Kikwete kuongelea ufa wa udini ni geresha tu

Asalaam aleykum wana bodi.
Sote humu ni mashahidi wakati wa kampeini mwaka 2010 Mgombea Urais wa Ticket ya CCM na wenzake wote walikuwa wanalia kuwa kuna chama kinachoendesha kampeini za Udini. na kwenye hotuba yake baada ya kuapishwa aliukemea kwa nguvu zote. Sote hapa ni mashahidi kuna aya moja kwenye Quran Tukufu inasema " Sema kweli ingawa inauma, sema kweli tupu hata kama unachinjwa." nami nasema ukweli inagawa inauma. Kwenye kampeini na baada ya kampeni Udini uliokuwa unasemwa ni dhidi ya Dr. Slaa na wakatoliki. Eti Rais wa mioyo ya Watanzania anapigiwa chapuo na Kanisa katoliki.

Kwa sasa nchi inazizima kwa vitendo vya ufunjifu wa utulivu(siwezi kusema kamwe tuna amani nina sababu za kusema hatuna amani - tuna utulivu) kutoka kwa makundi ya dini Kiislamu(Sio waislamu wote) dini ambayo haikutajwa na Kikwete wakati analia kupandikizwa mbegu ya Udini nchini.

maswali yangu ni haya:-
  1. Je, CCM baada ya kuhisi Chadema wanapigiwa upatu na Katoliki (Kama basi ni kweli) nao waliwafuata waislamu?
  2. Je. Matarajio waliowapa waislamu wameshindwa kuyatekeleza ndo maana Jambo dogo tu wanaharakati wa kiisamu wanalipuka na kuvunja sheria za nchi?
  3. Je Ule ujasiri waliokuwa nao CCM wakituhumu Kanisa kuwa linambeba Dr.Slaa umeishia wapi wakashindwa kuusimamia dhidi ya kina ponda na muamsho?
Mi nadhani the head of Gorvenment/CCM leaders are almost empty. Hawawezi kuongoza tena wanabaki kurukia rukia tu mambo mwisho siku wanatuingiza msituni na kuzalisha wakimbizi wa Kitanzania. Tuikataeni CCM kwa nguvu zote yani kama vile Sheikh na Kitimoto na Msabato na Kambale
 
Kisima wamekichimba wenyewe na sasa wanapaswa waingie wenyewe-by john komba
 
"Kipimo apandacho mtu ndicho atakachopimiwa." na "Apandacho mtu ndicho atakachovuna"
Aliona ili apate kura za huruma za waislamu asingizie CDM kuna udini na zinapigwa kampeni za udini,
wakati haikuwa kweli leo hii kwa macho ya watanzania tunajionea ule udini uliopandwa gharama yake
ndio hii inayoendelea.
 
akiongea katika kampeni zake katika viwanja vya jangwani Rais wetu mpendwa jakaya mrisho kikwete alisema kuwa kampeni za mwaka 2010 zimetawaliwa na udini, badala ya viongozi wa kiroho kumuunga mkono maaskofu wakamrukia kwa miguu miwili, ooh hakuna udini wewe ndiwe mdini, mara viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo nao wakifanya hivyo hivyo kwa tamaa za kwenda ikulu, leo taifa limegawanyika mapande mawili wakristo na waislam, kwa hili alaumiwe nani? Tahadhari. wanainchi jiepusheni na vyama vya mrengo wa kidini.
 
mkuu aliehubiri udin JK au Chadema? kama ndivyo katiba inasemaje? na JK alichukuwa hatuagani kuisimamia na kuilinda

katiba kama unachokisema kina ukweli.
 
akiongea katika kampeni zake katika viwanja vya jangwani Rais wetu mpendwa jakaya mrisho kikwete alisema kuwa kampeni za mwaka 2010 zimetawaliwa na udini, badala ya viongozi wa kiroho kumuunga mkono maaskofu wakamrukia kwa miguu miwili, ooh hakuna udini wewe ndiwe mdini, mara viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo nao wakifanya hivyo hivyo kwa tamaa za kwenda ikulu, leo taifa limegawanyika mapande mawili wakristo na waislam, kwa hili alaumiwe nani? Tahadhari. wanainchi jiepusheni na vyama vya mrengo wa kidini.

Mkuu, hoja yako ni dhaifu mno kujadiliwa.
Ulipata kuangalia sinema moja ikiitwa Coming to America? Hususan pale mfalme wa Zamunda alipokuwa akiongea na Malkia huku akisisitiza kuhusu taratibu zao za mwana mfalme Akeem, kuandaliwa binti wa kumuoa tangu akiwa mdogo. Kama kumbukumbu zangu ziko sawa, nadhani malkia alimshangaa mfalme na kusema "nilidhani wewe ndiwe mfalme"?.

