Hivi unaposema nchi inaongozwa kwa kanuni na sheria, unajua maana yake au umeropoka tuu!!!? Kwenye hii scandal ya ESCROW, raisi kama mamlaka ya uteuzi amekiuka kanuni kwa kushindwa kuwawajibisha aliowapa madaraka!
Halafu unaposema swala la media, napata shida juu ya ufaham wako. Swala la ESCROW limeibuliwa bungeni, ndipo media zikatufikishia taarifa. Nikueleweshe jambo moja; ofisi ya CAG, TAKUKURU na PAC, walifanya kazi kwa mujibu wa kanuni na wakadhibitisha makosa yaliyotokea na waliosababisha hayo makosa! Sasa raisi anapata kigugumizi gani kumwajibisha Muhongo!?
Msitufanye sisi ni wajinga kiasi hicho mkuu.!
Maajabu ya Musa ni pale alipomfukuza kazi Tibaijuka kwa kosa la kukiuka maadili....! Wakati huo huo raisi anadai fedha iliyochotwa ESCROW si za umma, swali linakuja kama sio za umma, AG na Tibaijuka wanakosa gani, kama pesa zilikua za watu binafsi?!
Nikupe mfano kidogo. Kuku imeibwa mahali kwa mfugaji, wewe unakuja kupewa paja ukala. Mwisho wa siku unaadhibiwa kwa kukubali kula paja ili hali alieiba kuku anaachwa na anaonekana hana hatia...!!!! This is nonsense...!