Kikwete kuvuliwa Uenyekiti wa CCM 2012? Makamba awajia juu wanaojipanga

Status
Not open for further replies.
WAKATI mambo yakizidi kwenda mrama ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), mkakati unasukwa kutaka kumuengua Rais Jakaya Kikwete kwenye nafasi yake ya uenyekiti wa chama hicho taifa, Tanzania Daima Jumatano limebaini. Mkakati huo unaoratibiwa na baadhi ya vigogo waandamizi wa CCM, unadaiwa kuwa na lengo la kutaka kukivua magamba chama hicho na uenyekiti wa Kikwete ni moja ya magamba yanayopaswa kuvuliwa.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa tayari baadhi ya makada wa chama hicho, wamesambaa mikoani kuwashawishi wajumbe wa Halmashauri Kuu wa CCM (NEC), kuunga mkono hoja hiyo itakapowasilishwa kwenye vikao vya juu vya chama kuanzia sasa na kukamilika mwakani kwenye mkutano mkuu wa chama.
Sababu kubwa inayotajwa na waumini wa mkakati huo ni kwamba kwa muundo wa sasa wa Rais kuwa na kofia mbili, umesababisha dhambi za chama kubebwa na serikali na zile za serikali kubebwa na chama. “Kwa mfano hivi sasa Rais Kikwete ndiye Rais na ndiye Mwenyekiti wa CCM Taifa, hivyo kama kuna jambo baya la serikali, linahusishwa na chama moja kwa moja na kama kuna jambo baya la chama linahusishwa na serikali. “Tumeshuhudia katika kipindi hiki kwamba ufisadi wa serikali umebebwa na chama na ule wa chama umebebwa na serikali. Dawa ya kuondoa hali hiyo ni kutenganisha kofia ya urais na uenyekiti,” alisema kada mmoja wa CCM.
Kwa mujibu wa habari hizo, sababu nyingine inayosukuma hoja hiyo ni kwamba nafasi hizo haziko kikatiba bali zilitokana na utashi wa kisiasa wa Mwalimu Nyerere alipoishawishi CCM ikubali kuunganisha kofia hizo baada ya kubaini kuwa alikuwa akitofautiana kimawazo na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi wakati Mwalimu Nyerere akiwa Mwenyekiti wa chama.

Duru za kisiasa kutoka ndani ya CCM, zinasema ingawa muundo huo wa kutenganisha kofia uliasisiwa na Mwalimu Nyerere kwa nia njema, lakini vinara wa mkakati huo safari hii, wana nia mbaya na Rais Kikwete kwani anaweza kutimuliwa kwenye urais kama atashindwa kutekeleza Ilani ya CCM aliyoinadi mwaka 2010.
“Unajua kuna watu wanaamini kabisa kuwa kama Rais Kikwete ataendelea kuwa Mwenyekiti wa CCM hadi 2015, chama kitakuwa kwenye hali mbaya na CHADEMA wanaweza kuchukua nchi. Ili kukinusuru, lazima Kikwete abaki na urais na chama kiongozwe na mtu mwingine,” kilisema chanzo chetu cha habari. Athari nyingine inayotajwa na duru za siasa ni kwamba muundo huo utampunguzia nguvu Rais Kikwete kwani hatakuwa na sauti ndani ya vikao vya chama na anaweza kushughulikiwa kama mwanachama mwingine yeyote kama ataenda kinyume na Ilani ya CCM. “Hata wakati ule Nyerere alipotaka kofia hizi ziunganishwe, aliangalia mbele kwamba ikitokea chama kimepata mwenyekiti ‘kichaa’ na ambaye haelewani na Rais, moto unaweza kuwaka na mfano mzuri ni Afrika Kusini ambako Thabo Mbeki alikuwa ni Rais na Mwenyekiti alikuwa Jacob Zuma. Kilichotokea, wote tunajua,” alisema kada huyo ambaye pia ni mjumbe wa NEC.