Akimaanisha kwamba mfalme ndiye mwenye mamlaka ya kubadilisha kile anachokiona hakina maslahi kwa kingdom yake, na aache kulalamika kana kwamba yupo mwenye mamlaka zaidi yake atakayeweza kurekebisha jambo lile.

Mkuu, naomba niishie hapa kwani wahenga walinena hapo kale kwamba, asiyejua maana haambiwi maana. Mwenye macho na aone na mwenye masikio na asikie.
 
Na sisi wapagani tufanyeje?? Ninyi wenye dini mnataka kuuwana si heri tu muwe kama sisi hamtakuwa na ugomvi wala chuki na mtu. Huku kwetu tunaamini sheria za nchi tu. Ni vyema dini zikaachwa kwani zimeshindwa kuleta amani na upendo. Au mnasemaje wajameni?? Mnawindana kwa majina ambayo mmeletewa ama na wazungu au waarabu. Ukoloni huu unawafanya mnabaguana na kugombana na misingi ya jina tu ukihisi jina fulani ndilo la mtu wetu. Heri sie kina mwawa, madeghesho, Kimweri, Mrisho, msambatavangu hakuna anayetujua.

Mkiendelea kushadadia udini na nani wengi nani wachache tutazamisha Taifa. mbona Iran, Iraq, Qatar , Saudia wote wana majina sawa na wengine wenye majina tofauti ni wachache ila wanaishi au huku Germany, mexico, sweeden wengi wanamajina ya mawe na wachache wanamajina yao lakini wanaishi??

Tatizo la Tanzania ni umasikini na ukosefu wa elimu. Heri tungenyukana ili kupunguza wezi serikalini watujengejee shule bora za watoto wetu wawe wagunduzi, wajitengenezee ajira wawe na uhakika wa kula milo minne kwa siku akili zifanye kazi zaidi. Naamini kila mtu akiwa na shughuli ya kufanya tukaondoa vigenge vyote kutwa nzima hutasikia haya mambo. Ukosefu wa ajira, elimu, uduni wa maisha ndio unatufanya tunakuwa na muda mwingi wa kuongelea non Issue too much.

Sioni kama dini ndizo tatizo la umasikini wetu? Umasikini unaletwa na sisi wenyewe kama Taifa. Watawala wamekuwa smart wametukamata wametugawa kwa misingi ya dini wao wanatuibia na hawafanyi kazi.

Jana niliwakuta wanashangilia sana baadhi ya mawaziri wanasema afadhali tumepata mambo ya kupigana nayo badala ya kuisumbua serikali ituletee maendeleo.

Ukweli usiofichika kama kweli unaamini kuna kundi linalokudidimiza hufikiri vizuri. Ukitaka kujua binadamu tumeumbwa sawa ila jinsi tunavyoishi tunapoteza hali ya kuwa responsible na maisha yetu. Tasisi zetu ni vioo vya maendeleo yetu ukiwa kwenye taasisi ambayo yenyewe imeshindwa kujiletea maendeleo ur r in big trouble. Kama mbunge alishindwa kutetea jimbo lake hawezi kutetea nchi, kama diwani alishindwa kutetea kata yake hawezi kutetea jimbo na kuliletea maendeleo. Ukiongoza watu kwenye Taasisi yeyote ukashindwa kuiendeleza ukaanza kulalamika wakati tayari una resources watu kazi kweli kweli.

Tanzania ni nchi nzuri sana yenye amani na upendo. Kati ya kundi ambalo limetengwa na huwa halilalamiki ni kundi letu sisi wapagani. Zaidi ya kingunge Ngombale Mwiru hakuna mpagani mwingine amewhi kuwa hata mbunge. Ila ninyi wenye dini mnagawana madaraka kama njugu halafu leo mnaanza kulaumiana eti huyu anatuonea ooh yule ndio mbaya. Si mmesha peana miaka kumi kumi. Kwanza kaeni chini muelewane je mlipena uraisi ili kunufaisha dini moja au watanzania??

Sisi wapagani nasi itabidi tujipange tunadai wakati wetu tena tutahitaji kuanzia raisi mpaka mwenyekiti wa kitongoji kwa miaka kumi. Na wakati wetu hatutaka kusikia makelele ya aina yeyote na mkae kimya na dini zenu.

