Kikwete, Museveni, Lowassa, Mwinyi kuzomewa UDSM, ni ishara ya nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete, Museveni, Lowassa, Mwinyi kuzomewa UDSM, ni ishara ya nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAGAMBA MATATU, Oct 22, 2011.

 1. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 609
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 60
  WANAFUNZI wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) jana walichafua hali ya hewa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho baada ya kumzomea Rais Jakaya Kikwete.

  Rais Kikwete ambaye alikuwa ameambatana na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa pamoja na viongozi wengine wa Serikali alikutwa na zomeazomea hiyo saa 6:23 mchana wakati akiingia katika Ukumbi wa Nkrumah ambapo yalifanyika maadhimisho hayo. Wanafunzi hao mbali na kumzomea Rais huyo wa awamu ya nne pia walikuwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali huku wakiimba, "Kama sio juhudi zako Nyerere mafisadi wangesoma wapi, hatukutaki ondoka,".

  Baadhi ya mabango hayo yalikuwa yameandikwa, ''Wao walisoma bure sisi tunalala nje, Miaka 50 ya uhuru mikopo hatupati, Tusiilipe Dowans, Wanafundisha UDSM makazi Bagamoyo je ni haki?, Kama sio juhudi zako Nyerere mafisadi wangesoma wapi.

  Awali wanafunzi hao walionekana wakiwa wameshika mabango hayo lakini walizuiwa na polisi na kuelezwa kuwa kama ni ujumbe tayari ulishafika hivyo waendelee na shughuli nyingine. Hata hivyo, wanafunzi hao ambao hawakutaka kutaja majina yao walizunguka nyuma ya Ukumbi wa Nkrumah na kuyaficha mabango hayo, huku wengine wakijipanga tayari kwa kumpokea Rais Kikwete ambaye alikuwa bado hajafika eneo hilo.

  Mara baada ya Rais Kikwete kufika chuoni hapo alikwenda kusaini katika kitabu cha wageni na wakati akielekea katika ukumbi huo huku akipunga mkono, wanafunzi hao walikuwa kimya.
  Rais Kikwete wakati akiendelea kuwapungia mkono wanafunzi hao, walianza kumzomea na kutoa mabango yao waliyokuwa wameyaficha huku wakiimba, "Kama sio juhudi zako Nyerere mafisadi wangesoma wapi".
  Polisi waliokuwa eneo hilo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana walilazimika kutumia busara kuwanyamazisha wanafunzi hao ambao waliendelea kuzomea na kuimba licha ya kuwa Rais Kikwete alikuwa ameshaingia katika ukumbi huo.
  Wakati shughuli za maadhimisho hayo zikiwa zinaendelea wanafunzi hao walikuwa bado wakiimba nyimbo hizo na kuzomea, mpaka walipoombwa kutoendelea kuimba na baadhi ya polisi ambao waliwaeleza kuwa kuzomea hakuwezi kuwaletea mikopo vyuoni, bali wajenge hoja za msingi na kuziwasilisha sehemu husika.

  Hata wakati Rais Kikwete akisoma hotuba yake na kugusia maendeleo ya chuo hicho pamoja na uboreshwaji wa utoaji mikopo vyuoni, wanafunzi hao waliokuwa wakifuatilia hotuba hiyo kupitia Televisheni kubwa walikuwa wakizomea.

  "Hivi Rais anajua jinsi tunavyopigika hapa chuoni, wengine inaonekana tumepewa mikopo, lakini mpaka leo hatujapata, hivi anajua tunaishi vipi huyu, anajua tunalala wapi," walisikika wakisema baadhi ya wanafunzi.
  Katika hatua nyingine, Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika alisema kuwa kilichofanywa na wanafunzi hao kinatakiwa kutazamwa kwa macho mawili.

  Mnyika alisema kuwa ahadi zilizotolewa na Rais Kikwete kuhusu maendeleo ya chuo hicho zinatakiwa kutekelezwa na kufafanua kuwa hata katika utawala wa Mwalimu Nyerere matatizo vyuoni yalikuwapo na kwamba dawa ni kuyatatua.
  Akizungumzia kitendo cha wanafunzi hao kumzomea Rais Kikwete mbele ya Rais Museveni, Mnyika alisema kuwa hilo ni jambo la kawaida kwa kuwa Museveni amewahi kusoma katika chuo hicho na anajua harakati za wanafunzi.
  "Wakati Museveni akisoma alikuwa na kikundi chake ambacho kilikuwa na msimamo mkali na kutoa kauli za kimapinduzi kwa viongozi mbalimbali wa Afrika, Museveni anakijua hiki chuo,"


  Hii ni ishara ya watz kudanganywa na ahadi hewa za serekali ya CCM au ni mpango wa upinzani dhidi ya Serikali ya JK.????
   
