Kikwete kuvuliwa Uenyekiti wa CCM 2012? Makamba awajia juu wanaojipanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete kuvuliwa Uenyekiti wa CCM 2012? Makamba awajia juu wanaojipanga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by AMARIDONG, Mar 30, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  Kikwete kuvuliwa uenyekiti wa CCM
  • Wajumbe wakamiana NEC Aprili 9, Dodoma

  na Mwandishi wetu

  [​IMG]
  WAKATI mambo yakizidi kwenda mrama ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), mkakati unasukwa kutaka kumuengua Rais Jakaya Kikwete kwenye nafasi yake ya uenyekiti wa chama hicho taifa, Tanzania Daima Jumatano limebaini.
  Mkakati huo unaoratibiwa na baadhi ya vigogo waandamizi wa CCM, unadaiwa kuwa na lengo la kutaka kukivua magamba chama hicho na uenyekiti wa Kikwete ni moja ya magamba yanayopaswa kuvuliwa.
  Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa tayari baadhi ya makada wa chama hicho, wamesambaa mikoani kuwashawishi wajumbe wa Halmashauri Kuu wa CCM (NEC), kuunga mkono hoja hiyo itakapowasilishwa kwenye vikao vya juu vya chama kuanzia sasa na kukamilika mwakani kwenye mkutano mkuu wa chama.
  Sababu kubwa inayotajwa na waumini wa mkakati huo ni kwamba kwa muundo wa sasa wa Rais kuwa na kofia mbili, umesababisha dhambi za chama kubebwa na serikali na zile za serikali kubebwa na chama.
  “Kwa mfano hivi sasa Rais Kikwete ndiye Rais na ndiye Mwenyekiti wa CCM Taifa, hivyo kama kuna jambo baya la serikali, linahusishwa na chama moja kwa moja na kama kuna jambo baya la chama linahusishwa na serikali.
  “Tumeshuhudia katika kipindi hiki kwamba ufisadi wa serikali umebebwa na chama na ule wa chama umebebwa na serikali. Dawa ya kuondoa hali hiyo ni kutenganisha kofia ya urais na uenyekiti,” alisema kada mmoja wa CCM.
  Kwa mujibu wa habari hizo, sababu nyingine inayosukuma hoja hiyo ni kwamba nafasi hizo haziko kikatiba bali zilitokana na utashi wa kisiasa wa Mwalimu Nyerere alipoishawishi CCM ikubali kuunganisha kofia hizo baada ya kubaini kuwa alikuwa akitofautiana kimawazo na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi wakati Mwalimu Nyerere akiwa Mwenyekiti wa chama.
  Duru za kisiasa kutoka ndani ya CCM, zinasema ingawa muundo huo wa kutenganisha kofia uliasisiwa na Mwalimu Nyerere kwa nia njema, lakini vinara wa mkakati huo safari hii, wana nia mbaya na Rais Kikwete kwani anaweza kutimuliwa kwenye urais kama atashindwa kutekeleza Ilani ya CCM aliyoinadi mwaka 2010.
  “Unajua kuna watu wanaamini kabisa kuwa kama Rais Kikwete ataendelea kuwa Mwenyekiti wa CCM hadi 2015, chama kitakuwa kwenye hali mbaya na CHADEMA wanaweza kuchukua nchi. Ili kukinusuru, lazima Kikwete abaki na urais na chama kiongozwe na mtu mwingine,” kilisema chanzo chetu cha habari.
  Athari nyingine inayotajwa na duru za siasa ni kwamba muundo huo utampunguzia nguvu Rais Kikwete kwani hatakuwa na sauti ndani ya vikao vya chama na anaweza kushughulikiwa kama mwanachama mwingine yeyote kama ataenda kinyume na Ilani ya CCM.
  “Hata wakati ule Nyerere alipotaka kofia hizi ziunganishwe, aliangalia mbele kwamba ikitokea chama kimepata mwenyekiti ‘kichaa’ na ambaye haelewani na Rais, moto unaweza kuwaka na mfano mzuri ni Afrika Kusini ambako Thabo Mbeki alikuwa ni Rais na Mwenyekiti alikuwa Jacob Zuma. Kilichotokea, wote tunajua,” alisema kada huyo ambaye pia ni mjumbe wa NEC.
  Mbeki alilazimishwa kujiuzulu urais kabla ya muda wake baada ya Kamati Kuu ya chama cha ANC, kumtaka aachie ngazi kwa madai kuwa alimbambikizia kesi Mwenyekiti wa chama hicho Jacob Zuma ambaye ndiye Rais wa sasa nchini humo.
  Mbeki ambaye alikuwa swahiba mkubwa wa Zuma kabla ya kuhitilafiana, alichaguliwa kuwa Rais wa Afrika Kusini mwaka 1999, akiwa Rais wa pili wa Afrika Kusini tangu utawala wa ubaguzi wa rangi ukomeshwe nchini humo. Alitarajiwa kumaliza muda wake wa urais mwaka 2009.
  Mwalimu Nyerere ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wakati Ali Hassan Mwinyi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
  Ilipofika mwaka 1985, Mwalimu Nyerere alitaka kofia hizo ziunganishwe kwa hofu kwamba kunaweza kutokea mgongano wa uendeshaji wa chama na serikali.
  Rais Benjamin Mkapa alipoingia madarakani mwaka 1995, alikabidhiwa uenyekiti na utaratibu huo uliendelea hadi sasa ambapo Rais wa CCM huwa pia Mwenyekiti wa chama hicho.
  Wakati huohuo, kile kikao cha Halmashauri Kuu (NEC), kilichokuwa kikisubiliwa kwa hamu na wajumbe wa chama hicho, kinatarajiwa kuitishwa Aprili 9 mjini Dodoma.
  Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata, zilisema tayari wajumbe wamejulishwa na hivi karibuni vikao vya Sekretarieti na Kamati Kuu (CC), vitakutana kwa ajili ya kupanga ajenda.
  Ingawa ajenda za NEC hazijajulikana, baadhi ya wajumbe waliliambia gazeti hili kwamba NEC hii itawaka moto kwani kuna mambo mengi yamejitokeza na hakukuwa na kikao tangu kumalizika kwa kikao cha uteuzi Agosti mwaka jana. Baadhi ya mambo yanayotarajiwa kuibuka ni pamoja na makovu ya uchaguzi kuanzia ngazi ya uteuzi, malumbano yanayoendelea ya wenyewe kwa wenyewe na tathmini ya hali ya kisiasa na sababu za kushindwa kwenye baadhi ya majimbo ya uchaguzi waliyotarajia kushinda.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,437
  Trophy Points: 280
  wapiga domo hawa
   
