Kikwete: Mwigulu endelea kukamata wakwepa kodi

Kazi ya mbunge ni kutetea maslahi ya jimbo lake na ya Tanzania nzima. Lini ulisimama Bungeni kupinga misamaha ya kodi? au ulikuwa unasubiri hadi uwe waziri?
Mwigulu amepinga sana misamaha ya kodi tangu akiwa mbunge wa kawaida mpaka sasa waziri tofauti na yale mavuvuzela yenu ya chadema yanajari matumbo yao tu.
 
Alitakiwa ajianzie yeye kwanza! Yeye analipa kodi? Wabunge kutolipa kodi ni ufisadi na ulafi usiokubarika! Mwalimu analipa kodi kwa nini Mwigulu asilipe! Ana uadilifu gani huyu km si usanii km wa babake JK kutudanganya wezi wa epa hawajulikani! Upuuzo huu ni hapa Tz tu! Hakuna mfanyabiashara hata mmoja mwenye kadi ya CCM analipa kodi halali,narudia,hakuna mfanyabiashara hata mmoja mwenye kadi ya CCM analipa kodi halali! Kodi wanalipa ndiyo lkn si halali! Badala ya 12 milioni utakuta analipa 3 milioni. Wala si wa kutafuta ni wote! Bila kukomeshwa kwa rushwa iliyokithiri atatudanganya tu hapa! Wizi,ulevi wa madaraka na kijilimbikizia mali kwa viongozi ndo kumetufikisha hapa! Aanzie viongozi kwanza ndo ashuke chini!
 
Miongoni mwa wakwepa kodi ninaowajua mimi ni pamoja na mbowe,mengi na wengine kibao ila kwa mwigulu atawanyoosha.
haa haa, ameshindwa jk ataweza huyu mtengeneza majungu na kesi feki za ugaidi?
 
Mwigulu amepinga sana misamaha ya kodi tangu akiwa mbunge wa kawaida mpaka sasa waziri tofauti na yale mavuvuzela yenu ya chadema yanajari matumbo yao tu.
mwigulu hana lolote zaidi ya kutishia nyau! Hawezi kupambana na mapapa yanayoifadhili ccm kamwe!
 
Alitakiwa ajianzie yeye kwanza! Yeye analipa kodi? Wabunge kutolipa kodi ni ufisadi na ulafi usiokubarika! Mwalimu analipa kodi kwa nini Mwigulu asilipe! Ana uadilifu gani huyu km si usanii km wa babake JK kutudanganya wezi wa epa hawajulikani! Upuuzo huu ni hapa Tz tu! Hakuna mfanyabiashara hata mmoja mwenye kadi ya CCM analipa kodi halali,narudia,hakuna mfanyabiashara hata mmoja mwenye kadi ya CCM analipa kodi halali! Kodi wanalipa ndiyo lkn si halali! Badala ya 12 milioni utakuta analipa 3 milioni. Wala si wa kutafuta ni wote! Bila kukomeshwa kwa rushwa iliyokithiri atatudanganya tu hapa! Wizi,ulevi wa madaraka na kijilimbikizia mali kwa viongozi ndo kumetufikisha hapa! Aanzie viongozi kwanza ndo ashuke chini!
haa haa huo ndo ukweli kabisa mkuu, tatizo la serikali ya jk ni unafiki na maigizo katika mambo mengi ya msingi, toka rais mpaka mfungua geti!
 
Wamekamatwa kadhaa mkuu haujauona ?!
View attachment 198000
Huyu ni mmoja wa wakwepa kodi aliyekamatwa

Masikini huyu alikuwa wapi kubadili jina la biashara yake!nchi hii ukibadilisha jina tu unaanza kupata msamaha wa kodi. Tangu niifahamu Sheraton ya enzi hizo mpaka leo imebadilisha majina mpaka nimechanganyikiwa,wapuuzi hawa wanatuzuga tu!
 
Huyu jamaa kwa kupenda LIGHT TOUCH NEWS! Sasa Mwigulu awakamate wakwepaji kodi fine, then what next?!

Yeye kama citizen number on of Tanzania angeonesha mfano wa kulipa KODI badala ya kuwa kinara wa ukwepaji KODI kwa kisingizio kwamba sheria inamuruhusu kukwepa kodi (read kutolipa kodi).