 2. Mb-one

  Mb-one JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 446
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  Saaafi,big up wanafunz wa UDSM
   
 3. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #3
  Oct 22, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,248
  Likes Received: 243
  Trophy Points: 160
  Mkuu samahani kama nitakua nimetoka nje ya mada... Hii habari inaonesha ni jinsi gani wanafunzi walivo hypocrites na jinsi gani walivo a perfect crew ya kufuata nyayo za mafisadi... Wako so set katika matwaka yao... Wanalalama boom na varieties za mikopo i.e grades from A, B, C & D. Hawa wanafunzi toka siku zoote migomo inatokea hawana jipya... I appreciate the fact kua huwa mara nyingi migomo yao ina nguvu saana mana mara nyingi hutoa end result....

  Haya basi Maktaba ya UDSM iko katika sorry state.... Vitabu kibao, BUT Vitabu vya Msingi vya courses mbali mbali hamna kabisa... Waweza kuta only one copy of a book ya course ambayo inasomwa na wanafunzi si chini ya 2000 (yaweza onekana mzaha - but its the reality..... Kwamba ushawahi sikia wanafunzi wanagoma Vitabu viwepo maktaba?

  OR kwamba zile laboratories za chuo ni za kizushi ziwe za kisasa?? OR kwamba waboreshe teaching system itoke kua kukalili kwa videsa ili tu kufaulu to reading books kuprocuce true elittes sio wasomi jina?? Kamwe sijawahi sikia na wala sitarajii....

  Katika jammii ni mangapi yanafanywa na viongozi.... matukio mangaapi ambayo serkali kwa uzembe wake imefanya watu waathirike ama wapoteze maisha?? Matukio mangapi ambayo yamedhalilisha wananchi?

  BUT Huwezi kuta wanafunzi wa chuo chochote hasa UDSM wameandamana kutaka "Change" kuwakilisha wale ambao hawajabahatika kusoma na hawajui haki zao.... Hao wanafunzi more than 90% are the future fisadiz..... Sad.
   
 4. y

  yaya JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2011
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu, It is a mixed grill. They did what they thought was right.
   
 5. k

  kambambovu Member

  #5
  Oct 22, 2011
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu nakuunga mkono hoja yako hapo juu, wanatakiwa kuandamana hata katika masuala mingine ya kijamii, wanachodai ni posho tu, nawakishapata nenda katika vyumba vyao utakuta wameenda kufanya shopping kubwa tu na wengine starehe. mbona huku nje ya nchi tunaona wenzetu wanjilipia ada ingawaje wanapunguzo fulani aijalishi wewe ni maskini au la, Majority yetu sisi ni wavivu tunapenda bure tu muda wote, High school na secondary zinafika mpaka mamilioni huko Tanzania mbona hatusikii kulalama? Mbona vyuo binafsi vimejaa lakini usikii kugoma au kwakuwa mnalipa wenyewe. Acheni kuiga vijana, someni kwanza hayo mengine mtayakuta baadaye. Na sababu ingine ni kuwa watoto ni wengi huko vyuoni sasa hivi, mbona hao wanaosoma master na PHD hatuwasikii katika mizozo? Kisha kutwa wote au almost ni washabiki wa Liverpool hapo chuoni.
  Maendeleo ya Tanzania yataletwa na Watanzzania wenyewe, si kusema tu huku hatufanyi kazi, tunanunuliwa kwa wali na kanga au fulana, nenda TRA, TPA wanalipwa na kuiba shilingi ngapi, bado hawafuati maadili ya kazi na wizi mtupu pamoja na rushwa , ndiyo maana hiyo product ikitoka hapo mlimani siku ya pili wanataka wawe na kila kitu kizuri.
   
 6. damper

  damper Senior Member

  #6
  Oct 22, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 187
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kweli wengi wao ni watoto na kwa utoto wao ndo maana inakuwa rahisi kutumiwa na wana siasa njaa.
   
 7. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 780
  Trophy Points: 280
  Naona kuna watetezi wengi wanajaribu kufunika lililotokea.Ni kweli rais wetu kazomewa na ieleweke hivyo.
  Nakumbuka alirushiwa mawe mbeya mwanzoni ikulu ikakanusha badae wakasema ni kweli ila ni walevi waliorusha mawe.
  Tusiwalaumu vijana eti kwa sababu wamelalamikia haki zao tu,ukitaka kupigia kelele matatizo yote ya hii serikali inabidi uwe kichaa kwanza.
   
 8. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #8
  Oct 22, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,640
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Kweli ashadii.. Hilo nalo neno. Ila huo uwe mwanzo maana ni ujasiri wa hali ya kumwonyesha Rais kuwa huna imani naye. Na kwanini Lowassa? Wanatuchezea sinema za ajabu hawa?!
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Oct 22, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 36,278
  Likes Received: 14,518
  Trophy Points: 280
  kwa nini lowasa alienda?
   
 10. mooduke

  mooduke JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 618
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Acha kuongea utumbo bana hakuna anaependa kunyanyasika kwa kuomba na kumbuka kuwa hiyo pesa wanayoomba ni haki yao na kama hawa wangekuwa na uwezo usingeona wanabembeleza hivyo viji pesa kidogo achane unafiki nyie wenye uwezo wenu.


   
 11. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #11
  Oct 22, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sasa ukiwa na raisi kama kikwete na ccm madarakani kwa miaka 50 hayo maabara na vitabu vya maktaba vitapatikanaje wakati dowans lazima ilipwe? Wewe unadhani ni UDSM tu ? vipi mashule ya sekondari au wale watoto wa primary wanaokaa kwenye vumbi ndani ya madarasa ya nyasi? Huyo kikwete wako anatumwa na majini yake ya ilimu dunia kudai ma PHD halafu unataka watu wenye akili zao wasimzomeeeee!!!!!
   
 12. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #12
  Oct 22, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Utovu wa adabu. Kama leo wanamzomea Rais mbele yake, unatarajia nini baadae kutoka kwa vijana hawa? Kambe wao ndio mafisadi watarajiwa?
   
 13. kholo

  kholo JF-Expert Member

  #13
  Oct 22, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  sasa we unatakaje?
   
 14. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #14
  Oct 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,217
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  ukiona hivyo ukombozi waja kwa kasi kuzidi ya ccm ambayo ni nguvu za kimpumu
   
 15. MGAWARIZIKI

  MGAWARIZIKI JF-Expert Member

  #15
  Oct 22, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 306
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  It's true.
   
 16. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #16
  Oct 22, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,623
  Likes Received: 375
  Trophy Points: 180
  Kwasababu yeye na Kikwete hawakukutana barabarani au umeisahau kauli hii ya Lowassa,hii ni serikali ya maigizo kuliko maelezo.
   
 17. T

  Tetere Enjiwa JF-Expert Member

  #17
  Oct 22, 2011
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 217
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tunachoweza kujifunza hapa ni kuwa watu wamechoka na akitokea mtu akawagawia vijana hawa AK.47 na kuomba aircover ya NATO si ajabu tukaona maiti za hawa waheshimiwa zikiwa paraded kama za Khadafi na Mwanae.
   
 18. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #18
  Oct 22, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,082
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  kama kweli wanafunzi hao wamemzomea rais me nadhani si jambo la ajabu sana na kwamba hiyo ni dalili mojawapo ya uhuru wa kuongea,kutoa maoni na utawala wa sheria........pia hali km hiyo ni ya kawaida kwa wanafunzi wa vyuo...............hongera kikwete kwa kutoa uhuru mkubwa wa kuongea na kutoa maoni.
   
 19. O

  Omr JF-Expert Member

  #19
  Oct 22, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hahaha, kweli wewe unaangalia sana TV. Mambo ya kiume waachie wanaume
   
 20. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #20
  Oct 22, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 6,905
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Mkuu nakushukuru kwa uchambuzi wako mzuri, ila nataka nikukumbushe kuwa huwezi kufanya mambo ya ziada wakati mambo yako ya msingi yatakuwa yamekushinda, namaanisha kuwa kaa ukijua kuwa mikopo ni jambo la msingi kwa mwanachuo yeyote hivyo basi asilimia 99 ya wanafunzi wa chuo wanaishi kwa kutegemea mikopo, na hakuna hata siku moja ambayo wanachuo wamewahi kutangaza kuwa kwa kiwango kilichopo cha mkopo kinawatoshereza kujikimu, wewe mwenyewe unaweza kuwa shahidi mwaka jana wanafunzi walipogoma na kudai waongezewe angalau shilingi elfu kumi lakini serikali badala yake ikaweka shilingi elfu saba, unafikiri ni mtu wa aina gani hata kama ni wewe anayeweza kutetea masilahi ya mwingine wakati hata masilahi yake ya msingi yamemshinda. Kuhusu suala la wanafunzi kuwa na vitu vya gharama chuoni linahitaji kuangalia background ya huyo mwanafunzi si wote wanaosoma chuo wanatumia hela ya mkopo kununua hivi vitu, kwa mwanfunzi wa kawaida ambaye hana chanzo kingine zaidi ya mkopo hili jambo haliwezekani kabisa kama huamini fanya survey ndogo kwenye chuo au mtu yeyote
   
Loading...