 3. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  SOURCE? Tanzania Daima!
   
 4. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2011
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Walishachelewa. Kwa power alizonazo mwenyekiti hawataweza hata siku moja. hapa wanapiga soga tu.
   
 5. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  "Kuna mkakakati wa kumwondoa Kikwete"
  "Safari hii kikao cha NEC kutakuwa na mambo!"
  Hizi ni porojo za kila siku ...
   
 6. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #6
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  Magufuli kajiuzulu.
  Sumaye kung'oka CCM.
  leo gazeti hili la udaku laja na hii mpya tena.
   
 7. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mbona halifungiwi?
   
 8. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  hainihusu!!!
   
 9. G

  Gurti JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hawawezi kumwengua ktk nafasi hiyo.
   
 10. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 415,867
  Trophy Points: 280
  Kikwete kuvuliwa uenyekiti wa CCM
  • Wajumbe wakamiana NEC Aprili 9, Dodoma

  na Mwandishi wetu

  [​IMG] WAKATI mambo yakizidi kwenda mrama ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), mkakati unasukwa kutaka kumuengua Rais Jakaya Kikwete kwenye nafasi yake ya uenyekiti wa chama hicho taifa, Tanzania Daima Jumatano limebaini.
  Mkakati huo unaoratibiwa na baadhi ya vigogo waandamizi wa CCM, unadaiwa kuwa na lengo la kutaka kukivua magamba chama hicho na uenyekiti wa Kikwete ni moja ya magamba yanayopaswa kuvuliwa.
  Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa tayari baadhi ya makada wa chama hicho, wamesambaa mikoani kuwashawishi wajumbe wa Halmashauri Kuu wa CCM (NEC), kuunga mkono hoja hiyo itakapowasilishwa kwenye vikao vya juu vya chama kuanzia sasa na kukamilika mwakani kwenye mkutano mkuu wa chama.
  Sababu kubwa inayotajwa na waumini wa mkakati huo ni kwamba kwa muundo wa sasa wa Rais kuwa na kofia mbili, umesababisha dhambi za chama kubebwa na serikali na zile za serikali kubebwa na chama.
  “Kwa mfano hivi sasa Rais Kikwete ndiye Rais na ndiye Mwenyekiti wa CCM Taifa, hivyo kama kuna jambo baya la serikali, linahusishwa na chama moja kwa moja na kama kuna jambo baya la chama linahusishwa na serikali.
  “Tumeshuhudia katika kipindi hiki kwamba ufisadi wa serikali umebebwa na chama na ule wa chama umebebwa na serikali. Dawa ya kuondoa hali hiyo ni kutenganisha kofia ya urais na uenyekiti,” alisema kada mmoja wa CCM.
  Kwa mujibu wa habari hizo, sababu nyingine inayosukuma hoja hiyo ni kwamba nafasi hizo haziko kikatiba bali zilitokana na utashi wa kisiasa wa Mwalimu Nyerere alipoishawishi CCM ikubali kuunganisha kofia hizo baada ya kubaini kuwa alikuwa akitofautiana kimawazo na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi wakati Mwalimu Nyerere akiwa Mwenyekiti wa chama.
  Duru za kisiasa kutoka ndani ya CCM, zinasema ingawa muundo huo wa kutenganisha kofia uliasisiwa na Mwalimu Nyerere kwa nia njema, lakini vinara wa mkakati huo safari hii, wana nia mbaya na Rais Kikwete kwani anaweza kutimuliwa kwenye urais kama atashindwa kutekeleza Ilani ya CCM aliyoinadi mwaka 2010.