Mbeki alilazimishwa kujiuzulu urais kabla ya muda wake baada ya Kamati Kuu ya chama cha ANC, kumtaka aachie ngazi kwa madai kuwa alimbambikizia kesi Mwenyekiti wa chama hicho Jacob Zuma ambaye ndiye Rais wa sasa nchini humo.
Mbeki ambaye alikuwa swahiba mkubwa wa Zuma kabla ya kuhitilafiana, alichaguliwa kuwa Rais wa Afrika Kusini mwaka 1999, akiwa Rais wa pili wa Afrika Kusini tangu utawala wa ubaguzi wa rangi ukomeshwe nchini humo. Alitarajiwa kumaliza muda wake wa urais mwaka 2009.

Mwalimu Nyerere ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wakati Ali Hassan Mwinyi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Ilipofika mwaka 1985, Mwalimu Nyerere alitaka kofia hizo ziunganishwe kwa hofu kwamba kunaweza kutokea mgongano wa uendeshaji wa chama na serikali. Rais Benjamin Mkapa alipoingia madarakani mwaka 1995, alikabidhiwa uenyekiti na utaratibu huo uliendelea hadi sasa ambapo Rais wa CCM huwa pia Mwenyekiti wa chama hicho.

Wakati huohuo, kile kikao cha Halmashauri Kuu (NEC), kilichokuwa kikisubiliwa kwa hamu na wajumbe wa chama hicho, kinatarajiwa kuitishwa Aprili 9 mjini Dodoma.
Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata, zilisema tayari wajumbe wamejulishwa na hivi karibuni vikao vya Sekretarieti na Kamati Kuu (CC), vitakutana kwa ajili ya kupanga ajenda.

Ingawa ajenda za NEC hazijajulikana, baadhi ya wajumbe waliliambia gazeti hili kwamba NEC hii itawaka moto kwani kuna mambo mengi yamejitokeza na hakukuwa na kikao tangu kumalizika kwa kikao cha uteuzi Agosti mwaka jana.
Baadhi ya mambo yanayotarajiwa kuibuka ni pamoja na makovu ya uchaguzi kuanzia ngazi ya uteuzi, malumbano yanayoendelea ya wenyewe kwa wenyewe na tathmini ya hali ya kisiasa na sababu za kushindwa kwenye baadhi ya majimbo ya uchaguzi waliyotarajia kushinda.

Source: Tanzania daima
 
Kama mtu ameshikilia kofi zote mbili na hakuna kitakachofanyika nje yake, hapo kama ni kuboronga ndo ataboronga atakavyo na hakuna wa kumnyooshea kidole kwa kuwa anashika hatamu zote kichana na kiserikali
 
Chama kinaongozwa na mafisadi, na ili hoja iwe na uzito mafisadi wanahitaji kutilia chumvi, na waliomweka madarakani na kumlinda ni mafisadi. Sitashangaa hoja hiyo kudhoofu kabla haijapata wafuasi wengi wanachama kwa vile wanaoakisi hoja hiyo ni kundi lililo kinyume na mafisadi
 
yangu majichooo...Naona tu kama kuku wanakula manyoya yao..!!!

Naye Shy-Rose Banji, akizungumzia matokeo mabaya ya uchaguzi kwa chama chake alisema, "Makamba is the problem (Makamba ndiye tatizo). Tumefika hapa kwa sababu yake kushindwa kazi," alisema Banji huku akielekeza macho yake kwa Makamba aliyekuwa miongoni mwa wajumbe wa mkutano huo.

Alisema, "Kila kukicha katibu mkuu anaandikwa kwenye vyombo vya habari, mara hivi, mara vile. Hili ni tatizo kwa chama…"

Lakini Makamba hakuwa na simile. Haraka aliinuka na kusema, "Shy Rose…mbona wewe unaandikwa sana . Unavaa nguo fupi na una hawara, tena mtu wa CHADEMA…?"

Hahaha, hapa ni vibaya nikimtafsiri Makamba kama kasuku asiyetumia hekima na busara kulingana na umri wake pamoja na uzoefu wa kimadaraka?
Mwaka huu bado kuna mengi tu tutayashuhudia.
 