Haya mambo ndiyo tulitaka yaondolewa kwenye katiba mpya, lakini ma-CCM wameyapuuza, very sad in deed.
 
Upuuzi mtupu!!! Kuna wakwepa kodi nchini wakubwa kama mawaziri na Wabunge ambao kila mwaka wanapata misamaha ya kodi ya shilingi Trilioni moja na nusu pamoja na kuwa Serikali ina matatizo makubwa ya kifedha!? Lini hao wataanza kukamatwa?

Kama huyu gamba ana ubavu wa kuwakamata wakwepa kodi aanze na HOME SHOPPING CENTRE, SUBASH PATEL na MOHAMED ENTERPRISES!!
 
Rais Jakaya Kikwete amewatuhumu baadhi ya wawekezaji kuwa Vitendo vya kukwepa kodi ni kikwazo katika kufanikisha masuala mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi.

Akifungua kongamano la miaka 10 ya Tume ya Utumishi wa Umma Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alikemea na kulaumu tabia ya baadhi ya watendaji wa Serikali ambao wamekuwa wakikwamisha kwa makusudi kasi ya viongozi wa kisiasa ya kuleta maendeleo.
Hivyo JK Anaunga mkono harakati za mh Mwigulu katika kupambana na wakwepa kodi na hivyo
Mwigulu aapa kupambana na wakwepa kodi
Na Angela Kiwia
NAIBU Waziri wa Fedha na Uchumi Mwigulu Nchema ameapa kuwa atahakikisha anapambana na wafanyabiashara wakubwa ambao wamekuwa wakikwepa kulipa kodi nchini.
Akiongea na gazeti hili jijini Dar es Salaam Mwigulu alisema kuwa wapo wafanyabiashara wakubwa nchini ambao wamekuwa wakikwepa kodi na kuikosesha Serikali mapato jambo ambalo halipaswi kufumbiwa macho na kiongozi yoyote mwenye nia njema na nchi yake.
Alisema kuwa yeye kama Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi atahakikisha ukwepa huo wa kodi unakomeshwa na kuwa historia kutokana na kuikosesha Serikali fedha.
“Haiwezekani tuwe na wafanyabiashara ambao kazi yao ni kukwepa kodi, nchi haiwezi kuwa na wafanyabiashara wasio tayari kulipa kodi stahiki, huu ni sawa na uhujumu uchumi, nitahakikisha mpaka natoka kwenye wadhifa huu wizarani napambana nao usiku na mchana mpaka tabia hii iliyojengeka kwa baadhi yao inakoma”alisema Mwigulu.
Aidha alisema kuwa iwapo kila mfanyabiashara nchini atafuata sheria na taratibu zilizowekwa katika masuala ya biashara mapato ya Serikali yataongezeka na kuweza kusaidia kutatua baadhi ya kero nchini.
Pia alisema kuwa ilikuweza kuwadhibiti wafanyabiashara hao atahakikisha wakusanya mapato nchini (TRA) wanatimiza wajibu wao na si kuwa sehemu ya wakwepa kodi.
“Ni lazima kuimulika TRA ili kuweza kufanikisha hili, ni kuhakikisha kuko safi, maana wao ndiyo wanahusika wa ukusanjaji wa kodi nchini, hivyo kila mfanyakazi anatakiwa kutii kiapo chake cha kazi kwa kuwa mwaminifu, na watakaoonekana kuwa ni kikwazo zipo hatua stahiki za kuwachukulia,”alisema.
Hata hivyo alieleza kuwa anaamini ya kuwa iwapo kila mfanyabiashara atalipa kodi inavyostahiki ongezeko la mapato litakuwepo tofauti na lilivyo hivi sasa.
Aliongeza kwa kusema kuwa mkakati wake wa kukomesha malipo hewa yanayofanywa na baadhi ya watendaji nchini ni endelevu maana wapo baadhi ya watendaji si waaminifu.
“Tumeweza kuanza kwa kuhakikisha mishahara hewa inakomeshwa na matunda tayari yameonekana, hivyo naamini kila sekta ikiguswa fedha hizo zitaongezeka mpaka hapo mwakani, ni lazima kila Mtanzania akawa tayari kutimiza wajibu wake sio kufikiria kumnyonya mwingine.Nchi hii ni yetu sote hivyo ni jukumu letu kulinda kinachopatikana na kukigawana kwa usawa,”alisema.
Alieleza kuwa Serikali imekuwa ikipoteza zaidi ya trillion 1.6- kila mwaka kutokana na malipo ya mishahara hewa jambo ambalo katu hawezi kulifumbia macho kama Naibu Waziri wa Fedha.