  “Unajua kuna watu wanaamini kabisa kuwa kama Rais Kikwete ataendelea kuwa Mwenyekiti wa CCM hadi 2015, chama kitakuwa kwenye hali mbaya na CHADEMA wanaweza kuchukua nchi. Ili kukinusuru, lazima Kikwete abaki na urais na chama kiongozwe na mtu mwingine,” kilisema chanzo chetu cha habari.
  Athari nyingine inayotajwa na duru za siasa ni kwamba muundo huo utampunguzia nguvu Rais Kikwete kwani hatakuwa na sauti ndani ya vikao vya chama na anaweza kushughulikiwa kama mwanachama mwingine yeyote kama ataenda kinyume na Ilani ya CCM.
  “Hata wakati ule Nyerere alipotaka kofia hizi ziunganishwe, aliangalia mbele kwamba ikitokea chama kimepata mwenyekiti ‘kichaa’ na ambaye haelewani na Rais, moto unaweza kuwaka na mfano mzuri ni Afrika Kusini ambako Thabo Mbeki alikuwa ni Rais na Mwenyekiti alikuwa Jacob Zuma. Kilichotokea, wote tunajua,” alisema kada huyo ambaye pia ni mjumbe wa NEC.
  Mbeki alilazimishwa kujiuzulu urais kabla ya muda wake baada ya Kamati Kuu ya chama cha ANC, kumtaka aachie ngazi kwa madai kuwa alimbambikizia kesi Mwenyekiti wa chama hicho Jacob Zuma ambaye ndiye Rais wa sasa nchini humo.
  Mbeki ambaye alikuwa swahiba mkubwa wa Zuma kabla ya kuhitilafiana, alichaguliwa kuwa Rais wa Afrika Kusini mwaka 1999, akiwa Rais wa pili wa Afrika Kusini tangu utawala wa ubaguzi wa rangi ukomeshwe nchini humo. Alitarajiwa kumaliza muda wake wa urais mwaka 2009.
  Mwalimu Nyerere ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wakati Ali Hassan Mwinyi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
  Ilipofika mwaka 1985, Mwalimu Nyerere alitaka kofia hizo ziunganishwe kwa hofu kwamba kunaweza kutokea mgongano wa uendeshaji wa chama na serikali.
  Rais Benjamin Mkapa alipoingia madarakani mwaka 1995, alikabidhiwa uenyekiti na utaratibu huo uliendelea hadi sasa ambapo Rais wa CCM huwa pia Mwenyekiti wa chama hicho.
  Wakati huohuo, kile kikao cha Halmashauri Kuu (NEC), kilichokuwa kikisubiliwa kwa hamu na wajumbe wa chama hicho, kinatarajiwa kuitishwa Aprili 9 mjini Dodoma.
  Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata, zilisema tayari wajumbe wamejulishwa na hivi karibuni vikao vya Sekretarieti na Kamati Kuu (CC), vitakutana kwa ajili ya kupanga ajenda.
  Ingawa ajenda za NEC hazijajulikana, baadhi ya wajumbe waliliambia gazeti hili kwamba NEC hii itawaka moto kwani kuna mambo mengi yamejitokeza na hakukuwa na kikao tangu kumalizika kwa kikao cha uteuzi Agosti mwaka jana.
  Baadhi ya mambo yanayotarajiwa kuibuka ni pamoja na makovu ya uchaguzi kuanzia ngazi ya uteuzi, malumbano yanayoendelea ya wenyewe kwa wenyewe na tathmini ya hali ya kisiasa na sababu za kushindwa kwenye baadhi ya majimbo ya uchaguzi waliyotarajia kushinda.
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 415,867
  Trophy Points: 280
  Kama kweli CCM sasa wameona mwezi yetu macho...............................Sioni CCM kama ina ubavu wa kujiletea mageuzi ya kweli ndani ya chama hicho zaidi ya kulindana hadi nguvu ya wananchi itakapowasarambatisha vipande vipande...................
   