:bange::bange::bange::bange::bange::bange::llama::llama::llama::llama::llama::llama::flame::flame::flame::flame::peace::peace::peace::peace::msela::msela::msela::msela::msela:
 
Kikwete kuvuliwa uenyekiti wa CCM
• Wajumbe wakamiana NEC Aprili 9, Dodoma

na Mwandishi wetu

amka2.gif
WAKATI mambo yakizidi kwenda mrama ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), mkakati unasukwa kutaka kumuengua Rais Jakaya Kikwete kwenye nafasi yake ya uenyekiti wa chama hicho taifa, Tanzania Daima Jumatano limebaini.
Mkakati huo unaoratibiwa na baadhi ya vigogo waandamizi wa CCM, unadaiwa kuwa na lengo la kutaka kukivua magamba chama hicho na uenyekiti wa Kikwete ni moja ya magamba yanayopaswa kuvuliwa.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa tayari baadhi ya makada wa chama hicho, wamesambaa mikoani kuwashawishi wajumbe wa Halmashauri Kuu wa CCM (NEC), kuunga mkono hoja hiyo itakapowasilishwa kwenye vikao vya juu vya chama kuanzia sasa na kukamilika mwakani kwenye mkutano mkuu wa chama.
Sababu kubwa inayotajwa na waumini wa mkakati huo ni kwamba kwa muundo wa sasa wa Rais kuwa na kofia mbili, umesababisha dhambi za chama kubebwa na serikali na zile za serikali kubebwa na chama.
"Kwa mfano hivi sasa Rais Kikwete ndiye Rais na ndiye Mwenyekiti wa CCM Taifa, hivyo kama kuna jambo baya la serikali, linahusishwa na chama moja kwa moja na kama kuna jambo baya la chama linahusishwa na serikali.
"Tumeshuhudia katika kipindi hiki kwamba ufisadi wa serikali umebebwa na chama na ule wa chama umebebwa na serikali. Dawa ya kuondoa hali hiyo ni kutenganisha kofia ya urais na uenyekiti," alisema kada mmoja wa CCM.
Kwa mujibu wa habari hizo, sababu nyingine inayosukuma hoja hiyo ni kwamba nafasi hizo haziko kikatiba bali zilitokana na utashi wa kisiasa wa Mwalimu Nyerere alipoishawishi CCM ikubali kuunganisha kofia hizo baada ya kubaini kuwa alikuwa akitofautiana kimawazo na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi wakati Mwalimu Nyerere akiwa Mwenyekiti wa chama.
Duru za kisiasa kutoka ndani ya CCM, zinasema ingawa muundo huo wa kutenganisha kofia uliasisiwa na Mwalimu Nyerere kwa nia njema, lakini vinara wa mkakati huo safari hii, wana nia mbaya na Rais Kikwete kwani anaweza kutimuliwa kwenye urais kama atashindwa kutekeleza Ilani ya CCM aliyoinadi mwaka 2010.
"Unajua kuna watu wanaamini kabisa kuwa kama Rais Kikwete ataendelea kuwa Mwenyekiti wa CCM hadi 2015, chama kitakuwa kwenye hali mbaya na CHADEMA wanaweza kuchukua nchi. Ili kukinusuru, lazima Kikwete abaki na urais na chama kiongozwe na mtu mwingine," kilisema chanzo chetu cha habari.
Athari nyingine inayotajwa na duru za siasa ni kwamba muundo huo utampunguzia nguvu Rais Kikwete kwani hatakuwa na sauti ndani ya vikao vya chama na anaweza kushughulikiwa kama mwanachama mwingine yeyote kama ataenda kinyume na Ilani ya CCM.
"Hata wakati ule Nyerere alipotaka kofia hizi ziunganishwe, aliangalia mbele kwamba ikitokea chama kimepata mwenyekiti ‘kichaa' na ambaye haelewani na Rais, moto unaweza kuwaka na mfano mzuri ni Afrika Kusini ambako Thabo Mbeki alikuwa ni Rais na Mwenyekiti alikuwa Jacob Zuma. Kilichotokea, wote tunajua," alisema kada huyo ambaye pia ni mjumbe wa NEC.
Mbeki alilazimishwa kujiuzulu urais kabla ya muda wake baada ya Kamati Kuu ya chama cha ANC, kumtaka aachie ngazi kwa madai kuwa alimbambikizia kesi Mwenyekiti wa chama hicho Jacob Zuma ambaye ndiye Rais wa sasa nchini humo.
Mbeki ambaye alikuwa swahiba mkubwa wa Zuma kabla ya kuhitilafiana, alichaguliwa kuwa Rais wa Afrika Kusini mwaka 1999, akiwa Rais wa pili wa Afrika Kusini tangu utawala wa ubaguzi wa rangi ukomeshwe nchini humo. Alitarajiwa kumaliza muda wake wa urais mwaka 2009.
Mwalimu Nyerere ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wakati Ali Hassan Mwinyi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Ilipofika mwaka 1985, Mwalimu Nyerere alitaka kofia hizo ziunganishwe kwa hofu kwamba kunaweza kutokea mgongano wa uendeshaji wa chama na serikali.
Rais Benjamin Mkapa alipoingia madarakani mwaka 1995, alikabidhiwa uenyekiti na utaratibu huo uliendelea hadi sasa ambapo Rais wa CCM huwa pia Mwenyekiti wa chama hicho.
Wakati huohuo, kile kikao cha Halmashauri Kuu (NEC), kilichokuwa kikisubiliwa kwa hamu na wajumbe wa chama hicho, kinatarajiwa kuitishwa Aprili 9 mjini Dodoma.
Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata, zilisema tayari wajumbe wamejulishwa na hivi karibuni vikao vya Sekretarieti na Kamati Kuu (CC), vitakutana kwa ajili ya kupanga ajenda.
Ingawa ajenda za NEC hazijajulikana, baadhi ya wajumbe waliliambia gazeti hili kwamba NEC hii itawaka moto kwani kuna mambo mengi yamejitokeza na hakukuwa na kikao tangu kumalizika kwa kikao cha uteuzi Agosti mwaka jana.
Baadhi ya mambo yanayotarajiwa kuibuka ni pamoja na makovu ya uchaguzi kuanzia ngazi ya uteuzi, malumbano yanayoendelea ya wenyewe kwa wenyewe na tathmini ya hali ya kisiasa na sababu za kushindwa kwenye baadhi ya majimbo ya uchaguzi waliyotarajia kushinda.

