Kikwete: MZEE NYERERE

Kikwete: MZEE NYERERE

Labda naye ameona atoke kivyake. Inawezekana ana taswira nyingine ya baba wa taifa.
 
Mwanzo, nilidhani utakua uzushi, ila leo kupitia maadhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa CCM, ndio nimeamini kupitia matamshi yake. Hv ni kwanini Ndg. Mrisho Kikwete huwa hataki kutamka Jina "Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere"????
Je na zile picha za kumbukumbu zenye Jina la Baba wa Taifa..., ziliandikwa kimakosa??


nawewe mbona hujamtendea haki rais wetu! ungetanguliza Dr. sio Ndg!
 
mkuu, nauliza ya kwa kwamba ni kwanini Ndugu Mrisho Kikwete, huwa hayuko tayari kumuita Nyerere, "Baba wa Taifa".
Maana leo amezihirisha kabisa kwa kumuita MZEE NYERFRE
sababu ziko nyingi lakini kubwa inaweza ikawa ni hizi juhudi zinazoendeleala za kubadilisha mkondo wa historia ambapo wanahistoria wanasema ni vigumu maana historia hutokaea yenyewe.
Si ajabu kukuta uzi huu unakuwa mrefu kiasi hichi na ukichunguza utakuta facts za swali ulilouliza


Uchochezi wa Mohamedi Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar



 
Mwanzo, nilidhani utakua uzushi, ila leo kupitia maadhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa CCM, ndio nimeamini kupitia matamshi yake. Hv ni kwanini Ndg. Mrisho Kikwete huwa hataki kutamka Jina "Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere"????
Je na zile picha za kumbukumbu zenye Jina la Baba wa Taifa..., ziliandikwa kimakosa??

Kwa kuwa hakusoma sawasawa haelewi umuhimu wa "Mwalimu"
 
Mwalimu aliwahi kumtukana sana Kikwete aliposhiriki kuanzisha fagio la chuma lengo likiwa kuwaondoa viongozi aina ya Kawawa Rashidi chamani.....Mwalimu alimtukana sana sana hata matusi ya ajabu kabisa!! kwamba wewe ni nani kwa mtu kama kawawa ktk nchi hii??....lkn alikuwa ameelezwa na Raisi Mwinyi wakati huo ktijibu kitu chochote.

Nihivi, Mwinyi alipotaka kumteua Kikwete uwaziri alimwambia aende kwanza kwa mwalimu akaombe msamaha kwa kuanzisha vuguvugu la kutaka kumng'oa Kawawa CCM......ndiyo yakamkuta hayo ya kutukanwa kama mtoto...kuwa wewe kijana mnafiki sana hata wenzio wanakujua kuwa mnafiki, n.k...

Sasa Kikwete, akichanganya hili, na lile la mwalimu kupeleka barua yake ya unafiki kwa mkuu wa majeshi(rejea jinsi alivyoondoka monduli kwa msukosuko)...bado ana kinyongo sana na Mwalimu!

Takataka za kwenye ubongo hizo, ulikuwa wap 2005 kuzungumza hayo?
 
ah hahaha ha! Jf ni watu. Na mkikosekana kama ninyi haina maana. Teh! Mkuu kweli umewachoka "jirani" zetu.




Hajawachoka,huo ndo ukweli,baba wa taifa la Zanzibar ni John Okello!!!!na c vinginevyo!!!!
 
Alikuwa na NYOMI la nguvu

13.jpg
 
nawewe mbona hujamtendea haki rais wetu! ungetanguliza Dr. sio Ndg!

Bw. Kinana na Mangula wametukataza hayo.
Kuhusu u Dr, hata mi nilipohapa naweza kua Dk. Ila siwezi kuwa "Baba wa Taifa"
 
kwani ni lazima atamke baba wa taifa, kwani akisema Mzee si inajulikana anamlenga nani, hata akisema Rais wa awamu ya kwanza inajulikana ni Baba wa Taifa tu.
 
Magari na ndege yetu ya "umma" naona yalitumika vilivyo katika shughuli ya CCM.......WHAT A WASTE!!!!!!!!!