 12. s

  smz JF-Expert Member

  #12
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naona kikombe cha babu kimeanza kufanya kazi kwa waliokinywa. Kama kweli wameanza kufikiri "beyond their next meals" hata kufikiria kumtolea kofia ya Uenyekiti JK, basi tiba wameanza kuivumbua. Lakini ninavyojua zitapigwa kampeni za fitina na wazo hilo lisifikishwe hata kwenye NEC yenyewe.

  tusubiri tuone nani mwenye ujasiri wa ku- table agenda kama hiyo, wakati atakayekuwa anaendesha kikao hicho ni yeye mwenyewe mlengwa-JK
   
 13. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #13
  Mar 30, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Hapo ni patamu, lazima kuna fisadi anataka urais 2015 na mipango yote inaweza kuwa JK ndo anaichonga yeye mwenyewe au kundi jingine. Tusubiri filamu hiyo kutoka CCMwoody.
   
 14. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #14
  Mar 30, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,496
  Likes Received: 2,742
  Trophy Points: 280
  Hata mimi naona hii story ni wishful thinking!!! Hakuna mwenye ubavu wa kuja na hoja hiyo CCM!!
   
 15. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #15
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Sina uhakika kama gamba linaweaz kujivua KWENYE GAMBA lingine!!!!!!!!!!!!
   
 16. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #16
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  No one can topple JK, mtaniambia.
   
 17. m

  msosholisti Member

  #17
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na nahisi Lowasa ataukwaa uenyekiti
   
 18. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #18
  Mar 30, 2011
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ila tz mwenyekit wa ccm si ndio muongoza nchi kama wanatawala au??? Nilemisheni mie
   
 19. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #19
  Mar 30, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  CCM ipi inaweza kufanya hivyo? Chama ambacho kila siku wanasifia na kupanga kuandamana kupongeza porojo bila matendo za Viongozi wao na hasa mwenyekiti! Nani wa kumfunga Kengele paka. Hata wanywe pipa moja moja la dawa ya babu hawawezi kupiga hatua hiyo.
   
 20. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #20
  Mar 30, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  kwa nini??
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...