Huu ni uzushi mkubwa toka kwenye gazeti la Mbowe , Tanzania daima.

habari ni za kizushi na siku zote dua la kuku halimpati mwewe
 
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM), umemgeuka Rais Jakaya Kikwete.

Unamtuhumu kushindwa kazi. Unamtaka kuachia nafasi ya uongozi katika chama chake ili kuwepo mchakato wa kukiimarisha.

MwanaHALISI limeelezwa kuwa Baraza la Vijana limeona kuwa Kamati Kuu (CC) ya chama, ambayo huwa chini ya mwenyekiti Kikwete, imeshindwa kusimamia serikali.

Baraza limetaka, pamoja na mambo mengine, Kikwete afanye mabadiliko kwenye muundo wa CC kwa kuwaondoa wajumbe ambao ni mawaziri ikiwa njia ya kukiimarisha chama.

Mapendekezo ya vijana ya kumtaka Kikwete kuachia ngazi katika nafasi ya mwenyekiti, yamepangwa kuwasilishwa kwake mwenyewe Alhamisi wiki hii na viongozi wa umoja huo wakiongozwa na kamanda wao, Kingunge Ngombale Mwiru.

“Pale Dodoma tulikubaliana kuwa na maamuzi ya aina mbili, ameeleza mjumbe mmoja wa baraza la vijana kwa sharti la kutotajwa gazetini.

Amesema, “Kwanza ni yale ambayo yatasomwa kwa waandishi wa habari na kufahamika na umma na pili, yale ya siri ambayo tutamkabidhi rais moja kwa moja.”