Kila kundi linahaki sawa Tanzania, kila rangi ina haki sawa TZ. Kama kuna kundi linaona linanyimwa haki yake ya kikatiba ni vyema kuweka haki zaki bayana na likipewa makundi yote nayo yapewe bila upendeleo.

Chief Mkwawa wa Kalenga
Kama dini zinashindwa kuwafanya Watanzania ziacheni. Warudishieni wazungu na waarabu dini zao turudi kwenye apango yetu.
 
Asalaam aleykum wana bodi.
Sote humu ni mashahidi wakati wa kampeini mwaka 2010 Mgombea Urais wa Ticket ya CCM na wenzake wote walikuwa wanalia kuwa kuna chama kinachoendesha kampeini za Udini. na kwenye hotuba yake baada ya kuapishwa aliukemea kwa nguvu zote. Sote hapa ni mashahidi kuna aya moja kwenye Quran Tukufu inasema " Sema kweli ingawa inauma, sema kweli tupu hata kama unachinjwa." nami nasema ukweli inagawa inauma. Kwenye kampeini na baada ya kampeni Udini uliokuwa unasemwa ni dhidi ya Dr. Slaa na wakatoliki. Eti Rais wa mioyo ya Watanzania anapigiwa chapuo na Kanisa katoliki.

Kwa sasa nchi inazizima kwa vitendo vya ufunjifu wa utulivu(siwezi kusema kamwe tuna amani nina sababu za kusema hatuna amani - tuna utulivu) kutoka kwa makundi ya dini Kiislamu(Sio waislamu wote) dini ambayo haikutajwa na Kikwete wakati analia kupandikizwa mbegu ya Udini nchini.

maswali yangu ni haya:-
  1. Je, CCM baada ya kuhisi Chadema wanapigiwa upatu na Katoliki (Kama basi ni kweli) nao waliwafuata waislamu?
  2. Je. Matarajio waliowapa waislamu wameshindwa kuyatekeleza ndo maana Jambo dogo tu wanaharakati wa kiisamu wanalipuka na kuvunja sheria za nchi?
  3. Je Ule ujasiri waliokuwa nao CCM wakituhumu Kanisa kuwa linambeba Dr.Slaa umeishia wapi wakashindwa kuusimamia dhidi ya kina ponda na muamsho?
Mi nadhani the head of Gorvenment/CCM leaders are almost empty. Hawawezi kuongoza tena wanabaki kurukia rukia tu mambo mwisho siku wanatuingiza msituni na kuzalisha wakimbizi wa Kitanzania. Tuikataeni CCM kwa nguvu zote yani kama vile Sheikh na Kitimoto na Msabato na Kambale

twende kwa padri slaa ama sheikh profesa lipumba ?
 
Nimeweza kupata nchi 10 tuu na mabalozi wetu huko kwenye mabano. Tanzania haina balozi katika nchi nyingi tuu za Ulaya.

1. Marekani (Mwanaidi Maajar)
2. Uingereza (Peter Kalaghe)
3. Japan (Salome Sijaona)
4. Italy (Ali Abeid Amani Karume)
5. Scandinavian (Mohamed Mzale)
6. Canada (Alex Massinda)
7. Germany (Ahmada Ngemera)
8. Australia (Didier Murcia)
9. China (Khalid S Mohamed)
10. Brazil (Francis Malambugi)

Simjui hata mmoja wa hao mabalozi hapo na wala sizijui dini zao. Lakini kama tukiamua kuendelea kufuata ujinga wetu wa kuamua dini ya mtu kwa kuangalia jina lake, basi utakuta hapo juu waislamu na wakiristo wapo 50%-50%.

Kwa mujibu wa CIA facts book kuhusu Tanzania, CIA wanasema kwamba watu wa Tanzania ni Muslims (35%); Christians (30%); Indigeneous belifs (35%). Kama takwimu hizi za CIA ni sahihi, basi wewe mkiristo unayelalamika kwamba JK anapendelea waislamu, fikiria tena. Natumaini kwamba wewe ni mtoto mdogo ambaye hujui unachokisema; lakini kama wewe ni mtu mzima isipokuwa ni mpumbavu tuu, basi upumbavu wako na watu kama wewe utaipeleka nchi pabaya.

ONYO.
Waislamu ndiyo waasisi wa nguvu zote za kisiasa zilizopigania uhuru nchi. Hivyo basi, kihistoria (Kwa wale wenye kujua umuhimu wa historia ) Waislamu wameshaonyesha kwamba wana uwezo wa kujipanga na kutimiza marengo yao. Wakiristo hawana historia hiyo katika nchi hii. Hivyo basi, kwa tabia yenu hii ya kupandikiza chuki za kidini, kuna siku moto.
unamsema mwenzako mdini, then mwishoni u talk rubbish! hizi ni hadithi za kipuuzi tumechoka kuzisikia, ooh sisi ndio tukliopigania uhuru and blabla! mbona wakristo hawasemi kwamba kiongozi wakupigania uhuru , nyerere alikuwa mkristo? why alwas u guys are selfish ? Huna unayemtisha na vurugu zenu, hata wakristo wakiamua wanaweza fanya vurugu kama mnazofanya. Kunyamaza kwa wakristo ni sababu imani yao haijawafundisha vurugu , na Mungu wao si wamachafuko! Thats all , ndio maana wananyamaza , otherwise msione kwamba mna nguvu sana kwa kufanya ujinga wenu na wewe hapaunatishia watu kwa data za uchochoroni! You are always proud of making troubles all over the world , and yet u tell us that nyinyi ni dini ya HAKI! Haki ipi ya vurugu, machafuko, ubinafsi na kila aina ya magomvi?
 
JK ana udini kupita kiasi. Alaaniwe milele

Hapana hata kidogo kwa watu wanayemfahamu jk hata kidogo jamaa hana time na dini na ndiyo maana alilalamika sana dr slaa kutumia mtandao wa makanisa mwaka 2010 kutafuta niia ya kuingilia ikulu
 
Mtu anayejikita sana kwenye udini namchukia sana. Watu wanalalamikia udini ukiangalia mijadala hata ya jf baadhi wanajikita kwenye kuukuza. Tena kwa kutojua wajatafsiri udini kwa kuangalia jina la mtu. Akiona halitumiki kwenye dini yake anamvamia mtu. Udini si majina pevukeni jamani. Eleza mtu amefanya jambo gani lenye kuashiria udini.
 
Hapana hata kidogo kwa watu wanayemfahamu jk hata kidogo jamaa hana time na dini na ndiyo maana alilalamika sana dr slaa kutumia mtandao wa makanisa mwaka 2010 kutafuta niia ya kuingilia ikulu

c wote ni wapumbavu kama wee unavyotaka kutuaminisha nikupe mfano mdogo 2 ule uchaguzi wa ccm dodoma akiwa kama m/kiti alihakiki kwenye ilesekritari kuu aliyo chagua yeye akiwa kama m/kit ina watu 9 ktk 8 ni waislam 1ndiyo mkristo achilia mbali baraza la mawaziri je ninani mdini hapo
 
Ndugu zangu watanzania wazalendo,

Kwa wale wanaofuatilia mwenendo wa maisha hapa nchini, mnaweza kukubaliana nami kuwa hakuna wakati ambapo suala la udini limeibuka waziwazi kama sasa chini ya uongozi wa kikwete. Hata wakati wa mzee mwinyi hali haikuwa hivi ukiondoa lile tukio la kuchoma moto bucha za nguruwe.

Jambo la kujiuliza ni je, kwa nini hali hii itokee sasa? Ukweli ni kwamba moja ya agenda ya kikwete katika uongozi wake ni eti kuwanyanyua waislam. Hilo limejidhihirisha wazi katika teuzi zake nyingi kwenye nafasi mbalimbali serikalini. Mfano mzuri tu, angalia balozi zeti nje ya nchi. Angalia mabalozi waliopo nchi tajiri za ulaya na asia na angalia nchi maskini hapa bara la afrika na asia. Utapata jibu.

Inasemekana hata suala la mahakama ya kadhi amewaambia waislam wenzie kuwa wakae kimya na kuwaahidi kuwa atalishughulikia kwa staili nyingine. Ndiyo maana sasa hivi halipigiwi kelele sana.

Ninachotaka watanzania wazalendo watambue ni kwamba tuna kiongozi mdini na hatari sana. Anachoongea jukwaani sicho kilichomo moyoni na wala sicho anachotenda. Muhimu ni kuomba Mungu amalize uongozi wake bila nchi kuingia ghasia za kidini. Vinginevyo, tunakoelekea ni hatari.

Hatua ya kuongelea suala la udini kwenye hotuba yake bungeni hivi karibuni kwamba ni mojawapo ya nyufa kubwa na hatari ni geresha tu ya kuwapumbaza wananchi ambao tayari wameanza kuwa na wasiwasi nae.
Membe ni mtu Wa karibu sana wa Kikwete mbona anamtumia Malecela kwenda kumshawishi Pengo ili kanisa limuunge mkono na je huu si udini huko CCM au tuanze kuanika kila harakati hapa ? CCM mna haring Nchi kisa madaraka
 
Back
Top Bottom