Kikwete: Mtaumbuka baada ya 2015

Kikwete: Mtaumbuka baada ya 2015

thatha

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Posts
15,340
Reaction score
1,571
Rais , Dr. Jakaya Mrisho Kikwete amesema wale wote wanaombeza kuhusu utendaji kazi wake wataona aibu atakapomaliza muhula wake 2015.

Rais ameyasema hayo wakati akizindua mradi wa kusambaza umeme katika mikoa ya Mwanza na Geita unaofadhiliwa na mfuko wa Changamoto wa Milenia(MCC).

Rais amesema Serikali yake itavunja recodi ya kusambaza umeme katika vijiji vingi nchini.

Jk amesema Tanzania inaongoza kwa mtandao wa barabara ambao ni bora afrika mashariki huku akiwahakikishia wakazi wa Kagera kuwa meli mbili alizowaahidi wakati wa kampeni ziko njiani zinakuja.

Rais alikuwa akishangiliwa na wananchi wakati wote wa hotuba yake.

Alisema Tanzania ni nchi kubwa kuliko nchi nyinine za Afrika Mashariki ,lakini ina mtandao mkubwa wa barabara kuliko nchi kama Kenya , lakini akawalaumu watu wanaoisifia nchi hiyo jirani na kubeza mafanikio ya serikali yake.

Aidha, Rais Kikwete amewashangaa baadhi ya viongozi wa CCM pamoja na wananchama kushindwa kuzungumzia mafanikio yaliyofikiwa na serikali ya CCM na badala yake wamekuwa hodari wa kujadili wanapobezwa na wapinzani"

Source: Mwananchi
 
Mzee wa porojo, mimi hata huwa sipotezi muda wangu kumsikiliza huyo dhaifu wenu.
 
Tunasubiri reli ya kati ya kisasa - train iendayo kwa kasi.
 
Ni lini Rais ataacha mipasho na ku think critically? anaongea mambo ya ajabu sana sometimes
 
siku CCM itaacha kuwatetea mafisadi ndio siku hiyo hata mafanikio yake yataonekana ambapo siku hiyo haitafika!
jk amefanya mengi ya maana ila yanachafuliwa na sifa mbaya ya chama chake
 
Rais , Dr. Jakaya Mrisho
Kikwete amesema wale wote wanaombeza kuhusu utendaji kazi wake wataona
aibu atakapomaliza muhula wake 2015.

Rais ameyasema hayo wakati akizindua mradi wa kusambaza umeme katika
mikoa ya Mwanza na Geita unaofadhiliwa na mfuko wa Changamoto wa
Milenia(MCC).

Rais amesema Serikali yake itavunja recodi ya kusambaza umeme katika
vijiji vingi nchini.

Jk amesema Tanzania inaongoza kwa mtandao wa barabara ambao ni bora
afrika mashariki huku akiwahakikishia wakazi wa Kagera kuwa meli mbili
alizowaahidi wakati wa kampeni ziko njiani zinakuja.

Rais alikuwa akishangiliwa na wananchi wakati wote wa hotuba yake.

Alisema Tanzania ni nchi kubwa kuliko nchi nyinine za Afrika Mashariki
,lakini ina mtandao mkubwa wa barabara kuliko nchi kama Kenya , lakini
akawalaumu watu wanaoisifia nchi hiyo jirani na kubeza mafanikio ya
serikali yake.

Aidha, Rais Kikwete amewashangaa baadhi ya viongozi wa CCM pamoja na
wananchama kushindwa kuzungumzia mafanikio yaliyofikiwa na serikali ya
CCM na badala yake wamekuwa hodari wa kujadili wanapobezwa na wapinzani"

Source: Mwananchi

wa kwanza kukumbuka ni dr slaa na freeman mbowe. hawa watu kila kukicha wanamtukana lakini kimoyomoyo wanampongeza. nakumbuka siku ile wakati JK alipofanya ziara yake jimboni kwa mbowe aliposhindwa kuzuia hisia zake na kutamka maneno yafuatayo: mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Jk kajenga marabara nzuri jimboni kwangu kuliko marais waliomtangulia. mwisho wa kunukuu
 
wa kwanza kukumbuka ni dr slaa na freeman mbowe. hawa watu kila kukicha wanamtukana lakini kimoyomoyo wanampongeza. nakumbuka siku ile wakati JK alipofanya ziara yake jimboni kwa mbowe aliposhindwa kuzuia hisia zake na kutamka maneno yafuatayo: mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Jk kajenga marabara nzuri jimboni kwangu kuliko marais waliomtangulia. mwisho wa kunukuu

Tatizo lenu ccm mmezubaa huo ndio udhaifu wenu mkubwa-jakaya. Yaani mpo lakini.
 
Ni lini Rais ataacha mipasho na ku think critically? anaongea mambo ya ajabu sana sometimes

kumbe sometimes na si always? najua kuongelea mambo ya ajabu kwa tafsiri yako ni kama alivyomshauri PK azungumze na waasi au kuwaita viongozi wa cdm ikulu kunywa nao juice. au siyo? kama sivyo basi tutajie kitu kimoja cha ajabu aliongea
 
Back
Top Bottom