Taarifa kutoka ndani ya baraza la vijana lililokutana jijini Dodoma, Jumamosi iliyopita, zinasema uamuzi wa kumtaka Kikwete kuachia nafasi ya mwenyekiti uliibuka wakati wa mjadala juu ya ajenda ya ushiriki wa vijana katika uchaguzi mkuu uliyopita.

Mjadala uliibuka pale baadhi ya wajumbe walipochangia kwa kudai kuwa matokeo mabaya ya uchaguzi yalitokana na Kikwete kusafiri sana nje ya nchi, jambo ambalo lilimfanya ashindwe kujenga chama chake.

Mbali na kutaka kutenganisha kofia ya mwenyekiti na ile ya rais, UV-CCM wanaituhumu Usalama wa Taifa kwa kile unachodai “kushindwa kumsaidia rais.”

“Idara hii imeshindwa kuisaidia serikali. Inashughulika na mambo madogo yanayohusu watu, badala ya kumshauri rais kuhusu mambo makubwa ya kitaifa yaliyo muhimu kwa wananchi,” inasema sehemu ya mapendekezo ya vijana wa CCM ambayo yatapelekwa kwa rais.

Mapendekezo ya vijana, taarifa zimeeleza, yatawasilishwa kwa Rais Kikwete kesho. Ujumbe utakaowasilisha mapendekezo hayo umetajwa kuongozwa na kamanda wao, Kingunge Ngombale-Mwiru.

“ Kama usalama wa taifa wangekuwa wanafanya kazi vizuri,” UV-CCM imenukuliwa ikihoji, “wangemweleza rais kuhusu makundi yaliyopo katika chama chake. Lakini badala ya kufanya kazi, wameingia katika siasa za makundi ya ndani ya CCM.”

Wanasema, “Hawa watu (usalama), wameshindwa kufanya kazi yao kwa weledi…”

Kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja huku kukiwa na habari kuwa mnyukano mkubwa uliibuka ndani ya kikao cha baraza la vijana, kati ya makundi mawili – lile linalomuunga mkono Edward Lowassa na ile linalompinga.

Hoja nyingine inayopelekwa kwa Kikwete inahusu “udhaifu wa mawaziri katika kutimiza kazi zao.” UV-CCM wanadai mawaziri hawafanyi maamuzi; badala yake wanategeana ili atakayethubutu kufanya maamuzi “aharibikiwe na aonekane mbaya.”

Umoja huo umesema mawaziri wanapofanya kazi zao wanatekeleza ilani ya uchaguzi ya chama chao, lakini hilo halifanyiki kwa kuwa mawaziri wengi wamejikita katika biashara zao binafsi au wanasaka madaraka ya urais kwa mwaka 2015.

“Mawaziri hawafanyi kazi kwa sababu hawataki kufanya maamuzi. Matokeo yake rais anaonekana hafai. Hatua ya mawaziri kuacha kufanya maamuzi mazito, imechangia kwa kiasi kikubwa rais kushambuliwa kila uchao na vyombo vya habari,” inasema sehemu ya taarifa hiyo.

Vyanzo vya taarifa vya gazeti hili vinasema, ndani ya baraza la vijana baadhi ya wajumbe walipangwa kutetea baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi.

Mmoja wao (jina tunalo), alinukuliwa akisema kuhusu kashfa ya Richmond na kujiuzulu kwa Lowassa kuwa, “ Kama kuwajibika katika kashfa hiyo, aliyepaswa kuwajibika ni rais mwenyewe aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la mawaziri.”

Kauli ya mjumbe huyo kumtetea Lowassa ilifuatia mjumbe wa baraza kutoka mkoani Arusha, Mrisho Gumbo kutaka chama chake kuwatosa watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini ambao wanashilikia nafasi katika chama.

Akichangia katika kikao hicho, Mrisho alisema, “Ukiwa kijana, na ukawa mnafiki, basi ukiwa mzee utakuwa mchawi. Kama tunataka chama hiki kijivue gamba, basi mwambieni Rais Kikwete awaondoe Lowassa, Rostam na Chenge katika vikao vya maamuzi.”

