupo chuoni, kumbe safari ya Dar ikawa imeanza...!! Jamaa alitembea uchochoroni kwa muda mrefu sana huku akiogopa kabisa kuingia barabara ya kuu...

Mashuhuda wanasema yule bwana akaja kupanda lift ya gari za vyama vya ushirika maeneo ya USA RIVER..na hiyo lift hakuiomba yeye bali alipofika pale alikutana na shimbo ambaye alikuwa arusha mjini kwa mjomba wake ndiye alimuombea lift kwenye magari hayo na kumuelekeza kikwete aende nyumbani kwa mjomba wake shimbo aliyekuwa akiishi arusha mjin.na huo ndio ulikuwa mwanzo wa urafiki wa kikwete na shimbo na hawa watu hawawezi kuachana na shimbo. Mpaka sasa shimbo ndiye msiri na anatumika sana katika kuhifadhi mali za kikwete...tuendelee na habari hii.. kikwete hakukumbuka kubeba mzigo wowote!! Just imagine kutoka Monduli hadi hapo jamaa aliteseka sana... lakini yeye hakujali, cha muhimu ilikuwa kusalimisha maisha yake......

Basi huo ndiyo ukawa mwisho wa JK Monduli,........... hukurudi akaja Dar na kupangiwa kazi nyingine na chama... lakini alikuwa anamlaani sana Nyerere eti kwanini alimfanyia vile!!

Hicho ndicho chanzo cha JK kumchukia mwalimu na kugoma katakata kumwita baba wa taifa hadi leo! Yeye humwita mzee Nyrere tu au mwalimu baasi...na mara chache akiwa nje ya nchi humwita 'Father of our Nation', lakini ni pale anapotaka kupigiwa makofi kwa nukuu za Mwalimu....
aya ya ya ya this is epic.i *%&% love JF.
 
Binafsi nadhani anatumia njia nyingine za kumuenzi. Kwa mfano kujiita JK (Julius Kambarage) ni wazi yeye ni JM (Jakaya Mrisho) inahitaji jicho la ziada kuona hili?
 
Huwa namshangaa yeye anapojiita eti Dr. Dokta gani hawezi hata kuongea!!!! Halafu udokta wenyewe wa kupewa chuo cha kata UDOM, ptuuuuuu!!!

ukumbuke pia prof wako Mukandara wa Udsm ashamtunuku pia.
 
Kweli mkuu, huyu jamaa atanichosha, sasa hivi akiuliza tena namkaushia.

hunijibu au huna jibu? Nyerere kumwita baba ni desire ya mtu sio lazima, ndio maana Kikwete anamuita Mzee, mimi namuita Babu au marehemu Nyerere kwasababu ana umri sawa na marehemu babu yangu!
 
Tatizo lenu hamuwi wawazi, unaposema kuwa Nyerer aliwakuta watu wameadvance na kuweka mtandao chama Tanganyika nzima, hivyo Nyerere hastahili kupewa heshima ya Baba wa Taifa una maanisha yupo unayemjua wewe/nyie kuwa anastahili kuitwa baba wa Taifa tofauti na Nyerere, ni vizuri ukatutajia ili na sisi tumuite huyo ndio baba wa Taifa,

Tatizo ni kwamba historia yote ya vuguvugu la Watanganyika wakati wa enzi za T.A.A haijaandikwa kwa makusudi na utawala wa Nyerere ili kuwapa Watanzania picha kwamba mambo yote ya kudai uhuru yalianzia T.A.N.U alipoingia yeye. Baba wa Taifa letu lazima awe muasisi wa T.A.A. kwani ndio mtandao ulioanza kuwaunganisha Watanganyika. Sasa waulizwe wazee wachache waliobaki waliokuwepo wakati T.A.A. ilipoanzishwa ndio watatuambia nani anastahili kuitwa Baba wa Taifa
 
Mwanzo, nilidhani utakua uzushi, ila leo kupitia maadhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa CCM, ndio nimeamini kupitia matamshi yake. Hv ni kwanini Ndg. Mrisho Kikwete huwa hataki kutamka Jina "Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere"????
Je na zile picha za kumbukumbu zenye Jina la Baba wa Taifa..., ziliandikwa kimakosa??

safi sana unajua ukisoma unatakiwa kila kitu ukifanye kwa kujiuliza sababu za msingi za kufanya kitu hicho ndo maana Jk akireason haoni sababu ya kumuita Nyerere Baba wa taifa maana baba wa taifa hili halali ni yule alieanzisha harakati za TAA na wala c nyerere na Historia hii imefichwa ili kuwabrainwash vilaza ila msomi wapaswa kijiuliza na kuzifuatilia harakati za Mwanzo ndio utajua nani alipaswa kuitwa Baba wa taifa na baada ya Uhuru kundi hilo la wazee wa TAA lilifanyiwa nn na mwisho wake ulikua nn. Tuache kuburuzwa
 
Tatizo ni kwamba historia yote ya vuguvugu la Watanganyika wakati wa enzi za T.A.A haijaandikwa kwa makusudi na utawala wa Nyerere ili kuwapa Watanzania picha kwamba mambo yote ya kudai uhuru yalianzia T.A.N.U alipoingia yeye. Baba wa Taifa letu lazima awe muasisi wa T.A.A. kwani ndio mtandao ulioanza kuwaunganisha Watanganyika. Sasa waulizwe wazee wachache waliobaki waliokuwepo wakati T.A.A. ilipoanzishwa ndio watatuambia nani anastahili kuitwa Baba wa Taifa
Wewe na huyo hansy wa East mmeandika kitu kimoja, sidhani kama ni coincidence ila nadhani mna source moja ya taarifa, kitu ambacho sitaki kuamini ni kama hao wanaowaeleza hayo hawawaelezi pia kuwa ni nani anaestahili kuitwa baba wa taifa, kama ndivyo, basi hawana hoja, huwezi kusema kuwa mtu flani hafai bila kuwa nambadala, Ningependa mkawaulize swali hao wanaowalisha hizo propaganda hivi,
Baba wa Taifa ni yule kiongozi wa kwanza wa taifa huru au ni yule aliekuwa wa kwanza kuanzisha chama?
Wakikujibu njoo tena tuendelee na mjadala.
 
Kwani ni lazima tuwe na baba wa Taifa? Kusipo kuwa na mdadala nini madhara yake? Cheo cha Ubaba wa taifa kinachangia kiasi gani kwenye GDP?
 
Kwani ni lazima tuwe na baba wa Taifa? Kusipo kuwa na mdadala nini madhara yake? Cheo cha Ubaba wa taifa kinachangia kiasi gani kwenye GDP?
Wewe ulishasikia Taifa gani duniani halina Baba waTaifa?, kama ni kweli unaamini kuwa cheo cha baba waTaifa hakina thamani, kwa nini wewe na huyo mwenzio mnalilia Nyerere asiitwe baba wa Taifa nabadala yake aitwe huyo mnaedai ameanzisha T.A.A?
 
Kwani ni lazima tuwe na baba wa Taifa? Kusipo kuwa na mdadala nini madhara yake? Cheo cha Ubaba wa taifa kinachangia kiasi gani kwenye GDP?
Yaani swali ni hivi, kama hicho cheo hakina thamani kama unavyodai, inawauma nini nyie Nyerere kuitwa hivyo?, mbona mnakuwa na roho za korosho sana nyie.
 
Wewe na huyo hansy wa East mmeandika kitu kimoja, sidhani kama ni coincidence ila nadhani mna source moja ya taarifa, kitu ambacho sitaki kuamini ni kama hao wanaowaeleza hayo hawawaelezi pia kuwa ni nani anaestahili kuitwa baba wa taifa, kama ndivyo, basi hawana hoja, huwezi kusema kuwa mtu flani hafai bila kuwa nambadala, Ningependa mkawaulize swali hao wanaowalisha hizo propaganda hivi,
Baba wa Taifa ni yule kiongozi wa kwanza wa taifa huru au ni yule aliekuwa wa kwanza kuanzisha chama?
Wakikujibu njoo tena tuendelee na mjadala.

Angalia list hii ya watu wanaotambulika kama Baba wa Taifa wa Mataifa yao na uniambie kama kuna uhusiano wowote wa wao kuwa viongozi wa kwanza wa Taifa huru: Hii ni mifano michache tu.

Country
Father of the Nation
Source
Cuba
Carlos Manuel de Céspedes del Castillo
Thomas, Hugh 1971. Cuba, or the pursuit of freedom. Eyre & Spottiswoode, London. Revised and abridged edition 2001, Picador, London. Chapters 16 & 17.
Croatia
Ante Starčević

Tanner, Marcus (2001). Croatia: A Nation Forged in War (2nd ed.). Yale University Press. p. 102.
Chile
Bernardo O'Higgins

Harvey, Robert (2000). Liberators: Latin America's Struggle for Independence. New York: The Overlook Press
India
Mahatma Gandhi
The Collected Works of Mahatma Gandhi, Government of India (CWMG), Vol I, p. 150
Bolivia
Simón Bolívar
Bushnell, David. The Liberator, Simón Bolívar. New York: Alfred A. Knopf, 1970
Israel
Theodor Herzl
Brenner, Michael, and Shelley Frisch. Zionism: A Brief History (2003)
Sierra Leone
Thomas Peters
Sanneh (2001), p. 50
France
Clovis 1
Brown, Peter (2003). The Rise of Western Christendom. Malden, MA, USA: Blackwell Publishing Ltd.. p. 137
Ireland
the seven signatories of the Proclamation of the Irish Republic: Patrick Pearse, James Connolly, Éamonn Ceannt, Tom Clarke, Seán Mac Diarmada, Thomas MacDonagh, and Joseph Mary Plunkett. Robert Emmett is also considered a founding father

Netherland
Prince William I of Orange (1533–1584)

Wewe na huyo hansy wa East mmeandika kitu kimoja, sidhani kama ni coincidence ila nadhani mna source moja ya taarifa, kitu ambacho sitaki kuamini ni kama hao wanaowaeleza hayo hawawaelezi pia kuwa ni nani anaestahili kuitwa baba wa taifa, kama ndivyo, basi hawana hoja, huwezi kusema kuwa mtu flani hafai bila kuwa nambadala, Ningependa mkawaulize swali hao wanaowalisha hizo propaganda hivi,
Baba wa Taifa ni yule kiongozi wa kwanza wa taifa huru au ni yule aliekuwa wa kwanza kuanzisha chama?
Wakikujibu njoo tena tuendelee na mjadala.

Na kama unataka kujua mtu mbadala basi Kleist Sykes anastahili sifa hiyo unless someone comes with a better candidate for that matter. Ukisoma hizi articles mbili zilizoandikwa na Citizen utapata picha ya ninachokizungumzia

TAA strikes fear in colonial hearts

The Sykes legacy lives on
 
Hilo jina lenyewe watu watashindwa hata kulimka kleist sykes? Baba wa Taifa kleist sykes? kwanza hata haiji.
 
Nimewahi kusikia kwa mtu kuwa Rais Kikwete huwa hamuiti Mwalimu Nyerere 'baba wa taifa', kama tunavyofanya watanzania wengi. Japo sina uhakika sana na hili, mimi pia nimemsikiliza JK mara kadhaa anapoongea kuhusu Nyerere hamuiti baba wa taifa bali humuita 'mzee Nyerere'.

Kuna sababu yoyote ya maana inayomfanya JK asimuite baba wa taifa? au ameamua mwenyewe tu kumuita hivyo? Kuna tatizo lolote kutokumuita baba wa taifa?
 
Nadhani halazimki kumwita hivyo kama vile wewe ambayo hujaanza na Mheshimiwa Rais JK.
 
Nimewahi kusikia kwa mtu kuwa Rais Kikwete huwa hamuiti Mwalimu Nyerere 'baba wa taifa', kama tunavyofanya watanzania wengi. Japo sina uhakika sana na hili, mimi pia nimemsikiliza JK mara kadhaa anapoongea kuhusu Nyerere hamuiti baba wa taifa bali humuita 'mzee Nyerere'.

Kuna sababu yoyote ya maana inayomfanya JK asimuite baba wa taifa? au ameamua mwenyewe tu kumuita hivyo? Kuna tatizo lolote kutokumuita baba wa taifa?

Wivu wa kike una msumbua......by Magufuri
 
Lakini hata akimwita babu nini kinaharibika? Lile ni jina tu lisikufanye ushindwe kuishi kwa amani!
 
Cheo chake ni Baba mtakatifu wa kato...i na si wa taifa, umesahau mkuu.
 
sisi hatujui - endelea kufanya utafiti uje utujuze. Pia unaweza kupitia hotuba zake may be zinaweza kukusaidia hasa ile aliyokuwa anatoa ufafanuzi kuhusu namna ya kumpata kiongozi tuliyemhitaji kwa wakati huo na nyufa za taifa.
 
Back
Top Bottom