Sophia Andrew
Senior Member
- Sep 19, 2014
- 114
- 7
Rais Jakaya Kikwete amewatuhumu baadhi ya wawekezaji kuwa Vitendo vya kukwepa kodi ni kikwazo katika kufanikisha masuala mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi.
Akifungua kongamano la miaka 10 ya Tume ya Utumishi wa Umma Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alikemea na kulaumu tabia ya baadhi ya watendaji wa Serikali ambao wamekuwa wakikwamisha kwa makusudi kasi ya viongozi wa kisiasa ya kuleta maendeleo.
Hivyo JK Anaunga mkono harakati za mh Mwigulu katika kupambana na wakwepa kodi na hivyo
Mwigulu aapa kupambana na wakwepa kodi
Na Angela Kiwia
NAIBU Waziri wa Fedha na Uchumi Mwigulu Nchema ameapa kuwa atahakikisha anapambana na wafanyabiashara wakubwa ambao wamekuwa wakikwepa kulipa kodi nchini.
Akiongea na gazeti hili jijini Dar es Salaam Mwigulu alisema kuwa wapo wafanyabiashara wakubwa nchini ambao wamekuwa wakikwepa kodi na kuikosesha Serikali mapato jambo ambalo halipaswi kufumbiwa macho na kiongozi yoyote mwenye nia njema na nchi yake.
Alisema kuwa yeye kama Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi atahakikisha ukwepa huo wa kodi unakomeshwa na kuwa historia kutokana na kuikosesha Serikali fedha.
Haiwezekani tuwe na wafanyabiashara ambao kazi yao ni kukwepa kodi, nchi haiwezi kuwa na wafanyabiashara wasio tayari kulipa kodi stahiki, huu ni sawa na uhujumu uchumi, nitahakikisha mpaka natoka kwenye wadhifa huu wizarani napambana nao usiku na mchana mpaka tabia hii iliyojengeka kwa baadhi yao inakomaalisema Mwigulu.
Aidha alisema kuwa iwapo kila mfanyabiashara nchini atafuata sheria na taratibu zilizowekwa katika masuala ya biashara mapato ya Serikali yataongezeka na kuweza kusaidia kutatua baadhi ya kero nchini.
Pia alisema kuwa ilikuweza kuwadhibiti wafanyabiashara hao atahakikisha wakusanya mapato nchini (TRA) wanatimiza wajibu wao na si kuwa sehemu ya wakwepa kodi.
Ni lazima kuimulika TRA ili kuweza kufanikisha hili, ni kuhakikisha kuko safi, maana wao ndiyo wanahusika wa ukusanjaji wa kodi nchini, hivyo kila mfanyakazi anatakiwa kutii kiapo chake cha kazi kwa kuwa mwaminifu, na watakaoonekana kuwa ni kikwazo zipo hatua stahiki za kuwachukulia,alisema.
Hata hivyo alieleza kuwa anaamini ya kuwa iwapo kila mfanyabiashara atalipa kodi inavyostahiki ongezeko la mapato litakuwepo tofauti na lilivyo hivi sasa.
Aliongeza kwa kusema kuwa mkakati wake wa kukomesha malipo hewa yanayofanywa na baadhi ya watendaji nchini ni endelevu maana wapo baadhi ya watendaji si waaminifu.
Tumeweza kuanza kwa kuhakikisha mishahara hewa inakomeshwa na matunda tayari yameonekana, hivyo naamini kila sekta ikiguswa fedha hizo zitaongezeka mpaka hapo mwakani, ni lazima kila Mtanzania akawa tayari kutimiza wajibu wake sio kufikiria kumnyonya mwingine.Nchi hii ni yetu sote hivyo ni jukumu letu kulinda kinachopatikana na kukigawana kwa usawa,alisema.
Alieleza kuwa Serikali imekuwa ikipoteza zaidi ya trillion 1.6- kila mwaka kutokana na malipo ya mishahara hewa jambo ambalo katu hawezi kulifumbia macho kama Naibu Waziri wa Fedha.
Ukisoma taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) utagundua ya kuwa zaidi ya sh. trillion 1.6 kila mwaka zinapotea kutokana na mishahara hewa, fedha hii ni sawa na bajeti ya Wizara nzima, haiwezekani tukaendelea kufumbia macho wizi huu.Huu ni ujambazi kama ujambazi mwingine, hivyo lazima wahusika washughulikiwe ipasavyoalisema.
Nchemba alisema- kuwa tayari ameunda kikosi kazi kwa ajili ya uchunguzi wa uovu huo ambacho kinafanyakazi zake kwa umakini na hivi karibuni ataweka bayana taarifa zilizokusanywa kutokana na uchunguzi huo.
Mimi binafsi sipo tayari kukaa tu ofisini wakati kuna watu wanatuibia bila kuwafuatilia, nakumbuka nilipotoka, katika familia masikini hivyo nayajua maisha ya Mtanzania aliyeko kijijini anayekosa mafuta ya taa huku watu watu wachache wakimsababishia Mtanzania mwenzao maisha magumu,haiwezekani na sipo tayari kuona hilo likitokea, nitapambana nao mpaka kieleweke,.
Aliongeza kwa kusema,Wale waliokuwa wanachukua fedha na kuwalipa watumishi hewa- tumeshakabidhi majina yao katika vyombo vya usalama, ila zoezi hilo linaendelea, mpaka tuwakamate wote,alisema Mwigulu.
Pia alisema kuwa tayari amenza kufanya taratibu za kupitia upya misamaha ya kodi ili kuweza kubaini mapungufu yaliyopo ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua stahiki katika kufanya marekebisho katika misamaha hiyo.
Katika suala la misamaha ya kodi ikifuatuiliwa kwa ukaribu,kunaweza kuokoa kiasi kikubwa cha fedha.Nimeshaanza taratibu za kuweza kupitia upya misamaha ya kodi, imekuwa ikilalamikiwa sana hivyo ni vyema kuweza kujiridhisha na kuondoa kasoro zilizopo ili kuokoa fedhaalisema Mwigulu.
-Akiongelea taarifa za uwepo wa mashine feki za EFD alisema kuwa tayari TRA iliweza kumkamata mfanyabiashara mmoja ambaye alielezwa kumiliki na kutumia mashine hizo hivyo hatua stahiki zinachukuliwa dhidi yake.
Katika suala la ukwepaji kodi hilo halina mjadala, yeyote atakayebainika kuwa amefanya udanganyifu atachukuliwa hatua stahiki bila kujali jina wala wadhifa alionao, haiwezekani kufumbia macho uovu huoalisema Mwigulu.
Alisema yeye kama mchumi ni jukumu lake na timu yake kubuni mbinu mbadala za kuongeza mapato nchini ili kuweza kukidhi mahitaji yaliyopo ikiwa ni pamoja na kutoa vipaumbele katika utekelezaji wa majukumu.