Alisema, “Naiomba meza kuu; mpelekeeni salamu mwenyekiti. Kama anataka chama kijisafishe awaondoe Lowassa, Rostam na Chenge katika vikao vya maamuzi. Hawa ndio wanaosababisha chama chetu kitukanwe.”

Naye Shy-Rose Banji, akizungumzia matokeo mabaya ya uchaguzi kwa chama chake alisema, “Makamba is the problem (Makamba ndiye tatizo). Tumefika hapa kwa sababu yake kushindwa kazi,” alisema Banji huku akielekeza macho yake kwa Makamba aliyekuwa miongoni mwa wajumbe wa mkutano huo.

Alisema, “Kila kukicha katibu mkuu anaandikwa kwenye vyombo vya habari, mara hivi, mara vile. Hili ni tatizo kwa chama…”

Lakini Makamba hakuwa na simile. Haraka aliinuka na kusema, “Shy Rose…mbona wewe unaandikwa sana . Unavaa nguo fupi na una hawara, tena mtu wa CHADEMA…?”

Alikuwa Edwin Sanda, mjumbe Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), kupitia UV-CCM, aliyeingilia kati “mipasho” ya Makamba.

Alisema, “… katibu mkuu anaingilia mambo binafsi ya watu. Hii si ajenda. Mjumbe amejadili tatizo la chama, linalosababishwa na mtendaji mkuu wa chama, lakini mzee Makamba unakuja kuelezea maisha binafsi ya mjumbe. Hii si sahihi.”

Naye Husseni Bashe akitetea Makamba na kuhusu madai kuwa uongozi wake ulichangia kufanya vibaya alisema, bunge lililopita pia lina mchango mkubwa sana katika kutofanya vizuri kwa chama chetu kwenye uchaguzi huo.

Alisema spika wa wakati huo, Samwel Sitta “aliongoza bunge ambalo lilizidisha mpasuko wa wabunge na hatimaye wana-CCM wote katika kipindi cha kuelekea uchaguzi.”

Alitoa mfano wa kashfa ya mkataba tata wa Richmond iliyosababisha kujiuzulu kwa Edward Lowassa katika nafasi yake ya uwaziri mkuu.

Bashe alidai ndani ya kikao kuwa ana ripoti mbili za Richmond , lakini zikizungumzia jambo moja, huku zikiwa na maudhui tofauti.

Alisema, “Jamani watu hapa wanazungumzia habari ya Richmond , ukweli mimi ninaujua…Hii ilikuwa ni chuki binafsi kati ya Sitta na Dk. Mwakyembe dhidi ya Lowassa.”

Kuhusu udhaifu wa Makamba, Bashe alisema, “Makamba hajajiteua. Ameteuliwa. Kama kuna makosa, basi aliyemteua ndiye awajibike” – bila shaka Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete.

Kwa upande wake, Ridhiwani Kikwete aliasa wajumbe kujadili hoja, akisema “wenzetu wa CHADEMA wana mikakati ya kufanya vitu vyao na wana uwezo wa kuitekeleza.” Hata hivyo, hakuna aliyejali rai yake.

Mtetezi mashuhuri wa Lowassa, James Millya alisema, “Chama hiki kinavurugwa na Sitta na Dk. Mwakyembe kwa kueneza vitu vya uwongo dhidi ya Lowassa.”

Katika hatua nyingine UV-CCM wamemtaka Kikwete kuagiza Makamba kumfukuza Tambwe Hiza kutoka idara ya porapaganda ya chama hicho kwa kuwa “ameshindwa kazi.”

Source: MwanaHalisi.

Magazeti yote haya yanazusha pamoja na nukuru za majibizano ndani ya kikao?:A S-cry:
 
ndugu yangu usipoteze muda kujibizana na watu hafif, leta news kwenda mbele... ccm watafukuzana wote naona, eti makamba amfukuze tambwe; mimi sielewi nani ana afadhali hapo kati yao! hiki chama kinahitaji kufanya re-shuffle ya uongozi wake mzima, sio wajumbe cc sio uvccm wala uwt. Bogus bogus bogus
 
Naye Shy-Rose Banji, akizungumzia matokeo mabaya ya uchaguzi kwa chama chake alisema, “Makamba is the problem (Makamba ndiye tatizo). Tumefika hapa kwa sababu yake kushindwa kazi,” alisema Banji huku akielekeza macho yake kwa Makamba aliyekuwa miongoni mwa wajumbe wa mkutano huo.