“ Ukisoma taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) utagundua ya kuwa zaidi ya sh. trillion 1.6 kila mwaka zinapotea kutokana na mishahara hewa, fedha hii ni sawa na bajeti ya Wizara nzima, haiwezekani tukaendelea kufumbia macho wizi huu.Huu ni ujambazi kama ujambazi mwingine, hivyo lazima wahusika washughulikiwe ipasavyo”alisema.
Nchemba alisema- kuwa tayari ameunda kikosi kazi kwa ajili ya uchunguzi wa uovu huo ambacho kinafanyakazi zake kwa umakini na hivi karibuni ataweka bayana taarifa zilizokusanywa kutokana na uchunguzi huo.
“Mimi binafsi sipo tayari kukaa tu ofisini wakati kuna watu wanatuibia bila kuwafuatilia, nakumbuka nilipotoka, katika familia masikini hivyo nayajua maisha ya Mtanzania aliyeko kijijini anayekosa mafuta ya taa huku watu watu wachache wakimsababishia Mtanzania mwenzao maisha magumu,haiwezekani na sipo tayari kuona hilo likitokea, nitapambana nao mpaka kieleweke,”.
Aliongeza kwa kusema,“Wale waliokuwa wanachukua fedha na kuwalipa watumishi hewa- tumeshakabidhi majina yao katika vyombo vya usalama, ila zoezi hilo linaendelea, mpaka tuwakamate wote,”alisema Mwigulu.
Pia alisema kuwa tayari amenza kufanya taratibu za kupitia upya misamaha ya kodi ili kuweza kubaini mapungufu yaliyopo ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua stahiki katika kufanya marekebisho katika misamaha hiyo.
“Katika suala la misamaha ya kodi ikifuatuiliwa kwa ukaribu,kunaweza kuokoa kiasi kikubwa cha fedha.Nimeshaanza taratibu za kuweza kupitia upya misamaha ya kodi, imekuwa ikilalamikiwa sana hivyo ni vyema kuweza kujiridhisha na kuondoa kasoro zilizopo ili kuokoa fedha”alisema Mwigulu.
-Akiongelea taarifa za uwepo wa mashine feki za EFD alisema kuwa tayari TRA iliweza kumkamata mfanyabiashara mmoja ambaye alielezwa kumiliki na kutumia mashine hizo hivyo hatua stahiki zinachukuliwa dhidi yake.
“Katika suala la ukwepaji kodi hilo halina mjadala, yeyote atakayebainika kuwa amefanya udanganyifu atachukuliwa hatua stahiki bila kujali jina wala wadhifa alionao, haiwezekani kufumbia macho uovu huo”alisema Mwigulu.
Alisema yeye kama mchumi ni jukumu lake na timu yake kubuni mbinu mbadala za kuongeza mapato nchini ili kuweza kukidhi mahitaji yaliyopo ikiwa ni pamoja na kutoa vipaumbele katika utekelezaji wa majukumu.[

AKAJARIBU KWA MOHAMED DEWJI aone moto wake
 
Mwigulu amepinga sana misamaha ya kodi tangu akiwa mbunge wa kawaida mpaka sasa waziri tofauti na yale mavuvuzela yenu ya chadema yanajari matumbo yao tu.

AENDE KWA MOHAMED DEWJ AONE MOTO WAKE - dah sifa za kijinga bana
 
Kamata wanaokwepa ila usiguse wanaotumia vibaya kwa maslahi yao binafsi
 
Ni danganya toto tu na kuzuga zuga machoni kwa watu, hata hiyo kodi ikikusanywa mbona ukali wa maisha upo pale pale na sasa umezidi kuwa mbaya zaidi? maendeleo hayaonekani maisha magumu , mwananchi wa kawaida ata kutengeneza milo 1 kwa siku ni shida. Lakini Rais kila wiki anaenda nje na group la watu akirudi hatuoni chochote wiki inayofuata anaenda tena. Sasaivi imekuwa kama deal tumuweke mtu madarakani ili apate kutalii akimaliza mda wake atafute kalamau na karatasi aweke tick nchi alizoenda na mara ngapi
 
Kumbuka UKAWA walisaini posho katika BMK ndio wakatoka bungeni na kwenda Kibanda maiti,Mh Mwigulu katika kupinga matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi alitoa maagizo kwa bank zote kutowalipa.

Matumizi sahihi kwani walobaki wamefanya nini la maana zaidi kuongeza gharama za tiba hospitalini?
 
Rais Jakaya Kikwete amewatuhumu baadhi ya wawekezaji kuwa Vitendo vya kukwepa kodi ni kikwazo katika kufanikisha masuala mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi.

Akifungua kongamano la miaka 10 ya Tume ya Utumishi wa Umma Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alikemea na kulaumu tabia ya baadhi ya watendaji wa Serikali ambao wamekuwa wakikwamisha kwa makusudi kasi ya viongozi wa kisiasa ya kuleta maendeleo.
Hivyo JK Anaunga mkono harakati za mh Mwigulu katika kupambana na wakwepa kodi na hivyo
Mwigulu aapa kupambana na wakwepa kodi
Na Angela Kiwia
NAIBU Waziri wa Fedha na Uchumi Mwigulu Nchema ameapa kuwa atahakikisha anapambana na wafanyabiashara wakubwa ambao wamekuwa wakikwepa kulipa kodi nchini.
Akiongea na gazeti hili jijini Dar es Salaam Mwigulu alisema kuwa wapo wafanyabiashara wakubwa nchini ambao wamekuwa wakikwepa kodi na kuikosesha Serikali mapato jambo ambalo halipaswi kufumbiwa macho na kiongozi yoyote mwenye nia njema na nchi yake.
Alisema kuwa yeye kama Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi atahakikisha ukwepa huo wa kodi unakomeshwa na kuwa historia kutokana na kuikosesha Serikali fedha.
“Haiwezekani tuwe na wafanyabiashara ambao kazi yao ni kukwepa kodi, nchi haiwezi kuwa na wafanyabiashara wasio tayari kulipa kodi stahiki, huu ni sawa na uhujumu uchumi, nitahakikisha mpaka natoka kwenye wadhifa huu wizarani napambana nao usiku na mchana mpaka tabia hii iliyojengeka kwa baadhi yao inakoma”alisema Mwigulu.
Aidha alisema kuwa iwapo kila mfanyabiashara nchini atafuata sheria na taratibu zilizowekwa katika masuala ya biashara mapato ya Serikali yataongezeka na kuweza kusaidia kutatua baadhi ya kero nchini.
Pia alisema kuwa ilikuweza kuwadhibiti wafanyabiashara hao atahakikisha wakusanya mapato nchini (TRA) wanatimiza wajibu wao na si kuwa sehemu ya wakwepa kodi.
“Ni lazima kuimulika TRA ili kuweza kufanikisha hili, ni kuhakikisha kuko safi, maana wao ndiyo wanahusika wa ukusanjaji wa kodi nchini, hivyo kila mfanyakazi anatakiwa kutii kiapo chake cha kazi kwa kuwa mwaminifu, na watakaoonekana kuwa ni kikwazo zipo hatua stahiki za kuwachukulia,”alisema.
Hata hivyo alieleza kuwa anaamini ya kuwa iwapo kila mfanyabiashara atalipa kodi inavyostahiki ongezeko la mapato litakuwepo tofauti na lilivyo hivi sasa.
Aliongeza kwa kusema kuwa mkakati wake wa kukomesha malipo hewa yanayofanywa na baadhi ya watendaji nchini ni endelevu maana wapo baadhi ya watendaji si waaminifu.
“Tumeweza kuanza kwa kuhakikisha mishahara hewa inakomeshwa na matunda tayari yameonekana, hivyo naamini kila sekta ikiguswa fedha hizo zitaongezeka mpaka hapo mwakani, ni lazima kila Mtanzania akawa tayari kutimiza wajibu wake sio kufikiria kumnyonya mwingine.Nchi hii ni yetu sote hivyo ni jukumu letu kulinda kinachopatikana na kukigawana kwa usawa,”alisema.
Alieleza kuwa Serikali imekuwa ikipoteza zaidi ya trillion 1.6- kila mwaka kutokana na malipo ya mishahara hewa jambo ambalo katu hawezi kulifumbia macho kama Naibu Waziri wa Fedha.
“ Ukisoma taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) utagundua ya kuwa zaidi ya sh. trillion 1.6 kila mwaka zinapotea kutokana na mishahara hewa, fedha hii ni sawa na bajeti ya Wizara nzima, haiwezekani tukaendelea kufumbia macho wizi huu.Huu ni ujambazi kama ujambazi mwingine, hivyo lazima wahusika washughulikiwe ipasavyo”alisema.
Nchemba alisema- kuwa tayari ameunda kikosi kazi kwa ajili ya uchunguzi wa uovu huo ambacho kinafanyakazi zake kwa umakini na hivi karibuni ataweka bayana taarifa zilizokusanywa kutokana na uchunguzi huo.
“Mimi binafsi sipo tayari kukaa tu ofisini wakati kuna watu wanatuibia bila kuwafuatilia, nakumbuka nilipotoka, katika familia masikini hivyo nayajua maisha ya Mtanzania aliyeko kijijini anayekosa mafuta ya taa huku watu watu wachache wakimsababishia Mtanzania mwenzao maisha magumu,haiwezekani na sipo tayari kuona hilo likitokea, nitapambana nao mpaka kieleweke,”.
Aliongeza kwa kusema,“Wale waliokuwa wanachukua fedha na kuwalipa watumishi hewa- tumeshakabidhi majina yao katika vyombo vya usalama, ila zoezi hilo linaendelea, mpaka tuwakamate wote,”alisema Mwigulu.
Pia alisema kuwa tayari amenza kufanya taratibu za kupitia upya misamaha ya kodi ili kuweza kubaini mapungufu yaliyopo ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua stahiki katika kufanya marekebisho katika misamaha hiyo.
“Katika suala la misamaha ya kodi ikifuatuiliwa kwa ukaribu,kunaweza kuokoa kiasi kikubwa cha fedha.Nimeshaanza taratibu za kuweza kupitia upya misamaha ya kodi, imekuwa ikilalamikiwa sana hivyo ni vyema kuweza kujiridhisha na kuondoa kasoro zilizopo ili kuokoa fedha”alisema Mwigulu.
-Akiongelea taarifa za uwepo wa mashine feki za EFD alisema kuwa tayari TRA iliweza kumkamata mfanyabiashara mmoja ambaye alielezwa kumiliki na kutumia mashine hizo hivyo hatua stahiki zinachukuliwa dhidi yake.
“Katika suala la ukwepaji kodi hilo halina mjadala, yeyote atakayebainika kuwa amefanya udanganyifu atachukuliwa hatua stahiki bila kujali jina wala wadhifa alionao, haiwezekani kufumbia macho uovu huo”alisema Mwigulu.
Alisema yeye kama mchumi ni jukumu lake na timu yake kubuni mbinu mbadala za kuongeza mapato nchini ili kuweza kukidhi mahitaji yaliyopo ikiwa ni pamoja na kutoa vipaumbele katika utekelezaji wa majukumu.[

AKAJARIBU KWA MOHAMED DEWJI aone moto wake

No stone will remain unturned
Wote watafukiwa kwani JK ameshabariki zoezi hili
 
Kamwe haiwezi kutokea gaidi mwigulu agundue Mbowe kakwepa kodi asimtangaze hadharani na kisha kumpandisha kizimbani.

Miongoni mwa wakwepa kodi ninaowajua mimi ni pamoja na mbowe,mengi na wengine kibao ila kwa mwigulu atawanyoosha.
 
Kazi ya mbunge ni kutetea maslahi ya jimbo lake na ya Tanzania nzima. Lini ulisimama Bungeni kupinga misamaha ya kodi? au ulikuwa unasubiri hadi uwe waziri?

Acha kujiweka pamba masikioni ni Mwigulu na Zitto kwa mara ya kwanza walipeleka mswaada kwa spika juu ya marekebisho ya misamaha ya kodi
 
Back
Top Bottom