3.jpg
 
Na wewe kwanini hutaki kumtambua na kumpa heshima yake kwa kumuita rais. Jakaya kikwete na sio ndugu. Acha roho mbaya isiyo na ustaarabu au wewe sio mtanzania . Unahangaika kutoa heshima kwa marehemu wakati walio hai wanaokutawala huwaheshimu au kwani akimuita mzee nyerere wewe utaongezewa mshahara kibaruani kwako

huwenda wewe ndio sio Mtanzania. Au kama ni mtanzania basi ulikua mkimbinzi. Kwa kukusaidia jaribu kufanya utafiti kwa kuangalia Picha ya rais ya huyo Ndugu. Kikwete. Alafu soma maneno yalio andikwa chini ya hiyo picha ndio utajua kwanini nimemuita Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete.. Maana ndio jina lililo anza kabla hata ya hicho cheo unacholilia nimuite.
Umeamkaje ndungu yangu????
 
kwani ni lazima atamke baba wa taifa, kwani akisema Mzee si inajulikana anamlenga nani, hata akisema Rais wa awamu ya kwanza inajulikana ni Baba wa Taifa tu.

kwa mtazamo wako, niuonao hata angemuita Babu Nyerere kwako ingekua sawa tu.??
 
Binafsi sijakuelewa mkuu.

Nadhani itakuwa ni aina au staili yake ya kuongea lakini hata hivyo alitakiwa kumpa heshima yake kama "BABA WA TAIFA" kujifanya uko juu ya sheria wakati mwingine kunamharibia mtu heshima.
 
Mwalimu aliwahi kumtukana sana Kikwete aliposhiriki kuanzisha fagio la chuma lengo likiwa kuwaondoa viongozi aina ya Kawawa Rashidi chamani.....Mwalimu alimtukana sana sana hata matusi ya ajabu kabisa!! kwamba wewe ni nani kwa mtu kama kawawa ktk nchi hii??....lkn alikuwa ameelezwa na Raisi Mwinyi wakati huo ktijibu kitu chochote.

Nihivi, Mwinyi alipotaka kumteua Kikwete uwaziri alimwambia aende kwanza kwa mwalimu akaombe msamaha kwa kuanzisha vuguvugu la kutaka kumng'oa Kawawa CCM......ndiyo yakamkuta hayo ya kutukanwa kama mtoto...kuwa wewe kijana mnafiki sana hata wenzio wanakujua kuwa mnafiki, n.k...

Sasa Kikwete, akichanganya hili, na lile la mwalimu kupeleka barua yake ya unafiki kwa mkuu wa majeshi(rejea jinsi alivyoondoka monduli kwa msukosuko)...bado ana kinyongo sana na Mwalimu!

Tupe yote mkuu wengine hatuijui hii habari!
 
SABABU NI HII HAPA


JINSI KIKWETE ALIVYOONDOKA MONDOLI


Kipindi hicho mkuu wa chuo alikuwa Gideon Sayore, Kikwete alikuwa ni mmoja wakufunzi wa siasa chuoni hapo.

Sasa ilikuwa hivi,

Mzee Sayore alikuwa anafuga ng'ombewengi pamoja kufanya shughuli za kilimo kwawingi wakati huohuo akiwa mkuu wa chuo cha kijeshi Monduli.

Hivyo basi baada ya kuona ng'ombe wanatoa maziwamengi mno na mazao yametapakaa mashambani,. akaamua kuwa awe analiuzia jeshi mazao kama vile maharage na mahindi pamoja na maziwa na nyama kutoka kwenye mifugo yake.......na pesa anachukua yeye mwenye mazo.

Aliendelea kufanya hivyokwa kipindi kirefu tu.. ikiwa ni kama sehemu yake ya maisha....

Sasa bwana ,,kumbe Kikwette (JK) ilikuwa inamuuma sana sana, yaani mno! sasa haieleweki kama ilikuwa kweli ni kwa uzalendo ua wivu tu....akaandika barua kwa raisi kipindi hicho JK Nyerere.

Katika barua hiyo akaandika lawama nyiingi mno na majungu mengi sana dhidi ya Sayore, akimwita bepari, bwenyenye, mnyonyaji n.k huku akisema hafai kuwa mkuu wachuo hicho kwakuwa navunja miiko ya uongozi na mambo mengine meengi (si mnamjua JK anavyojua kupiga fitna!)...

Basi bwana, akamalizia mwisho kwakujiandika jina lake na sahihi yake huku akijiita mzalendo kamili barua ikapostiwa ikiwa imeadresiwa kwa rais wa nchi wakati huo!......

Mwalimu, aliipata barua ile aliifungua akaisomaaaa kisha akapiga hesabu zake....sijui aliwaza nini mzee yule, akaihifadhi ile barua ikaa sana ofini kwake bila kuchukua uamuzi wowote.

Siku moja alipokuja mkuu wa majeshi wakati huo "General Mtukula" (David Musuguli) ofisini kwa Mwalimu ndipo kipindi hicho, mwalimu akampa ile barua kutoka kwa Kikwete "akisema hayo ni maMbo yenu kayamalizeni hukohuko".

Basi bwana ile barua Mkuu wa majeshi alikaa nayo muda hivi kwenye makabrasha yakee...., sasa siku moja alikuja Mkuu wa chuo cha kijeshi Monduli(Sayore) Dar es salaam kufanya shughuli za kikazi akaenda hadi ofisini kwa Mkuu wa majeshi.

Baada ya shughuli kwisha na Sayore akiwa anajiandaa kwenda Monduli Mkuu wa majeshi alimwita, akampa ile barua ya Kikwete aliyomwandikia rais!!....

Sayore akaisoomaaa wee akashangaa mno!! na akafura kwa hasira yule mmasai...., akuliza mwalimu kasemaje? Akaambiwa mwalimu kasema yamalizeni wenyewe!!.... Akasema naam, na akaondoka na ile barua hadi Monduli...

Alipofika tu yule mmasai aliitisha kikao cha wakufunzi wote na wakuu wengine pale chuoni, wakati wanajikusanya kwenda kwenye chumba cha mkutano yeye aliamua kwenda kutoa copy ile barua ya Kikwete, kopi nyingi idadi sawa na wajumbe wa mkutano ule....

Alipoingia mkutanoni akawaona wakuu na wakufunzi wote wameketi wakimsubiri wajue alicho waitia,.. akaanza kwa kuwauliza..jamani kama kuna mtu ana matatizo, au anaona kuna jambo haliendi sawa anyooshe mkono na aseme kinacho mkereketa......watu wote wakawa kimya huku wengine wakisema hamna kitu wala tatizo mkuu akiwemo Kikwette!!!

Basi bwana, tumalizie mkasa huu wa kikwete..

Sayore akaanza kuwagawia zile nakala (copies) za ile barua ya Kikwete kwenda kwa rais akawagawia wooote including Kikwete!!! Huku yule mmasasi Sayore akiwa amefura kwa hasira, macho mekunduuu! Akagonga ngumi juu ya meza kwa hasira na kusema someni hiyo barua!! kisha akatoka na kusema anakuja muda si mrefu...

Hapo Kikwete akajua kifo chake kimefika, akikumbuka macho ya yule mmasai! akatetemeka macho yakamtoka kwa woga!.. na wenzie wakamwanzishia zogo mle ndani......

Alichokifanya ni kuondoka haraka pale kikaoni wenzie wakajua bado yupo chuoni, kumbe safari ya Dar ikawa imeanza...!! Jamaa alitembea uchochoroni kwa muda mrefu sana huku akiogopa kabisa kuingia barabara ya kuu...

Mashuhuda wanasema yule bwana akaja kupanda lift ya gari za vyama vya ushirika maeneo ya USA RIVER..na hiyo lift hakuiomba yeye bali alipofika pale alikutana na shimbo ambaye alikuwa arusha mjini kwa mjomba wake ndiye alimuombea lift kwenye magari hayo na kumuelekeza kikwete aende nyumbani kwa mjomba wake shimbo aliyekuwa akiishi arusha mjin.na huo ndio ulikuwa mwanzo wa urafiki wa kikwete na shimbo na hawa watu hawawezi kuachana na shimbo. Mpaka sasa shimbo ndiye msiri na anatumika sana katika kuhifadhi mali za kikwete...tuendelee na habari hii.. kikwete hakukumbuka kubeba mzigo wowote!! Just imagine kutoka Monduli hadi hapo jamaa aliteseka sana... lakini yeye hakujali, cha muhimu ilikuwa kusalimisha maisha yake......

Basi huo ndiyo ukawa mwisho wa JK Monduli,........... hukurudi akaja Dar na kupangiwa kazi nyingine na chama... lakini alikuwa anamlaani sana Nyerere eti kwanini alimfanyia vile!!

Hicho ndicho chanzo cha JK kumchukia mwalimu na kugoma katakata kumwita baba wa taifa hadi leo! Yeye humwita mzee Nyrere tu au mwalimu baasi...na mara chache akiwa nje ya nchi humwita 'Father of our Nation', lakini ni pale anapotaka kupigiwa makofi kwa nukuu za Mwalimu....
 
Back
Top Bottom