Alisema, “Kila kukicha katibu mkuu anaandikwa kwenye vyombo vya habari, mara hivi, mara vile. Hili ni tatizo kwa chama…”

Lakini Makamba hakuwa na simile. Haraka aliinuka na kusema, “Shy Rose…mbona wewe unaandikwa sana . Unavaa nguo fupi na una hawara, tena mtu wa CHADEMA…?”

Hahaha, hapa ni vibaya nikimtafsiri Makamba kama kasuku asiyetumia hekima na busara kulingana na umri wake pamoja na uzoefu wa kimadaraka?
Mwaka huu bado kuna mengi tu tutayashuhudia.

huyo ndiye Makamba bana.
 
WAKATI mambo yakizidi kwenda mrama ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), mkakati unasukwa kutaka kumuengua Rais Jakaya Kikwete kwenye nafasi yake ya uenyekiti wa chama hicho taifa, Tanzania Daima Jumatano limebaini. Mkakati huo unaoratibiwa na baadhi ya vigogo waandamizi wa CCM, unadaiwa kuwa na lengo la kutaka kukivua magamba chama hicho na uenyekiti wa Kikwete ni moja ya magamba yanayopaswa kuvuliwa.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa tayari baadhi ya makada wa chama hicho, wamesambaa mikoani kuwashawishi wajumbe wa Halmashauri Kuu wa CCM (NEC), kuunga mkono hoja hiyo itakapowasilishwa kwenye vikao vya juu vya chama kuanzia sasa na kukamilika mwakani kwenye mkutano mkuu wa chama.
Sababu kubwa inayotajwa na waumini wa mkakati huo ni kwamba kwa muundo wa sasa wa Rais kuwa na kofia mbili, umesababisha dhambi za chama kubebwa na serikali na zile za serikali kubebwa na chama. “Kwa mfano hivi sasa Rais Kikwete ndiye Rais na ndiye Mwenyekiti wa CCM Taifa, hivyo kama kuna jambo baya la serikali, linahusishwa na chama moja kwa moja na kama kuna jambo baya la chama linahusishwa na serikali. “Tumeshuhudia katika kipindi hiki kwamba ufisadi wa serikali umebebwa na chama na ule wa chama umebebwa na serikali. Dawa ya kuondoa hali hiyo ni kutenganisha kofia ya urais na uenyekiti,” alisema kada mmoja wa CCM.
Kwa mujibu wa habari hizo, sababu nyingine inayosukuma hoja hiyo ni kwamba nafasi hizo haziko kikatiba bali zilitokana na utashi wa kisiasa wa Mwalimu Nyerere alipoishawishi CCM ikubali kuunganisha kofia hizo baada ya kubaini kuwa alikuwa akitofautiana kimawazo na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi wakati Mwalimu Nyerere akiwa Mwenyekiti wa chama.

Duru za kisiasa kutoka ndani ya CCM, zinasema ingawa muundo huo wa kutenganisha kofia uliasisiwa na Mwalimu Nyerere kwa nia njema, lakini vinara wa mkakati huo safari hii, wana nia mbaya na Rais Kikwete kwani anaweza kutimuliwa kwenye urais kama atashindwa kutekeleza Ilani ya CCM aliyoinadi mwaka 2010.
“Unajua kuna watu wanaamini kabisa kuwa kama Rais Kikwete ataendelea kuwa Mwenyekiti wa CCM hadi 2015, chama kitakuwa kwenye hali mbaya na CHADEMA wanaweza kuchukua nchi. Ili kukinusuru, lazima Kikwete abaki na urais na chama kiongozwe na mtu mwingine,” kilisema chanzo chetu cha habari. Athari nyingine inayotajwa na duru za siasa ni kwamba muundo huo utampunguzia nguvu Rais Kikwete kwani hatakuwa na sauti ndani ya vikao vya chama na anaweza kushughulikiwa kama mwanachama mwingine yeyote kama ataenda kinyume na Ilani ya CCM. “Hata wakati ule Nyerere alipotaka kofia hizi ziunganishwe, aliangalia mbele kwamba ikitokea chama kimepata mwenyekiti ‘kichaa’ na ambaye haelewani na Rais, moto unaweza kuwaka na mfano mzuri ni Afrika Kusini ambako Thabo Mbeki alikuwa ni Rais na Mwenyekiti alikuwa Jacob Zuma. Kilichotokea, wote tunajua,” alisema kada huyo ambaye pia ni mjumbe wa NEC.

Mbeki alilazimishwa kujiuzulu urais kabla ya muda wake baada ya Kamati Kuu ya chama cha ANC, kumtaka aachie ngazi kwa madai kuwa alimbambikizia kesi Mwenyekiti wa chama hicho Jacob Zuma ambaye ndiye Rais wa sasa nchini humo.
Mbeki ambaye alikuwa swahiba mkubwa wa Zuma kabla ya kuhitilafiana, alichaguliwa kuwa Rais wa Afrika Kusini mwaka 1999, akiwa Rais wa pili wa Afrika Kusini tangu utawala wa ubaguzi wa rangi ukomeshwe nchini humo. Alitarajiwa kumaliza muda wake wa urais mwaka 2009.

Mwalimu Nyerere ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wakati Ali Hassan Mwinyi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Ilipofika mwaka 1985, Mwalimu Nyerere alitaka kofia hizo ziunganishwe kwa hofu kwamba kunaweza kutokea mgongano wa uendeshaji wa chama na serikali. Rais Benjamin Mkapa alipoingia madarakani mwaka 1995, alikabidhiwa uenyekiti na utaratibu huo uliendelea hadi sasa ambapo Rais wa CCM huwa pia Mwenyekiti wa chama hicho.

Wakati huohuo, kile kikao cha Halmashauri Kuu (NEC), kilichokuwa kikisubiliwa kwa hamu na wajumbe wa chama hicho, kinatarajiwa kuitishwa Aprili 9 mjini Dodoma.
Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata, zilisema tayari wajumbe wamejulishwa na hivi karibuni vikao vya Sekretarieti na Kamati Kuu (CC), vitakutana kwa ajili ya kupanga ajenda.

Ingawa ajenda za NEC hazijajulikana, baadhi ya wajumbe waliliambia gazeti hili kwamba NEC hii itawaka moto kwani kuna mambo mengi yamejitokeza na hakukuwa na kikao tangu kumalizika kwa kikao cha uteuzi Agosti mwaka jana.
Baadhi ya mambo yanayotarajiwa kuibuka ni pamoja na makovu ya uchaguzi kuanzia ngazi ya uteuzi, malumbano yanayoendelea ya wenyewe kwa wenyewe na tathmini ya hali ya kisiasa na sababu za kushindwa kwenye baadhi ya majimbo ya uchaguzi waliyotarajia kushinda.

Source: Tanzania daima

Hata gazeti likaamini upupu huu na watu wakaushabikia inaonyesha vipi Watanzania tulivyokwisha kata tamaa. Tumebaki kuishi kwa mategemeo na udaku basi!
 
Sioni mjumbe wa NEC ama CC ya CCM mwenye ubavu wa kuwasilisha hoja hyo.May be you are underestimating the power of JK
 
Watoto bwana CCM siyo mara ya kwanza kupitia hali hizi! mara nyingi imekuwa hivyo....na mara nyingi yanaishia hivyo hivyo...

The challenge how to remove CCM from power, kwa sababu inaonekana wakifanya lile ambalo linatakiwa basi wengi kuhamia CCM!

Sitaki kufika huko! kwa matendo yenu mnaonekana wengi bado ni wana CCM damu kwa sababu ni chama cha Nyerere!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom